"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Wednesday, March 6, 2019

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 56


SWALI 1: Ndugu zangu baada ya yule mwanamke Hawa kuvuka mpaka wa maagazo ya Bwana na kula lile tunda alilokatazwa asile:Baada Pale tunaona Bwana akimuadhibu kwa adhabu tofauti-tofauti" mojawapo ni kuzidishiwa uchungu wa kuzaa. Nataka kufahamu hii adhabu nyingine hapa anaambiwa"[TAMAA YAKO ITAKUWA KWA MUMEO.Mwanzo3:16]"-Ni tamaa Ipi hiyo Bwana Mungu aliyozungumzia hapo ndugu zangu?

JIBU: Kumbuka jambo la kwanza shetani alilolidadisi kwa mwanamke kwa muda mrefu na kuliona ndani yake ni TAMAA. Tamaa ya kuwa fulani, tamaa ya kuwa juu, tamaa ya kuwa juu ya vitu vyote, tamaa ya kutawala, tamaa ya kudiriki hata kutaka kuwa kama Mungu mwenyewe aliyemuumba..Na ndio maana nyoka alipokuja kumdanganya mwanamke hakumwambia maneno mengine yeyote labda utakuwa mzuri, au utapendwa zaidi au vinginevyo lakini badala yake alimwambia pindi utakapokula tunda utafumbuliwa macho na KUWA KAMA MUNGU!..

Unaona? “Kuwa kama Mungu”. Jambo hilo lilimfurahisha sana, pengine labda kwa kujiona yeye aliumbwa wa mwisho zaidi ya viumbe vingine vyote, halafu leo hii anasikia habari za kuwa kama Mungu lilimpa faraja sana..Lakini jambo hilo halikuwa ndani ya Adamu wakati wowote, japo yeye ndiye aliyeumbwa wa kwanza hakuwahi kutamani kuwa kitu fulani zaidi ya pale alipo, hakuwahi kuwa na tamaa ya kuwa juu ya kila kitu japo Mungu alimtawaza juu ya vyote, wala hakuwahi kumtawala mwanamke japo alitoka katika ubavu wake,.

Sasa mwanamke alipoasi tu, mambo yakageuka, Ndipo Mungu akamlaani na kumwambia “tamaa yako itakuwa kwa mumewe”..Hiyo tamaa ya kutaka kuwa juu, hiyo tamaa ya kutaka kuwa kichwa, ya kutaka kutawala sasa imehamishwa na kupelekwa kwa mumeo na matokeo yake, yeye ndiye atakayekutawala. Na ndio maana hayo mambo tunayaona sasa..wanaume wanatawala nyumba zao kwa nguvu, wanataka kujionyesha kuwa wao ni vichwa kati ya wake zao,wanawatiisha wanawake chini, wanataka waonekane kuwa wao ni watawala tu, wao wapo juu tu na wanawake wapo chini. jambo ambalo kiuhalisia halikupaswa kuonyeshwa kwa mwanaume yeyote yule, japo yeye ndiye aliyeumbwa wa kwanza. Umeona hiyo ndiyo laana iliyomkumba mwanamke.. na ndio maana mpaka leo jambo hilo ni Mwiba kwao, hususani kwa wanaume ambao hawajampa Bwana maisha yao, Lakini pia kumbuka Laana sio maagizo..Hatujaagizwa kuwatawala wanawake kwa mabavu katika maandiko.

Tunanapokuwa wakristo na kumpa Bwana maisha yetu, tunabadilika kutoka katika laana hiyo, na badala yake tunakuwa sio wa kuwaonyesha mabavu yetu kwa wanawake badala yake tunatumia mamlaka yetu KUWAPENDA na kuwajali na kuwatunza kama vile Kristo alivyoonyesha kielelezo kwa kanisa..

mwanaume anapaswa ampende mke wake, kwa Upendo wote...Lakini hilo haliwapi wanaume mamlaka ya kuwatawala wanawake kwa namna isiyopasa bali tuwapende na tusionyeshe tabia kama hizo katika ndoa zetu.

Waefeso 5:25 "Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake".

Unaona?. Kristo hatupigi sisi, Kristo hatutesi sisi, Kristo haonyeshi tabia ya kutokutujali sisi, au kutokutupenda sisi..Vivyo hivyo na wanaume wanaomcha Mungu wanapaswa waonyeshe tabia hizo hizo kwa wake zao.. Na wanawake pia wafahamu wasipojinyenyekeza na kujishusha na badala yake kutaka wao wawe vichwa katika nyumba, hawatawaki kuwatii waume zao, wafahamu kuwa laana hiyo haikwepeki juu yao..Watatawaliwa tu kwa mabavu, wapende au wasipende!!.


