"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Monday, October 29, 2018

MNGOJEE BWANA

KUNGOJA maana yake ni kukaa katika hali ile ile huku ukisubiria kitu ulichokuwa unakitarajia kifike mara, na tunajua kwa namna ya kibinadamu, kungojea kitu Fulani kwa muda mrefu huwa kunachosha, kwamfano leo mtu akitumia saa moja kwenye kufanya shughuli fulani labda tuseme kupika au kufua, na akitumia saa hilo hilo moja katika kumngojea rafiki yake kituoni kwa namna ya kawaida yule mtu ataona ule muda aliotumia kumgojea rafiki yake kituoni umekuwa mrefu zaidi kuliko ule muda ambao alikuwa anapika. Ni kwasababu gani? Ni kwasababu alipokuwa kituoni, hakuwa anajishughulisha na jambo lingine lolote isipokuwa kumtarajia rafiki yake tu. Muda wake mwingi haukupotea katika migawanyo ya shughuli nyingi bali katika jambo moja tu, hivyo muda ukaonekana kuwa mrefu zaidi.

Kadhalika sisi tunapokuwa watoto wa Mungu kwa kuzaliwa mara ya pili [yaani kwa kubatizwa kwa maji na kwa Roho] Mungu analigeuza tumaini letu na tegemeo letu lote kuanzia huo wakati na kendelea tunakuwa tunamtazamia yeye.

Biblia inasema Luka 12.36 ''nanyi IWENI KAMA WATU WANAOMNGOJEA BWANA WAO, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara''.

Hivyo kukaa huku katika hali ya kungojea kutaingia ndani ya kila mkristo halisi aliyezaliwa mara ya pili, tumaini lake likiwa ni kukamilishwa kwanza hapa duniani, pili akamilishwe katika siku ya UNYAKUO. Hivyo hatuna budi kungojea kwa saburi nyingi na kujizuia na mambo mengi. Lakini biblia inasema katika.

Isaya 40: 29 “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;
31 BALI WAO WAMNGOJEAO BWANA WATAPATA NGUVU MPYA; WATAPANDA JUU KWA MBAWA KAMA TAI; WATAPIGA MBIO, WALA HAWATACHOKA; WATAKWENDA KWA MIGUU, WALA HAWATAZIMIA”.l;l

Unaona hapo, wote watumainio nguvu zao ziwasaidie katika maisha yao, watumainiao mambo yao wenyewe yawafikishe katika malengo yao, wote wanaodharau rehema za Bwana,na wokovu wake, wanaosema tangu umekuwa mkristo umepata faida gani, wote wanaosema huyo YESU mnayemngojea yupo wapi? Angalia sisi tumeshapiga hatua kubwa tuna hiki na kile, tuna maendeleo na mafanikio lakini ninyi mnaomtaja YESU mbona haji huo wokovu mnaousubiria miaka 2000 upo wapi? Huo utawala wa YESU mnaousubiria upo wapi? Huyo Yesu ameshakufa, na miaka hiyo yote hajawafaidia kitu.

Unaona hao wote wanaosema hivyo biblia inasema wao watachoka, watazimia na kuanguka, japo watajifariji kwa nguvu zao za sasa lakini ni kwa kitambo tu ipo siku watachoka tu, siku moja wataona na wengine walishaona tayari kwamba vitu wanavyovitumaini siku zote havituwapi uzima wa milele, wanaanza kuona mbona hivi vitu tulivyoviwekea matumaini na kuvitaabikia na kuvingojea havutupi furaha ya kudumu?, Biblia inasema watazimia wote bali wale WAMNGOJEAO BWANA WATAPATA NGUVU MPYA, watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. Haleluya.

Hatushangai kuona Ulimwengu ulishangaa kipindi cha mitume na bado utaendelea kushangaa wakati wa sasa ni kwanini hawa watu hawakati tamaa kwa hicho wanachokingojea?. Hawajui Ni kwasababu sio kwa uweza wao wapo vile, bali ni kwasababu ya NGUVU wanazozipata kutoka kwa yeye WANAYEMNGOJEA.

Lakini mtu anayemngojea Bwana ni mtu wa namna gani? Ni mtu yule aliyeweka tumaini lake lote kwa Mungu, na kama vile tunavyosema kungojea ni kusubiria kwa uvumilivu na kusubiria huko kunakugharimu kuacha kufanya shughuli nyingine kikitazama hicho kitu, vivyo hivyo na mtu yule anayesema anamngojea Mungu ni yule aliyejitenga na ulimwengu, aliyeamua kutokumchanganya Mungu na dunia, aliyesema tangu sasa, ulevi basi, zinaa basi, fashion basi, uchawi basi, wizi basi, usengenyaji basi, pornography basi, kampani mbovu basi, aliyesema tangu sasa namwishia Mungu katika mwenendo wangu wote, tangu sasa nautafuta utakatifu na weupe wa moyo, tangu sasa naanza mwanzo mpya na Bwana..Sasa watu kama hawa biblia inasema japo dunia itaona kama hiyo njia ya kujizuia na mambo yao ni ngumu, lakini Mungu yeye mwenyewe ndiye atakaye wapa NGUVU mpya ya kupaa juu, Mungu atawapa nguvu ya kuendelea kuishi maisha ya kujitakasa kila siku. Utakatifu kwao hautakuwa mgumu kuutimiza japo watu wa nje wataona inawezekanaje kanaje kwao wao kuishi vile?.

Na itaendelea vivyo hivyo mpaka siku ile ya kuipokea ahadi yake hapa duniani na katika siku ile ya UNYAKUO.

Pale Mungu atakapomnyeshea mvua zote mbili, yaani mvua ya masika na mvua ya vule
Ni kwa nini Bwana anataka sisi tumngojee? Je! ni kwa lengo la kututesa?. Jibu ni hapana. Bali ameruhusu tukipitie hicho kipindi ili kututengeneza sisi, tuweze kuzimudu wingi wa hizo Baraka na hizo AHADI alizoziweka mbele yetu.

Zaburi 37: 9 Maana watenda mabaya wataharibiwa, Bali wamngojao Bwana ndio watakaoirithi nchi.

Bwana alipowatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri, hakuwafikisha moja kwa moja katika nchi ya AHADI, badala yake aliwapitisha kwanza nyikani katika kipindi cha kumngojea yeye kwa muda wa miaka 40, kuwapa sheria itakayowasaidia kuitawala ile nchi ili iwazalie wenyewe. Jaribu kufikiri kama moja kwa moja baada ya kutoka Misri wangeingia kaanani ni kitu gani kingetokea?. Ni wazi kuwa wangeingia na miungu waliyotoka nayo Misri katika nchi takatifu, wangekuwa na tabia zao za uuaji, uchawi, visasi n.k. katika nchi ambayo Mungu ameibariki wao wangeifanya kuwa laana. Lakini iliwapasa wapitie kipindi Fulani cha kumngojea Mungu ili siku watakapofika waingie na kanuni za kuwasaidia kuishi mule.

Lakini tunasoma wengi wao hawakuwa wavumilivu kumngojea Mungu, wakaanza kurudia mambo ya Misri ambayo walishayaacha zamani, wakaona mbona nchi yenyewe ipo karibu lakini miaka hii yote hatuifikii, hivyo wakakata tamaa na kuasi kama tunavyosoma. katika

Zaburi 10: 7 Baba zetu katika Misri Hawakufikiri matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu.
8 Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake, Ayadhihirishe matendo yake makuu.
9 Akaikemea bahari ya Shamu ikakauka, Akawaongoza vilindini kana kwamba ni uwanda.
10 Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia, Na kuwakomboa na mkono wa adui zao.
11 Maji yakawafunika watesi wao, Hakusalia hata mmoja wao.
12 Ndipo walipoyaamini maneno yake, Waliziimba sifa zake.
13 Wakayasahau matendo yake kwa haraka, HAWAKULINGOJEA SHAURI LAKE.
14 Bali walitamani sana jangwani, Wakamjaribu Mungu nyikani.
15 Akawapa walichomtaka, Akawakondesha roho zao.
16 Wakamhusudu Musa matuoni, Na Haruni, mtakatifu wa Bwana.
17 Nchi ikapasuka ikammeza Dathani, Ikaufunika mkutano wa Abiramu.
18 Moto ukawaka katika mkutano wao, Miali yake ikawateketeza wabaya.
19 Walifanya ndama huko Horebu, Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.
20 Wakaubadili utukufu wao Kuwa mfano wa ng'ombe mla majani.
21 Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri.
22 Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu, Mambo ya kutisha penye bahari ya Shamu.
23 Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake kama mahali palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.
24 Wakaidharau nchi ile ya kupendeza, Wala hawakuliamini neno lake.
25 Bali wakanung'unika hemani mwao, Wala hawakuisikiliza sauti ya Bwana.
26 Ndipo alipowainulia mkono wake, Ya kuwa atawaangamiza jangwani,
27 Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa, Na kuwatapanya katika nchi mbali.
28 Wakajiambatiza na Baal-Peori, Wakazila dhabihu za wafu.
29 Wakamkasirisha kwa matendo yao; Tauni ikawashambulia.
30 Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu; Tauni ikazuiliwa.
31 Akahesabiwa kuwa ana haki Kizazi baada ya kizazi hata milele.
32 Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,
33 Kwa sababu waliiasi roho yake,…..”
Hivyo kaka/dada, ikiwa wewe umeshakuwa mkristo, usichoke kumtazama Bwana, usichoke kumngojea Bwana ukayatamani mambo uliyoyaacha nyuma, mngojee Bwana baki katika hali hiyo hiyo ya utakatifu mpaka Bwana ajapo, faida zake utaziona utakapoingia katika nchi yako ya Ahadi pale Bwana atakapokuangazia rehema zake ukiwa hapa duniani kwanza, na kisha baadaye kule mbinguni utakapong’aa kama JUA.

Biblia inasema;

Maombolezo 3: 25 ''Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. 26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu''.


Usibabaishwe na chochote, usiyumbishwe na ulimwengu huu wala mambo ya ulimwengu huu kwasababu yanapita.Lakini wote wamngojeao Bwana watadumu milele.

Zaburi 27: 14 Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.
Ubarikiwe sana.

Tafadhali “share ” ujumbe huu kwa wengine.

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

Moja ya dhambi zinazowaangusha wengi ni “kutokusamehe”. Na hii inatokana mara nyingi na kutokuelewa nini maana ya msamaha. Ni rahisi kujilazimisha kusamehe lakini kama msamaha haujatoka ndani basi huo sio msamaha.

