"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Sunday, September 18, 2016

"MWONYE MCHUNGAJI WAKO"

Mtume Paulo alitoa ONYO kali kwa mtu yeyote ambaye angefundisha mafundisho mengine ambayo ni kinyume na mitume waliyoyafundisha, kama ilivyo katika wagalatia 1:6-9 ( ..lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe..)

Wahubiri wengi wametoka nje ya biblia na kufundisha mafundisho mengi ya uongo 2thimotheo 4:3 " maana utakuja wakati watakapo yakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli na kuzigeukia hadithi za uongo."

Mungu anatafuta wahubiri waaminifu ambao wako tayari hata kupoteza umaarufu wao, marafiki na hata pesa kwa ajili ya kuisimamia kweli ya neno la Mungu.pasipo hofu na kukemea kwa ujasiri uovu unaoendelea katika kanisa la Mungu
MTAHADHARISHE MCHUNGAJI WAKO!!!

Je! ni sahihi kukugeuza wewe kuwa chombo chake cha kujipatia kipato/ fedha.
Kwasababu maandiko yanasema karama za Mungu zinatolewa bure pasipo malipo. mathayo 10;1 &8 "Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo MMEPATA BURE TOENI BURE, msichukue dhahabu wala FEDHA, wala mapesa mishipini mwenu.
 Ni kinyume na Biblia kuuza UPAKO wa ROHO wa Mungu.kugeuza injili ya Mungu kuwa njia ya kujipatia kipato Mungu atawahukumu hao wote.MTAHADHARISHE MCHUNGAJI WAKO!!!

Wakumbushe viongozi wako wa kiroho na washirika wenzako kuwa Ni machukizo kwa kanisa, kuwaruhusu wanawake wao kujihusisha na mitindo (fashion) ,kwa mfano wa wanawake wa ulimwengu huu. kumb. 23:17-18, hesabu 25:1-5, kwenye kumb.22;5 inasema
"mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanaume asivae mavazi ya mwanamke kwa maana kila afanyae mambo hayo ni machukizo kwa Bwana Mungu wako".
Hayo yote ni mambo ya kidunia yasiyokuwa na manufaa yoyote kwa mwanamke wakikristo aliyetayari kwenda mbinguni.

MTAHADHARISHE MCHUNGAJI WAKO!!!

Ni machukizo kukusanya fedha za fungu la kumi, sadaka za viapo, kwa mtu yeyote aliyemuumini wa kanisa anayejihusisha na upatikanaji wa fedha haramu kama kupitia ukahaba, madawa ya kulevya, ufisadi, wizi n.k. Kwa mchungaji yeyote kuyajua hayo na kuyafumbia macho ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu. kumb.13:28 (USILETE UJIRA WA KAHABA WALA MSHAHARA WA MBWA KATIKA NYUMBA YA BWANA MUNGU WAKO...NI MACHUKIZO).

MTAHADHARISHE MCHUNGAJI WAKO!!! 

muulize si vyema kuwadanganya watu kwamba Mungu kamwambia tabaka fulani la watu kanisani walete kiasi fulani cha hela kwa ajili ya shughuli fulani ya kanisa kwa mfano: ujenzi wa jengo la kanisa, kiongozi kama huyu ni mwongo, Biblia inasema sadaka ni siri na mtu anatoa kwa jinsi Mungu alivyomjalia kuwa navyo. na sio kumshurutisha mtu kutoa kiwango fulani alichokipanga mchungaji. mambo kama haya ni dhambi kubwa mbele za Mungu. mathayo.6: 1-4, 2wakoritho9:7, kumbukumbu 16:16-17.

mkumbushe kiongozi wako wa kiroho kama anafanya mambo kama hayo! Na Ikiwa hataki kugeuka CHUKUA TAHADHARI.


