"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Friday, December 30, 2016

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO


Majaribu matatu Yesu aliyojaribiwa na shetani akiwa njikani siku 40, yanaweza yakachukuliwa kivyepesi lakini ukiyachunguza kwa undani yana tafsiri kubwa sana na maana kubwa sana katika maisha ya kila mkristo akiwapo hapa duniani, na yanahitaji uongozo wa Roho Mtakatifu kuyaelewa yale majaribu yana maana gani kama yalivyoandikwa pale. 



Wengi wetu tunafikiri kuwa Yesu alipandishwa nyikani siku 40, kujaribiwa na ibilisi, na alipomaliza kujaribiwa alirejea katika maisha yake ya kawaida halafu basi yaliishia pale. Watu pia wanafikiria kuwa shetani alimtokea Yesu kwa mfano wa nyoka au vinginevyo na kuanza kumjaribu kumpa yale majaribu matatu. Lakini hiyo sio kweli dhumuni kuu la Yesu kupandishwa nyikani ni kwenda kukutana na Mungu wake kwa dhumuni la kupokea maagizo fulani au ufunuo fulani, Tunaona sehemu fulani kristo aliwaambia wanafunzi wake mwenyewe Mathayo 17:21  [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] Yesu Kristo hakuongozwa na Roho na kufunga siku 40 nyikani kwenda kukutana na shetani hapana bali ni kwenda kukutana na Mungu wake. Tunaweza tukaona mfano mwingine kama Musa alivyoitwa na Mungu mlimani kwenda kuchukua zile amri 10, alifunga siku 40 usiku na mchana, na alikuja kufunga tena siku nyingine  40 mchana na usiku kuwaombea wana wa israeli kwa makosa waliyoyafanya ya kuabudu sanamu. Kwahiyo Bwana Yesu Kristo kufunga nyikani siku 40 ilikuwa ni kwa ajili ya huduma yake iliyokuwa inakaribia kwenda kuanza, ndipo huko Mungu alipomfunulia huduma yake itakavyokuwa pamoja na yale majaribu makuu matatu atakayokutana nayo katika maisha yake ya huduma.


JARIBU LA KWANZA:

Tunasoma katika luka 4:1-4 "1 Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,
2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.
3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate.
4 Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu."
Hapa tunaona Bwana Yesu baada ya siku 40 kuisha aliona njaa na alipoona njaa akiwa kama mwanadamu alitamani chakula, lakini safari yake ya nyikani ilikuwa bado haijakwisha kwahiyo shetani alipoona kuwa huyu mtu anauhitaji wa chakula alimletea ushawishi moyoni wa kugeuza  jiwe kuwa mkate kwasababu alifahamu kuwa anaweza kufanya hivyo. Sasa hapa inadhaniwa kuwa shetani alimtokea akamwambia hivyo la! hakumtokea bali alimletea ushawishi moyoni kufanya vile, biblia inasema mtu anajaribiwa kwa tamaa zake mwenyewe,(yakobo 1:14 ). Yesu kama asingeona njaa asingejaribiwa, njaa ilipokuja shetani naye akapata nafasi lakini pamoja na hayo Bwana alishinda kwa kuwa aliyajua maneno ya Baba yake kuwa "mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litakalotoka katika kinywa cha Mungu", aliona sio vema kuyakatiza mapenzi ya Mungu kwa sababu ya chakula, alitambua kuwa ni Mungu ndiye aliyempeleka kule kwa hiyo hata kama siku za kukaa kule nyikani zingeongezeka mpaka kufikia 60,au 70 au 100. angeendelea kuishi kwasababu anaishi kwa neno linalotoka katika kinywa cha baba yake na sio kwa chakula cha mwilini tu. Kwahiyo tunaweza kuona Yesu Kristo aliweza kushinda kwa namna hiyo.

Lakini jaribu hili sio kwamba liliishia pale nyikani tu, ule ulikuwa kwake ni kama ufunuo wa mambo atakayokwenda kukutana nayo mbeleni katika huduma yake, Mungu alimuonyesha  ni moja ya jaribu kuu ambalo shetani atampelekea katika maisha yake ya huduma.


Maana ya kugeuza jiwe kuwa mkate ni ipi?
kugeuza jiwe kuwa mkate inatokea pale mtu anayopitia hali ya uhitaji au shida ya kitu fulani na anafahamu kuwa ni Mungu ndiye aliyempitisha katika hiyo hali, lakini yeye anatafuta njia mbadala ya kujing'amua na hiyo shida angali iko katika uwezo wako wa kufanya hivyo, mfano Yesu Kristo alitambua kuwa anapitia katika hali ya taabu na alikuwa na uwezo wa kugeuza lile jiwe kuwa mkate lakini hakufanya vile kwasababu alijua kuwa angeenda nje ya mapenzi ya Mungu sio kana kwamba hakuwa na njaa au alikuwa anajinyima au hakuweza kufanya la! bali alijinyenyekeza chini ya Mungu katika hali ngumu aliyokuwa nayo..Tunaona jaribu kama hili liliwapata  wana wa Israeli  lakini walilishindwa pale walipopitishwa miaka 40 nyikani wakaanza kumnung'unikia Mungu wakitaka watimiziwe matakwa yao wenyewe na sio matakwa ya Mungu. Tunaona katika hali ngumu waliyokuwa nayo nyikani ukafikia wakati wakasikia njaa kama Yesu Kristo alivyosikia njaa, na kwajinsi  Yesu alivyokuwa na uwezo wa kubadilisha jiwe kuwa mkate vivyo hivyo na wao pia walikuwa na uwezo huo huo wa kubadilisha jiwe kuwa mkate mfano huu tunawaona badala ya kujinyenyekeza chini ya mapenzi ya Mungu wakaanza kumnung'unikia Mungu wakitaka nyama nyikani na Mungu aliwapa nyama, alikuwa akiwapa chochote walichokuwa wanakihitaji(huku ndio kugeuza jiwe kuwa mkate)..kumbuka wana wa israeli walikuwa wanajua kuwa lolote watakalomwomba Mungu atawapa kama vile Yesu alivyojua kuwa lolote atakalomwomba Baba yake atampa,  tunaona wana wa israeli walikuwa wanashushiwa mana kule jangwani kwa hiyo wakatumia kigezo hicho kwa tamaa zao kutaka vitu ambavyo sio sawasawa na mapenzi ya Mungu kwa kisingizio kuwa wanasikia njaa lakini hawajui kuwa shetani ameshawashinda kwa kutoweza kulishinda hilo jaribu.

