"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Sunday, April 15, 2018

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 21



SWALI 1: Ndugu Zangu Ebu Nielewesheni Haya? HIvi Hii Siku Ya "IJUMAA KUU"Inayoadhimishwa na WAKRISTO HATA WALIOOKOKA IMEANDIKWA KWENYE BIBLIA? Maana sijuwi neno "IJUMA KUU" SIJUWI LINAMAANISHA NINI. 2.je,ni vizuri kwa WAKRISTO wa leo hii kupanga siku zao na kusema YESU KRISTO ANAKUFA LEO NA ANAFUFUKA KESHO KUTWA? NA ANGALI YESU KRISTO ALISHA-KUFA NA KUFUFUKA IMESHAPITA MIAKA MINGI TU.(Tunaruhusiwa na maandiko matakatifu kufanya hivyo?.


JIBU: Kuhusu Ijumaa kuu haipo kwenye biblia...ni mapokeo tu...na pia kusema Yesu amefufuka leo au amefufuka kesho sio sawa, kama ulivyosema Bwana alishafufuka miaka mingi iliyopita, lakini si dhambi mtu kama kwa mapenzi yake mwenyewe akiamua kutenga siku ya kukumbuka kifo cha mwokozi wake, japo inapaswa iwe ni kila siku lakini pia wanaofanya hivyo hawatendi dhambi shida inakuja ni pale watu wanavyozigeuza hizo siku na kuwa kama sherehe za kipagani, wengine hawajui hata maana yake, wengine ndio wanatumia kufanya maovu, wengine kufanya ibada za masanamu kwa kuziabudu, wengine anasa, wengine uasherati n.k kama tunavyoona  watu wanavyofanya sasa hivi...sasa Hiyo ni harafu mbaya sana mbele za Mungu,..lakini kama watu wangekuwa ndo wanatumia siku kama hizo kuutafakari msalaba, na umuhimu wake katika maisha yao na kumwimbia Mungu kwa shangwe mioyoni mwao kuonyesha kuwa wanathamini walichofanyiwa na mwokozi wao YESU KRISTO, ingekuwa ni sawa, lakini inavyofanyika sasahivi sio sawa japo si kwa wote.
 SWALI 2: PASAKA INASHEREHEKEWAJE NDUGU ZANGU (Hebu nielewesheni hapa?)tufanyeje wakati wa kusheherekea PASAKA? MAANDALIZI/MAHITAJI YAKE NINI? Mbarikiwe Wapendwa.
JIBU: Katika ukristo hakuna sheria yoyote ya kusheherekea pasaka...kwahiyo hakuna maandalizi yoyote, wala sharti lolote...ikiwa umeona ni vema kukumbuka kufa na kufufuka kwa Bwana wako kikubwa unachoweza kumfanyia ni kumwimbia kumwabudu na kumshukuru katika hizo siku..na zaidi ya yote ni kuwahubiria na wengine habari njema ya msalaba...hilo tu hakuna lingine.


SWALI 3: Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja KUITANGUA TORATI AU MANABII; La!, SIKUJA KUTANGUA, bali KUTIMILIZA. Ndugu hebu nielewesheni  haya mawili 1.BWANA anaposema "sikuja kutangua torati na manabii" anamaanisha nini? 2.na BWANA anaposema amekuja "KUTIMILIZA"anamaanisha nini?)



JIBU: BWANA aliposema hakuja kuitangua torati wala manabii bali kuitimiliza...alikuwa ana maana kuwa hakuja kuondoa neno lolote la torati lililosemwa bali alikuja kulifanya kuwa IMARA ZAIDI..kwa mfano torati ilisema usizini...lakini Bwana Yesu alikuja akasema amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye nafsini mwake...si umeona hapo.. hajaiondoa torati bali ndio ameikolezea..sio tu kwenda kuchukua hatua ya kuzini ndio iwe kosa bali kumtamani tu tayari ni kosa, hivyo haupaswi kutamani kabisa...na pia torati ilisema usiue..lakini Yesu alisema amchukiaye ndugu yake ni sawa na muuaji..umeona hapo sio tu
Kuua, bali hata hilo wazo la kuua tu halitakiwi liwepo ndani ya mtu. Na ndivyo ilivyo pia kwa maneno mengine yote yote ya torati Bwana hakuyaondoa bali aliyathibitisha zaidi.