MTAHADHARISHE MCHUNGAJI WAKO MWANAMKE!!!
Mchungaji mwanamke anafanya jambo ambalo hakuagizwa kulingana na biblia haijalishi ana upako namna gani ni kinyume na maandiko. Mtume Paulo aliweka utaratibu katika kanisa, akikemea na kukataza wanawake kuhubiri sababu imeandikwa katika 1timotheo 2:11 ( mwanamke na ajifunze katika utulivu akitii kwa kila namna, simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha wala kumtawala mwanamume bali awe katika utulivu kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza na Hawa baadaye, wala Adamu hakudanganywa ila mwanamke alidanganywa kabisa, akaingia katika hali ya kukosa" tunasoma pia katika 2korintho 14:34 " WANAWAKE NA WANYAMAZE KATIKA KANISA maana hawanaruhusa ya kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. nao wakitaka kujifunza neno lolote wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; MAANA NI AIBU WANAWAKE KUNENA KATIKA KANISA....mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo ya Bwana. lakini mtu akiwa mjinga na awe mjinga".
 Ofisi kuu tano ambazo zimenenwa na mtume Paulo katika waefeso 4:11-16 yaani MITUME, MANABII, WAALIMU, WACHUNGAJI, NA WAINJILISTI, hakuna hata moja inayomhusu mwanamke ikiwemo mashemasi na maaskofu kwani biblia inasema Askofu anapaswa kuwa mume wa mke mmoja haikusema mke wa mume mmoja. Mwanamke yeyote aliye mkristo hapaswi kumtawala mwanamume iwe kanisani au manyumbani, anatakiwa abaki katika utiifu akitii kwa kila jambo kama iwapasavyo wanawake wamchao Mungu.
wote tunaokolewa sawa chini ya damu ya Bwana Yesu Kristo lakini katika suala lolote la uongozi na utawala mwanamke hana sehemu yeyote katika jambo hilo.
muonyeshe hayo maandiko mchungaji wako mwanamke aache kufanya hivyo ni kinyume na maagizo ya Mungu!

MTAHADHARISHE MCHUNGAJI WAKO!!!
Ikumbukwe waebrania 13:4 kwamba hilo andiko linaishi hata sasa, kwamba kufanya uasherati, na kuzaa nje ya ndoa ni machukizo mbele za Bwana. hata kubusiana sio sawa angali bado hawajatangazwa kuwa mume na mke kanisani na mchungaji. na kama wamefanya hivyo inawapasa watubu wasijisifu kwa kufurahia dhambi yao  huku mchungaji kuona sawa. ndoa yeyote ni lazima ihalalishwe mbele za Bwana kwanza ndipo iwe halali nje ya hapo ni uasherati, na mchungaji anapaswa akemee.
wanawake hawapaswi kuvalia mavazi yanayo onyesha miili yao nusu nusu kama vimini, vesti, suruali,, hereni, kaptula, kuweka vishikishi kama kusuka nywele mitindo mitindo, na wakati wa ibada kutokufunika vichwa vyao. hayo yote ni machukizo.
mjulishe mchungaji wako ayafundishe hayo na kuliongoza kanisa kulingana na NENO linavyosema (BIBLIA).


MTAHADHARISHE MCHUNGAJI WAKO!!!
Muulize hivi vyeo vimetolewa wapi?? NABII MKUU!, mchungaji kiongozi, Baba askofu mkuu, nabii kiongozi, PAPA, Baba Mchungaji, mheshimiwa Nabii, BABA wa kiroho?  je! hivi vyeo havimpasi  Bwana Wetu YESU KRISTO?? sasa sisi tunavitolea wapi, Kristo anasema tusimuite mtu yeyote baba au rabi au kiongozi maana kiongozi wetu ni mmoja ndiye Kristo. Ni vema aulizwe kavitolea wapi hivi vyeo.
Mitume ambao walituletea injili ni mfano mzuri wa kuigwa tujifunze kwao kwa unyenyekevu wao waliojiitwa wao kuwa WATUMWA WA KRISTO, wasio na faida hivyo hivyo na BWANA wetu YESTU KRISTO aliye kiongozi wetu alijinyenyekeza ingawa alikuwa mkubwa kuliko wote.


