"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Saturday, October 22, 2016

CHAPA YA MNYAMA

Ndugu William Branham alifundisha sana, kuhusu chapa ya mnyama, alisema kuwa kuipokea chapa ya mnyama ni kuukataa muhuri wa Mungu ambao ni Roho Mtakatifu, alisema kuna pande mbili tu, upande wa Mungu na upande wa shetani, hivyo ukikosa kuwa na Roho wa Mungu, maana yake ni una roho ya shetani nayo ndiyo chapa ya mnyama.

Kwahiyo roho ya mpinga kristo ambayo ndani yake imebeba chapa ya mnyama iliyozungumziwa kwenye kitabu cha ufunuo 17:1-6 tusome..


 " Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; 2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu".


Habari hii inamwonyesha mwanamke aliyeketi juu ya mnyama mwekundu sana, na juu ya paji la uso wake, alikuwa na jina limeandikwa la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA, NA MACHUKIZO YA NCHI, 

Sasa huyu mwanamke anayezungumziwa katika sura hii, ni KANISA fulani kwasababu mwanamke siku zote katika biblia anawakilisha kanisa, na pia mwanamke huyu tunaona anaitwa MAMA WA MAKAHABA, Hii ikiwa na maana kwamba ni kanisa-kahaba mama, na ikiwa ni "mama" basi ana "MABINTI", na hao mabinti ni makahaba kama mama yao  alivyo. Kwahiyo kahaba ni mwanamke anayezini na wanaume wengi mbali na mume wake. Na tunaona kuwa kanisa pekee lililofanya uasherati kwa kuchanganya mafundisho ya Mungu na mafundisho ya kipagani ni kanisa Katoliki, Hivyo basi yule mama wa makahaba aliyezungumziwa pale ni kanisa Katoliki, Na wale mabinti ni madhehebu mengine yote ya dini yaliyobakia, yaliyoacha uongozi wa Roho Mtakatifu na kuiga desturi zile zile za kipagani kama za mama yao kahaba yaani kanisa katoliki. Na sasa hivi tunaona madhehebu yote ulimwenguni na dini zote ulimwenguni zinaungana, pamoja na mama yao mkuu kahaba katoliki (ecumenical council) na KUIUNDA ILE CHAPA YA MNYAMA.

CHAPA YA MNYAMA INATENDA KAZI KWA NAMNA MBILI:
Chapa ya mnyama ipo rohoni na mwilini, (nje na ndani). kwa NDANI ni kama hauna Roho Mtakatifu, umeshaipokea ile chapa ya mnyama, kwahiyo ndugu tafuta kuwa na Roho wa Mungu angali muda upo, maana biblia inasema huo ndio muhuri wa Mungu, (soma waefeso 4:30). Na pia kuipokea chapa ya mnyama kwa NJE ni kama upo au umejiunganisha au umejifunga  na mifumo yote ya madhehebu ambayo yameuacha uongozi wa Roho Mtakatifu, na kuweka mifumo ya kipagani, pamoja na taratibu za kibinadamu na desturi zisizoendana na NENO la Mungu. hivyo kuipokea chapa ya mnyama ni kujishona na madhehebu na kuwa na utambulisho mwingine wowote nje ya UKRISTO mfano, kujitambulisha kama mlutheri, mwanglikana, msabato,mbaptisti, mkatoliki, mbranhamite n.k. badala ya kujitambulisha kama MKRISTO. (kumbuka maana ya haya majina sio mbaya, lakini madhehebu ambayo yamebeba hayo majina yana ile chapa ya mnyama ndani yake kwasababu yameshafanya uasherati kama wa mama yao katoliki, na Mungu ameyakataa soma ufunuo 3:1 " ...Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. ")  kwahiyo kwa kujiita tu hivyo tayari umeshakwisha kubaliana na ile chapa bila ya wewe mwenyewe kujijua. Fikiria tu hili kama sisi sote ni WAKRISTO huo utambulisho mwingine unatoka wapi?. Ujue tu unatoka kwa mpinga kristo ambao mwisho wake unapelekea kuiunda ile alama ya mnyama. Na nguvu ya hii chapa itakuja kujidhihirisha sana katika kipindi cha dhiki kuu, baada ya kanisa (bikira safi)  kunyakuliwa.