 kumbukumbu 8:1-5"Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki.
2 Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.
3 Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana.
4 Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini.
5 Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo. "
Vivyo hivyo kristo katika huduma yake ambayo Mungu alikuwa akimtuma alijifunza kutokutazama vitu vya nje kama mali,chakula, mavazi hakujali hata sehemu ya kulala japokuwa alikuwa na uwezo wa kupata mali, kula na kunywa, na sehemu za kulala kwasababu alihesabu kutenda mapenzi ya Mungu kwanza ni bora kuliko njaa ya vitu vya nje 
yohana 4:30-34 Basi wakatoka mjini, wakamwendea.
31 Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule.
32 Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi.
33 Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula?
34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake."
 Kwahiyo alifahamu eneo shetani atakalomtesea katika maisha yake ya huduma ni hapo kwenye njaa ya mambo ya nje, lakini kwa kujua ufunuo huo alikuja kuweza kuyashinda yote. Na ndio maana aliwaambia mahali fulani wanafunzi wake
 mathayo 6:26" Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? " aleluya!!

Jambo hili hili linajirudia kwa Mkristo anayesema ameamua kumtumikia Mungu, kumbuka haya majaribu matatu kila mkristo lazima ayapitie na hakuna majaribu makubwa zaidi ya hayo shetani anaweza akamjaribu mtu, vivyo hivyo kwa mkristo aliyeamua kumtumikia Mungu atambue kuwa ni lazima akutane na hili jaribu, pale shetani anapokuona upo karibu na Mungu wako sana na upo katika hali ya nyikani(kumbuka nyikani ndipo Mungu anaposhushia mana, na nyikani ni sehemu yoyote isiyokuwa na tumaini lolote, inawezekana katika maisha sana sana katika safari ya wokovu mtu anapoanza kumwangalia Kristo) hapo ndipo shetani analeta ushawishi kama huo alioupata Bwana ili uache njia yako, anatumia Neno kukufanya wewe utimize tamaa yako ambayo sio sawasawa na mapenzi ya Mungu, atakwambia fanya hivi au fanya vile ili uishi vizuri ndipo umtumikie Mungu, atakwambia acha hicho unachokifanya fanya kwanza hichi ujikwamue kimaisha..atakwambia sasa tafuta kwanza maisha ndipo uje kumtumikia Mungu baadaye, tafuta pesa kwanza maana unashida ya pesa sasa hivi halafu Mungu utamtafuta baadaye, atakwambia jiweke vizuri kiuchumi kisha utaenda baadaye kuhubiri injili, atakwambia huoni watumishi wote wanafanya hivyo,?? na atakupa sababu zote kwamba una uwezo wa kufanya hayo yote na ni kweli ukiangalia unao huo uwezo lakini nia yake yeye sio wewe kuyakidhi mahitaji yako bali ni kukufanya utoke katika kusudi la Mungu la kumtazama yeye, anakufanya usilifahamu neno la "mtu hataishi kwa mkate tu," kwahiyo anatumia tamaa zako kukufanya uende kinyume na mapenzi ya Mungu. kumbuku wana wa israeli walivyokuwa Mungu kuwapitisha nyikani ilikuwa sio kwenda kuwakomoa, lakini wangejuaje kama Mungu anaweza kuwalisha pasipo kazi ya mikono? wangelifahamu vipi hilo neno la MTU HATAISHI KWA MKATE TU ?? kama wasingepitishwa nyikani. unaona ni kusudi kabisa la Mungu kumpitisha mtoto wake nyikani ili ajifunze kumtegemea lakini shetani anavumbua njia mbadala kumchonganisha na Mungu haya ndiyo yaliyowakuta wana wa Israeli.


Jambo hili hili linawatokea wakristo wengi wanapopitishwa nyikani(kumbuka kila mkristo lazima apitishwe nyikani) wanashindwa na hili jaribu la shetani wanashindwa kufahamu kuwa mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litakalotoka katika kinywa cha Mungu, mtu hataishi kwa pesa tu, mtu hataishi kwa kazi tu, mtu hataishi kwa mifumo tuliyoizoea tu, mtu hataishi kwa gari na nyumba tu, mtu hataishi kwa umaarufu wala chochote cha ulimwengu huu, bali mtu ataishi kwa neno la Mungu tu!! Mungu ni zaidi ya mali na kila kitu Kristo anasema .(mathayo16:25-26.."Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? ).kila siku unasema ngoja nisubirie kidogo, nisubirie kwanza nifanye kitu fulani nikishakipata ndipo nianze kumtafuta Mungu, mwingine yupo katika taabu anasema ngoja kwanza nitafute pesa nitoke katika hii tabu ndipo nianze kumtafuta Mungu huko ndiko kugeuza jiwe kuwa mkate, unadhania kuwa mtu ataishi kwa pesa tu pasipo pesa huwezi kuishi(wana wa israel hawakuwa na fedha lakini walilishwa miaka 40 jangwani), unasema pasipo nyumba huwezi kuishi(yesu alilala milimani ambaye ndiye tunayemwita Bwana wetu na mfalme wetu),