Ili kuelewa vizuri, tuchukue mfano una mtoto mdogo labda wa umri wa miaka 6 hivi, ukamkuta siku moja kachukua takataka kaweka ndani ya Friji, kwa namna ya kawaida ni lazima utakasirika na kuamua kumuadhibu ili kwamba siku nyingine asirudie...lakini je! Baada ya kumwadhibu utamwekea kinyongo?..Ni wazi kuwa hutamwekea kwasababu unajua ni mtoto tu! Laiti angefikia umri Fulani wa kujielewa asingefanya hivyo. Kwahiyo unamsamehe tu! Kwasababu unaelewa ni utoto tu ndio ulio ndani yake! Ndio unaomsumbua. Huwezi kwenda huku na kule na kwenda kutangaza kila mahali kwamba mwanao ni mbaya na kuanza kumchukia na kumwekea uadui.

Sasa usingeweza kuamua kumsamehe kabisa kutoka ndani ya moyo wako kama usingeelewa sababu ya kina ya yeye kufanya vile. Na ulipogundua kwamba sababu ni UTOTO ndipo ulipoamua kumsamehe kabisa kabisa.

Kadhalika tunapokuwa wakristo hatuwezi kusamehe watu wanaotuudhi au wanaotufanyia ubaya kutoka ndani ya mioyo yetu,kama hatutaelewa sababu ya wao kutufanyia huo ubaya ni ipi.

Leo tutajifunza sababu kubwa ya watu kutufanyia ubaya, au kutuudhi, au kutuumiza, au kutupangia mabaya, au kutuonea au kutufanyia chochote kile ambacho hakistahili kufanyiwa. Ambayo ukiielewa hiyo itakufanya uweze kumsamehe mtu kutoka ndani ya moyo wako kabisa.
Na sababu hiyo si nyingine zaidi ya DHAMBI ndani ya Mtu.

Mtu yoyote ambaye hajampa Bwana Yesu maisha yake, anakuwa ni milki ya shetani asilimia 100, Na kama anakuwa ni milki ya shetani, tunajua matunda ya shetani ndani ya mtu, ni yapi, Mwovu akiwa ndani ya mtu, Yule mtu lazima atakuwa ni mtu wa chuki, ni lazima atakuwa ni mtu wa kiburi, ni lazima atakuwa ni mtu wa hasira, ni lazima atakuwa ni mtu wa matusi, ni lazima atakuwa mtu wa kujipenda mwenyewe na kujijali nafsi yake, na kujiona yeye ni bora kuliko mwingine,ni lazima atakuwa ni mtu wa mashindano, ni lazima atakuwa mtu wa shari siku zote, mtu wa majivuno na wa dharau, na wakati mwingine atakuwa hata muuaji, n.k Kwa ufupi tabia zote mbaya ambazo zinajulikana zitakuwemo ndani ya huyo mtu ambaye hajampa Kristo maisha yake.

Sasa kama vile mtoto anapokosa, moja kwa moja unaelewa kabisa tatizo la Yule mtoto ni UTOTO uliopo ndani yake na laiti kama angekuwa mtu mzima asingefanya vile, Vivyo hivyo mtu yoyote ambaye hajampa Yesu Kristo maisha yake anapokutendea ubaya, anapokuonea wivu, anapokutukana pasipo sababu, anapokudharau, anapotafuta kukuangusha, anapokutegea mitego ya kila aina ili uanguke, anapokuchukia bure, anapokusengenya huku na huku, anapokuonea hasira, anapokuumiza kwa njia yoyote ile n.k Unapaswa uelewa kwamba tatizo sio yeye bali ni DHAMBI iliyo ndani yake, unapaswa uelewe laiti angekuwa Mkristo kweli kweli kama wewe asingefanya vile, laiti angekuwa amempa Bwana maisha yake asingekuwa na chuki,asingekulaani,asingekutukana, asingekuonea wivu n.k...

hivyo sio yeye bali ni ile dhambi iliyo ndani yaki, Kama vile unavyoielewa hali ya mtoto mdogo anapofanya kosa vivyo hivyo unapaswa uielewa hali ya Mtu asiye ndani ya Kristo anapokukosea.
Ndio maana pale Kalvari Bwana Yesu hakutusamehe sisi kwasababu tu aliamua kutusamehe, au alituvumilia,hapana! bali alitusamehe kwasababu alijua hatujui tutendalo, Alijua laiti tungemjua yeye ni nani kwa wakati ule Tusengelimsulibisha pale msalabani. Alijua laiti tungefunguliwa macho yetu tusingefanya yale mambo...Hivyo alitusamehe katoka ndani ya moyo wake kabisa.

Sasa ukishindwa kuelewa haya, utajikuta kila mtu anakuwa adui yako, utashinda kuelewa tofauti ya mtu aliye ndani ya Kristo na mtu asiye ndani ya Kristo, utajikuta unakesha katika maombi ya kuangamiza maadui zako, utajikuta na wewe unaanza kulipiza mabaya badala ya mema. Utajikuta na wewe shetani amekuingia unaanza kuwa na chuki, unaanza kuwa msengenyaji, unaanza kulipiza visasi n.k

Hakuna sababu ya mtu kuwa adui yako, anapokutukana, hakuna sababu ya mtu kuwa adui yako anapokusengenya, hakuna sababu ya mtu kuwa adui yako anapokuchukia, hakuna sababu mtu kuwa adui yako anapokusaliti, hakuna sababu mtu kuwa adui yako anapokutendea ubaya wowote ule, kwasababu unaelewa kabisa kwamba tatizo sio Yule mtu, TATIZO NI DHAMBI ILIYOPO NDANI YAKE, laiti angekuwa mkristo kweli kweli asingefanya vile, hivyo unachopaswa kufanya ni kuchukua hatua ya wewe kumwombea Bwana ampe wokovu ile Dhambi hizo ziondoke ndani yake, lakini sio kushindana naye...Kwasababu ukishindana naye huwezi kumbadilisha kuwa kama wewe, wala hawezi kuvutiwa na kile kilichoko ndani yako. Suluhisho pekee ni kumwombea Rehema na Neema mbele za Mungu.

Ndugu jifunze kusamehe kutoka ndani ya moyo, kwa kuelewa hali ya mtu aliyopo. Kama kuwa na maadui hakuna mtu aliyekuwa na maadui kama Bwana wetu Yesu Kristo, na maadui zake namba moja tulikuwa ni mimi na wewe. Tulimtemea mate...je! wewe katika maisha yako ulishawahi kutemewa mate kama yeye?.. tulimtukana na kumdhihaki, na zaidi ya yote tukampeleka msalabani na kumwaibisha..je! wewe katika maisha yako ulishawahi kuaibishwa hivyo? Lakini yeye hakuwahi kutuita sisi maadui zake.. zaidi sana alisema “Baba wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo” na zaidi ya yote akatuita sisi tuliokuja kumwamini baadaye rafiki zake.


Kama Bwana Yesu alitusamehe madeni makubwa kama hayo, unadhani sisi tunapaswa tuwafanyieje wanaotukosea?..tunapaswa tufanye zaidi ya hapo. Bwana alisema mwenyewe kwamba sisi tusipowasamehe waliotukosea hata Baba yetu wa mbinguni hatatusamehe makosa yetu. Ikiwa na maana kuwa kama kuna mtu yoyote ambaye hatujamsamehe kwa dhati kabisa kutoka ndani ya mioyo yetu, na sisi hatutasamehewa dhambi zetu, hivyo ni ziwa la moto litakuwa linatungoja, na Kristo hawezi kuzungumza uongo.

Ndugu yangu, epuka maombi yakupiga maadui zako, epuka kupeleka mashtaka mabaya mbele za Mungu juu ya watu wanaokuudhi, au kukuumiza, usimtaje ndugu yako kwa ubaya mbele za Mungu, wala usimtakie shari, bali mwombee rehema..ili atubu awe mkamilifu, Biblia inasema katika

Mithali 24: 17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”

Unaona? Hapo Bwana hafurahii, kuanguka kwake mtu mwovu, wala hafurahii mashataka mabaya tunayompelekea dhidi ya watu wengine, maombi tunayopaswa kuomba mbele zake ni Bwana atuepushe na madhara yao lakini sio awapige, au awaue, au awalaani. Adui yetu mkubwa ni shetani na sio watu.

Ni maombi yangu kuwa Bwana atakupa Moyo wa Rehema na Toba dhidi ya ndugu wanaotukosea.
Ubarikiwe sana.

Tafadhali “Share” ujumbe huu kwa wengine

Tembelea pia tovuti yetu hii >>> www.wingulamashahidi.org

Saturday, October 27, 2018

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 41

SWALI 1: Shalom,mtumishi wa BWANA!Mimi ninataka kujua je, ni halali kwa mtu wa Mungu kutumia njia za uzazi wa mpango,ikiwamo mipira?Jambo la pili,Je! taratibu za kufunga ndoa [yaani harusi] ni agizo la Mungu au ni mapokeo tu ya kibinadamu? Asante!!

JIBU: Biblia haijaeleza moja kwa moja kuhusu suala la uzazi wa mpango aidha utumike au la, kwasababu njia zinazotumika sasa hazikuwepo katikati ya watu wa kale, Lakini ni vizuri kufahamu lengo la kufanya hivyo ni nini, wapo wengine wanafanya hivyo kwasababu ya matatizo ya kiuchumi, wengine kwasababu ya mapungufu ya kimwili, wengine kwasababu ya kuzuia kuathiriwa kwa kazi yake Fulani, na pia wapo wengine ni kwasababu tu za kiasherati/zinaa n.k..

Hivyo njia nyingi za sasa zitumiwazo kwa uzazi wa mpango zinachukuliwa kwa taswira ya kiasherati kwasababu iko wazi nyingi zinatumiwa hivyo. Lakini ikiwa ni kwa wana ndoa, na dhamira zao zikiwa ni safi mbele za Mungu, na malazi yao ni masafi siku zote, na wanazo sababu za muhimu zinazowalazimu kufanya hivyo labda kwasababu za uleaji wa watoto n.k. Si dhambi wanaweza kutumia. Kwasababu kumbuka pia maandiko yanasema Katika 
1Timotheo 5: 8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

Unaona hapo? Uzaaji wa watoto usio na mpango, hususani pale usipokuwa na uwezo wa kuwalea, ni sawa na umeikana Imani. Hivyo ni vizuri kama wewe ni mwanandoa, ukae chini katika maombi na kumuuliza Mungu, na mapatano na mwenzako, na kisha zitumike. Lakini mambo hayo hayamuhusu mtu asiye mwana-ndoa.

b) Kufunga ndoa ni agizo la Mungu, lakini Harusi ni karamu/sherehe ya Ndoa mpya. Na hizo ni desturi tu ambazo zipo katika mataifa mbalimbali kulingana na chimbuko lao. Hata taifa la Israeli walikuwa na desturi za harusi. Hivyo ikiwa ndoa mpya itaambatana na harusi kwa Mungu hakuna dhambi, wala hakuna maagizo yoyote kwenye biblia kwamba mtu akioa au akiolewa ni lazima afanyiwe harusi au asifanyiwe…Ni jinsi mtu mwenyewe atakavyopenda isipokuwa tu, tumeagizwa lolote tufanyalo kwa Neno au kwa tendo tufanye kwa jina la Yesu Kristo. Ikiwa na maana kuwa hiyo arusi isivuke vigezo vya kikristo.