Kwahiyo hii chapa ya mnyama kwasasa ipo sana katika roho na watu wanaendelea kuipokea kwa kukosa Roho Mtakatifu, lakini kwa nje, ipo wanakubaliana nayo ila itakuja kutenda kazi kwa Nguvu katika kipindi cha dhiki kuu. pale mpingakristo atakaponyanyuka na kupewa mamlaka juu ya ulimwengu mzima, na huyu mpinga kristo atakuwa sio mwingine zaidi ya Papa kiongozi wa kanisa katoliki wa Roma. Sio kwamba wakatoliki ni watu wabaya, Hapana ni watu wazuri wote bali ni vizuri kujua roho inayoliendesha kanisa katoliki ni roho ya mpinga kristo na haitokani na Mungu, Hivyo watu wa Mungu lazima waujue ukweli watoke huko.

Tunaweza tukaona leo hii, mambo  mengi ya ajabu, yakitokea ulimwenguni ikiwemo vitendo vya kigaidi vikizidi  kukithiri, amani inazidi kutoweka duniani,watu wanaishi kwa hofu za machafuko na vita, siasa na umoja wa mataifa umeshindwa kuihifadhi amani ya dunia, dunia inatafuta suluhisho la mambo hayo na bado haijapata, hivyo anatafutwa kiongozi atakayeonekana ana uwezo wa kurejesha amani duniani  naye atakuwa si mwingine zaidi ya PAPA ili maandiko yatimie. Kama tunavyomwona leo hii anajulikana ulimwenguni kote kama mtu wa amani(MAN OF PEACE). Hivi karibuni tunaweza tukaona jinsi kiongozi huyu wa kanisa Katoliki (papa Francis), akirejesha mahusiano kati ya Marekani na Cuba, ambayo yalikuwa yamevunjika kwa muda mrefu. Leo analeta dini zote ulimwenguni pamoja, anakubalika na kuheshimika na watu wote, Ni kiongozi mwenye ufuasi mkubwa wa watu kushinda kiongozi yeyote ulimwenguni.
                                      (papa akiwa na viongozi wa dini mbalimbali duniani)

Kwahiyo katika kipindi cha ile dhiki kuu, atakuja na wazo la kukomesha ugaidi na vitendo viovu duniani akitaka watu wote, wasajiliwe kulingana na madhehebu yao na mashirika yao ya dini, kwasababu vitendo vinavyosababisha amani kutoweka vinasababishwa na dini na ndivyo ilivyo. kwahiyo ni lazima tatizo litatuliwe kwa namna ya KIDINI na si vinginevyo. Hivyo itahitaji kiongozi wa kidini na hakuna mwingine anayekidhi hivi vigezo zaidi ya Papa kiongozi wa kanisa katoliki.

 Leo hii duniani vita vya kidini vimeiweka dunia katika mtazamo mpya, mfano mabomu ya kujitoa muhanga, na vikundi vya kigaidi, kama ISIS, Alqaeeda, Alshabaab, Boko haram Anti-balaka, LRA n.k.vimekuwa ni tatizo sugu kwa dunia nzima, ni mada iliyopo mezani kila siku sio kwa mataifa maskini wala matajiri wote wamevamiwa na tatizo hili .Hivyo kiongozi huyu atapewa nguvu kwa kujipendekeza (danieli 11:21), Jambo hili  litatimiza ule unabii wa Daniel 9:27 "Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja;..... " Agano hili la amani litafurahiwa na dunia nzima, kwani litadhaniwa kuwa litaleta amani duniani, 

Hapo ndipo utakapowekwa utaratibu mpya wa ulimwengu (NEW WORLD ORDER). chini ya uongozi wa papa (mpinga kristo)  baada ya kupewa nguvu na mataifa yote duniani kumbuka hatajiita mpingakristo wala hatakuwa na uso wa shetani, wala usidanganyike kama atakuwa freemason au illuminati, au kikundi chochote cha kichawi hapana bali ATATOKEA NDANI YA KANISA ni mtu anayekubalika na watu, anaonekana mpenda amani, anapenda dini, anajali watu wote wa dini zote, anabusu watoto na zaidi ya yote ataonekana ni mnyenyekevu kuliko watu wote duniani, lakini ndani yake ni SHETANI katika utendaji kazi wake. Biblia inasema "Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ufunuo17:8"

