UTUMWA/UHURU
1wakorintho 7:20-24" Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa. 21 Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia.
22 Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo.
23 Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu.
24 Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo. "
Kuna watu ambao wameitwa katika hali ya utumwa lakini sio utumwa ambao utaathiri imani yake kwa Mungu yaani utumwa wa kuwa chini ya mtu fulani mfano kujishughulisha na kazi za kidunia kama kuajiriwa ambazo zitahusisha muda mwingi wa huyo mtu kuitumikia kazi yake, hivyo basi kwa kuwa amekuwa mtumwa wa mtu mwingine basi mtu huyo amefanyika kuwa huru kwa Mungu(tunazungumzia katika kazi ya utumishi) kulingana na biblia, yaani mtu huyo hawezi kutumika kwa muda wote katika kazi ya Mungu(au kuwa mnadhiri wa Mungu) biblia inasema mtu hawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja mathayo 6:24, " Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. "...Kwahiyo wakristo kama hawa hawawezi wakawa watumwa wa Kristo lakini Mungu atawabariki katika huduma nyingine za mwilini kama za utoaji n.k katika utakatifu wote ( ukisoma 2wakorintho 9:11"mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu; ",..pia soma 1timotheo 6:17-19),
Na pia watu hawa wanao uwezo wa kuhudumu katika kazi nyingine za kanisa kwa jinsi Mungu atakavyowajalia kwa karama zote za rohoni kama miujiza,uponyaji, neno la maarifa,unabii kunena kwa lugha,au wakawa mashemasi n.k lakini zile huduma tano kuu kama tukisoma katika waefeso 4:11-16 " Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; " hizi huduma kuu tano ni ofisi za Mungu, kwahiyo zinahitaji muda wote wa uangalizi wa watakatifu, na Mungu anazitumia kwa jinsi apendavyo yeye, Hawa wameitwa katika hali ya utumwa kwa Mungu kwa hiyo ni lazima wawe huru na mambo mengine yote ya ulimwengu mfano shughuli za ulimwengu huu zinazoweza kumtinga mtu na kuathiri kazi ya huduma.
Na hawa hawatakiwi kujiingiza katika shughuli yoyote ambayo itawachukulia muda wao wote mbali na Mungu, hawa ni watiwa mafuta wa Bwana kazi yao ni moja tu kuifanya kazi ya Mungu na sio kitu kingine. Mungu pekee ndiye anayejua jinsi ya kuwalisha na kuwavisha na ndio maana mahali pengine Mungu ameruhusu kwasehemu wapate fungu lao kutoka katika vitu vya madhabahu na pia Mungu ana njia nyingine mbali na hizo za kuwahudumia hao watu, kama vile hakuna mwajiri yeyote asiyemlipa mfanyakazi wake, vivyo hivyo na kwa Mungu hatazidi sana kuwajali watendakazi wake? 1wakorintho 9:12-14 "Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili. ".
Kwa ufupi neno hili Bwana aliwaambia mapema wanafunzi wake kuwa mtu hawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, kwamfano mtu hawezi kuajiriwa katika ofisi mbili tofauti na zote mbili akatumika asubuhi mpaka jioni, lazima moja ya hizo iwe ni ya part time tu! au aamue kufanya moja na aache nyingine, ni dhahiri kabisa inajulikana hivi kuwa hakuna manager yeyote anayeweza kumuajiri mtu anayetumika na shirika lingine full time mbali na lake, na vivyo hivyo kwa Mungu.
Kwahiyo biblia inasema 1 wakorintho7:20-23 "Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa. Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia. ". .kwahiyo kama umeitwa katika hali ya utumwa usione ni vibaya kuwa mwaminifu na muhubiri Kristo katika hali uliyoko, tenda wema,ukristo wako ujulikane na watu wote wanaokuzunguka ili watazamapo mwenendo wako wengi waokolewe katika wewe,biblia inazungumzia 1 timotheo 6:1-2,waefeso 6:5-8," Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo; 6 wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;
7 kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;
8 mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru. "
kumbuka maneno haya Paulo alikuwa anawaandikia wakristo na sio watu wa mataifa.
pia Mungu anaweza akakutumia kuhudumu katika kanisa kwa karama ya Roho aliyoiweka ndani yako kwamfano uimbaji, utoaji,ushemasi na kwa namna nyingine yeyote ambayo unaweza ukaona unawito wa kufanya katika kanisa lakini sio huduma yoyote ya uongozi katika kanisa kama kuwa mchungaji, mwalimu, nabii, muinjilisti,mitume hizi hazijishikishi na mambo mengine yoyote nje na kazi za kanisa. Ni ofisi za Mungu katika kanisa. kwahiyo kama ukitaka kuwa na mojawapo ya huduma hizo ni lazima ujitoe kikamilifu, ni lazima uachane na moja ushikamane na lingine, hauwezi ukatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.
