"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Saturday, December 17, 2016

MASWALI YALIYOULIZWA NA MAJIBU YAKE:SEHEMU YA 5

SWALI 1: Tangu mwanadamu aumbwe kwa maana ya Adamu mpaka sasa zimepita miaka mingapi?
JIBU: Kulingana na historia na utafiti wa kibiblia inasemekana kuwa tangu Adamu kuumbwa hadi sasa ni takribani miaka 6000..kuanzia wakati wa Adam mpaka Nuhu ni miaka 2000, tangu wakati wa Nuhu mpaka wakati wa Bwana Yesu akiwepo hapa duniani ni miaka 2000, na kuanzia ule wakati wa Bwana Yesu mpaka sasa ni miaka 2000...kwahiyo jumla ni miaka 6000..sio miaka 6000 kamili inawezekana ikawa imepungua kidogo au imeongezeka kidogo hayo ni makadirio.

SWALI 2: Je, kwanini Yesu hakukaa siku 3 kamili kaburini?
JIBU: Mimi nadhani Yesu kukaa kaburini siku 3 Ni ili maandiko yatimie..lakini suala la kukamilisha Masaa 72 sidhani kama lilikuwa ni la umuhimu sana..lakini ukiangalia pale utaona alika kaburini kama Masaa 40 hivi, na tunafahamu 40 Ni namba  ya Mungu ya hukumu na kujaribiwa. Kwamfano tunaona gharika ilinyesha juu ya nchi siku 40, Watu wa Ninawi walipewa siku 40 za kutubu kabla ya maangamizi,Musa alifunga siku 40 akapewa amri kumi kule mlimani, hivyo hivyo na Yesu alifunga siku 40, Mungu aliwahukumu wana Wa Israel miaka 40 jangwani, n.k nadhani hii Ni Moja ya sababu na pia kumbuka kristo alitabiriwa kuwa mwili wake hautaonja uharibifu kwahyo kama angetimiza  masaa 72 kamili pengine mwili wake ungeshaanza kuona uharibifu na maandiko yasingetimia kama yalivyotabiriwa zaburi 16:10 " Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu. "

SWALI 3: Mathayo 13:33 Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia. Pishi tatu hizi ni nini ambazo zimechacha zote? Na mwanamke ni kitu gani katika mfano huu? Maana Yesu aliongea kwa mifano pasipo mifano hakunena.
JIBU:  Mfano huu unaweza ukatafsiriwa kwa namna tofauti tofauti kwajinsi Roho wa Mungu atakavyomfunulia mtu..lakini ufunuo dhahiri wa mstari huu kulingana na wakati tuliopo sasa mfano huu unaelezea wazi hali ya kanisa katika hichi kipindi cha mwisho tunajua kabisa mwanamke siku zote katika biblia anawakilisha kanisa na chachu inawakalisha mafundisho fulani (mathayo 16:6-12 Kristo alisema jihadharini na chachu ya mafarisayo ambayo ni mafundisho yao. ), na tunajua pia chachu ni amira na amira ina uhai ni wadudu wale wanafanya kazi ya kubadili maumbile ya vitu (kuumua) vionekane kama halisi lakini sio halisi na zile pishi tatu za unga ni hatua tatu za ukamilifu Wa mwanadamu kwa Mungu nazo Ni
1.) Kuhesabiwa haki kwa imani...
2) utakaso kwa damu ya Yesu...
3) ubatizo Wa Roho mtakatifu.
kwahiyo huyo mwanamke ufunuo wake ni kanisa katoliki ndilo lililoingiza mafundisho ya kipagani kama ibada za sanamu,ubatizo wa kunyunyizwa,kutoruhusu karama za Roho kanisani kutenda kazi,n.k. (inafahamika katika historia ya kanisa) ikapelekea kanisa liingie katika kipindi kirefu cha giza zaidi ya miaka 1000 na hiyo ndio ile chachu iliyoharibu hizo hatua tatu za ukamilifu Wa mwanadamu kwa Mungu tangu kanisa la kwanza na kwa sehemu kubwa lilifanikiwa...lakini pamoja na hayo Mungu alianza kulitengeneza tena kanisa upya na kuzirejesha tena hizo hatua tatu za neema hii ilianza kuonekeana katika kipindi cha matengenezo ya kanisa (kuanzia karne ya 16 kuja juu)mpaka sasa, Bwana alianza kuwanyanyua watumishi wake kutengeneza upya kulifanya kanisa kurudi katika hali yake ya mwanzo ambapo tunaona Mungu alimnyanyua kwanza Martin Luther alikuja na ujumbe sahihi, warumi 5:1'' Wa kuhesabiwa haki kwa imani,ipatikanayo kwa njia ya Bwana Yesu Kristo" dhidi ya mafundisho potofu yaliyokuwepo hapo mwanzo ya kanisa katoliki ambayo ilidhaniwa kuwa mtu anahesabiwa haki mbele za Mungu kwa kuwa mshirika wa kanisa katoliki tu.
na baada ya Martin luther Bwana akamnyanyua John Wesley na ujumbe Wa utakaso katika damu ya Yesu inayoleta utakatifu (holiness) waebrania 12:14"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;".
na kwa wakati wetu huu wa mwisho Mungu alimwaga tena kipawa cha Roho Mtakatifu mwaka 1906(kwa mara nyingine huko Azusa street, Calfornia Marekani) tangu pentekoste ya kwanza ya mitume ilipotokea.Vile vipawa vya Roho vilivyouliwa na kanisa Katoliki hapo mwanzo Bwana alivirejesha tena kama kunena kwa lugha, karama za uponyaji, miujiza, unabii n.k.Na ulipofika wakati  Mungu alimtuma William branham na ujumbe huu tena Wa ubatizo Wa Roho Mtakatifu ambao ndio utimilifu mambo yote na ndio muhuri Wa Mungu kwa mkristo yoyote aliyetayari kwenda kwenye unyakuo, waefeso 4:30"Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi. "..kwahiyo hizi hatua tatu ni muhimu kwa kila mkristo.pasipo hizo huwezi ukawa mkamilifu tafuta Roho Mtakatifu.