 Yesu alisema mathayo 6:31-34" Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake." 
Na pia Yesu alisema chakula changu ni kuyatenda mapenzi ya baba yangu (yohana 4:34) vivyo hivyo na sisi tuseme hivyo chakula chetu ni kuyatenda mapenzi ya baba yetu na kuyamaliza. Tusigeuze jiwe(vitu visivyo na uhai)  kuwa mkate. Mungu anapotuita tuwe tayari kutii na kusema ndio pasipo kuangalia mambo mengine ya kando kando, kwa kufanya hivyo ndivyo tutakavyoshinda hilo jaribu la mkate vinginevyo hatutaweza.

JARIBU LA PILI:

Luka 4:5-6"  Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.
6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. "
Kwenye Jaribu hili tunaona Kristo akihamishwa kutoka nyikani mpaka kwenye milki zote za ulimwengu akaonyeshwa fahari zote za ulimwengu. Hapa sio shetani alimchukua katika mwili bali ni alichukuliwa na Mungu katika maono kuonyeshwa lile jaribu la shetani litakavyokuwa katika maisha yake ya huduma''. Kwa namna ya kawaida ni vigumu adui yako akuambie nisujudie halafu nitakupa vitu vyote, unafahamu kabisa huwezi kumsujudia kwasababu unajua kabisa anakujaribu kwahiyo ni wazi kabisa shetani hakumtokea Yesu bali ni Mungu ndiye aliyemwonyesha yale maono, na hili jambo lilikuja kutimia katika maisha yake kule mbeleni pale huduma yake ilipoanza kuwa kubwa, alipojulikana kila mahali na watu wote mfano huu tunaona alipokwenda Samaria wale watu wa ule mji walitaka kumshika na kumfanya mfalme
(Yohana 6:14-15 "Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.15 Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake. ")
 Jaribu kufikiria leo hii kama Bwana Yesu angekuwa mfalme wa wasamaria msalaba tungeujulia wapi, kwahiyo tunaliona hilo ni jaribu shetani alilomletea lakini alikumbuka alionyeshwa na baba yake akiwa jangwani, ya kwamba utamsujudia Bwana Mungu wako yeye peke yake, sasa kusujudia pale sio kwenda kumpigia magoti shetani bali ni kukubaliana na jambo lolote shetani atakalokuletea mbele yako kinyume cha mapenzi ya Mungu, tunaona hata leo hii watu wanamsujudia shetani pasipo hata wao kujua pale wanapotenda dhambi, unadhani shetani angemtokea mtu na kumwambia nisujudie nani angekubali?? yeye siku zote anatumia hila kuabudiwa anamfanya mtu adhani kuwa anamwabudu Mungu kumbe anamwabudu shetani. Vivyo hivyo shetani alivyokuwa anajaribu kufanya kwa Bwana Yesu Kristo kwa kutaka kusujudiwa kwa kupitia ufahari,lakini Kristo alishinda, aliona ni vyema kuiendea njia ya msalaba aliyowekewa na baba yake kuliko kukubali sifa na heshima na vyeo na ukuu na ufalme kutoka kwa watu.Lakini leo hii angeonekana ni mtu anayechezea bahati.

Vivyo hivyo jaribu hili pia linawakuta wakristo sana sana watumishi wa Mungu walio katika huduma, mwanzoni wataanza vizuri katika huduma na Mungu atatembea nao lakini shetani anapoona hivyo ili kumwaribu anamletea jaribu kama hili lililomkuta Bwana Yesu, anaanza kwa kumpa umaarufu wa ghafla, watu watakuja kumwambia njoo uwe kiongozi wetu tutakupa pesa, nyumba, magari, tutakufanya kuwa maarufu kushinda hapo ulipo, tutaikuza huduma yako zaidi ya hapo ilipo, ila acha tu huo mtindo wako wa kale wa kuhubiri, punguza ukali wa maneno tutakupa kila kitu, we hubiri tu kama sisi tunavyohubiri, wengine wanaitwa na wanasiasa wawasaidie katika siasa zao na wanaahidiwa kupewa pesa nyingi. kwahiyo mtu huyu badala ya kukaa chini na kutafakari kama huduma yake itaathirika au la! yeye anakubali bila kufahamu kuwa hizo ni hadaa za shetani kutaka asujudiwe. Na watumishi wengi wa Mungu wameshindwa hili jaribu wameacha kusudi lao la kufundisha, na kuiendea njia ya msalaba, wakaiendea njia ya watu wa mataifa ili kupata umaarufu na heshima. luka 6:26"  Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo. "

JARIBU LA TATU:

Luka 4:9-12" Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini;
10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde;
11 na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. "
Katika jaribu la tatu tunaona Yesu Kristo akipelekwa katika kinara cha hekalu, unaweza ukajiuliza kwa nini alipelekwa Yerusalemu, na ni kwanini kwenye kinara cha hekalu na sio penginepo?
Ono hili alipewa kuonyeshwa mwisho wa safari yake ya huduma, kwamba mwishoni atawekwa kwenye kinara cha hekalu ambacho ni msalaba, Yesu Kristo safari yake ya mwisho ilikuwa ni msalabani(hata sio ajabu kuyaona makanisa yakiwa na msalaba juu, hii inaleta picha kuwa pale juu ya kinara cha hekalu alipowekwa Yesu ni msalabani) na kumbuka hata pale msalabani shetani alikuwa akimjaribu kwa maneno hayohayo kama tunayoyaona hapo juu, shetani alimwambia kipitia vinywa vya wale watu