SWALI 2: Ndugu zangu ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku ya kuzaliwa kwake[Birth day]?

JIBU: Sherehe yoyote ile iwe ni ya kuzaliwa, au mahafali, maadhimisho ya miaka ya ndoa, harusi, kumbukumbu n.k. Biblia haitatoa katazo lolote kufanyika, isipokuwa imetoa katazo tu kwa KARAMU ZA ULAFI. Tukisema karamu za ulafi tunamaanisha karamu/sherehe zozote zinazovuka mipaka ya Neno la Mungu, kwamfano sherehe zinazochanganyikana na pombe,Disco, miziki ya kidunia, uvaaji mbovu, na mambo yote yafananayo na hayo ambayo ni kunyume na Neno la Mungu, hizo zote ni karamu za ULAFI ambazo biblia imezikataza.
Ukisoma..

1Petro 4: 4.3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na KARAMU ZA ULAFI, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;

Unaona hapo pia ukisoma …

2Petro 2: 13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu WAKIFUATA ANASA ZISIZO KIASI KATIKA KARAMU ZAO ZA UPENDO, wafanyapo karamu pamoja nanyi;

Unaona pia hapo karamu/sherehe zenye mambo kama hayo ndani yake ni dhambi kwa mkristo kufanya, lakini ikiwa ni kwa ajili ya kuhitimu, au kuzaliwa, au ndoa, au mahadhimisho unaweza ukasheherekea upendavyo lakini hapo ndio kuzingatia lile neno linalosema Wakolosai 3: Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

Na ndio maana Bwana YESU alitushauri pale tunapojisikia kufanya karamu au kusheherekea kwa namna yoyote ile tufanye kwa manufaa ya kimbinguni zaidi, yaani kuliko kuwaalika watu wenye cheo, ni vizuri kusheherekea na watu maskini, ili thawabu yetu iwe kubwa mbinguni(Luka 4:12)..Kuliko kukata keki na ndugu zetu au na marafiki zetu tu, ni vema tukaongeza pia kukata na yatima waliokaribu nasi pamoja na wajane.. Ndio karamu yenye harufu nzuri mbele za Mungu.

 SWALI: Biblia inasema askofu anapaswa awe mume wa mke mmoja! Je! Wale wasiooa kwa ajili ya injili hawawezi kuwa maaskofu?..1 Timotheo 3 :1 "Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja,..”

JIBU: swali zuri, na pia wengi wanachanganyikiwa kuhusu hilo, wakidhani kuwa mtu yeyote anayeitwa askofu ni lazima aoe…lakini unapaswa uelewe kuwa hapo Mtume Paulo alisema hivyo kwa mantiki ipi?, hakuwalenga wale ambao hawajaoa bado hapana, bali aliwalenga wale ambao wanao wake zaidi ya mmoja..kwamba hao ndio hawapaswi kuwa maaskofu, kwasababu ni lazima waonyeshe kielelezo kwanza wao wenyewe katika nyumba zao na ndio waje kuchunga wa nje, sasa kama mtu alikuwa na wake 6 kabla hajaamini na akaingia kwenye ukristo na ukristo unasema mtu anapaswa awe na mke mmoja, sasa unadhani wale atakaowachunga yeye kama askofu atakuwa anacho kielelezo gani?

Na ndio maana haipaswi mtu yeyote anayeitwa askofu au mchungaji awe na mke zaidi ya mmoja…Lakini haikumaanisha pale kwamba ni lazima kila anayetaka kuwa askofu awe na mke, huo ni uelewa hafifu wa maandiko.

Kumbuka mtume Paulo naye hakuwa na mke, lakini alikuwa mwangalizi wa makanisa yote, Kristo naye hakuwa na mke lakini yeye ndiye Askofu wa maaskofu. Hivyo hapo maneno hayo yaliwalenga wale ambao tayari wanao mke zaidi ya mmoja.

Friday, October 26, 2018

TAFUTA KUJUA MAMBO YAJAYO:

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, aliye Mfalme wa wafalme, na mkuu wa uzima, libarikiwe!

Karibu tujifunze Neno la Mungu, leo tutajifunza umuhimu wa kutaka kutafuta kujua mambo yajayo, Kwasababu biblia inasema katika..
Mathayo 7: 7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
8 KWA MAANA KILA AOMBAYE HUPOKEA; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa’.
Umeona! Bwana amesema kila aombaye hupokea, na kila atafutaye ataona ikiwa na maana kwamba, chochote mtu atakachokihitaji kama akikitafuta kwa bidii atakipata, kama atakitamani na kukihangaikia kwa bidii atakipata, na sheria hiyo haipo tu kwa wakristo bali hata kwa watu wasio wa Kristo, na viumbe vyote mtu yeyote hata asiye mcha Mungu akiamua kutafuta kitu chochoe katika ulimwengu huu kwa bidii atakipata tu! kwasababu ndivyo ilivyo “kila atafutaye atapata”…

Lakini leo hatuzungumzii namna ya kutafuta vitu vya ulimwengu huu, kwasababu Bwana Yesu mwenyewe alisema…”itatufaidia nini kuupata ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi zetu ?”

Akimaanisha kuwa tusiwekeze nguvu zetu kubwa kutafuta mambo ya ulimwengu huu yanayopita badala yake tuwekeze nguvu kubwa kutafuta kujua mambo ya ulimwengu ujao yasiyoweza kuharibika. Na sheria ni ile ile kwamba “tukitafuta kwa bidii tutapata”

Lakini kama tunavyojua zipo gharama za kutafuta kitu, katika maisha ya kawaida hakuna mtu yeyote anayetafuta elimu ya kidunia katika hatua za awali akajihusisha na mambo ya ulimwengu huu, kwanza kabisa wengi wa wazazi huwa wanawapeleka watoto wao shule za bweni, na shuleni kule wanazuiliwa kuwa na vitu vyovyote vitakavyoweza kuathiri taaluma ya watoto wao, ndio hapo mwanafunzi atazuiliwa kuwa na simu, redio, atazuiliwa pia kuwa mzururaji, zaidi ya yote atazuiliwa hata kuingia jikoni,au kujishughulisha na kazi yoyote ya kujipatia kipato, yeye kazi yake iliyompeleka pale ni moja tu!! yaani kutafuta elimu. Kwahiyo waalimu wanafahamu endapo mwanafunzi akijihusisha na mojawapo ya mambo hayo, wanajua kabisa mwanafunzi yule hatapata kile alichoenda kukitafuta pale.

Hivyo analazimika kufungiwa shuleni, ananyimwa uhuru kwa asilimia kubwa, anakuwa ni sawa na kama yupo gerezani hivi, ananyimwa kujihusisha na mahusiano yoyote yale,tena wakati mwingine analazimika kupelekwa shule ya jinsi moja tu! isiyo ya mchanganyiko, Na zaidi ya yote kama mwanafunzi yule anajielewa atazidi kujiweka kwenye utumwa mwingine ulio mkali zaidi ya ule, ndio hapo masaa yake mengi atatumia kusoma hata ya usiku wa manane, muda anaolala utakuta ni masaa machache sana…ataendelea kwenye hicho kifungo kwa muda wa miaka kadhaa akitafuta tu! kilicho bora na hatimaye atakipata! Lakini je! asingeingia gharama za kuingia kwenye hicho kifungo kikali na cha kijitaabisha hivyo je! angekipata kilicho bora??

Ndio maana Bwana Yesu alisema katika Mathayo 17: 21 “[Lakini namna hii haitoki ila kwa KUSALI NA KUFUNGA.]”

Unaona hapo aliposema kufunga hakumaanisha kuacha kula tu! bali alimaanisha kuacha kujishungulisha na mambo mengine ya kando ambayo yanaweza kuathiri kile kitu unachokitafuta. Hiyo ndio maana ya “kufunga” Kama vile mwanafunzi anavyofunga kwa kujizuia na mambo mengi ili apate anachokitafuta, anafunga kuwa mzururaji, kumiliki simu, kuangalia tv n.k

Mfano mzuri tunaweza kujifunza kwa kiumbe kama kuku, yeye atakapofika wakati wa kuyahatamia mayai yake, analazimika kufunga siku 21, lengo la yeye kufunga sio kwasababu anataka kuutesa mwili wake bila sababu, au kwasababu kapewa masharti ya kufanya hivyo, au kwasababu anatimiza wajibu Fulani, hapana bali ni kwasababu anajua endapo akienda kutembea huko na huko yale mayai aliyokuwa akiyahatamia yatapoteza lile joto na hivyo kuwa viza, na aambulie kutoata kile alichokuwa anakitafuta.

Kadhalika na tunapoutafuta ufalme wa mbinguni, tunapaswa tufunge! Na kufunga sio kuacha kula tu, hiyo ni moja, maana kuu pale ya kufunga ni tunatakiwa tufunge mambo ya ulimwengu huu yanayotuzuia tusifikie malengo yetu, kama vile kuku anavyolihifadhi joto lake kwa siku 21 kwa uvumilivu wote, na sisi vivyo hivyo tunapaswa tulihifadhi joto letu, kwa Roho Mtakatifu tuliyepewa kwa kipindi chote tunachoishi hapa duniani, Bibli inasema katika Luka 12: 35 “taa zenu ziwe zinawaka;…nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao,” hivyo tunapaswa tufunge uasherati, tufunge anasa, tufunge kiburi, tufunge kuzurura huku na kule kutafuta mambo ya ulimwengu huu yanayoharibika na utafutaji wa mali uliopitiliza…zaidi tuelekeze macho yetu mbinguni..kwasababu muda uliobaki ni mchache sana.

Kadhalika na maana ya kusali pia sio tu kujifungia ndani tu, na kupeleka mahitaji mbele za Mungu, hapana ni zaidi ya hapo, maana ya kusali pamoja na kupeleka mahitaji yetu na haja zetu mbele za Mungu ni kukaa katika uwepo wa Mungu muda mrefu ukitafuta kujua na kujifunza huku na kule kuhusu mahali ulipotoka, ulipo sasa na unapoeleka. Hiyo ndio maana ya sala.

