"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Saturday, September 17, 2016

WINGU LA MASHAHIDI WA KRISTO NA MJUMBE WA MUNGU, NDUGU WILLIAM BRANHAM

Blogu hii imeanzishwa mahususi kwa kusambaza ujumbe wa siku za mwisho kwa BIBI ARUSI safi wa  YESU KRISTO waliokwisha wekwa tayari kwenda katika unyakuo. Hatufangamani na dhehebu lolote wala shirika lolote la kidini, ila tunawakaribisha Wakristo Wote ulimwenguni wenye kumpenda Bwana. Tunaamini Biblia kuwa ni kitabu pekee kitakatifu kilichoshushwa na Mungu kumwongoza mwanadamu,na hivyo misingi ya mafundisho yetu yote unakitegemea hicho.

pia tunaamini kulingana na  malaki 4:5 kama inavyosema " angalieni nitawapelekea Eliya Nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogfya. Naye ataigeuza mioyo ya Baba iwaelekee watoto wao na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana."

kama Mungu alivyoahidi angemtua Eliya nabii. ambaye kulingana na maandiko tunafahamu Yohana mbatizaji aliyatimiza hayo maandiko kwa sehemu "A"( Yaani kuja kabla ya ile siku KUU YA BWANA) ambaye yeye alitangulia kuja kwake Kristo kwa mara ya kwanza kwa kusudi la kuigeuza Mioyo ya Baba iwaelekee Watoto. hii inamaanisha kwamba Yohana alihubiri injili ya kuwarejeza waalimu wa sheria na marabi wa torati ili waiamini injili ya Kristo ambayo baadaye ilikuja kuhubiriwa na wana wa pentecoste yaani Mitume wa Yesu Kristo.Lakini hawakumpokea kuwa kama nabii wa Bwana bali walimkataa kama maandiko yanavyosema.

Lakini ile sehemu 'B' ya maandiko ambayo inasema Eliya atakuja kabla haijaja ile siku ya KUOGOFYA , yaani ile siku ya kutisha ya Mungu Mwenyezi. hapa Eliya atakuja tena ili kuigeuza mioyo ya Watoto iwaelekee Baba zao.kumbuka Yohana mbatizaji alikuja kuigeuza Mioyo ya Baba iwaelekee wana lakini sasa huyu atakuja kuigeuza mioyo ya Watoto iwaelekee Baba zao. katika siku za mwisho ambazo ndizo tunazoishi sasa. Na watoto wanaozungumziwa hapo ni sisi tunaoishi sasa katika nyakati hizi za mwisho, na mababa ni Mitume wa Kristo wa kanisa la kwanza ambao mafundisho yao ni biblia ambayo ndio msingi wa Ukristo wa kweli.

hivyo basi Eliya huyu wa mwisho alioahidiwa ni kwa kazi moja tu ya kuturudisha sisi katika Ukristo wa biblia ambao kwa muda mwingi kama tunavyosoma katika historia ya ukristo uliingiliwa na mafundisho ya uongo nayo ni mafundisho ya mpinga Kristo ambayo kwenye ufunuo 2:6 "Kristo ameyakemea kama mafundisho ya wanikolai" ambayo leo hii tunaweza tukayaona katika kanisa la Kristo.

hivyo basi Eliya wa kwanza alitangulia kuja kwa kwanza kwa Kristo, na katika siku hizi za mwisho Mungu alimtuma ndugu WILLIAM MARRION BRANHAM kama Eliya  kwa kuliandaa kanisa kwa ajili ya kuja kwa pili kwa Kristo,na ujumbe Mkuu Bwana aliompa ni kuwarudisha watu kwenye ukristo wa kimaandiko yaani biblia na kulingana na ufunuo 18:4.''.....tokeni kwake enyi watu wangu msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake."..huu ndio ujumbe wa bibi arusi safi wa  Kristo wa wakati huu wa mwisho.  .


(katika eneo hili la mto Ohoi karibu na barabara ya Spring jeffersonville Marekani ndugu Branham alipokuwa akibatiza mnamo juni 1933 picha hii ilipopigwa  hapo ndipo aliposikia sauti  ikisema "kama Yohana mbatizaji alivyotangulia kule kuja kwa kwanza kwa Kristo, wewe nawe utatangulia kuja kwake kwa pili"..na mwanga mkubwa ulitokea mahali pale ulioambatana na hiyo sauti na maelfu ya watu waliohudhuria waliuona huo mwanga, na magazeti mengi pia siku uliyofuata yalitangaza jambo hilo kuu la kustaabisha"


(Nguzo ya moto ilionekana juu ya kichwa cha ndugu William branham alipokuwa akihubiri huko houston texas, Marekani, januari 1950. nguzo hiyo ilionekana miongoni mwa mamia ya watu na kuchukuliwa katika picha kama inavyoonekana hapo juu, nguzo hii hii ndiyo iliyomtokea alipokuwa akibatiza kwenye ibada yake ya ubatizo katika mto ohio huko indiana na sauti ilisikika katika hiyo nguzo ya moto ikisema ''kama yohana mbatizaji alivyotangulia kule kuja kwa kwanza kwa Kristo wewe nawe utakutangulia kuja kwake kwa pili" sauti hii pia ilisikiwa na watu wengi walio hudhuria mahali pale.

5 comments:

  1. Haleluiaa, hakika BWANA ana njia sahihi kwa wakati sahihi

    ReplyDelete
  2. Wapendwa nimefurahishwa na juhudi yenu katika Bwana.

    ReplyDelete
  3. Je ni kwa namna gani naweza kupata uthibitisho wa hakika kuwa huyu alikuwa nabii wa Mungu?

    ReplyDelete