 ''mathayo 27: 39-44" Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa vyao, wakisema,
40 Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani.
41 Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe.
42 Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.
43 Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.
44 Pia wale wanyang'anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile. "
 Lakini kama Bwana Yesu Kristo asingetambua hayo majaribu ambayo alionyeshwa na baba yake akiwa nyikani angejishusha chini msalabani na watu wote wangeamini kwasababu alikuwa anao huo uwezo, picha hii hii tunaiona pale usiku ule walipokuja kumshika Yesu na petro alipotaka kumwokoa Bwana  alimwambia (mathayo 26:52-54 " Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?" ) Kwahiyo tunaona Yesu Kristo alikuwa ana huo uwezo wa kujishusha msalabani lakini je! angejishusha msalabani mapenzi ya baba yangetimizwaje? na sisi tungepataje wokovu?.

Vivyo hivyo na kwa mkristo yeyote anayeipenda njia ya msalaba(japo sio wote watakayoipitia ) jaribu kama hili atakutana nalo ndilo la mwisho kumbuka shetani hatakuacha hata katika dakika ya mwisho ya wewe kukata roho atakuwa karibu yako kukufanya uanguke. Msalaba ndio hatua yetu ya mwisho, Yesu alisema mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa baba isipokuwa kwa njia ya mimi, njia hapo anayoizungumzia ni maisha yake yeye sasa tunayaamishia kwetu, na alisema pia mtumwa sio mkuu kuliko Bwana wake, kama yeye walimwita belzebuli, mwenye pepo, alienda msalabani kufa kifo cha aibu je! inatupasaje sisi? hatupaswi kuionea haya njia ya msalaba, watazame mitume na manabii na wakristo wa kale kwa kuitetea kweli na kuisimamia kweli hawakupenda maisha yao hata kufa, walihesabu kuwa utukufu wa Mungu ni bora kuliko utukufu wa wanadamu, Kristo alisema mtu yeyote akitaka kunifuata ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake anifuatae kila siku (mathayo 16:24),na unajua msalaba ni nini?, mwisho wake ni golgotha. 


Kwahiyo utakapofikia katika jaribu la tatu na la mwisho ambalo shetani atakuacha ni pale utakapoona unaenda kutiwa mikononi mwa shetani kama Yesu Kristo na  mitume na manabii. walivyofanyiwa, angali una uwezo wa kujiepusha nalo kama Yesu tunaweza kuona shetani alimvaa hata Petro akijaribu kumshawishi Yesu asiipitie njia ya msalaba, lakini Yesu alimwambia nenda nyuma yangu shetani huyawazi ya Mungu bali ya wanadamu, lakini Yesu alijinyenyekeza kama kondoo aendaye kuchinjwa na ndivyo walivyofanya mitume watu wa Mungu kama stephano, yohana n.k huko ndiko kulishinda hilo jaribu( na kumalizia kusema Baba wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo).

Yesu Kristo anasema (ufunuo 3:20-22" Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. ). kwahiyo kushinda ni nini?? kushinda ni kule kushinda yale majaribu matatu kama Bwana Yesu alivyoyashinda."

  • Kwa ujumla haya majaribu matatu yanapita  kwa mkristo katika hatua tatu za maisha yake ya wokovu,..hatua ya kwanza ni pale anapomwamini Kristo, anapolazimika kuacha maisha ya ulimwengu huu na kumfuata kristo(anapotoka Misri kuelekea kaanani ni lazima apitie jangwani imani yake kwa Mungu ijaribiwe). ndipo shetani atakapokuja na jaribu la kwanza la kugeuza jiwe kuwa mkate.
  • Hatua ya pili inakuja pale mtu anapoingia kwenye huduma, anapotiwa mafuta kuifanya kazi ya Mungu.shetani atatafuta kila njia ya kuiaribu/kuivuruga huduma yako, atakuja na lile jaribu la pili kwamba atakupa kila kitu ila tu umsujudie, atatumia pesa, umaarufu, ukuu, ufalme, mafanikio n.k.ili kuibatilisha njia Mungu aliyokuitia kuiendea.
  • Hatua ya tatu na ya mwisho ni pale utakapomaliza safari yako duniani shetani atakuja na njia mbadala ya kukiepuka kifo angali unajua kabisa ni njia Mungu aliyokusudia uipitie, hivyo atakufanya utumie uweza wako kutaka kulipindisha kusudi la Mungu juu yako. Ndipo atakapokuletea jaribu la tatu.
Sio kwamba usipopitia hiyo njia itakufanya usiende mbinguni la! Labda utaenda lakini utakuwa hujashinda kwasababu hujapigana kikamilifu, thawabu yako itapunguzwa kama utashindwa na majaribu hayo ya shetani, 
1wakorintho 9:24" Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.
25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.
26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;
27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
Na pia mtume Paulo anasema,
 2timotheo 2:5"4 Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
5 Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali. "
mtume Paulo pia aliandika..
wafilipi 3:10-14"10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;
11 ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.
12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. "
mwisho mtume Paulo aliandika 
2timotheo 4:6-8"6 Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. "

Mungu akubariki sana ndugu yetu mpendwa.

