"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Sunday, December 25, 2016

MASWALI YALIYOULIZWA NA MAJIBU YAKE: SEHEMU YA 6

Katika Dan 9: 25 "Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.
27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.

SWALI 1; Watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji; je hii tayari imeisha tendeka au bado?.

JIBU:hii tayari imeshatendeka..ilitokea AD 70 pale jeshi la Rumi lilipouzunguka mji..na kuuteketeza Yerusalemu historia inaonyesha hivyo maandiko yalitimia huo wakati kama Yesu alivyowaonya wanafunzi wake. luka 21:20-24"20 Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia.
21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.
22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.
23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia. "

SWALI 2; Naye atafanya agano na watu wengi kwa mda wa juma moja. Huyu ni nani  anaye zungumziwa hapa anayefanya agano na watu wengi kwa mda wa juma moja?
JIBU: anayezungumziwa hapo ni mpinga kristo ambaye atakuja kufanya agano na mataifa mengi katika juma moja la mwisho lililobakia ambalo ni miaka 7..sasa huyu mpinga kristo aliyezungumziwa hapa ndiye mkuu wa watu watakaouangamiza mji..sasa kumbuka wakati wa AD 70, watu wake ndio waliouteketeza mji(ambao ni warumi), yeye alikuwa bado hajaja ..ndio maana maandiko yanasema ''watu wa mkuu atakayekuja'' watauteketeza mji kwahiyo hapo yeye alikuwa bado hajaja, huyo ndiye (baadaye)atakayefanya agano na  watu wengi kwa muda wa lile juma moja la mwisho ambalo litaanza baada ya kanisa kunyakuliwa.

SWALI 3; Na mahali pake litasimama chukuzo la uharibifu. Chukizo hilo la uharibifu ni kitu gani?.

JIBU:chukizo la uharibifu linatokea  pale mpinga kristo atakapohamia Yerusalemu(mji mtakatifu) na kukaa katika hekalu la Mungu na kutaka kuabudiwa kama Mungu,(ambayo ni machukizo makubwa mbele za Mungu ) 2 wathesalonike 2:3 " Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. (haya ndiyo yatakayoleta ghadhabu ya Mungu ya kuharibu)" lakini pia yapo machukizo mengine kama msikiti wa omar al aqsa uliojengwa pale yerusalemu (mahali patakatifu) na pia uovu unaonendelea kufanyika Yerusalem sehemu takatifu haya yote ni sehemu ya machukizo ya uharibifu. Lakini chukizo kuu ni hilo la mpingakristo(papa). atakapokwenda kuketi mahali patakatifu na kutaka kuabudiwa yeye kama Mungu, na jambo hili lipo mbioni kutimia.
SWALI 4; kulingana na majuma 70 ya Daniel; Izraeli wamebakiza muda gani?
JIBU: Israeli watakuwa wamebakiza juma moja na ndio ile miaka 7 ya mwisho ambayo mpinga kristo atafanya agano na mataifa mengi kulingana na danieli 9:27 ambapo miaka 3.5 ya kwanza israeli watahubiriwa injili na wale manabii wawili, na miaka 3.5 ya mwisho itakuwa ni ile dhiki kuu.

SWALI 5; Je baada ya unyakuo mataifa wanaanza dhiki kuu na Izraeli wanahubiriwa injili au dhiki kuu itakuwa kwa wote mataifa na Izraeli?

JIBU: dhiki kuu ilipaswa iwe ni kwa wayahudi peke yao tukisoma  yeremia 30:7"Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo. " kwahiyo tunaona hii ni tabu ya Yakobo(izraeli) lakini wapo watakapitia dhiki kuu ambao ni wale wanawali wapumbavu waliopaswa kwenda kwenye unyakuo wakashindwa watajumuishwa pamoja na wayahudi maana yule mnyama ambaye atafanya vita na wayahudi atafanya vita nao pia.Habari hii tunaweza tukaiona kwenye ufunuo sura ya 12, ule mstari wa 7 unasema "
joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari. "kwahiyo tunaona hao waliosalia wazishikao amri za Mungu ni wayahudi na hao wenye ushuhuda wa Yesu ni wale wanawali wapumbavu ambao hawakwenda kwenye unyakuo. kwahiyo dhiki kuu itakuwa kwa wote wayahudi na wakristo watakaobakia wasioenda katika unyakuo.