 Kumbuka shetani ananyanyua sasa hivi kwa kasi vikundi vya kuvunja amani na ugaidi duniani kama mbinu yake ya sasa ya kutafuta kuwaangamiza wakristo, kama alivyofanya kwa wakristo katika kanisa la kwanza kwenye utawala ule ule wa KIRUMI chini ya Nero (AD 64),ambapo wakristo wengi waliuawa baada ya kusingiziwa kuwa wameuchoma mji, na ANGALI sio wao waliofanya hivyo. Na kwa njia kama hiyo hiyo shetani anawatafuta wakristo leo hii awaangamize, kwa vitu vya KUSINGIZIWA, maana anajua hakuna namna yeyote mkristo anaweza akashitakiwa na kuuawa kwa makosa yeyote ya kihalifu kwasababu wakristo sikuzote wanaishi maisha ya haki. Hivyo sasa hivi ameunyanyua ugaidi katika uislamu na vikundi vingine kama anti-balaka, ISIS, alshabaab,Boko Haramu, Al-qaeda, Hizbolah,Ku klax klan, pamoja na vikundi vyote vya siri vinavyouchafua ulimwengu, ili baadaye aweze kuwasingizia wakristo kwa urahisi kuwa wao ndio magaidi na kuwaangamiza wote).


                             (wakristo wasingiziwa kuuchoma mji, kusababisha wapitie dhiki kubwa ya                                                kuuawa  kikatili dhidi yao chini ya utawala wa Nero AD 64)
      
Hivyo basi utaratibu huo mpya utakapokuja watu wote watapaswa wahakikiwe taarifa zao muhimu zinazohusiana na DINI ZAO, itahusisha pia na kazi mtu anayofanya, kwenye makampuni, na mashirika. Kila mmoja ni lazima atambuliwe yeye ni dhehebu gani au dini  gani katika shughuli anayoifanya kwa dhumuni la kuwapata watu wachafuaji wa amani duniani, kwamfano waislamu wenye itikadi kali, wanaojihusisha na vikundi vya kigaidi, pamoja na vikundi vya kihalifu vinavyohusisha vita vya kidini na mauaji ya kikatili ya watu watambulike na kukamatwa. Lakini nia ya shetani itakuwa sio kuleta amani wala kuwalenga waislamu au makundi mengine  BALI NI KUWALENGA WAKRISTO,  (kama ilivyotokea kwenye utawala wa NERO,)

Lakini wale ambao hawatakubaliana kujiunga na huo mfumo wa yule mnyama ambao ni MUUNGANIKO WA MADHEHEBU NA DINI ZOTE. Mtu huyo hataweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa asipokuwa na huo utambulisho, Hataruhusiwa kuabudu kwenye kanisa ambalo halijasajiliwa na muungano wa madhehebu, ndugu Branham alitabiri akasema itafika wakati haya makanisa tuliyonayo sasa yatafungwa yote.kwahiyo huu usajili utaanza karibu duniani kote, katika kila nyanja na kila taasisi, kwa waajiriwa na wasio waajiriwa, katika vitambulisho vya taifa,kura na serikalini na taasisi binafsi kama mabenki, ATM cards, VISA n.k. na sehemu nyingine zitatumika MICRO-CHIPS sana sana kwa mataifa yaliyoendelea.

 Itakuwa ni sheria kila raia lazima ahakiki taarifa zake za kidini, na huo mfumo mpya. watu wengi wataukubali na kuupenda na kuhakiki taarifa zao pasipo kujua kuwa ndio wanaipokea ile chapa ya mnyama, na mfumo huo utafanikiwa kukamata wahalifu wengi.Ni wazi kuwa itakuwa ni ngumu kwa mtu kufanya biashara yeyote ya kuuza wala kununua wala kuajiriwa usipokuwa na huo utambulisho wa kidini. kwahiyo ukishahakikiwa taarifa zako utakuwa huru kufanya shughuli yako yoyote unayotaka.lakini sio kujiita MKRISTO tu! haitafanya kazi tena kipindi hicho, huko kutakuwa ni kuonyesha tu ID au CHIP ambayo imebeba taarifa zako zilizohakikiwa na huo mfumo mpya wa mpingakristo,

 Tazama mwenyewe video hii hapa chini, Papa akizungumza juu ya jambo hili ya kwamba kuwa mkristo ni lazima uwe mshirika wa kanisa fulani (dhehebu)..je! Ni nyakati gani hii tunaishi??




