"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Monday, October 21, 2019

BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU.

Zaburi 23:1 "Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.  2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.  
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.  4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji"

Mchungaji ni tofauti kidogo na Mchungaji…Mfugaji anawafuga Wanyama nyumbani labda kwenye Boma au zizini na anawaletea chakula nyumbani. Wanyama wanakuwa hawana uhuru wa kwenda kutembea huko na kule kuchagua wenyewe aina za nyasi na kuruka ruka.

Lakini Mchungaji, ni mfugaji ambaye Wanyama wake wapo huru kuachiwa huku na kule kula watakacho…lakini wapo katika Ulinzi wa Mchungaji!...

Na sisi mbele za Kristo ni kondoo tulio huru…Tupo huru kwenda huko na kule, tupo huru katuachia tukae katikati ya uovu wa huu ulimwengu, …lakini tupo chini ya Ulinzi wa Mchungaji wetu Mkuu Yesu Kristo.

Ijapokuwa tutakwenda huku na huko, ijapokuwa tutakuwa tupo huru kuruka ruka na kupata mwanga wa jua, lakini siku zote jicho lake linatutazama..Hivyo hatutaogopa!

Kwasababu Gongo lake na fimbo yake vya tufariji, Fimbo yake ni kwaajili ya kumpiga adui.

Bwana ndiye jabali letu na ngome yetu Tumwogope nani?



MASWALI YALIYOULIZWA:

No comments:

Post a Comment