 SWALI 6;
Baada ya Izraeli kuhubiriwa injili baada ya unyakuo, wale waizraeli   144,000 watakao mkubali Yesu na kujazwa roho mtakatifu wao watakuwa na unyakuo wao pia?

JIBU: hapana wale 144,000 habari yao inaelezwa katika ufunuo sura ya 12. kama tunavyosoma "1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.
5 Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
13 Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari."
sasa huyu mwanamke aliyevikwa jua na mwezi na mwenye taji ya nyota 12 ni taifa la israeli kulingana na ile ndoto aliyoiota yusufu mwanzo 37:9....kwahiyo huyu mwanamke ni israel-144000 ambaye atapewa mabawa mawili kama ya tai.na yule mtoto ni Yesu Kristo haya mabawa mawili aliyopewa huyu mwanamke  ni injili watakayohubiriwa  na wale manabii wawili itakayowawezesha kujiepusha na mpinga kristo kwasababu watamjua. Na biblia inasema huyu mwanamke atakimbilia nyikani ambapo atalishwa huko siku 1260 yaani miaka 3.5 mbali na yule joka, hichi kitakuwa ni kipindi cha dhiki kuu kwahiyo wale wayahudi waliosalia ambao hawakupokea injili ya manabii wawili hao ndio watakaopitia dhiki kuu na kuuliwa na mpinga kristo lakini wale 144000 Mungu atawahifadhi hapa hapa duniani hawataenda mbinguni na wataingia katika utawala wa miaka 1000. ijulikane kuwa sio wayahudi wote watakaoipokea injili ya wale mashahidi wawili isipokuwa ni wale 144,000 tu, na ndio hao watakaoiepuka dhiki kuu. lakini wayahudi waliosalia hao ndio watakaopitia dhiki kuu pamoja na wanawali wapumbavu.

SWALI 8; Baada ya unyakuo kutokea, itapita muda gani Yesu na Bibi arusi wake kurudi kwa ajili ya siku ya BWANA?

JIBU: Baada ya unyakuo kupita itabaki miaka 7 kwa wayahudi ndio lile juma la mwisho la Daniel. baada ya hilo juma kuisha ndipo itakapokuja siku ya Bwana atakayoshuka  pamoja na watakatifu wake.ufunuo 19:11-14”11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.” 

SWALI 9;
Katika siku ya BWANA, yale mapigo yatakayo achiliwa na BWANA mwenyewe kwa mkono wa Malaika wa mapigo yataua watu wote au wapo watakao salia na kuingia katika utawala wa miaka 1000?.

JIBU: siku ya Bwana haitamaliza watu wote, biblia inarekodi kuwa wapo watu wachache sana,  watakaosalia, wanadamu wataadimika kuliko dhababu tena ni kwa kusudi tu la kuijaza nchi ndio maana watabakizwa wanadamu wachache sana..isaya 13:3-9”9 Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.
13 Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali. “ Kama biblia inavyosema siku ya Bwana sio ya kuitamani ni giza wala sio nuru ndugu usitamani kuwepo katika hiyo siku tafuta Roho Mtakatifu maana siku hiyo i karibu ufunuo 6:16”12 Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama? “

SWALI 10; Je, wale watu waovu  atakao washawishi shetani kuishambulia kambi ya watakatifu wakati wa vita vya Gogu na Magogu,ufu 20:8,  itakapotokea,  watakuwa hai hapa duniani au watafufuliwa ndipo awashawishi?

JIBU: ni wazi kuwa watakuwa hai hapa duniani watakapoivamia kambi ya watakatifu...biblia inasema ufufuo wa wafu kwaajili ya hukumu utakuja baada ya miaka 1000 kuisha ufunuo 20:5" Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. "  kwahiyo kutakuwa hakuna ufufuo wowote hapa katikati wale watakaokuwa wanaishi ndio watakaoizunguka kambi ya watakatifu.