Wednesday, December 28, 2016

MASWALI YALIYOULIZWA NA MAJIBU YAKE: SEHEMU YA 8

SWALI 1; Wale manabii 400 waliomtabiria mfalme Ahabu wakati wa Mikaya walikuwa ni manabii wa Mungu au?
JIBU:ndio wale manabii 400 waliomtabiria Ahabu (1wafalme 22 )walikuwa ni manabii wa Mungu, na hapo kabla walikuwa wanapokea unabii sahihi kutoka kwa Mungu kwasababu manabii zamani walikuwa wanajaribiwa kabla ya kuitwa mbele za wafalme, kwahiyo ni dhahiri walikuwa wanatoa unabii na unatimia, japo mioyo yao haikuwa mikamilifu mbele za Mungu kama ilivyokuwa kwa nabii Mikaya...walikuwa wanapenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu na ndio maana walikuwa wanakaa katika majumba ya kifalme, wakisifiwa na wafalme mfano wa manabii wengine kama hawa tunamwona nabii Balaamu(hesabu 22)..huu ni mfano pia wa manabii wengi tulionao sasa wanapenda pesa,umaarufu,ukubwa, wanawatolea watu unabii ili wapate pesa, watu kama hao ni rahisi kuingiwa na roho zidanganyazo, na kuwafanya leo wasikie kutoka kwa Mungu kesho wasikie kutoka kwa shetani..lakini manabii kama Mikaya ambao ni wachache sana wao  husimama katika Neno, huishi maisha matakatifu na kusema kile Mungu anachotaka tu waseme  pasipo kujali cheo cha mtu, hivyo Mungu anawaepusha na roho zidanganyazo na unabii wao unakuwa thabiti na hakika, lakini kwa hao wengine wanafungua milango kwa roho zidanganyazo kama ilivyowatokea wale manabii 400.

SWALI 2; Isaya 4:1 na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu wenyewe lakini tuitwe  tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu. Je; andiko hili linamaanisha nini? Kwanini wanawake? Kwanini wawe saba? Kwanini chakula chao na nguo zao na sio za mume wao? maanake mume akioa moja ya majukumu ya kwake kufanya kwa mkewe ni kumlisha na kumvika sasa hawa wanakula na kuvaa vya kwao ni kitu gani hawa wanawake?

JIBU:ufunuo wa mstari huo ni huu..wanawake saba ni makanisa saba (katika vipindi saba vya kanisa kama inavyooneka katika ufunuo 2 & 3)..mtu mume mmoja ni Yesu Kristo,.Lakini hao wanawake wote 7 wanasema watakula chakula chao wenyewe na kuvaa nguo zao wenyewe bali waitwe tu kwa jina la yule mtu mume mmoja ambaye ni Yesu Kristo.Jambo hili la kusema tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu wenyewe ni tabia za hayo makanisa yote 7 yalivyokuwa, kila kanisa lilikuwa na tabia yake pekee, na yote yanatafuta kumpendeza Yesu Kristo lakini kwa njia zao wenyewe, kwahiyo hicho "chakula" kinachozungumziwa hapo ni mapenzi yao wenyewe, na mienendo yao wenyewe hawataki chakula cha Bwana wao,(ambalo ni neno la Kristo lisiloghoshiwa), wala hawataki "mavazi" ya Bwana wao(Ambao ni utakatifu na matendo mema soma ufunuo 19:8,) bali waitwe tu kwa Jina la Bwana Yesu aibu yao iwaondoke hii aibu ina maana waiepuke hukumu itakayokuja na ndio maana yale makanisa yote hayakuweza kuoana na Kristo kikamilifu yalikuwa na mapungufu yake, na sisi pia tupo katika kanisa la mwisho la saba la LAODIKIA ni kanisa vuguvugu,na ndilo lililomkinai Bwana wake kuliko mengine yote yaliyotangulia soma..

ufunuo 3:14-22,"14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa."


lakini tunapaswa wote tushinde ili tuvuke kutoka kuwa masuria na kuwa bibi-arusi safi wa Yesu Kristo waliokubaliwa tayari kwenda kwenye arusi ya mwanakondoo itakayofanyika mbinguni kwa Baba.Kumbuka bibi-arusi sio sawa na suria.Kwahiyo ndugu watakaoshiri karamu ya mwanakondoo ni bibi-arusi tu, je! wewe ni bibiarusi? umepokea Roho Mtakatifu? umejiweka tayari kumpokea Bwana wako atakaporudi? matendo yako yanastahili wokovu? jibu lipo moyoni mwako. Tubu sasa umgeukie Bwana kumbuka tunaishi kizazi ambacho kitashuhudia kuja kwa pili kwa Kristo.

ufunuo 19: 7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing'arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

SWALI 3: je ni lini Yesu atajitambulisha kwa ndugu zake, ni wakati wa dhiki kuu au baada ya ile dhiki kuu kuisha?

JIBU: Yesu Kristo atajitambulisha kwa ndugu zake, kwa kupitia injili ya wale manabii wawili(ufunuo 11)...hao manabii watawahubiria kuwa Yesu kristo waliyemsulubisha miaka 2000 iliyopita ndiye masihi wao. watawaamini kutokana na ishara kuu na miujiza watakayoitenda hao mashahidi wawili, kama manabii wao wa kale mfano wa Musa na Eliya. kwahiyo wale wayahudi 144,000 wataamini na kutubu kwa kumuombolezea waliyemchoma mkuki pale kalvari..zakaria 12:10"  Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. ". Kwahiyo wakati wa hao manabii wawili ambao watahubiri siku 1260 ambayo ndiyo ile miaka mitatu na nusu ya kwanza ya lile juma la 70 la danieli, kipindi hicho ndicho wayahudi watamwamini YESU KRISTO, wakati kanisa la mataifa(bibi arusi wa Kristo) litakuwa limeshakwenda kwenye unyakuo.