SWALI 4: Shetani anapofungwa kwa muda wa miaka 1000  kama tunavyosoma kwenye ufunuo 20, kisha akaachiwa kwa muda mfupi atampata nani wakati watu wote hawakuwa na dhambi
JIBU:Kumbuka wale watakaoingia katika utawala wa miaka 1000 watakuwa bado wana miili yao ya asili ya dhambi mbali na bibi arusi na wale ambao watafufuliwa katika ufufuo wa kwanza pamoja na wale wayahudi 144,000 hawa wote watakuwa na miili ya utukufu isiyoweza kutenda dhambi...lakini hao wengine biblia inasema dhambi itakuwepo katikati yao isaya 55:20 ''Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wale mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; Bali mtenda dhambi mwenye umri Wa miaka mia atalaaniwa'' hapa  unaona anazungumzia wakati wa utawala wa miaka 1000 ambapo watenda dhambi watakuwepo..pia katika zekaria 14 inazungumzia adhabu watakazopewa mataifa wasiokwenda kumwabudu mfalme na kuishika sikukuu ya vibanda. Kwahiyo kwenye utawala wa miaka 1000 wenye dhambi watakuwepo, biblia inasema Kristo atakapokuwa mfalme katika utawala huo atawachunga mataifa kwa fimbo ya chuma, hii ina maanisha kutakuwa na utiisho na adhabu dhidi ya vitendo viovu kwa wale wasioitii mamlaka ya Kristo na ndio maana fimbo ya chuma itakuwepo..kwahiyo dhambi itakayokuwepo ndani ya baadhi ya watu ila haitakuwa na nguvu kiasi cha kuleta mapinduzi kwasababu shetani atakuwa amefungiwa..lakini baadae mwishoni mwa utawala shetani atafunguliwa na kuichochea dhambi iliyopo ndani yao wale wote ambao hawakuupenda utawala Wa mfalme na watakatifu wake..na hapo ndipo  watakapoizunguka kambi ya watakatifu na kujaribu kufanya mapinduzi lakini biblia inasema moto utashuka na kuwala wote, na shetani atakamatwa na kutupwa katika lile ziwa la moto na hapo ndipo utakapokuwa mwisho wa dhambi na mambo yote.

SWALI 5:Mungu akubariki ndugu nina swali je! Tunda walilokula Adamu na Eva ni tunda la aina gani?
JIBU: Amina ndugu Mungu akubariki. Maana ya kula tunda kama inavyoonekana  pale ni kusikiliza na kutafakari na kukubadiliana na jambo Fulani unaloambiwa..kwamfano Leo hii mwanaume mwasherati anapotafuta mwanamke wa kuzini naye atakwenda kumwambia(kumlisha) maneno ya kumuhadaa kama vile kumwahidi kumuoa, atamfanya kuwa malkia wake, atampa vitu vya kifahari na maisha mazuri n.k..lakini nia ya yule mwanaume Ni kuzini nae tu kisha akishamaliza aachane naye kwahiyo ni lazima atumie njama hizo ili kumpata vinginevyo hatampata. Kwahiyo hicho kitendo cha mwanamke kusikiliza na kushawishika na hayo maneno ya hadaa ndio kulishwa tunda. Hivyo hivyo ndivyo ilivyotokea kwa hawa na nyoka. Kitendo cha hawa kusikiliza hadaa za nyoka aende kinyume na maagizo ya Mungu kule ndio kula tunda hasaa na  uasherati na mambo mengine yote yakafuata mbele,  Hivyo hivyo kula matunda ya mti Wa uzima ni kusikiliza na kulitafakari na kukubaliana na maneno ya Yesu kristo ambapo ndani yake kunatoka chemichemi ya Maji ya uzima na utakatifu na upendo. na huu mti wa uzima ni Bwana Yesu Kristo mwenyewe..vile vile na mti wa ujuzi Wa mema na mabaya ni shetani mwenyewe na matunda yake ndio uasherati ambao Hawa aliufanya na nyoka,uongo, uoga,laana,uuaji n.k.
Kwahiyo ni muhimu kufahamika tunda lililolika pale sio tunda kama apple au mengine kama wengi wanavyodhani, kula apple au peas hakuwezi kumfanya mtu ajione kuwa uchi, na kama kula apple lilikuwa ni kosa lililomsababisha mwanadamu aanguke ingekuwa mpaka leo wanadamu wanaanguka kwa kula ma-apple, lakini ni dhahiri kilichofanyika pale ni uasherati, ni dhambi ambayo Mungu anaichukia tangu kile kipindi mpaka leo, hiyo ndiyo dhambi ya asili.Na ndio dhambi inayowaangusha watu wengi hata leo, na hilo tunda mpaka leo bado watu wanalila kila siku.

No comments:

Post a Comment