WITO WA MTU BINAFSI
Kuoa/ kutokuoa
Mungu pia anaweza akamwita mtu katika hali ya kuoa au kutokuoa, wahubiri wengi wanafundisha kuwa ni lazima watu wote waoe au kuolewa, lakini wanasahau pia kufundisha kuwa Mungu ana wito tofauti tofauti kwa watu tofauti tofauti, wako walioitwa waoe na pia wapo walioitwa kutokuoa au kutokuolewa. BWANA YESU KRISTO alisema mathayo 19:10-12."Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa. Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee. "
..Katika agano la kale matowashi walikuwa ni watu walioasiwa kwa ajili ya kazi ya Mungu (aidha kazaliwa hivyo,au kaasiwa na watu wake au kaamua kujiasi mwenyewe kwa ajili ya Mungu) lakini katika agano jipya jambo hili linaweza likawa kwa mtu yeyote aliyeasiwa au ambaye hajaasiwa lakini anaweza akayaweza mapenzi yake( kujizuia na tamaa)..hivyo mtu wa namna hii haoi wala haolewi kajiweka mwenyewe wakfu au mnadhiri kwa Bwana..mfano wa watu hawa tunaye Bwana wetu YESU KRISTO, Mtume Paulo,Yohana mbatizaji n.k
Hapa tunaona Bwana Yesu alisema sio wote wawezao kulipokea hilo neno la kutokuoa ila wale tu waliojaliwa, Bwana alisema 'awezaye kulipokea neno hilo na alipokee'
Pia Mtume Paulo alisema katika 1 wakorintho 7:1,8,32-35(1 Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke......8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.....32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana; 33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.
34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine. )
.Hivyo tunaona Mtume Paulo anashauri kuwa kutokuoa au kutokuolewa ni vizuri zaidi kwa sababu mtu kama huyo atajishughulisha zaidi na mambo ya Mungu zaidi ya Mtu aliyeoa au kuolewa.Lakini pia sio vibaya au dhambi mtu kuoa au kuolewa, wala mtu hapaswi kulazimishwa kutokuoa wala kutokuolewa, Mtume Paulo alisema kuwa kila mtu ana karama yake jinsi alivyoitwa, lakini tunaona jinsi vile Bwana YESU KRISTO, Mtume Paulo,Eliya,Yohana Mbatizaji hawakuoa na tunaona matunda makubwa waliyotoa ya kazi zao, Mtume Paulo hakupata nafasi ya kutembea na Kristo kama Mitume wengine lakini yeye ndiye aliyefanya kazi kubwa kushinda mitume wengine wote.
Kwahiyo ndugu kama ukiwa na wito ndani yako wa kutokuoa au kutokuolewa, na unajiona kupata amani kuhusu jambo hilo, na unaweza ukajizuia, na unatamani kumtumikia Mungu katika hali hiyo usimzimishe Roho,hiyo ni kazi ya Roho wa Mungu ndani yako kuwa mwaminifu tu, inawezekana hiyo karama Mungu ameiweka ndani yako. Na hii ni kama tu unaona amani na unaona uko huru zaidi kuliko kuoa/kuolewa sasa huo ndio wakati wa kupeleka mapenzi yako yote kwa Mungu (Bwana YESU awe mpenzi wako) naye Bwana siku zote ni mwaminifu atakutunza. Kumbuka hiyo inakuwa kama nadhiri kwahiyo usiwe mtu wa kusitasita leo huku kesho kule kuwa na uhakika na maamuzi unayoyafanya naye Bwana atazidi kukuimarisha kidogo kidogo nawe utakuwa imara katika jambo hilo. Wito wa namna hii ni kwa mtu binafsi na ni kama moja ya nadhiri ya hiari mbele za Bwana, na ina thawabu kubwa sana,
Isaya 56:3-5 "Wala mgeni, aambatanaye na Bwana, asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu. 4 Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu;
5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. "
Hapa tunaona Bwana amewaahidia watu wa namna hii(matowashi) kuwa atawapa jina lililo jema lidumulo milele,zaidi ya kuwa na wana na binti.
kumbuka maaskofu(wachungaji) na mashemasi kama wakitaka kuwa na wake wanapaswa wawe na mke mmoja kulingana na kazi ya huduma walizoitiwa za uangalizi wa makanisa, hivyo ni lazima waonyeshe vielelezo kwanza kwenye familia zao, kisha ndio waje kulichunga kanisa. lakini pia kama wanaweza kujizuia wasioe ni vizuri zaidi kwa ajili ya kazi ya Bwana.

Kwahiyo ndugu mkristo ukitaka kuwa na huduma yeyote katika ofisi kuu za Mungu kama vile uchungaji, uinjilisti, ualimu, utume, na unabii fahamu tu ni lazima ujitoe kikamilifu na ndio maana Bwana Yesu alisema hauwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja..tusijidanganye kama hatuwezi kuwatumikia mabosi wawili wa kiduniani kwa wakati mmoja, si zaidi Mungu wetu aliye mkuu kushinda Bosi yeyote duniani na aliye na ofisi kuu kushinda ofisi yoyote duniani na bado tunataka kuigeuza kazi yake kuwa part time,
Hauwezi ukawa ni mchungaji -- na bado ukawa mbunge
Hauwezi ukawa ni mchungaji---na bado ukawa mwana siasa
Hauwezi ukawa ni mchungaji---na bado unajihusisha na harambee za kijamii
Hauwezi ukawa ni mchungaji---na bado ukawa mtu wa kupenda pesa
Kuwa mtumwa wa Kristo ni kuwa huru na shughuli za ulimwengu na kuwa mtumwa wa shughuli za ulimwengu ni kuwa huru wa Kristo..".Lakini Paulo alisema kama unaweza ukawa huru ni afadhali kuutumia huo uhuru, TUMENUNULIWA KWA THAMANI TUSIWE WATUMWA WA WANADAMU".
Jiangalie ni utumishi wa namna gani wewe uliopo?..
Mungu akubariki!