Kaka/Dada tafuta mambo yajayo kwa “KUFUNGA NA KUSALI” wafunge marafiki wasio na maana wanaokuvuta katika mambo ya ulimwengu huu, ni afadhali uwe peke yako lakini unaenda mbinguni kuliko kuwa miongoni mwa kundi kubwa linalokwenda Jehanamu ya moto. Rafiki anayekudharau wewe unapomtafuta Mungu au anayekushauri namna ya kumtafuta Mungu wakati yeye mwenyewe hamtafuti ni Mlevi, msengenyaji, mla rushwa huyo atakupeleka jehanamu, tangu lini kipofu akamwongoza kipofu mwenzake? Bwana Yesu alisema wote watatumbukia shimoni..

Dada unayesoma hapa usipotaka kufunga mambo ya ulimwengu huu na kutazama macho yako..usipotaka kufunga uvaaji mbaya, usipotaka kufunga uvaaji wa mawigi, na kupaka wanja na lipstick, usipotaka kufunga usengenyaji wako, usipotaka kufunga tamaa za kuwa maarufu kama wanawake wa ulimwengu huu Kristo atakapokuja hutajua chochote…Hebu jifunze kwa mwanamke Ana wa kwenye biblia aliyefunga mambo yake yote na kuamua kutazama na kutafuta mambo yanayokuja ya mbinguni..

Mwanamke Ana, alifiwa na mume wake akiwa na umri mdogo, na akaamua kutokuolewa tena akafunga mambo yote na kuanza kujishughulisha katika kutafuta mambo yanayokuja tu…Wakati huo Masihi (Yesu Kristo) bado alikuwa hajazaliwa, lakini kwa jinsi alivyokuwa anatia bidii kutafuta sana…Bwana akamfunulia MAJIRA YA KUJA KWAKE, akashuhudiwa kumwona Bwana uso kwa uso. Hivyo wakati wakuu wa dini, hawajui majira ya kuzaliwa Bwana, Mwanamke Ana tayari alikuwa anajua kalenda ya Mungu. Wakati wanawake wengine wanafurahia fashioni za ulimwengu mwanamke Ana, alikuwa anajua Kristo yupo mlangoni kuja ulimwenguni. Tunasoma habari hiyo katika..
Luka 2:36 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana KWA KUFUNGA NA KUOMBA.38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake”
Na mambo haya haya yatatokea katika siku hizi za mwisho, wakati wewe dada unaendelea kujifurahisha na mambo mabovu ya ulimwengu huu, wapo wanawake wenzako mahali fulani Bwana ameshawapa kalenda yake ya kurudi kwake mara ya pili, wakati wewe unasema Kristo haji leo wala kesho wapo wanawake wenzako mahali Fulani ambao dunia inawaona washamba leo, wanazungumza na Bwana uso kwa uso, na wameshuhudiwa mambo mengi.

Kadhalika ndugu unayesema Kristo, haji leo wala kesho, hivyo ni wakati wa kuishi unavyotaka, ni vizuri ukafahamu kuwa ni maelfu wanaowaza kama wewe, lakini wapo wachache wanaofahamu nyakati za kujiliwa kwao, wapo wachache ambao wameamua kweli kufunga mambo ya ulimwengu huu na kuamua kumtafuta muumba wao, ambao tayari wameshapewa kalenda yote ya kurudi kwa Bwana..wakati ulevi wako unastawi, rushwa yako inastawi, kiburi chako kinastawi, anasa zako na uasherati wako unastawi..wenyewe wanainua vichwa vyao juu wakiitazama jinsi ile siku inavyokaribia…

Jifunze kwa Simeoni ndugu yangu, mtu aliyeishi wakati mmoja na mwanamke ANA, yeye naye Roho alimshuhudia kwamba hatakufa hata atakapomwona Kristo akifika ulimwenguni.. Wakati dunia nzima haielewi chochote..Tunayasoma hayo katika..

Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,
29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;
30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,
31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;”

Ni maombi yangu kuwa Bwana ataigeuza nia yako na mtazamo wako kuanzia leo na kuendelea, uanze kutamani kujua mambo yajayo, Roho yule yule aliyemfunulia ANA na SIMEONI kuja kwake, mara ya kwanza, Roho huyo huyo anaweza kuyafunua macho yako leo ukaona jinsi kuja kwake mara ya pili kulivyo karibu, endapo tu utakusudia KUFUNGA mambo yote ya ulimwengu na kujitenga kumtafuta Mungu kama Ana na Simeoni.

Kama hujampa BWANA YESU maisha yako, ni vizuri ukafahamu kuwa Hakuna Uzima nje ya yeye, wasanii maarufu wamepita, maraisi washupavu wamepita,.Raisi tu wa Marekani aliyemaliza muda wake, leo hii umeshaanza kumsikia anafifia lakini huyu YESU mpaka leo hii anatangazwa, habari zake hazichakai na ndivyo ilivyo kwa wale wote wanaomcha yeye, hivyo nakushauri kama hujampa maisha yako, tubu leo na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo upate ondoleo la dhambi zako nawe utakuwa na uhakika wa uzima wa milele.

Mungu akubariki.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana akuongezee Neema yake.

MSHIKE SANA ELIMU.

ELIMU ni UFUNGUO wa maisha, hiyo ni kweli, lakini ELIMU ILIYO SAHIHI sio tu ufunguo wa maisha, bali pia ni ufunguo wa kila kitu. Na kwa jinsi elimu ya mtu huyo itakavyozidi kuwa kubwa zaidi ndivyo uwezekano wa mtu huyo kufanya mambo yote unavyozidi kuwa mkubwa zaidi.

Kumbuka zipo Elimu kuu tatu zilizopo ulimwengu sasa. 

1)Elimu ya ufalme wa mbinguni.
2)Elimu ya kidunia
3)Elimu ya ufalme wa giza


Leo hii tunaweza kufurahia mafanikio tuliyoyafikia ya kiteknolojia kwa mfano kuchat na watu mitandaoni, kupaa angani kwa ndege, kuzungumza na ndugu zetu walio mbali kwa simu, kutunza vyakula katika majokofu, katazama tv n.k..sio kwasababu dunia imebalika maumbile yake tofauti na ya zamani hapana!, Ni kwasababu wapo watu waliokaa chini kwa muda mrefu mahabara, na katika makarakana usiku na mchana, wengine hata kutokuoa au kuhatarisha maisha yao, wakisoma na kujifunza kanuni za huu ulimwengu jinsi ya kuendana nazo na kwa namna gani watazitumia kubudi njia mbadala ya kuunda vitu. Na kwa bidii yao ya kujifunza na kusoma sana kwa muda mrefu ikawapelekea kugundua vitu ambavyo hata kwa namna ya kawaida unaweza ukasema haviwezakani kutokea. Lakini tunaviona katika jamii zetu kila siku vipo..

Kadhalika shetani naye hakuna jambo ameweza kufanikiwa kulipata kwa mwanadamu kirahisi rahisi kama sio kwa Elimu. Alisoma kanuni za Mungu za uumbaji kwa muda mrefu sana, hivyo kwa kuwatazama viumbe wake na vitu vya asili na nguvu na mamlaka Mungu aliyoweka ndani yao, akagundua kuwa akiwafanya waende kinyume na zile kanuni basi yeye atakuwa na uwezo wa kuzitumia kwa manufaa yake. Na ndio maana jambo la kwanza pale Edeni Shetani hakuja kwa utisho wowote wa silaha kwa Adamu na Hawa hapana bali alikuja na UDANGANYIFU. Ambao alijua kwa huo ataweza kuwadhoofisha UWEZO wao hivyo kirahisi atawapokonya mamlaka yao waliyopewa na Mungu katika hii dunia..

Na ndivyo alivyofanya na kufanikiwa kuuweka ulimwengu chini yake mpaka tunaona alipokuja Bwana wetu Yesu Kristo kuyachukua yale mamlaka tena Adamu aliyoyapoteza. Na haishii hapo tu! kwasababu shetani lengo lake ni kutaka kuwa kama Mungu, na kwasasa ameshafahamu kuwa hawezi tena kufikia malengo yake kwasababu ya YESU basi anachokifanya ni kuwa piga upofu wanadamu wote wasifikie katika viwango vya MAARIFA/ELIMU ambayo Bwana anataka watu wake wavifikie.

Na ndio maana biblia inasema katika Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;”..Shetani ataendelea kutuangamiza kama tutakosa maarifa ya kimbinguni.

Sasa Elimu hizo mbili yaani (Elimu ya dunia na Elimu ya ufalme wa giza), japo kila moja inajitahidi kwa upande wake, kutatua kila jambo, lakini hata moja haijaweza kuleta suluhisho la mambo ya msingi yamuhusuyo mwanadamu. Kwamfano hakuna elimu yoyote inayoweza kuleta dawa ya kifo na kutoa uzima wa milele, au kufufua mfu, au kuumba, au kusimamisha jua, au kuupiga mwezi, au kuamisha visiwa na milima, hakuna hata moja inayoweza kutabiri mambo yanayokuja,..hakuna hata moja ya hizo inazoweza kufanya jambo kama hilo. Wanasayansi wote pamoja na shetani mwenyewe hawana maarifa hayo.

Ni ELIMU moja tu YA KWELI ambayo Mungu aliiweka tangu mwanzo ndiyo inayoweza kufanya mambo yote, nayo ni ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI BASI!!.

Hivyo pale Biblia inaposema katika Mithali 4:13 “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.”

Haimaanishi ELIMU yoyote tu ile, iliyopo kila mahali, hapana sio elimu ya ulimwengu huu, kama vile isivyokuwa elimu ya wachawi, bali Elimu inayozungumziwa pale ni Elimu inayohusiana na hicho kitabu chenyewe (yaani BIBLIA).

Na kama vile Elimu yoyote ile ilivyo na gharama kuipata kadhalika na kuisoma, vivyo hivyo na hii ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI izidiyo elimu zote inayo gharama nyingi za kuipata. Kila mkristo anapoamini na kumpa Bwana maisha yake ni sawa na mtoto kwa mara ya kwanza alienda kuanzishwa elimu ya awali, anaitwa mwanafunzi, tunafahamu kuwa siku hiyo hiyo hawezi kujua kila kitu kinachohusu shule, siku hiyo hiyo hawezi kupaisha ndege, au kufanya operesheni, hapana bali atakavyozidi kuonyesha bidii ya kujifunza kila siku, kidogo kidogo atajikuta anaongeza kitu katika kichwa chake, atavuka darasa moja, anakwenda lingine hivyo hivyo mpaka baadaye akifika chuo kikuu, ambapo kiwango cha yale maarifa kitakuwa kimeshakolea ndani yake sasa hapo ndio anakuwa na uwezo wa kurusha ndege.

