"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Monday, December 11, 2017

UFUNUO: Mlango wa 7 & 11


Dalili zote zinaonyesha kuwa tunaishi katika wakati wa kumalizia, kurudi kwa YESU KRISTO mara ya pili kulinyakua kanisa na kuleta utawala mpya hapa duniani wa miaka 1000 umekaribia sana. Kama tukitazama unabii wa biblia tunaona kuwa baada ya Israeli kumkataa MASIA wao (YESU KRISTO), injili iliondoka kwao na kuhamia kwetu sisi mataifa.

Matendo 13:46 " Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza(Wayahudi); lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. " ... 
Matendo 28:28 ” Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa, nao watasikia! “

Tukiendelea kusoma mahali pengine mtume Paulo alisema kwenye (Warumi 11:17-24 ) kwamba Israeli kama mzeituni halisi, ulikatwa ukupachikwa mzeituni mwitu ambao ndio sisi mataifa. Hivyo kuanzia kile kipindi walichomkataa Masia, Bwana akawaacha na kuanza kushughulika na watu wa mataifa kwenye zile nyakati tofauti tofauti saba za makanisa kama tunavyosoma katika ( Ufunuo 2 & 3). Na sasa ndio tupo katika lile kanisa la mwisho linaloitwa LAODIKIA.

Lakini kumbuka ukiendelea kusoma utaona pia NENO linasema..

Warumi 11 :24" Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe?
25 Kwa maana, ndugu zangu, SIPENDI MSIIJUE SIRI HII, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UWASILI.
26 HIVYO ISRAELI WOTE WATAOKOKA; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. "


Kwahiyo unaona hapo juu,Kuna SIRI imejificha, anasema pale UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI ndipo Israeli watarudiwa tena na kuokoka, pale ule mzeituni halisi utakapopachikwa tena na ule mwitu kuondolewa.
Swali ni je! huu utimilifu wa mataifa unawalisi wakati gani? utawasili pale zile nyakati za yale makanisa saba zitakapoisha, Kanisa la Laodikia likiwa kama la mwisho BWANA atakapomaliza kulinyakua kwenda mbinguni, sasa kuanzia wakati huo na kuendelea utakuwa ni wakati wa BWANA kushughulika na watu wake Israeli, na kitakuwa ni kipindi kifupi sana yaani MIAKA SABA tu! baada ya hapo ni hukumu ya mataifa na mwisho wa Dunia.

Tukisoma katika ufunuo sura ya pili na ya tatu, tunaona yale makanisa saba na malaika wake 7 kama hujafahamu bado tafadhali fuata link hii >>>> https://wingulamashahidiwakristo.blogspot.com/2016/09/nyakati-saba-za-kanisa-na-wajumbe-wake_19.html . utaona kuwa wale malaika ni wajumbe na ni wanadamu Mungu aliowanyanyua kuangaza NURU ya Mungu ambayo ilikuwa inakaribia kuzimika kwa kila nyakati, mfano Mtume Paulo alikuwa ni malaika wa kanisa la kwanza linaloitwa EFESO, Irenius-mjumbe wa kanisa la pili, Martin la tatu, ...Luther la tano...William Branham la saba.

Na kama vile kila mjumbe alikuwa anamulika NURU ya wakati ule kwa kila kanisa, vivyo hivyo baada ya Mungu kuamishia INJILI Israeli kuna watu ambao Mungu atawanyanyua kuwahubiria INJILI ambayo itawafanya wao wamwamini YESU KRISTO waliyemkataa miaka 2000 iliyopita, Kumbuka leo hii Wayahudi hawamwamini YESU kuwa ndiye masia aliyetabiriwa juu yao atakayewakomboa wanasema "Kama huyu YESU ndiye Masia, na leo hii afanye zile ishara walizozifanya manabii nasi tutamwamini", wakiwa na maana ishara kama vile za MUSA na ELIYA, Kushusha moto, bahari kuwa damu, n.k.

Kwasababu hiyo basi kwa kuwa wayahudi walikataa kumwona Mungu katika rehema na neema ya msalaba, Hivyo katika nyakati za mwisho Mungu atawapa ISHARA wanazozitaka wao. Na ukisoma biblia katika kitabu cha Ufunuo 11, utaona habari ya wale manabii 2 ambao Mungu atawanyanyua katika siku za mwisho, hawa ndio watakaoipeleka injili ya KRISTO aliye hai Israeli, zile ISHARA na yale MAPIGO yakifuatana nao..tusome 

                                              **** UFUNUO 11****

1 Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo.
2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili.
3 Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.
4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi.
5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.
6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.
7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua.
8 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa.
9 Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini.
10 Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.
11 Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.
12 Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.
13 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.

Hawa manabii wawili watafanya kazi yao miaka mitatu na nusu ya kwanza kati ya ile saba ya mwisho, kumbuka wakati huo kanisa la Kristo litakuwa limeshanyakuliwa na wafu wameshafufuliwa neema haipo tena kwa mataifa mzeituni mwitu umeshang'olewa waliobaki ambao hawakunyakuliwa ni wale ambao walichezea neema waliyopewa wakati Kristo analia katika mioyo yao watubu, hao ndio watakaopitia DHIKI KUU na wengi wao ndio watakaoshirikiana na mpinga-kristo kuwaua wale wayahudi na wale ambao watakataa kuipokea ile chapa ya mnyama.