Lakini wale wakristo watakaokuwepo watamtambua yule mpingakristo na chapa yake, watakataa kuupokea huo utambulisho na usajili wake (chapa ya mnyama). Sasa hao ndio watakaotafutwa na kuitwa magaidi, na hao tu ndio watakaopitia dhiki kuu wakati dunia inaendelea kufurahi. Na hawa hawatauliwa ovyo ovyo tu, kama inavyodhaniwa. bali watachukuliwa na serikali,(maana serikali itawatambua kama wahalifu na sio raia wa kawaida kwa maana serikali itashirikiana na mpingakristo kufanya kazi). Maana hawatakuwa wengi, na watapelekwa kwenye magereza maalumu ya mateso ya siri (concentration camps), huko ndiko kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea wala haitakaa itokee kama Bwana YESU KRISTO alivyosema. 

Wakristo wengi watateswa kama magaidi, watasingiziwa wao ndio wanaoharibu amani ya dunia kama sivyo kwanini wakatae kusajiliwa, lazima kuna mambo ya siri wanayo. watakataliwa na jamii nzima, hata ndugu za hao jamaa hawatawaelewa.Hapo ndipo ndugu atamsaliti ndugu ili auawe, Tunaona kama vile wayahudi walivyofanyiwa na Adolf Hitler katika vita ya pili ya dunia kwenye zile concentration camps. watu jinsi walivyokuwa wakiuliwa kikatili na mateso makali yasiyoelezeka ndivyo itakavyokuwa tena na zaidi ya hapo katika wakati wa dhiki kuu kwa wakristo , mpinga kristo atawaua wote, (Na dhiki hii kuu itawahusisha na wayahudi pia) na itadumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu ya mwisho wa lile juma la 70 la Danieli. Na kwa mataifa yote yaliyobaki ambayo yamepokea ile chapa (yaani kwa kuukubali mfumo na utambulisho wa yule mnyama katika vitambulisho vyao na ID, na CHIP zao na vyeti vyao). wataingia katika ile siku ya KUOGOFYA ya BWANA ambayo itaanza mara tu baada ya ile miaka mitatu na nusu kuisha (baada ya dhiki kuisha),hapo ndipo hukumu ya mataifa itakapoanza.
                                    (wayahudi katika mateso kipindi cha utawala wa Hitler)