Na ndivyo tunavyojifunza kwa Bwana wetu YESU KRISTO, tunamwona kama vile alivyo, hakuzaliwa na kipawa tu basi cha kuwa na hekima nyingi kiasi kile na kujawa uwezo mkuu kama ule. Biblia haitufundishi hivyo bali tunamwona Bwana tangu akiwa mdogo alikuwa ni mtu mwenye bidii sana KUSOMA ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI, alikuwa akijifunza kupita kiasi hata akiwa na umri wa miaka 12 tu, biblia inarekodi siku tatu usiku na mchana alikuwa akijifunza habari za YEHOVA kwa marabi(Waalimu wa Torati), akiuliza maswali, pale ambapo hakuwa anapaelewa, alisahau hata kula kwa ajili ya KUSOMA TU! Aliwasahau wazazi wake, aliona ule muda walioenda Yerusalemu na wazazi wake ni mchache sana wa yeye kujifunza,

Tunasoma;
Luka 2:45 "na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta.
46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, AKIWASIKILIZA NA KUWAULIZA MASWALI.
47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake".
Biblia inasema pia aliendelea kuwa mtu wa namna hiyo hiyo, akitoka katika hatua moja ya hekima hadi nyingi.. Tunasoma

Luka 2:52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika HEKIMA NA KIMO, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Unaona hapo aliendelea katika Hekima, siku baada ya siku na KIMO kinachozungumziwa hapo sio urefu wa mwili, bali ni KIMO cha KUMJUA MUNGU. Aliweza kuona mahali waandishi walikwama, yeye hakuridhika akavuka pale na kuzidi kujifunza zaidi mpaka siku moja akawa ZAIDI ya wale MARABI waliokuwa juu yake wakimfundisha.

Tunasoma;

Mathayo 13:51 “Yesu aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam.
13.52 Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake VITU VIPYA NA VYA KALE”.


Bwana yeye kama mwandishi mkuu pia aliweza kutoa katika hekima yake vitu vipya na vitu vya kale (Agano jipya na Agano la Kale), kwasababu Elimu ya Ufalme wa mbinguni ilikuwa imemkaa sana ndani yake.

Hiyo ni sababu leo hii tunamwona Bwana kuwa mtu ambaye hakushindwa na jambo lolote, hakukuwa na tatizo lolote lililoweza kusimama mbele yake, alipewa maarifa yote na Mungu, alipewa maarifu ya namna ya kuutoa uhai wake na kuurudisha, ni nani leo hii anaouwezo huo?, aliweza kuamrisha mbingu, bahari, na upepo vyote vikamtii,hakukuwa na mgonjwa yoyote aliyeletwa mbele zake asiweze kumponya, Mungu alimpa kila kitu angali akiwa bado hapa duniani.. Na ndipo hapo shetani akajua kuwa hakuna tena tumaini kwake kwasababu vyote alivyovitarijia siku moja avipate vyote vimeshafunuliwa kwa BWANA wetu YESU KRISTO. Haleluya!. Kazi aliyobakiwa nayo sasa ni kutuangamiza kwa kukosa kwetu maarifa ya kumjua YESU KRISTO BWANA WETU.

Bwana YESU alitupa ushauri sisi wote, kwamba “TUJIFUNZE KWAKE” (Mathayo 11:29). Na pia alisema yeye ndiye njia kweli na uzima, mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye (Yoh 14:6). Hivyo ni lazima tujifunze katika NJIA ZAKE ili na sisi tupate akili tupone.

Kama wachawi na wanasayansi hawalali kila siku wapo wanachunguza na kutafiti juu ya mambo yao na ufalme wao, inatupasaje sisi wakristo ambayo ELIMU YETU inaweza kufanya makubwa zaidi ya hayo?
Ukristo mwanzo wake ni kuamini na kubatizwa, lakini pia ni zaidi ya hapo. Bwana anataka kutupa maarifa ya ziada katika maisha yetu ya kumjua yeye, ili na sisi pia tukue katika kimo na hekima, kama Bwana, lakini tunakuwa wavivu wa KUSOMA na KUJIFUNZA NENO LA MUNGU kila siku.

Japokuwa Paulo alikuwa ni mtume wa Kristo aliyejaa mafunuo mengi, na ambaye mpaka sasa tunatumia nyaraka zake kama urejesho wetu wa kimaandiko, lakini hakuacha KUSOMA na KUJIFUNZA kila siku Elimu ya Ufalme wa mbinguni. Tunasoma akimwambia Timotheo..

2Timotheo 4: 4.13 Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, NA VILE VITABU, HASA VILE VYA NGOZI.


Unaona hapo?, alihitaji Kusoma, kwasababu Elimu ya ufalme wa mbinguni ni kuu sana haina mwisho wake. Hakujiona kuwa amefika au anafahamu kila kitu bali alitaka zaidi na zaidi kujifunza kumjua Mungu katika upana wake na marefu yake. Na hakuishia hapo bali alimwagiza pia Timotheo afanye vivyo hivyo, kama tunavyosoma katika

1Timotheo 4:12 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
13 Hata nitakapokuja, UFANYE BIDII KATIKA KUSOMA na kuonya na kufundisha.”


Hivyo na sisi pia kama watoto wachanga, tuitafute sana Elimu ya ufalme wa mbinguni, kwa kutafiti na kuchunguza mambo yote yamuhusuyo MUNGU wa ISRAELI na YESU KRISTO BWANA WETU katika maandiko angali tunaishi sasa, ili tukifikie kile cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. Amen.

Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, NA KUCHUKULIWA NA KILA UPEPO WA ELIMU, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”

Ubarikiwe sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Kwa mpangilio mzuri wa masomo haya tembelea website yetu >>> www.wingulamashahidi.org

Thursday, October 25, 2018

TUZIJARIBU HIZI ROHO.

Biblia inatuambia katika 2Timotheo 3:1 kwamba siku za mwisho kutakuwa na NYAKATI ZA HATARI SANA, na kama ni nyakati za Hatari tunapaswa tuchukue tahadhari kubwa zaidi kuliko hata za watakatifu waliokuwa wanaishi nyakati za kale kabla yetu, kwasababu biblia pia inasema shetani angali akijua kuwa muda wake ni mchache anafanya juu chini awaangushe wengi kwa njia yoyote ile. Mkristo ni kuwa makini huu sio wakati wa kuamini kila “roho” inayodai kuwa ni ya Mungu, biblia imetuonya na kutuambia,

1Timotheo 4:1 "Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani"
Sasa mambo ya duniani yanatufundisha nini?, kwamba tunajua hakuna mtu yeyote asiyependa kununua kitu kilicho katika uhalisia wake (original), na kama kitu hicho kitasifika kweli kuwa ni original basi hakitakosa kuwa na feki yake baada ya muda fulani,

Lakini utakuta kwa mwanzo kilipoanza kutolewa masokoni labda tuseme ni simu utaona kuwa karibia simu hizo zote zilikuwa ni original, lakini kwa jinsi siku zilivyokuwa zinazidi kwenda, kidogo kidogo utashangaa kuona feki chache zipo humo humo zikifanana kabisa na zile original, na kwa jinsi siku zitakavyozidi kuendelea kwenda, hata zile original huwa zinazidiwa na feki sokoni, Feki zinakuwa ni nyingi, na matokeo yake huuzwa kwa bei rahisi, na hizo ndio watu hupenda kuzikimbilia kwasababu ni bei nafuu..Lakini baadaye wanajikuta wanaangukia katika majuto pale wanapogundua kuwa hazidumu, halafu bado hazikidhi mahitaji yale ambayo aliyoyatarajia kuyaona kutoka katika hizo simu..

Na ndio hapo inampelekea mtu kuhangaika kutoka kwa fundi huyu hadi fundi yule,na kutumia gharama kubwa zaidi hata ya ile aliyoinunulia, akiona tatizo bado lipo anachukia kabisa kuwa na simu na kujuta ni kwanini alinunua simu na mwisho wa siku kuitupa..tatizo sio AINA YA ILE SIMU bali tatizo ni U-FEKI wa simu.

Kadhalika katika ukristo hakuna kitu ambacho shetani hajafanikiwa kukiundia feki chake, biblia inasema, anao wachungaji wa uongo (Yer 23:1), anao mitume wa uongo (2Kor 11:3), anao waalimu wa uongo, watumishi wa uongo na manabii wa uongo (2Petro 2:1). Kama vile tu Bwana alivyokuwa na watumishi wake wanaomtumikia, Sasa shetani kuwa na watumishi wa uongo tu haitoshi ni vema pia kujua hao watumishi wanamtumikia nani, au wanamtangaza nani, au wanamuhubiri nani?.

Kama vile tu mitume, wainjilisti, waalimu, na manabii wa Bwana walikuwa wanafanya kazi moja ya kumtangaza YESU KRISTO ili watu wote wamwamini yeye, kadhalika hawa nao wanafanya kazi moja ya kumtangaza “yesu” wao ambaye siye yule YESU tunayemwambudu wa kwenye maandiko, na wanafanya hivyo ili watu tu wamwamini huyo waangamie siku za mwisho.

Biblia ilishaweka wazi kabisa, kuwa yupo “yesu” mwingine, yupo “roho” nyingine, kadhalika ipo nayo “injili nyingine” ambayo sio ile Bwana aliyoitoa kupitia mitume wake watakatifu tangu mwanzo, soma

2Wakorintho 11:4 “Maana yeye ajaye akihubiri YESU MWINGINE ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea ROHO NYINGINE msiyoipokea, au INJILI NYINGINE msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!”
Unaona hapo? Kazi ya hawa watumishi wa uongo ni kumtangaza yesu mwingine anayoonekana kama ni YESU halisi, na roho mwingine anayeonekana kama ni ROHO wa Mungu halisi ya Mungu na Injili nyingine ineyoonekana kama ni injili halisi ya Mungu lakini kumbe ni yesu-FEKI, roho-FEKI, na injili-FEKI. Lakini tunajua kitu feki kwa mwonekano wan je! ni ngumu kugundua kwasababu vyote vitaonekana kuwa ni sawa lakini utendaji kazi wake, na udumuji wake ndio vitakavyowatenganisha..wote watalijata jina la YESU katika shughuli zao za ibada, watatolea mapepo na kutabiri n.k..