SWALI 4: mwanzo 4:15 "Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. " je! hiyo alama ni ipi Bwana aliyomtia Kaini mpaka mtu akimwona asimuue?.

JIBU: Baada ya Hawa kuzini na yule nyoka kwenye bustani ya edeni(kumbuka nyoka hakuwa reptilia/ au kiumbe fulani kinachotambaa kwa tumbo kama huyu nyoka tunayemwona sasa hivi, bali alikuwa anakaribia kufanana na mtu, akitoka nyani, alikuwa anafuata nyoka kisha mwanadamu, alikuwa anatembea kama mtu, anazungumza, anafikiri n.k lakini baada ya kuasi Mungu akamlaani ndipo akawa nyoka kama tunavyomwona leo, anatembea kwa tumbo, kwa ufupi ni mnyama aliyelaaniwa kuliko wanyama wote kama biblia inavyomwelezea.). Hivyo basi kitendo kilichofanyika pale bustani ya Edeni ni uasherati, Hawa alizini na nyoka, kisha Hawa akaenda kuzini tena na mumewe(Adam) ikapelekea Hawa kubeba mimba ya mapacha wasiofanana, kila mmoja akiwa amebeba asili ya baba yake(jambo hili limehakikiwa na wanasayansi kwamba inaweza ikatokea mama mmoja kubeba mimba ya mapacha wenye baba wawili tofauti,) tazama picha hapa chini, ni matukio ya kawaida na yanatokea kila siku duniani;
        
              (mapacha wenye baba wawili tofauti, kila mmoja na baba yake lakini mama mmoja)
Kwahiyo Kaini baba yake alikuwa ni nyoka, na Habili baba yake alikuwa ni Adamu. Hivyo baada ya kuzaliwa Habili kama mzao wa Mungu alimtolea Mungu dhabihu bora kuliko mwenzake, na ndipo Kaini akamwonea wivu akamuua ndugu yake. Mungu akamlaani Kaini kwa kosa la kumuua ndugu yake. Kaini baada ya kuona adhabu aliyopewa na Mungu ni kubwa  kama tunavyosoma mwanzo 4:8-15 "8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.
9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. "

    Kwahiyo hii alama Bwana aliyomtia Kaini sio alama kama chapa fulani kwenye mwili(tatoo) wake, Bali tukichunguza maandiko tunaona kuwa Mungu alimwongezea ukubwa wa mwili wake na akili nyingi(inteligency), tunaona katika kipindi cha Nuhu ule uzao wa Kaini ulikuwa ni wa watu wakubwa walioitwa "majitu (wanefili)" kwahiyo kwa ukubwa huu mtu yeyote asingeweza kupigana nao au kuwatishia, na kwenye upande wa akili tunaona katika mwanzo 4 wana wa kaini walianza kuwa na ustaarabu kwa haraka kama ugunduzi wa vyuma, shaba, ustadi wa vyombo vya miziki n.k.waliitwa watu hodari na wenye sifa wakati ule(mwanzo 6:4) inaelezea..wao ndio waliotengeneza mapiramidi ambayo yamesimama mpaka sasa  kwahiyo tunajua hata leo taifa lenye ujuzi mwingi kama teknolojia kubwa ni dhahiri kuwa taifa hilo litaogopeka na hakuna mtu atayakayedhubutu kwenda kulidhuru ndivyo ilivyokuwa kwa Kaini, Mungu alimpa ukubwa na ujuzi mwingi ambao ulikuwa kama ulinzi kwake. Lakini ule uzao mwingine wa Adamu ambao ni uzao wa Mungu wao walikuwa ni wafugaji tu na wakulima, na walikuwa ni wanadamu wenye miili ya kawaida.

MASWALI YALIYOULIZWA NA MAJIBU YAKE: SEHEMU YA 7


SWALI 1; Je, kwa mwanamwali mpumbavu yeye katika Yerusalemu mpya ya milele itakayokuwa hapa duniani atakuwa na maisha ya kawaida ya kufanya kazi kama maisha tuliyonayo duniani ya kulima na kufuga?

JIBU:Mimi nadhani hili kundi linalojumuisha (wanawali wapumbavu, na wayahudi, pamoja na bibi arusi wa kristo) hawa watakuwa na miili ya utukufu hivyo basi kulima au kupanda itakuwa siyo sehemu yao, pengine watakuwa na shughuli nyingine tofauti na hizo. watakaokuwa wanapanda na kufuga watakuwa wale watu wenye miili ya asili watakapenya kuingia katika utawala wa miaka 1000. kwasababu watakuwa ni watu wa asili tu, wanaohitaji kula, kunywa n.k. lakini hao wengine watakuwa na miili kama ya malaika. Hivyo vitu havitakuwa vya muhimu kwao.

SWALI 2; Je, kule mbinguni kwenye maisha ya milele wanyama watakuwepo?
JIBU:Tukienda mbinguni sifahamu vizuri kama wanyama watakuwepo au la. lakini katika umilele tutakaotawala na Kristo hapa duniani biblia inasema wanyama watakuwepo, isaya 11:6" Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.
7 Ng'ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng'ombe.
8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.
9 Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari. " kwahiyo wanyama watakuwepo na biblia inasema pia warumi 8:29-22"19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.
20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;
21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.
22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa. " kwahiyo wanyama nao wataokolewa

 
SWALI 3; wale 144000 hata kule mbinguni watakuwa pia ni watumishi wa bibi arusi au ni katika utawala wa miaka 1000 tu?
JIBU:Hawa 144000 hawataenda mbinguni..kule mbinguni watakuwepo bibi arusi tu wa Kristo(watakaonyakuliwa). hawa wayahudi 144,000 hawatakufa wala kunyakuliwa, watakuja kuungana na bibi arusi baadaye katika utawala wa miaka 1000, biblia inawaita bikira ufunuo 14:4" Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa. " kwahiyo hawatakuwa watumwa wa bibi arusi, hawa nao ni bikira wa Mungu safi watakaokuja kutawala pamoja na watakatifu wengine katika utawala wa miaka 1000.

