"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Saturday, December 8, 2018

MWANA WA MUNGU.

Biblia inasema katika 
Waefeso 4: 13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, KRISTO.”
Hapo anasema NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, ikiwa na maana kuwa, kuna uwezekano tukamfahamu kidogo, hivyo inahitajika kumfahamu sana MWANA WA MUNGU (YESU KRISTO) Na kusudi lenyewe la kumfahamu sana Yesu Kristo, sababu zimeshatolewa hapo mbele nazo ni “ili tusiwe tena watoto wachanga tukichukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja,na kuzifuata njia za udanganyifu”.

Moja ya jukumu la muhimu sana kwa mkristo yoyote aliyezaliwa mara ya pili ni KUJIFUNZA KUMJUA YESU KRISTO NI NANI??...Kwa maana neno lenyewe Mkristo, limetokana na neno KRISTO yaani yeye aliyetiwa mafuta na Mungu, kwa hiyo kama Yesu ndiye Kristo moja kwa moja wafuasi wake wataitwa Wakristo. Taifa la Tanzania lina watu wake wanaoitwa watanzania, kadhalika na taifa la Marekani, watu wake wanajulikana kama wamarekani, vivyo hivyo Taifa la Yesu Kristo, watu wake wataitwa Wakristo..

Kwahiyo ni wajibu wetu na haki yetu kumjua Yesu Kristo kwa undani kuwa yeye ni nani? Katoka wapi? Je! Ni Mungu au ni mwanadamu wa kawaida tu? Anaokoaje okoaje watu!, alikuwa wapi kabla ya ulimwengu kuumbwa, yupo wapi sasahivi, na atakuwa wapi baadaye,? Na kama yupo ana mamlaka gani sasa na anafanya nini sasahivi, na atakuwa na mamlaka gani baadaye?, je! kuna umuhimu wowote kumfuata na kumwamini? Je! kuna sababu yoyote ya kujitumainisha kwake au la!? Kwanini afe? Na kisha azikwe na kisha afufuke? Je! kulikuwa na umuhimu wowote wa yeye kufanya hivyo? Na kwanini aondoke na asingeendelea kubaki duniani? Na kwanini apae kurudi alikotoka sababu kuu ya kufanya hivyo ni nini?..Kwanini alikuwa anajiita mwana wa Adamu, hilo neno mwana wa Adamu maana yake ni nini? na lina mahusiano gani kati yake na sisi? Kwanini anajiita yeye ni mwana wa Daudi? Ana uhusiano gani na Daudi? Na kwanini sehemu nyingine anasema yeye ndiye aliye na ufunguo wa Daudi? Huo ufunguo wa Daudi ndio upi? Na unafungua nini (Ufu 3:7)? …Na kwanini sehemu nyingine anajiita mwana wa Mungu,.. kwanini wanamwita simba wa Yuda kwanini sio simba wa mwituni?,… na kwanini anajiita yeye ni Jiwe kuu la pembeni?, hilo jiwe kuu la pembeni ndio kitu gani? Kwanini anajiita yeye ni mwana kondoo? na wala si ng’ombe?... Kwanini anajiita yeye ndiye ile nyota ya asubuhi,… Kwanini anasema yeye ndio njia na kweli na uzima? Mtu anawezaje kuwa njia?.... Kwanini anajiita shahidi mwaminifu? ….Kwanini anasema yeye ni mzaliwa wa kwanza wa waliokufa? Je! wafu wana wazaliwa wa kwanza na wa mwisho? Nk..nk…nk

Sasa kama huna majibu ya maswali hayo kwa angalau asilimia themanini (80%) na bado unasema wewe ni mkristo, unahudhuria kanisani na kuwa mshirika mwema…Basi jua kuwa HUMFAHAMU YESU KRISTO NI NANI. Na kwasababu hiyo basi utabakia kuwa mtoto mchanga na utachukuliwa na kila aina ya upepo wa Elimu unaokuja mbele yako, mtu Fulani akitokea akikwambia Yesu yuko hivi, utafuata tu! mwingine akitokea akikuambia yuko vile…utafuata tu! hata mganga wa kienyeji akivua hirizi zake na kuvaa suti na kuanza kukuhubiria habari za Yesu kwa jinsi anavyojua yeye, UTAMWAMINI TU! kwa kwasababu HUMJUI YESU KRISTO, Kwasababu wewe ni kama mshabiki wake tu YESU! sio mtu wa Taifa lake, hustahili kuitwa Mkristo, ni Mkristo jina tu!...


Swali maarufu na la kipekee Bwana Yesu alilowahi kuwauliza mitume wake ni hili “Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?”… Unaona swali hilo? Mitume hawakuwa na bahati mbaya sana kuulizwa hilo swali na Bwana Yesu, hata leo Roho Mtakatifu anakuuliza wewe unayesoma ujumbe huu moyoni mwako “Nawe wasema kuwa mwana wa Adamu ni nani?”…je! ni Bwana na mwokozi tu? au ni nani zaidi?..

Nataka nikwambie tu ndugu wa thamani? Unayesoma ujumbe huu…Tafuta sana kumjua Yesu Kristo kuliko kitu kingine chochote! Kuliko hata hizo mali unazozihangaikia, kwasababu uzima, mauti, tumaini, hatima, na mambo yote yanatoka kwake…Dunia yote sasahivi imewekwa chini yake, hakuna chochote kinachotokea kiwe kibaya au kizuri ambacho hajakiruhusu yeye?... Hakuna mtu yeyote ambayo anaweza kutenda jambo lolote liwe baya au zuri kabla yeye hajalipitisha..
Maombolezo 3: 37 “Ni nani asemaye neno nalo likafanyika, Ikiwa Bwana hakuliagiza?
38 Je! Katika kinywa chake Aliye juu Hayatoki maovu na mema?”
Unaona hapo? Bwana ndiye muhasisi wa kila kitu! Kwaufupi tu hatuwezi kumwelezea hapa jinsi alivyo lakini yeye ndiye aliyetiwa mafuta na Mungu mwenyewe, nyota iliyosahihi kabisa ya kufuata! Isiyoelekeza upotevuni.
Matokeo ya watu kuzombwa na mafundisho mengi ya uongo yaliyopo duniani sasa ni kutokana na kwamba watu hawamjui Yesu waliyempokea, kwasababu biblia inasema yupo yesu mwingine anayehubiriwa duniani.(2Wakoritho 11.4 Maana yeye ajaye akihubiri YESU MWINGINE ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!).

Tukiyajua hayo, tutakuwa makini na tutatia bidii kutaka kumjua YESU KRISTO mwokozi wetu kwa undani kila iitwapo leo ili tusimame upande ulio salama, vinginevyo hatuwezi kwepa kuchukuliwa na wimbi hili la upotevu lilipo duniani pasipo hata sisi kujua. Maana biblia inasema watawadanganya yamkini hata walio wateule.

Ni maombi yangu kuwa kuanzia leo,utamtafuta kumjua Huyu Yesu Kristo kwa undani wake?, uweza wake Kumbuka Biblia pia inamtaja yeye kuwa ni SIRI YA MUNGU, hivyo kama ni siri inahitajika bidii kuijua, hivyo basi tumepewa jukumu la kuzidi kumjua Yesu Kristo kwa undani kwa kadri siku zinavyozidi kwenda hata tutakapoufikia umoja wa Imani unaozungumziwa hapo..

Mungu akubariki.

No comments:

Post a Comment