Na ndio maana Bwana alisema mtawatambua kwa MATUNDA YAO, hicho tu!.

Mathayo 7.15-23 “ Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa MATUNDA YAO. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu"
Ndugu kumbuka ili uwe na uhakika YESU uliyempokea katika maisha yako, ni HALISI, ni lazima ujiulize, JE! UNAUHAKIKA UMEOKOLEWA NA KUSAFISHWA DHAMBI ZAKO KWA DAMU YAKE?, Kiasi kwamba hata ukifa sasa bila shaka yoyote utakwenda mbinguni moja kwa moja?. Kwasababu kumbuka kiini cha Kristo kuja duniani mpaka kufikia hatua ya kuitoa nafsi yake sio wewe kuwa bilionea hapana bali ni suala la UKOMBOZI, je! wewe tangu umfahamu YESU, alishawahi kuyabalisha maisha yako, na kupata uhakika wa wokovu ndani ya nafsi yako?. Jana yako inatofauti na leo yako? Kama sivyo basi! Ujue ulimpokea YESU mwingine ambaye siye aliyehubiriwa na mitume.

Kadhalika unasema unaye ROHO MTAKATIFU, je! huyo Roho aliyeko ndani yako anakufanya kuwa MTAKATIFU kama jina lake lilivyo?, na Je! anakuongoza katika kuijua kweli yote kama maandiko yanavyosema (Yohana 16:13)?, na Je! anakushuhudia kila siku katika maisha yako kuwa wewe ni mwana wa Mungu?(Warumi 8:16). Kama sio basi ufahamu kuwa ulipokea roho nyingine ambayo sio ROHO MTAKATIFU. Kadhalika ulihubiriwa injili nyingine ambayo sio injili iliyohubiriwa na watumishi wa Mungu hao mitume (yaani biblia).

Na ndio maana hauwezi kudumu katika IMANI, ni kwasababu gani? Ni kwasababu hukumpokea Kristo HALISI katika maisha yako, leo unasimama kesho unaanguka, Huyo ni yesu mwingine ulimpokea asiyeweza kukupa wokovu wa uhakika katika maisha yako. Dhambi inakutawala, unashindwa kuitawala dhambi na bado unasema umeokoka, unashidwa KUJILINDA hapo ndugu hujaokoka, biblia inasema wote waliozaliwa na Mungu hawatendi dhambi, ikiwa na maana kuwa dhambi haiwatawali 1Yohana 5.18 “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu HUJILINDA, wala yule mwovu hamgusi.”
Na ndio sababu huwezi kudumu katika imani kwasababu ni yesu-feki ulimpokea ukidhani ni BWANA YESU KRISTO. Kumbuka kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kasoro, Kristo akimwokoa mtu kamwokoa kweli kweli wala habahatishi kwasababu msalaba una nguvu kuliko kitu chochote kilichowahi kusikika chini ya jua hili.

Ulikuwa hivyo ni kwasababu ulikuwa radhi kusikiliza injili isiyo ya gharama,(unayoweza kuipata sokoni muda wowote), ile ambayo manabii wa uongo wanayoifundisha kwamba unaweza ukawa ni mkristo bado pia ukawa ni wa kidunia, unaweza ukawa mkristo bado usijikane nafsi yako usiishe kama mitume walivyoishi kujikana nafsi zao, bado uwe unaishi maisha kama mfano wa watu wa ulimwengu huu na huku umeokoka, ukristo usioweza kuachana anasa, ukristo ambao unaruhusu mwanamke kuvaa suruali na vimini, pamoja na mawigi, na Kupaka lipsticks na wanja, ukristo unaosema Mungu siku zote ni wa rehema, hawezi kuwaangamiza watu wake aliwaumba hivyo ishi tu atakurehemu kwa neema zake maadamu umemkiri kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako inatosha.

Injili ambayo haina muda kusisitiza mtu kuishi maisha ya kujilinda roho yako kila siku, bali unasisitiza kila siku kuulinda mfuko wako. Ukristo unatoa tu mafundisho ya mafanikio ya kidunia na kupuuzia mafanikio ya kimbinguni..

Hizo zote ni INJILI nyingine zisizoweza kumwokoa mwanadamu, na zinatumia jina la “yesu” mwingine linalofanana na BWANA YESU KRISTO kuwatumainisha watu wajione kuwa wapo salama kumbe Kristo hawatambui!, Kinachowatambulisha kwamba wao sio WA-KRISTO ni matunda yanaonekana ndani ya maisha ya watu wanaowahubiria.

Ndugu shetani ni wa HILA tangu mwanzo, alimdanganya ADAMU na kufanikiwa. hashindwi kutundanganya sisi na kufanikiwa kama hatutathamini roho zetu. Tusijipe matumaini ya bure kwamba tumeokoka na huku maisha yetu hayauhakisi wokovu. Ukristo halisi sio rahisi kuupata kama vile kitu original kisivyo rahisi kukipata, Ukristo wa YESU KRISTO MWOKOZI wa ulimwengu una gharama zake.

Ikiwa umekubali kweli ayaokoe maisha yako dhamiria kweli kweli kutoka moyoni, kwamba upo tayari kumwishia yeye, kwa gharama zozote zile atakazokuambia, na yeye akishaona hiyo nia yako na utayari wako basi moja kwa moja ATAKUPA UWEZO WA KUFANYIKA MTOTO WA MUNGU (Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;).

Sasa UWEZO huo wa kufanyika mtoto wa Mungu hauji kwa kila mtu tu ambaye anasema kampokea YESU bure bure, hapana bali unakuja kwa wale tu! waliodhamiria kwa dhati ndani ya mioyo yao kuanzia huo wakati na kwendelea kumwishia BWANA kwa gharama zozote zile, hapo ndipo yule Roho Mtakatifu sasa anaushusha huo uwezo, na hapo ndipo utakapoweza kuishinda dhambi na kudumu katika Imani ya YESU KRISTO BWANA wetu.

Ni maombi yangu kuwa ikiwa tunatamani kweli tuponywe roho zetu, basi tumtafute YESU HALISI, bila kukwepa vigezo vyote vitakavyoambatana na kumfuata yeye. Vinginevyo tutajikuta tumeangukia katika matumaini ya uongo ya manabii na watumishi wengi wa uongo ambao hawana huruma na hatma ya maisha ya mtu bali mambo ya ulimwengu huu tu, na katika siku ile tukajikuta tunaanza kumwambia Bwana mbona nilinena kwa lugha?, mbona niliongozwa sala ya toba?, mbona nilibatizwa? mbona nilikuona wewe kwenye maono? Na yeye atakwambia “Sikukujua kamwe; ondoka kwangu, wewe utendaye maovu”!!.

Ni hali gani utajisikia siku hiyo ukingundua kuwa ulimpokea yesu mwingine ambaye siye yeye HALISI?. Hizi ni nyakati za mwisho za HATARI mtafute YESU KRISTO wa kwenye Biblia, ambaye hasa lengo lake la kwanza ni kuigeuza roho yako kukupa uzima wa milele, na si kitu kingine.SIMAMA IMARA! BWANA ATAKUIMARISHA.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

MAISHA YETU NI MILKI YA YESU KRISTO.

Kanisa linafananishwa na mwanamke, Bwana ndio kapenda kulifananisha kanisa lake na mwanamke, akifunua kwamba kama vile mwanaume ampendavyo mkewe ndivyo Kristo anavyolipenda kanisa lake. Na kama ijulikanavyo huwa kuna hatua zinafuatwa kabla ya mwanamume kumtwaa mwanamke awe mkewe, na moja ya hatua muhimu sana inakuwa ni MAHARI. Mahari kazi yake ni kumwongezea ujasiri mwanamume kwamba hakumpata mke wake kirahisi, amemgharimia. Na baada ya kulipa mahari ,ni ndoa kufungwa,hapo Yule mwanamke anahama kwao na kuhamia kwa mume wake, na zaidi ya yote jina lake la ukoo linabadilika, Jina la ukoo linabadilika kuonyesha kwamba kuanzia huo wakati na kuendelea yeye sio milki ya ukoo wa wazazi wake tena, bali anakuwa milki ya ukoo mwingine wa mume wake.

Sasa Bwana aliruhusu huo utamaduni uendelee kuwepo mpaka leo katikati ya wanadamu, ili kuufanya wokovu ueleweke kirahisi kwetu, kwa kulinganisha namna mwanamke anavyotwaliwa kutoka kwa wazazi wake, mpaka anapotolewa mahari, mpaka anapokuwa mke halali wa mwanaume tutapata picha namna kanisa la Kristo navyo lilivyotawaliwa kutoka katika dunia.


Hatua ya kwanza Kristo anawahubiria watu wake watoke katika ulimwengu kwa ishara na miujiza mingi, kama vile mwanamume amshawishivyo mwanamke katika hatua za awali, kisha baada ya hapo Bwana Yesu ni kulipia mahari, na Mahari anayolipa ni damu yake aliyoimwaga pale Golgotha ambapo alitoa nafsi yake kama fidia kwa mkewe (YAANI KANISA), Gharama hii aliyoingia ilimfanya yeye awe na uhalali wa kulimiliki kanisa asilimia 100%.

Na hatua ya mwisho ni mtu kubadilishwa jina na kupewa jina lipya la mumewe, kama vile jina la mwanamke la ukoo linavyobadilika na kuhamia moja kwa moja kwa mumewe. Sasa mwanamke au mwanamume asipopitia hatua zote hizo ndoa yeke inakuwa sio halali.

Sasa mimi na wewe, ili kwamba tuweze kuwa wake halali wa Bwana wetu Yesu Kristo, sharti lazima tukubali kumwamini na kumgeukia yeye na kuacha wazazi wetu waliotuzaa, yaani kuuacha ulimwengu na mambo yake yote, sharti lazima tumtii kwa kutubu na kumaanisha kabisa kuacha dhambi na maisha ya nyuma ya anasa na kufanyika viumbe vipya.

Kisha hatua inayofuata baada ya kumkubali Yesu moyoni mwetu, Ni Bwana Yesu mwenyewe kutusafisha kwa maji na kwa damu kwa gharama aliyoingia pale Golgotha, Na ndio maana pale Golgotha wale askari wa kirumi walipomchoma mkuki ubavuni, kulitoka maji na damu, ambayo ile ni kama ishara ya mahari kwetu, kwamba tunasafishwa kwa maji na damu.
1 Yohana 5: 6 Huyu ndiye aliyekuja KWA MAJI NA DAMU, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli”.