SWALI 4; Yule joka kubwa jekundu, na yule mnyama, na yule nabii wa uongo ni kitu kimoja au wanatofautiana?
JIBU: Hizi ni roho 3 za uovu lakini zinafanya kazi moja..kwa ufupi lile joka kubwa jekundu linalozungumziwa kwenye ufunuo 12 & 13 ni shetani mwenyewe (ibilisi/lucifer)..ukiendelea kusoma kwenye ufunuo 13:1"
1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.


tunaona hap lile joka  lilimpa nguvu zake yule mnyama aliyetoka kwenye bahari mwenye vichwa saba na pembe 10, sasa huyu mnyama mwenye vichwa saba na pembe 10 ni roho ya shetani iliyovaa mataifa kupambana na uzao wa Mungu, na utawala wa Mungu tangu zamani Mungu alipoanza kuweka agano na Ibrahimu. sasa vile vichwa saba vya yule mnyama ni falme 7. nazo ni MISRI, ASHURU, BABELI, UMEDI &UAJEMI, UGIRIKI, RUMI-ya kipagani, RUMI-YA KIDINI...ukifuatilia mataifa haya shetani aliyatumia kupambana na kuuteketeza uzao wa Mungu(wayahudi),

kumbuka taifa la kwanza ambalo lilianza kupambana na uzao wa Mungu lilikuwa ni MISRI, Tunaona jinsi shetani alivyomtumia Farao kuwatesa watu wa Mungu (wayahudi),hata walipokuwa wanatoka utumwani bado Farao alitafuta kwenda kuwaangamiza kabisa lakini jambo hilo halikufanikiwa kwasababu Mungu anawapigania watu wake.

Na baada ya miaka mingi baadaye lilinyanyuka taifa lingine lililotawala dunia kama Misri nalo ni Ashuru hilo liliwachukua wana wa Israeli tena (ukisoma 2wafalme 17 inaelezea ) yale makabila 10 yalichukuliwa kwenda ASHURU utumwani na hayakurudi tena mpaka ilipofika mwaka 1948.

Na baada ya Ashuru lilinyanyuka taifa lingine tena lililotawala dunia nalo ni BABELI chini ya mfalme nebkadneza(2 wafalme 24), Hili lilichukua lile kabila la Yuda na benyamini lililobaki na kulipeleka utumwani, lakini baada ya miaka 70 kupita Mungu alilirejesha tena kwenye nchi yake ya ahadi.

Na baada ya Babeli kudondoka lilinyanyuka taifa lingine lililotawa dunia nalo ni UAJEMI & UMEDI,(Daniel 5:30-31).Wayahudi waliendelea bado kutiishwa chini ya huu utawala.

kisha likaja taifa UYUNANI(UGIRIKI),lilitawala kuanzia mwaka BC331-BC168.Wayahudi bado waliendelea kutiishwa chini ya utawala huu wa kipagani wa kigiriki.

Na baada ya hapo ndipo ikanyanyuka ngome ya RUMI (ya kipagani ilitawala dunia kuanzia mwaka BC 168-AD 476),hilo ndilo lililotawala kwa mabavu na nguvu, utawala wake biblia unaufananisha na utawala wa chuma.Adhabu kali zilikuwa zikitolewa kwa mtu yeyote atakayekwenda kinyume na utawala, na ndipo adhabu za kutundikwa kwa wahalifu msalabani zilipozaliwa.Wayahudi waliteseka sana chini ya utawala huu wakimtazamia MASIHI wao wanaomtarajia aje kuwakomboa na utawala wa kimabavu wa Rumi.

Baada ya huo ulinyanyuka utawala mwingine ambao ni uleule wa kirumi isipokuwa huu ni wa kidini zaidi (RUMI ya kidini).huu ulianza kutawala kuanzia mwaka (AD 476- hadi wakati wa sasa).Hichi ndicho kile kichwa cha saba cha yule mnyama chenye pembe 10,ndipo kiti cha enzi cha shetani kilipo sasa, Na ndio chimbuko la kanisa katholiki,na upapa.tunafahamu katika historia ni utawala uliongoza kwa kuuwa watakatifu wengi wa Mungu takribani wakristo milioni 68 waliuliwa kikatili, Na huu utawala ndio unaoendelea kutawala ulimwengu mpaka sasa na upo katika roho na pia katika mwili na unaendelea kuuwa watu kiroho unapeleka mamilioni ya watu kuzimu,ni utawala wa shetani unaowafanya watu wamwabudu yeye pasipo kujua wakidhani kuwa wanamwabudu Mungu.

Mafundisho ya kanisa katholiki ndiyo yaliyouharibu ukristo na biblia inaliita BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI (Ufunuo 17), kama kanisa katholiki ndiyo mama wa makahaba inamaanisha anao mabinti ambao ni makahaba na hao mabinti si mengine zaidi ya madhehebu yote yaliyosalia yanayoiga desturi za mama yao kahaba kanisa katholiki mfano wa hayo ni lutherani,anglikana,SDA,orthodox n.k.lakini biblia inasema ufunuo 18:4-5"..Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.
.Hivyo basi biblia inasema 
Unaona ni jinsi gani shetani alivyoweza kutumia hizi falme za dunia ambao ndio vile vichwa saba vya yule joka na yule mnyama kuharibu uzao wa Mungu?,

Kwahiyo ndugu kama upo huko toka haraka madhehebu hayakufikishi mbinguni,sio kutoka kwa miguu bali katika roho, uwe bikira safi iepuke alama ya mnyama.