MTAHADHARISHE MCHUNGAJI WAKO!!!
Mwonye mchungaji aache kuwafundisha watu kunena kwa lugha au kuona maono, hivi ni vipawa vya Mungu na Roho hutoa kwa jinsi apendavyo yeye na sio kama mchungaji apendavyo, sio wote waliojaliwa kipawa cha kunena kwa lugha au kuona maono 1wakorintho 12:1-11,.Paulo alionya kanisa liende katika utaratibu, watu wote wakinena kwa lugha akiingia mtu asiyeamini watu wote si wataonekana kama wamerukwa na akili na kanisa litajengwaje?..katika kanisa wako waliopewa karama ya maono, wengine unabii, wengine kunena kwa lugha, wengine ndoto, wengine neno la maarifa lakini sio wote watanena kwa lugha. mwonye mchungaji wako aache kuwafundisha watu wanene vitu wasivyovijua kwa akili zao wenyewe...na uthibitisho wa Roho mtakatifu sio kunena kwa lugha tu! mtu anaweza kunena kwa lugha na bado asiwe na Roho mtakatifu bali ni kubadilishwa kuwa kiumbe kipya kwa kuzaliwa mara ya pili.


MTAHADHARISHE MCHUNGAJI WAKO!!!
Kufungua vitalu(branches) na kanisa mama(headquarter) kutawala makanisa mengine madogodogo na kuwapangia miamala ya kuhubiri(lutrujia),na ratiba ya mafundisho ya mwaka mzima,kuwachagua viongozi kutoka katika kanisa mama na kuwatawanya katika makanisa madogomadogo na kukusanya pesa,sadaka na fungu la kumi na kuziwasilisha katika kanisa mama ni kinyume na maandiko,.
katika kanisa la Kwanza hatukuona mitume wakienda kufungua makanisa madogomadogo na kuchagua moja la kuwaongoza na kupeleka sadaka makao makuu..kazi ya uinjisti ikishakwisha kanisa dogo lililoanzishwa linapaswa liongozwe na Roho mtakatifu kama maandiko yanavyosema linapaswa kujitegemea katika uongozi kwa kupitia zile karama tano yaani mitume,manabii,waalimu,wainjilisti na wachungaji na sio kupokea maelekezo,mafundisho au miamala kutoka katika kanisa mama, na muamala wetu ni biblia tu.


MTAHADHARISHE MCHUNGAJI WAKO!!!
Muulize mchungaji wako ubatizo wa kunyunyuziwa na ubatizaji wa watoto wachanga upo wapi katika maandiko?, na kudai kwamba iwe maji ya kuzamishwa au ya  kunyunyuziwa haijalishi??..."HIVI NI KWELI HAIJALISHI??" Si vema  kwa mtu wa Mungu kusema hivyo kwani biblia inasema aaminiye na kubatizwa ataokoka na maana ya kubatizwa ni kuzikwa au kuzamishwa,..na kitendo cha kubatizwa (kuzamishwa) ni jambo muhimu kwa mkristo kwa ondoleo la dhambi zake.Kwahiyo kwa mtu anayebatizwa ubatizo kimakosa dhambi zake hazijaondolewa kulingana na matendo 2:38.."..tutendeje ndugu zetu.....tubuni mkabatizwa kila mmoja kwa JINA LAKE YESU KRISTO  mpate ONDOLEO LA DHAMBI ZENU nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu.." 

kwa mtu aliyebatizwa kinyume na maandiko haya anapaswa akabatizwe tena, kama Paulo alivyoagiza katika matendo 19:5, na ubatizo sahihi ni KWA JINA LAKE YESU KRISTO na sio kwa jina la Baba,na Mwana na Roho mtakatifu..kwa sababu baba,mwana na roho mtakatifu sio jina bali ni vyeo lakini Baba Mwana na Roho mtakatifu ni Yesu mwenyewe na ndio maana mitume sehemu zote walibatiza kwa jina la Yesu Kristo..na pia hakuna mahali popote kwenye maandiko mtu alibatizwa kwa jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu hayo ni mafundisho yasiyosahihi yalioanzishwa na kanisa mama roman katoliki katika baraza la Nikea mwaka 315AD.
soma mistari ifuatayo..matendo 2:38.,matendo 8:9-13,16...matendo 10:48..matendo 19:5
sehemu zote hizo mitume walibatiza kwa JINA LAKE YESU KRISTO na sio jina la BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU

Mkumbushe mambo hayo mchungaji wako kwa upendo naye atabadilika, na kwa kufanya hivyo nuru yako itakuwa imeangaza.

MUNGU AKUBARIKI
 MARANATHA!

No comments:

Post a Comment