Hatua hii inamfanya mtu kuwa mke halali aliyetwaliwa kwa gharama, Bwana anakusafisha dhambi zako zote, na kukuweka kuwa huru na dhambi. Na Neno lake ndio maji yanayotusafisha na Neno lake linasema...
Matendo 2: 37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.

Unaona hapo? namna mke halali wa Yesu Kristo anavyoandaliwa?...sio kwa kujiunga na dhehebu au kanisa bali ni kwa KUTUBU, Na KUBATIZWA KATIKA JINA LA YESU KRISTO, na kupokea kipawa cha Roho. Na kuanzia huo wakati jina lako linabadilika, na kuitwa Mkristo au wa-Yesu Kristo. Kwasababu umebatizwa kwa hilo jina, na Huwezi kuwa mkristo kama hujapitia hizo hatua.


Huwezi kuitwa wa Yesu Kristo kama haujabatizwa kwa hilo jina, sehemu zote kwenye maandiko watakatifu walibatizwa kwa hilo jina, yaani jina la Yesu, ukisoma mistari ifuatayo utaona jambo hilo {Matendo 2:38. Matendo 8:12, Matendo 8:16, Matendo 10:48 na Matendo 19:5}


Kwahiyo kama tu mwanamke aliyeolewa,anakuwa hawezi kujiamulia tu mambo, kwamba anaweza akalala popote atakapo, au akafanya chochota atakacho juu ya mwili wake, bali anakuwa ameingia kama kwenye kifungo Fulani, ambacho hakimpi uhuru wa kuwa na mahusiano ya karibu na kila mtu. Vivyo hivyo na kwa mkristo aliyempa Bwana maisha yake kwa kutubu na, na kubatizwa kwa jina lake Yesu Kristo, anakuwa ni milki halali ya Yesu Kristo, hana ruhusa ya kujiamulia mambo tu, au kufanya chochote anachojisikia akiwa katikati ya mahusiano yake yeye na Bwana.. Na ndio maana Biblia inasema katika
1 Wakoritho 6: 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? WALA NINYI SI MALI YENU WENYEWE;
20 maana MLINUNULIWA KWA THAMANI. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.

Unaona hapo, biblia inasema “SISI SI MALI YETU WENYEWE” ikiwa na maana kwamba ni “sisi tuliozaliwa mara ya pili ni milki ya mtu mwingine” na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO, hivyo hatuwezi kujiamulia chochote katika miili yetu, au katika aina ya maisha tunayotaka tuishi, Kwasababu yeye (Yesu Kristo) alitununua kwa thamani, nyingi maandiko yanasema hivyo.


Kwahiyo Bwana anao uhalali wa kutufanya chochote endapo tukijihusisha na mambo yoyote katika maisha yetu au katika miili yetu yatakayomtia wivu, au kumuudhi au kumhuzunisha. Kama bibli inavyosema katika..
1 Wakoritho 3: 16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 KAMA MTU AKILIHARIBU HEKALU LA MUNGU, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

Sasa tukiliharibu hekalu la Mungu yaani miili yetu, Bwana naye atatuharibu, kwahiyo tunapokuwa wakristo sio suala la kujichagulia maisha hapana ni suala la kuchaguliwa maisha na yeye aliyetutolea mahari sisi, Wivu wa Bwana unakuwa kwa wale aliwatolea mahari yaani wale aliowasafisha dhambi zao kwa damu yake, Maovu makubwa yanayomchukiza sio ya watu waliomkataa, hapana bali ni yale ya watu walio wake na bado wanafanya dhambi,(wanakuwa vuguvugu) katika maisha ya kawaida hakuna mwanamume yeyote aonaye wivu akiona mwanamke mwingine asiye wake anafanya uasherati, lakini ataona wivu zaidi endapo akimwona mke wake aliyemtolea mahari na kumwoa anamsaliti na kufanya uasherati. Na ndio maana Bwana baada ya kuwatoa wana wa Israeli Misri aliwapatia amri 10 wao tu! Hakuwapa zile amri kumi watu wote wa ulimwengu mzima, au watu wa Misri. Kwanini? Ni kwasababu Misri hakuwa mke wake halali bali Israeli.


Dada/kaka unayesoma ujumbe huu, kama kweli umeamua kumfuata Bwana na umepita hizo hatua tatu, yaani KUTUBU, na KUBATIZWA KATIKA JINA LA YESU na kupokea ROHO MTAKATIFU. Na bado unajiamulia maisha, nakushauri usifanye hivyo tena, badilisha mtazamo wako, usiwe kama mwanamke mpumbavu aliyeingia kwenye ndoa na asijue mikataba na makubaliano ya hiyo ndoa, kama umeamua kuwa mkristo mwili wako ni hekalu ya Roho Mtakatifu, usilichore tattoo, usifanye uasherati, usiunyweshe pombe, wala usiuvutishe sigara, usiuvalishe nusu uchi, wala usiuvalishe mavazi yasilolipasa ya jinsia nyingine, wala usiufanye usiwe katika hali yake ya asili. Kwasababu mwili huo sio milki yako mwenyewe ni Milki ya mtu mwingine ambaye anaweza kukufanya lolote endapo ukiuharibu na hautapata mtetezi.

Zipo faida leo ukidumu katika uaminifu wako kama bibi-arusi wa Kristo, asiye na hila wala mawaa, kwasababu biblia kama inavyosema katika mbingu mpya na nchi mpya Uje mji mtakatifu wa Mungu yaani YERUSALEMU mpya ushukao kutoka mbinguni ndio bibi-arusi wa Kristo(Ufunuo 21), Mungu atakaa ndani yake, Na katika huo (ambao ndio sisi) Mungu ndio atafanya maskani kumbuka hatafanya maskani kwa kila mtu tu atakayekuwepo huko hapana, bali kwa bibi-arusi tu.. Hivyo tukaze mwendo kama bibi-arusi wa kweli wa Kristo.

Ubarikiwe.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine, na Bwana akubariki.

Monday, October 22, 2018


UTUKUFU WAKO UMEJAA, MBINGUNI NA DUNIANI...Ee BWANA NI NANI KAMA WEWE?, UMEUMBWA ULIMWENGU NA VIUMBE KWA NAMNA YA KUSHANGAZA, NA YA AJABU,UNASTAHILI KUABUDIWA, UNASTAHILI KUPEWA SIFA, HESHIMA NA UTUKUFU...NI WEWE PEKEE ULIYETOA UHAI WAKO KWA AJILI YETU. JINA LAKO LIHIMIDIWE MILELE NA MILELE AMINA



ITAMBUE KARAMA YA MUNGU.

Bwana Mungu wetu kaumba vitu vyote vya mwilini, kufunua vitu vya rohoni, aliumba milima, kufundisha kuwa kuna milima ya rohoni, aliumba maji kuonyesha kwamba kuna maji ya rohoni, aliruhusu mauti iwepo kufunua kwamba kuna mauti ya kiroho,aliruhusu vyakula viwepo ili kufunua kwamba kuna vyakula vya rohoni, kwasababu mwanadamu ameumbwa katika pande mbili, rohoni na mwilini. Na ndio maana alisema kwenye Neno lake “Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu (Mathayo 4:4)”.

Hivyo kama kuna mauti ya mwilini, ni wazi kuwa ipo pia mauti ya rohoni. Na kama vile, mauti ya mwilini ilivyo na nguvu leo, kiasi kwamba kila nafsi lazime ipitie, vivyo hivyo mauti ya rohoni ina nguvu ile ile ambayo inalazimisha kila kiumbe kife kwa namna ya roho. Na hii mauti ya rohoni iliingia pale Edeni, Adamu na Hawa walipoasi. Na kama tunavyojua leo hii hakuna dawa ya kifo cha mwilini, Kifo ni kifo tu! Vivyo hivyo na dawa ya Kifo cha rohoni haikuwepo mpaka njia ya mti wa uzima YESU KRISTO ALIPOFUNULIWA. Ndio tiba ya kifo ikapatikana vinginevyo hakungekuwa na uzima wa milele kwa kiumbe chochote kile.

Kwahiyo mara nyingi Bwana anapenda kutufundisha kwa kutumia mifano ya mwilini, kufunua vitu vya rohoni, kwamfano tunamwona yule mwanamke msamaria siku moja alipokwenda kisimani kuteka maji akakutana na Bwana, na Bwana akamwomba maji, na yule mwanamke alipotaka kuanza maandalizi ya kumpatia maji kutoka katika kisima kile, kwa kumuuliza baadhi ya maswali,Bwana alimkatisha palepale na kumwambia… “ kama ungaliijua KARAMA YA MUNGU, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, UNGALIMWOMBA YEYE, NAYE ANGALIKUPA MAJI YALIYO HAI (Yohana 4:10)”

Na palepale yule mwanamke alidhani Bwana anazungumzia habari za maji yale ya mwilini ya kwenye kwenye visima, akafurahi akatamani apewe yale maji. Tunaweza kuona mistari hiyo tuone jambo..

11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai. 12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? 13 YESU AKAJIBU, AKAMWAMBIA, KILA ANYWAYE MAJI HAYA ATAONA KIU TENA; 14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi HATAONA KIU MILELE; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, YAKIBUBUJIKIA UZIMA WA MILELE. 15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka”



Unaona hapo, Bwana anazidi kumtoa yule mwanamke Msamaria kwenye mawazo ya maji ya mwilini na kumpeleka kwenye mawazo ya maji ya rohoni, lakini bado alikuwa hajamwelewa. Alijaribu kutumia mfano wa maji ya mwilini ili kumwonyesha umuhimu wa maji ya rohoni lakini bado hakumwelewa vizuri mpaka baadaye kidogo. Alijaribu kumfunulia KARAMA YA MUNGU lakini bado ilimuwia ngumu kumuelewa kwa wakati ule kwasababu ya mapokeo ya kibinadamu aliyokuwa nayo. Bwana alichotaka kwa yule mwanamke ni KUTUBU, NA KUACHA DHAMBI ALIZOKUWA ANAZIFANYA, NA KUMGEUKIA MUNGU kwa moyo wake wote! Na kuishi maisha mapya yanayompendeza Mungu Hicho tu! ndio Bwana alichokuwa anatafuta kwa yule mwanamke. Hiyo ndiyo KARAMA YA MUNGU aliyokuwa anataka kumpa yule mwanamke…ili asife kwa kukosa maji ya uzima akaukosa uzima wa milele..Na ndio maana biblia inasema katika..