  
Kwahiyo falme tano za kwanza zilitumika kwa kuwaangamiza wayahudi pekee, lakini mbili za mwisho zinawatesa wayahudi pamoja na wakristo  na hata sasa bado yanawatesa. na yatawatesa zaidi wakati wa kipindi cha dhiki kuu. na zile pembe kumi juu ya kichwa cha yule mnyama ni mataifa 10 ya ulaya yaliyogawanyika (divided kingdoms ) ambayo hiyo roho inayaendesha, ikiongozwa na Roma.

Na yule mnyama wa 3 ALIYE MFANO WA MWANAKONDOO naye ananena kama joka (ufunuo13:11) ni roho ile ile ya shetani iliyotoka kwa yule joka, ikaenda kwa yule mnyama mwenye vichwa saba na pembe kumi sasa imehamia kwa huyu mnyama aliyemfano wa mwanakondoo, biblia inamwita nabii wa uongo. na roho hii inaliendesha taifa la Marekani kwa sasa, na kazi yao ni moja tu. kupambana na kuuangamiza kabisa uzao wa Mungu kwa kutumia mifumo iliyojiwekea kwa kuunganisha  umoja wa dini zote na madhehebu yote  duniani kuunda ile alama ya mnyama.


kwa ufupi hawa 3, joka(ambaye ndiye shetani), yule mnyama na nabii wa uwongo. ni roho za mashetani..zinazotenda kazi kwa pamoja duniani.

 SWALI 5; Kwanini Mungu anawashugulikia Izraeli kama taifa na Mataifa mtu mmoja mmoja?
JIBU:Mungu siku zote, hashughuliki na taifa, bali anashughulika na mtu mmoja, mmoja, Mungu aliweka agano na Ibrahimu na uzao wake baada yake. sio pamoja na ukoo wa ibrahimu au na familia yake hakuweka na watu wanaoitwa wayahudi bali ibrahimu, basi wote waliofuata nyumba yake katika viuno vyake, watakaoenda katika imani ile ile ya ibrahimu hao ndio taifa la israeli.vivyo hivyo katika ukristo tunapozaliwa mara ya pili tunaingia katika taifa la YESU KRISTO (uzao wa kifalme) nasi tunakuwa wana wa uzao. kwahiyo tofautisha kati ya uzao wetu na uzao wa wayahudi, uzao wa wayahudi ni wa asili, lakini uzao wetu sisi ni wa rohoni, na taifa letu ni la rohoni. nasi ndio maana tunahesabika kuwa ni uzao wa Ibrahimu izrael wa kiroho.
kwahiyo Mungu anashughulika na Israel katika mwili kama watu wake kwa agano alilowekeana na Ibrahimu lakini sisi mataifa hakuna agano lolote Mungu aliloweka na mababa zetu katika mwili.

SWALI 6; Hosea 6:1-2 "Njooni rumeudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; nae amepiga na yeye atatufunga jeraha zetu. Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. Neno hili lina maana gani siku kufufuliwa baada ya siku mbili na siku ya tatu kuinuliwa na kuishi mbele zake?
JIBU:neno hili, picha ya kwanza tunayoiona hapo ni ya Bwana Yesu Kristo, kufa na kukaa kaburini na siku ya tatu kufufuka, na picha nyingine tunayoiona tunafahamu siku moja kwa Mungu ni sawa na miaka 1000 kwa wanadamu, hivyo basi ni miaka 2000 imepita tangu ujio wa Kristo mara ya kwanza, na sasa tupo au tunaukaribia mwaka wa 3000 ambayo ndiyo siku ya tatu,..ndiyo siku yetu sisi ya kuinuliwa mbele zake.

SWALI 7; Je wale ambao watakutwa wakiwa hai wakati wa unyakuo wakanyakuliwa wao watakuja wafe lini au hawatakufa maisha yao yote?
JIBU: Mtu akishanyakuliwa na kwenda mbinguni hawezi kufa tena kwasababu atakuwa na mwili wa utukufu kama wa malaika.wataishi milele.

SWALI 8; Ni kosa gani walilolifanya wana wa Izraeli lililofanya Mungu kuwapeleka utumwani Misri miaka 400?
JIBU: mimi ninadhani kosa  mojawapo walilofanya mpaka  Mungu kuwapeleka misri ni lile la kumuuza ndugu yao yusufu kule misri lakini pia sio sababu kuu iliyowafanya wakae utumwani miaka 400, kulikuwa na kusudi lingine la Mungu ndani yake kwamfano kwa kuenda kule Misri taifa la Izraeli pamoja na mataifa yote ulimwenguni kwa wakati ule na wakati tuliopo sasa tunaweza kujua na kufahamu uweza wa Mungu jinsi ulivyo na mkono wake unavyoweza kuokoa na kuangamiza, hebu fikiria bahari inagawanyika, maji yanakuwa damu, nchi inapigwa giza siku tatu, nzige, vyura, chawa taifa zima kulishwa mana na nyama kwa muda wa miaka 40 n.k. hakika tusingemjua Mungu pasipo maajabu hayo mi naona hii ndiyo sababu kuu ya wao kupelekwa Misri ...maana habari yao ya kukaa utumwani miaka 400 ilikuwa imeshatabiriwa hata hapo kabla.