Kumbuka miaka 7 ya mwisho itakuwa imegawanyika katika vipindi viwili, nusu ya kwanza (yaani miaka mitatu na nusu ya kwanza) injili itahubiriwa Israeli na wale manabii 2, na nusu ya pili itakuwa ni kipindi cha ile DHIKI KUU,mpinga-kristo atakaponyanyuka na kuwaua wayahudi na wale wote wasioipokea ile chapa ya mnyama, kutakuwa na mateso mengi yasiyoweza kuelezeka.

Hivyo WAYAHUDI baada ya kuona zile ishara na yale mapigo ya wale manabii 2, watagundua kuwa waliokosea, na kwamba yule waliyemsulibisha miaka 2000 iliyopita alikuwa ni MASIA wao,na hakuna mwingine, maandiko yanasema watatubu kwa kulia na kuomboleza..ukisoma

Zakaria 10:10-14" Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.
12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.
14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao. "

Unaona hapo wayahudi watamwombolezea yule WALIYEMCHOMA(mkuki), pale KALVARI. Hivyo Mungu atawamwagia Roho ya kumwamini ndipo hapo watakapotiwa MUHURI WA ROHO MTAKATIFU, kama vile watakatifu wote wanavyotiwa muhuri kwa Roho Mtakatifu leo, kumbuka muhuri wa Mungu ni ROHO MTAKATIFU(waefeso 4:30, 1:13 ) .

Jambo hili tunaona katika kitabu cha Ufunuo 7, pale wayahudi 144,000 walipotiwa muhuri, kwahiyo kumbuka sio wayahudi wote waliotiwa muhuri bali ni wale 144,000 tu, kama vile sio wakristo wote watakaokolewa bali ni lile kundi dogo tu lilipokea Roho Mtakatifu muhuri wa Mungu, vivyo hivyo itakavyokuwa kwa wayahudi nao baada ya kanisa kuondoka
                                                        *** UFUNUO 7 ***

1 Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.
2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,
3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.
4 Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.
5 Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu.
6 Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu.
7 Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu.
8 Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. "

Umeona hapo yule malaika aliwapigia kelele wale malaika wengine akiwaambia wasiidhuru nchi mpaka watakapotiwa muhuri watumwa wa Mungu, ikiwa na maana kuwa baada ya wale wayahudi 144,000 kutiwa muhuri kitakachofuata ni mapigo ya GHADHABU YA MUNGU WENYEZI dhidi ya waovu wote walioko duniani walioipokea chapa na utawala wa mpinga-kristo.

Hivyo ndugu huu ni wakati wa kujiweka tayari hili ni kanisa la mwisho la LAODIKIA na mjumbe wa hili kanisa alishapitia (William Branham) akiwa na ujumbe wa kuwaita watu watoke katika mifumo ya madhehebu na ile dini ya uongo Katoliki, yule Babeli mkuu mama wa makahaba, Hivyo ndugu ni muhimu kufahamu saa unayoishi, na ujumbe wa wakati wako.

Angalia sasa hivi taifa la Israeli linanyanyuka biblia inasema kwa MTINI JIFUNZENI, pindi mnapoona unaanza kuchipua tena basi mjue wakati wa mavuno umekaribia, kumbuka Mtini ni Israeli na tunaona Israeli inazidi kuchipua kuonyesha kwamba neema inavyoanza kuondoka kwetu na kuhamia Israeli, Neema ikishageukia Israeli huku kwetu mlango utakuwa umefungwa na jambo hili lipo karibuni sana kutimia, Bwana Yesu alisema AMIN! AMIN! nawaambia KIZAZI HIKI HAKITAPITA, HATA HAYO YOTE YATAKAPOTIMIA, sasa kizazi kinachozungumziwa hapo sio kile kizazi cha akina Petro, bali ni KIZAZI HIKI KILICHOONA MTINI KUCHIPUA TENA (yaani ISRAELI).

Kumbuka waisraeli hakuwa na taifa huru kwa zaidi ya miaka 2500 hadi ilipotimia juzi mwaka 1948 walipopata uhuru wao (yaani kuchipuka tena). Hivyo kizazi hichi kilichoshuhudia Israeli kuwa taifa tena hakitapotea kabla ya YESU KRISTO Kuja mara ya pili. unaweza ukaona ujue ni wakati gani tunaishi!. Injili ipo karibuni kurudia Israeli ilipotokea, je! umejiweka tayari kwa unyakuo?, JE! TAA yako inawaka? Umepokea ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye MUHURI WA MUNGU.

Luka 13:23-28”
23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. “

FAHAMU KUWA PASIPO ROHO MTAKATIFU HAKUNA UNYAKUO.

Mungu akubariki!

No comments:

Post a Comment