Nawe pia Ukiwa na swali lolote, tutumie tutakujibu na kukutimia kwa neema za Bwana.

SWALI 2: Je, kama hauna ubatizo sahihi hauwezi kuwa na Roho Mtakatifu?

JIBU: shalom! mtu wa Mungu, natumaini u mzima katika Bwana

Utendaji kazi wa Roho Mtakatifu ni kama ufuatavyo,

Mungu anapomchagua mtu aliye dhambini, huwa anamtumia Roho wake mtakatifu kumvuta mtu yule ndio hapo mtu huyo anaanza kusikia kuhukumiwa dhambi zake moyoni, na hatimaye anafikia toba, sasa huyo ni Roho Mtakatifu siku hizo zote anakuwa anamvuta mtu yule, anakuwa anatembea na yule mtu kama rafiki yake wa pembeni, lakini bado hajaingia ndani yake, ni kama mwanamume anapokuwa katika hatua za awali za kumchumbia mwanamke, anakuwa anaweza kuwa karibu naye, kumpa zawadi chache chache, kuzungumza naye maneno mazuri, kumwonyesha vitu vyake n.k, hayo yote mwanamume anayafanya ili tu kumvuta yule mwanamke, lakini bado yule mwanamke sio mali yake mpaka siku atakayoamua kumkubalia na kufunga naye ndoa, ndipo siku hiyo atakuwa milki halali ya yule mwanamume.

Na Roho Mtakatifu ndio hivyo hivyo, katika hatua za awali, Roho Mtakatifu anaweza akazungumza na mtu, wakati mwingine akampa hata maono,kumfanikisha katika mambo yake n,k lakini akawa bado hajaingia ndani yake, yote hayo Roho Mtakatifu anayafanya ili kuzidi kumshawishi kuielekea njia sahihi ya wokovu...…Na kama mtu yule bado atakuwa hajachukua hatua ya kumkaribisha ndani ya moyo wake kwa kutubu kabisa kwa kumaanisha kuacha dhambi zake na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, ataendelea kumshiwishi ndani yake mpaka siku atakapokubali..

Sasa siku yule mtu yule atakapoamua kubatizwa katika ubatizo sahihi, siku ile ile yule Roho Mtakatifu ambaye alikuwa anatembea naye anaingia ndani yake na kuwa milki halali ya Roho Mtakatifu mwenyewe, wanakuwa ni kama wamefunga ndoa na Roho Mtakatifu, kwasababu ubatizo ndio kibali cha Roho Mtakatifu kuingia ndani ya mtu, ni ishara ya dhambi za mtu kuondolewa kwa damu ya Yesu, na ni muhimu sana na ndio maana Bwana aliyaagiza, sasa baada ya hapo ndipo Roho Mtakatifu anakuja kufanya makao ndani ya yule mtu. Biblia inasema Roho Mtakatifu ndio Muhuri wa Mungu, kama unavyojua barua yoyote isiyokuwa na muhuri halisi hiyo ni batili. Roho Mtakatifu ni kama Pete ya ndoa kwa wanandoa.

Waefeso 4: 30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi”.

2Wakorintho 1: 22 “..naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu”.

Na akishaingia ndani ya yule mtu anaanza kupitishwa madarasa mengine ya kiroho zaidi, na huyo mtu shetani hawezi kumpata tena kwasababu ni kama kashakatiwa leseni mbinguni kuwa milki halali ya Roho mtakatifu,

Na pia maandiko yanasema katika ….Warumi 8:9 “……Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.”…kwa lugha nyepesi mtu yoyote ambaye hajafunga ndoa na Roho Mtakatifu kwa njia ya UBATIZO SAHIHI huyo sio wake, haijalishi Roho Mtakatifu anamwonyesha maono, anazungumza naye n.k bado huyo sio wake.

Mwingine atasema mbona wapo ambao wamebatizwa huo ubatizo sahihi lakini bado ni waovu? je! wewe unamkosoa Bwana wako aliyekupa hayo maagizo kwamba alichokisema hakina umuhimu sana katika kazi ya ukombozi?..Mbona husemi hivyo kwa mitume waliobatizwa kwa njia hiyo?..

Nakushauri usiwaangalie wanadamu kama ni kipimo cha wokovu wako, hujui mtu huyo aliuendea ubatizo kwa kidini tu, au kuwaridhisha wanadamu, au kwa faida zake mwenyewe..Lakini fahamu kuwa Ubatizo sahihi wafaa sana kwa wokovu wako mwenyewe.

Ubarikiwe.

No comments:

Post a Comment