SWALI 4: JE! Ni sahihi kwenda kumfuata kiongozi wa dini na kumpigia magoti kumweleza dhambi zako?. Kwasababu nilimuuliza mtu mmoja ni kwanini anakwenda kwa Padre na kumwambia dhambi zake akasema..imeandikwa  “Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa;(Yohana 20:23)” hivyo Padre anaouwezo wa kumwondolea mtu dhambi..Hili mnalizungumziaje ndugu zangu?


JIBU: Kwa kuongezea Bwana Yesu pia alisema.. Mathayo 16 15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGA DUNIANI, LITAKUWA  LIMEFUNGWA MBINGUNI, NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGULIWA MBINGUNI
Hapo tunaona Petro alipewa funguo za kufunga na kufungua, na vivyo hivyo na mitume wengine wote walipewa funguo hizo, lakini haikuwa na maana kuwa "wana uwezo wa kumwondolea mtu dhambi kwa kumtamkia tu basi" hapana! bali walipewa ''FUNGUO'' za kumfanya mtu aondolewe dhambi zake, na ndio maana petro na mitume wengine walipowahubiria watu na kuamini waliwaambia WATUBU na WAKABATIZWE KILA MMOJA WAO ili dhambi zao ziondolewe (matendo 2:38) lakini hawakuwaambia.."njooni sisi tumepewa uwezo wa kuwaondolea dhambi zenu hivyo pokeeni msamaha"....unaona hapo huo ufunguo ni ufunuo wa jinsi ya kufanya dhambi za mtu ziondolewe ....Lakini papa na mapadre wengine hawafanyi kama mitume walivyofanya bali wao wanawatamkia watu wamesamehewa kwa kisingizio cha hayo maandiko....(kutokana na kukosa UFUNUO wa Roho Mtakatifu ndani yao wanayatafsiri maandiko kwa akili zao ili kutimiza matakwa yao wenyewe.)


SWALI 5 : Ahsante Kwa majibu mazuri. lakini katika kujibu swali, umetoa mfano wa namna ya kufungua, kuwa ni kumhubiria mtu habari njema ambayo Kwa hiyo humpelekea kutubu!
Je! Ni namna gani mtumishi wa Mungu anaweza kumfunga mtu?.

JIBU: Kadhalika na kumfungia  mtu dhambi, sio kazi yetu kwenda kumtamkia "nakufunga kwa jina la Yesu" hapana! hivyo ni kinyume na maandiko, kumfunga mtu inatokea pale mtu fulani au jamii fulani ya watu wamepelekewa habari njema za wokovu, na kuzikataa, watu hao wanakuwa wamefungwa kwenye vifungo vya giza wakingojea hukumu, kwasababu wamepelekewa kweli lakini wameikataa, Hivyo, Mtu anapoonywa mara nyingi kuhusu jambo fulani na hataki kubadilika au ana puuzia, mtu yule anaachwa na Mungu, na hiyo kwake inakuwa kama kifungo (mlango wa neema kwake unafungwa )..Bwana Yesu kuna sehemu alisema..

Mathayo 18: 15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni".

Bwana pia kuna mahali alisema, Yesu kuna mahali alisema.. mathayo 10: 14 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu.
15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule". 

Unaona hapo mtu akishupaza shingo anapoonywa mara nyingi na hataki kubadilika anakuwa amefungiwa dhambi, mlango wa neema unaondoka juu yake, kadhalika na kizazi hichi cha siku za mwisho, muda wa mataifa unakaribia kuisha, neema inafungwa kwa watu wa mataifa, (mataifa wanafungiwa dhambi) kwasababu wameisikia injili kwa muda mrefu na hawageuki, hivyo neema inahamia kwa israeli, na ule mwisho kufika, hivyo ni kujitathimini kila siku, tusiichezee hii neema tuliyopewa, thamani ya msalaba ni kubwa sana.



SWALI 6: Wapendwa nini maana ya huu msemo "Ushuhuda wa YESU ndio ROHO YA UNABII” (ufunuo 19:10)?.