 SWALI 11a;
Yale mapigo ya Mungu vitasa yatadumu kwa muda gani?

JIBU: yale mapigo ya Mungu (vitasa saba),  vita vya harmagedoni, pamoja na hukumu ya mataifa..yatatokea ndani ya siku 75 zilizoongezwa baada ya lile juma la 70 kuisha kama inavyoonekana katika danieli 12:11-12.

SWALI 11.b; siku za dhiki kuu ni miaka 3.5 sawa na siku 1260. kwanini katika Dan 12:11-12 zinaongezeka kuja 1290 na zinanaongezeka zaidi kuja siku 1335?.

JIBU: Daniel 12:11-12" Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini. Heri angojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano. "
kwahiyo katika siku 30 za kwanza zilizoongezeka baada ya dhiki kuu kuisha yaani 1290-1260=30 itakuwa ni ile siku ya Bwana ambayo vitasa vitaanza kumiminwa katika dunia. na siku 45 zilizosalia yaani 1335-1290=45 itajumuisha huko huko vita vya harmagedoni, matengenezo kwa ajili ya milenium na kufufuliwa kwa wafu. kwahiyo jumla ya siku zilizoongezeka baada ya dhiki kuu kuisha mpaka mwanzo wa utawala wa miaka 1000 zitakuwa ni siku 75...biblia inamwita heri mtu yule atakayeweza kuzifikia hizo siku 1335 kwasababu wanadamu wakati huo watabaki wachache sana isaya 13:12 wataadimika kuliko dhahabu..unaweza ukapata picha ni maangamizi makubwa kiasi gani yatatokea duniani katika ile siku ya hasira ya Bwana.
SWALI; Ubarikiwe mtumishi naomba kuuliza kati ya Unyakuo wa kanisa, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?

JIBU: Kwa ufupi kulingana na kalenda ya Mungu, kwasasa tunasubiria unyakuo wa Bibi-arusi ambao huo upo karibuni sana kutokea. Wakati wowote katika kizazi chetu hichi tunachoishi jambo hilo tunaweza tukalishuhudia mbele ya macho yetu, Hivyo huo ndio utakoanza kwanza... Sasa baada ya unyakuo kupita ambao ni watu wachache sana watakaokwenda mbinguni . Kwasababu Bwana mwenyewe alishatuonya akasema "kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na Luthu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake mwana wa Adamu, wakati ule watu wachache sana waliokoka (yaani nane kwa watatu kati ya mamilioni ya watu waliokuwepo duniani) ndivyo itakavyokuwa katika siku za unyakuo..Na sehemu nyingine alisema

Mathayo 22:14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.

Hivyo...

Luka 13:24 "Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze".

Unaona hapo hivyo hili kundi litakalonyakuliwa ambalo lilishakwisha jiweka tayari tangu zamani kwenda na Bwana litakuwa dogo sana tofauti na wengi wanavyodhani kwamba watu watotoweka mabarabarani,na dunia nzima kutaharuki kwa tukio hilo n.k. Hilo jambo halipo. Kundi hili litakapoondoka hakuna mtu asiyemjua Mungu atakayejua, dunia nzima itaendelea na shughuli zake kama kawaida...watakuja kufahamu baadaye mambo yakishabadilika.

Hivyo ukishapita unyakuo, sasa ndio Dhiki kuu itaanza, hii itakuwa ndani ya kile kipindi cha miaka 7 ya mwisho, wakati huo mpinga-kristo atanyanyuka ili kuhimiza ile chapa ya mnyama ianze kutenda kazi haraka, kutakuwa na dhiki isiyokuwako kwa wale wote(wanawali wapumbavu) watakaokosa unyakuo. Ndugu Wakati huo sio wa kutamani kuwepo, kwasababu mfano wa mateso yatakayokuwepo hupo Bwana anasema hayakuwahi kutokea katika kipindi chochote katika historia na wala hayatakaa yatokee mengine mfano wa hayo baada ya hapo.