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; BALI KARAMA YA MUNGU ni UZIMA WA MILELE katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Na baada ya Bwana kumfunulia siri ya moyo wake kwamba anao waume watano na yule aliyenaye sasa si wake, ndipo alipotambua kwamba yeye ni mwenye dhambi, na kwamba Bwana alikuwa hazungumzii maji ya mwilini bali ya roho yake, yatakayompa uzima wa milele.

Tunaweza tukajifunza tena mfano mwingine katika maandiko wa Mtu aliyeielewa haraka KARAMA YA MUNGU pasipo Bwana kutumia nguvu nyingi kumfafanulia, na huyu si mwingine zaidi ya Petro. Wakati Fulani Bwana alimwendea Petro kwa mara ya kwanza kama alivyomwendea yule mwanamke Msamaria, akamkuta anaosha nyavu, kwasababu wamefanya kazi ya kuchosha usiku mzima bila kupata kitu, Na Petro alipomwona Bwana alidhani ni muhubiri tu wa kawaida, mwalimu wa torati kama walimu wengine, hivyo kwa heshima yake akaona bora amtii tu, Tunasoma hayo katika..

Luka 5: 4 “Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
 
5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. 
6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika; 
7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama. 
8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, ONDOKA KWANGU, KWA KUWA MIMI NI MTU MWENYE DHAMBI, BWANA.
9 Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata”;
Unaweza ukaona hapo, Petro baada ya kuiona ile ishara ya kupata samaki wengi namna ile, akatambua KARAMA YA MUNGU nyuma ya ile ishara, akatambua kuwa mtu aliyesimama mbele yake ni MKUU WA UZIMA, na yeye ni mtakatifu na hachangamani na uchafu, akaogopa akamwangukia chini akamwambia “ONDOKA KWANGU, KWA KUWA MIMI NI MTU MWENYE DHAMBI, BWANA” alitambua Bwana Yesu hakuja kumpa yeye VIKAPU VYA SAMAKI, hakumfanyia ile ishara ili kumfanya yeye kuwa milionea, bali aliifanya ile ishara ili kumwonyesha Petro kwamba yeye ni mwenye dhambi kiasi gani na kwamba anahitaji UZIMA WA MILELE. Bwana hakumfanyia ile ishara Petro kwasababu anavutiwa sana na ile kazi aliyokuwa anaifanya ya kuvua samaki, hapana alimfanyia Petro ile ishara kwasababu aliona dhambi ndani ya Petro na hakutaka Petro apotee, Na Petro alilitambua hilo akatubu mbele zake.


Na jambo hili hili linaendelea leo, Bwana Yesu anakutembelea kwenye mambo yako unayoyafanya, labda shughuli Fulani ya kujipatia kipato, au labda elimu, au mali, au afya…Inatokea umepitia au ulipitia hali Fulani ulikuwa unaugua sana na Bwana akakuponya kimiujiza, na ndani ya moyo wako ukashuhudiwa kuwa ungestahili kufa lakini umepona… Sasa huu si wakati wa kuanza kutazama mambo ya mwilini, kwamba sasa umepata afya ndio wakati wa kusaka fedha kwa nguvu uwe tajiri kwasababu Mungu kakunyanyua tena, au ukadhani kwamba Bwana alikuponya kwasababu alikuhurumia sana ulipokuwa unateseka na maumivu ya magonjwa yako,

Nataka nikwambie ndugu Bwana hakukuhurumia kwasababu ulikuwa unateseka na maumivu ya ugonjwa bali alikuhurumia akakuponya kwasababu alikuhurumia usije ukafa na dhambi ulizo nazo ndani yako na ukaingia kwenye lile ziwa la moto hivyo ni muhimu sana kuielewa KARAMA YA MUNGU juu maisha yako? Bwana alikuponya kimiujiza ili UKATUBU, ukaache uasherati, ukaache anasa, ukaache usengenyaji, ukaaache rushwa,ukaache kuishi na mume au mke ambaye hamjafunga ndoa, ukaache kuiba, ukaache pombe, alikuponya magonjwa ya zinaa ili ukaache uasherati na uzinzi n.k

Bwana hakukufanikisha kwenye kazi yako ya kujipatia kipato, kwasababu anataka sadaka au fungu la kumi kutoka kwako, au kwasababu alikuhurumia sana ulikuwa maskini kwa muda mrefu na ulikuwa unateseka hapana!! Bwana alikufanikisha kwenye shughuli zako kwasababu anaona maisha yako kuna sehemu pengine hayajakamilika mbele zake, anakufanyia ishara kubwa namna hiyo kama alivyomfanyia Petro, anataka UANGUKE CHINI utambue kwamba, Jicho la Mungu linakutazama kuliko unavyodhani, mambo yako na dhambi zako za siri anayoana kuliko unavyofikiri, ziko wazi mbele zake, anataka uone kwamba MTAKATIFU WA WATAKATIFU AMEKUSOGELEA, Anataka uone kwamba hatua moja mbele yako kasimama mtu asiyechangamana na dhambi. Na anataka akupatie uzima wa milele!

Biblia inasema mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa mbinguni, (Yohana 3:3). HIYO NDIYO KARAMA YA MUNGU KWAKO.

Bwana Azidi kukubariki sana

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine

Kwa Mpangilio mzuri wa mafundisho haya tembelea website yetu >>> www.wingulamashahidi.org

UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?

Jaribu kufikiria dikteta Adolf Hitler wa ujerumani Yule aliyesababisha vita ya pili ya dunia, na kuhusika kwa mauji ya mamilioni ya raia wasiokuwa na hatia ulimwenguni kote, mfano leo hii angekuwa hai, unadhani hatma ya maisha yake ingekuwa ni nini?, watu wa ulimwengu mzima wangetaka Yule mtu apewe adhabu gani?, Ni wazi kuwa kila mtu angetoa maoni ya adhabu yake ya kipekee ya mateso yasiyokuwa ya kawaida ambayo walau yangeweza kulipiza kisasi cha yale mabaya yote aliyowafanyia watu wasiokuwa na hatia, wale watu aliowachoma katika matarunu ya gesi na kuwaua kwa vifo vya kikatili na mateso na kusababisha vita ya pili ya dunia. Yeye naye angepewa adhabu mojawapo ya hizo watu wangeridhika kumuona analipa deni la alichokipanda.

Lakini pia jaribu kufikiria mfano amekamatwa na kwenda kuhifadhiwa mahali Fulani pa siri, kisha ukasikia baada ya siku chache kaachiwa huru, sasa ni raia wa kawaida kama raia mwingine ambaye hajafanya kosa lolote, na cha kushangaza zaidi sio tu kutokupewa adhabu yoyote bali hata MAHAKAMANI penyewe mahali ambapo ni pa haki hajapandishwa kushitakiwa. Badala yake kaachiwa yupo huru na anaendelea na maisha yake ya kawaida...

Kwa namna ya kawaida hilo ni jambo lisilokaa liwezekane, lakini kwa Mungu limewezekana..

Bwana Yesu anasema.. Yohana 5:24 "Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; WALA HAINGII HUKUMUNI, BALI AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI".




Ndugu yangu mimi na wewe nafsi zetu zinatushuhudia kabisa sio wakamilifu kwa asilimia zote, na kama sio wakamilifu mbele za Mungu amri ni moja tu, ni lazima tukahukumiwe adhabu kwa kutokukamilika mbele zake, Na biblia ipo wazi juu ya hilo, Lakini ashukuruwe Kristo alisema amwaminiye yeye, yuna uzima wa milele, WALA HAINGII HUKUMUNI, BALI AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI.

Ikiwa na maana kuwa siku ile Kristo atakaposimama kuyahukumu mataifa yote ulimwenguni katika kile kiti chake cheupe cha enzi wale wote waliomwamini yeye hawatakuwepo hapo, badala yake wao ndio watakaosimama na Kristo kuyahukumu mataifa yote.Tunasoma..
Ufunuo 20.11 "Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapon mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto".

Unaona hapo? Leo hii wewe ni mlevi,mtazamaji wa pornography, mfanyaji wa mustarbation, msengenyaji, mwizi, mzinzi, maisha yako hayana matumaini, unaishi kwa hofu, kila siku unahisi kuhukumiwa ndani ya nafsi yako, kuwa njia unayoiendea ni ya mauti, na unafahamu kabisa kuwa hata ukifa leo utahukumiwa tu na kwenda katika ziwa la moto, kwanini unaendelea kuyahatarisha maisha yako, kwa kuishi maisha ya namna hiyo ya kutokujali?, kwanini unaipuuzia neema hii ya kipekee ya kuvukishwa toka mautini mpaka uzimani? Neema ya kutokuingizwa hukumuni? Bwana anasema NJOO! KWANGU unywe maji ukate hiyo kiu..Lakini bado upo vuguvugu, unadhani kwa matendo yako utaweza kusimama mbele zake siku ile? hii neema haitadumu milele..Ni neema ambayo mwanadamu yoyote asingestahili kupewa.

Ni maombi yangu, tusitamani KUSIMAMA MBELE YA KITI CHEUPE CHA HUKUMU CHA MUNGU siku ile kwasababu tukishajikuta tu tumesimama pale, habari yetu imekwisha hatutakuwa na cha kujitetea, kwa njia yoyote makosa ni lazima tu yaonekana ndani yetu. Na baada ya hapo ni safari ya moja kwa moja kwenda katika lile ziwa la moto.

Tuipishe hukumu ya Mungu hakuna anayependa kupandishwa mahakamu hata kwa katika mahakama za kibinadamu tu hakuna anayenda kufikishwa kule, itakuwaji siku ile kukutana uso kwa uso wa Mungu mwenyewe katika mahakama? Ni jambo la kutisha sana, tusitamani tuwepo.

Tubu sasa maadamu muda upo, salimisha maisha yako kwa Kristo leo, kesho haipo, kabatizwa katika ubatizo sahihi baada ya kuamini kwako kama haujafanya hivyo haraka iwezekanavyo ili upate ondoleo la dhambi zako, na ubatizo sahihi ni ule wa kuzamishwa kwenye maji mengi na uwe ni kwa jina la YESU KRISTO ubatizo mwingine nje ya huo ni batili, Kisha Bwana atakupa Roho wake mtakatifu na hapo utakuwa UMESHAZALIWA MARA YA PILI..Na kama hizo hatua hazijakamilika ndani yako, hapo bado hujazaliwa mara ya pili. Bado hujavuka toka mautini kwenda uzimani, bado hujaikwepa hukumu...


Fanya bidii kumtafuta YESU siku hizi ni za hatari.

Ubarikiwe sana.


Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu, pia “LIKE” page hii uwe unapata machapisho mapya kila wakati.

Kwa mafundisho mengine mengi ya ziada tembelea website yetu >>> www.wingulamashahidi.org