JIBU: Anaposema ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii...inamaana kuwa mtu yeyote ambaye anajiona kuwa anayo roho ya unabii ndani yake au anayejiita nabii, kama maisha yake au mahubiri yake hayalengi kwa YESU KRISTO BWANA WETU,..basi huyo ni nabii wa uongo..hata kama anaona maono kiasi gani, au anatabiri na kutenda miujiza kiasi gani huyo bado sio nabii, au ni nabii wa uongo...hivyo ili umtambue kama huyu ni nabii kutoka kwa Mungu ...je! anakurudisha kwa YESU? au anakupeleka katika mambo mengine?... Unamkumbuka Yohana mbatizaji, yeye hakuwahi kufanya muujiza hata mmoja, wala ishara yoyote..lakini ushuhuda wake ulikuwa ni nini?..ni kuwapeleka watu kwa YESU, na si kingine..lakini Bwana alimwambiaje?...yeye ni zaidi ya NABII..na hakuna aliyetokea kama yeye. Lakini kitu gani kilichopo sasahivi...watu wanajiita manabii wanakutabiria lakini hawana chochote cha kukusaidia wewe kumjua Kristo na uweza wa wokovu wake   ..ni mafanikio tu, uponyaji na miujiza basi..(sasa hawa hawana ushuhuda wa YESU)...Hivyo sio manabii wala roho ya unabii haipo ndani yao..



 SWALI 7: 1.ZAKA ni nini? kwa agano la kale na kwa sasa Agano jipya likoje je,ni la zima? 2.FUNGU LA KUMI ni nini? kwa agano la kale ilikuaje na kwa agano jipya ikoje? ni lazima? 3.DHABIHU ni nini? 4.SADAKA ni nini? 5.sadaka ya MALIMBUKO ni SADAKA GANI? 6.sadaka ya KUMKOMBOA MZALIWA WA KWANZA NI SADAKA GANI.?



.
JIBU:
1)
zaka na fungu la kumi ni kitu kimoja....ni moja ya kumi ya mapato yako unayopata....Hivyo ni vyema kwa mtu yeyote anayejishughulisha na kazi ya mikono yake kumtolea Bwana sehemu ya kumi ya mapato yake kwa faida yake mwenyewe...

Dhabihu ni sadaka ya kuteketezwa ambayo katika agano jipya hatuna...dhabihu yetu ni BWANA YESU KRISTO, yeye ndiye aliyeteketezwa kwa ajili yetu sisi... Na SADAKA.. ni kingine chochote ambacho mtu anaweza kumtolea Bwana kwa hiyari..kama fedha, vyakula, mali, n.k...na hazina masharti ni kwa jinsi mtu aguswavyo kumtolea Mungu wake.

5) Malimbuko ni sehemu ya mazao ya kwanza unayopata ...hayo yanakuwa ni ya Mungu.. kwa mfano kwa agano la kale mzaliwa wa kwanza alikuwa ni malimbuko kwa Mungu..huyo anakuwa ni wa Mungu...pia mazao ya kwanza ya shambani sehemu yake yalikuwa yanaenda kwa Bwana..n.K vivyo hivyo na sasa hivi kama mtu anafanya kazi ikiwa ndio anaanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza..mshahara wake wa kwanza unaenda kwa Bwana au sehemu ya huo mshahara kwa jinsi atakavyopenda kumpa Mungu.

6) Sadaka za kukomboa hizo zilifanyika katika agano la kale...lakini kwasasa katika agano jipya hatuna sheria ya kukomboa kitu chochote kwa sadaka ikiwemo hiyo ya kumkomboa mzaliwa wa kwanza....Lakini sasahivi kuna baadhi ya madhehebu yanafanya hivyo kwa nia tu ya kukusanya fedha kutoka kwa watu au yanafanya kwa kukosa maarifa..utakuta kuna sadaka ya kukomboa nyumba, ukoo, viwanja, n.k....mpaka unakuta mtoto wa Mungu analemewa na asipofanya hivyo anajihisi kuwa anafanya dhambi... Kumbuka sadaka yoyote ni HIARI ya mtu.. Mungu hajamtwika mtu kongwa la kumlazimisha kumtolea ili kwamba amuhudumie..yeye hayupo hivyo..isipokuwa ni wajibu wetu kila mmoja kumtolea Mungu kwasababu tunampenda na yeye pia alijitoa kwa ajili yetu. Ubarikiwe sana.

No comments:

Post a Comment