Na pia kumbuka dhiki hiyo vile vile haitamuhusu kila mtu duniani, hapana bali nalo litakuwa ni kundi dogo tu, tena wale watakaogundua kuwa ule ni mfumo wa shetani, wakati huo dunia nzima itaifurahia mfumo wa mpinga-kristo. kwasababu wakati huo mpinga-kristo atakuwa mwerevu ili awapate wengi hivyo Utaonekana kama ni ustaharabu mzuri sana wa amani aliouleta, na utapendwa na wengi. Na wale wote watakaojaribu kuufichua uovu wake wao ndio wataonekana kama wenyewe ndio wapinga-kristo badala yake. Sasa baada ya hawa watu (bikiria wapumbavu) kuuliwa. Kitakachofuata kitakuwa ni ile siku kuu ya Bwana ya kutisha. Ambayo Bwana aliiweka mahususi kwa ajili ya watu wote waovu.

Amosi 5: 18 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru.
19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.

Sasa Hapo ndipo Bwana atajilipizia mwenyewe kisasi juu ya mataifa yote yaliyosalia ulimwenguni yaliyopokea ile chapa ya mnyama, na watu wote yasiyomcha Mungu, hii itaambatana na yale mapigo ya vitasa 7 (Ufunuo 16).

Na ndio humo humo katikati vile vita vya Har-magedoni vitapangwa, pale mataifa yote duniani yatakusanyika ili kufanya vita na mwanakondoo, Hii haitakuwa kabisa vita kwasababu Mungu hapigani na wanadamu,.Bwana anasema ule upanga(Neno lake) utokao katika kinywa chake ndio utakaowaua.(Ufunuo 19:11-21) Hao waliokusanyika. Hivyo Bwana atawaua wote, na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani.

Hapa ndipo mataifa yote ulimwenguni yataomboleza wakitamani milima iwaangukie wajisitiri na ghadhabu ya Mungu mwenyezi, (Ufunuo 6:12).

Hivyo Mungu akishayahukumu mataifa kitakachofuata ni utawala wa amani wa Bwana wetu Yesu Kristo wa miaka1000. Huko dunia itarejezwa tena katika hali yake nzuri ya mwanzo kama Edeni au zaidi ya hapo, dhambi haitatawala tena (kwasababu shetani atakuwa amefungwa wakati huo), japoo waovu biblia inarekodi watakuwepo na ndio hao baada ya ule utawala kuisha, shetani atakapofunguliwa tena kwa kipindi kifupi akawadanganye ili walete madhara, Biblia inasema moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza..Hiyo ndio hiyo vita ya Gogu na Magogu inayozungumziwa kwenye(Ufunuo 20:8), Hivyo hiyo nayo hakutakuwa vita kabisa kwasababu pindi watakapotaka kujaribu kufanya hivyo moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza wote.

Kisha baada ya hapo YESU KRISTO Bwana wetu atakaa katika kiti chake cha enzi CHEUPE, na wafu wote watafufuliwa wale ambao hawakuwepo katika ufufuo wa kwanza pamoja na hao waliokuwa wanataka kufanya vita na watakatifu wa Mungu ndani ya ule utawala wa miaka 1000. Wote kwa pamoja watahukumiwa kulingana na matendo yao.

Kisha baada ya hapo watatupwa katika lile ziwa la moto alipo shetani na malaika zake. Na ndipo mbingu mpya na nchi mpya zitakapokuja...Kuanzia huo wakati na kuendelea muda utaondolewa, na umilele utaanza, mambo ya kwanza yatakuwa yamekwisha pita tazama yamekuwa mpya...Haleluya..Huko tutazidi kumjua Mungu kwa namna isiyo ya kawaida.Tuombe tusikose kuwepo huko,.Biblia inasema mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, wala kuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu amewaandalia wale wampendao (1Wakorintho 2:9).

Mungu wetu ni mwema. Libarikiwe jina lake. Milele na milele. Amina.

No comments:

Post a Comment