USHUHUDA WETU:
kuna ushuhuda tungependa kukushirikisha kwa uhakika zaidi na uhalisia wa hili jambo.
Sisi wawili mwezi wa 4 mwaka 2015...Tulipokuwa tunaishi kule kigamboni,  tulikuwa na rafiki yetu muislamu alikuwa yupo na mpenzi wake ambaye ni mkristo wanaishi pamoja, siku moja ya mkesha wa pasaka, walituomba tuwasindikize kanisani kwenye mkesha wa maigizo ya pasaka. Hilo kanisa lilikuwa ni kanisa kubwa maarufu la katoliki. kwa kuwa ilikuwa ni usiku, hawakujua shortcut ya kufika pale kwahiyo walituomba sisi tuwapeleke kwasababu sisi tu ndio tulikuwa tunaifahamu shortcut ya kufika pale. Basi tulienda tukawafikisha hadi getini tukawaingiza ndani, wakati sisi tumeachana nao tunatoka nje getini. Walinzi wa geti wakatusimamisha wakaanza kutuhoji, kwanini mnaondoka kabla ya ibada kuisha, sisi tukawaelezea tumewaleta tu ndugu zetu na kuondoka.hatujaja kwenye ibada. kulikuwa na mmoja ambaye ni kiongozi wa kanisa lile mahali pale akaja karibu, akatuuliza nyie ni dhehebu gani? ..Tukamwambia sisi hatuna dhehebu sisi ni wakristo. kitendo cha sisi kusema tu vile, tuliwasha moto, wakaitana wengine, wakaanza kutushambulia kwa maneno mengi, nikizungumza yote hapa muda hautatosha. tulikuwa tunajaribu kuwajibu kulingana na NENO kuwa ukristo sio madhehebu, bali ni kuamwamini YESU KRISTO. Lakini jinsi tulivyozidi kuwaeleza ndivyo walivyozidi kutushambulia na kutukasirikia. kulikuwa na vijana wengine pale, wakawaachia wote wapate nafasi ya kutugeukia sisi.Walikuwa hawana nia nyingine bali kusikia kutoka katika vinywa vyetu sisi ni madhehebu gani lakini tulipokataa kufunua madhehebu bali ukristo ndipo vita vilipoanza, saa hiyo hiyo tulipigwa pingu. tukakalishwa chini, defender ya polisi ikaitwa, simu ilipigwa kituoni wakisema tumewakamata ma-alshababu, tukafikishwa kituoni, tukapigwa na makuni, tukasingiziwa kwanini tumeiba,wakatutupa ndani gerezani, wafungwa kule, walidhani sisi ni magaidi wa ajabu kwajinsi tulivyokuwa tunapigwa, ile alfajiri walitudekisha lile gereza,.Lakini Mungu alitupa neema asubuhi alfajiri sana tukatoka kule, hiyo siku tukio hilo lilipotokea ilikuwa ni siku ya kupatwa kwa mwezi, (maarufu kama bloodmoon duniani), hiyo ilikuwa ni uthibitisho wa somo Mungu alilotufundisha. Lakini kwanini tulifikia mpaka huku magerezani na kupigwa? jibu ni dhahiri ni kwasababu tuliukiri UKRISTO na sio madhehebu, shetani hapendi kuona mtu anaukiri UKRISTO anatamani uendelee hivyo hivyo kujitambulisha kwa madhehebu yako ili iwe rahisi kwako baadaye kuipokea ile CHAPA YA MNYAMA.

Kwahiyo Baada ya tukio hilo ndipo Mungu alituthibitishia hili somo. jinsi wakristo watakavyokuja kupitia katika dhiki ile kuu. Kanisa Katoliki ndio linaloongoza kwa kuwaua na kutesa wakristo wengi, na inakadiriwa kuua zaidi ya wakristo milioni 68 katika historia ya kanisa. Na ndivyo linavyofanya hata sasa kwa siri na litakavyokuja kufanya katika kile kipindi cha dhiki kuu ambacho kipo karibuni kuanza. Na ndio maana yule mwanamke aliyeonekana kwenye ufunuo 17 alionekana amelewa kwa damu ya watakatifu. Kuna wakristo wengi wanaoteswa na kuawa kwa siri duniani kote, kwa ajili tu wao ni wakristo na sio jambo lingine.
Shetani hapendi kuona mtu anajiita MKRISTO, kama vile asivyopenda kuona watu wakibatizwa kwa jina la YESU KRISTO, na ndivyo asivyopenda kumwona mkristo anautambulisho wa asili wa KUMKIRI KRISTO, Hakuna mahali popote mkristo katika biblia alikuwa anajiita mpaulo au mpetro au m-yohana mbatizaji, au m-eliya au m-timotheo, biblia inasema wote walikuwa wanaitwa wakristo. Kwahiyo utambulisho mwingine zaidi ya huo unatoka kwa shetani, na hiyo ndiyo chapa ya mnyama yenyewe. amina.

KUHUSU 666
Papa akiwa kama kiongozi wa kanisa katoliki ana nembo katika enzi yake inayojulikana na kusomeka kama VICARIUS FILII DEI. tafsiri  yake kwa kiswahili ni  "BADALA YA MWANA WA MUNGU."
 kwahiyo papa kulingana na kanisa katoliki anasimama hapa duniani badala ya mwana wa Mungu, anauwezo kama vile, kusamehe dhambi, kubariki, na kusujudiwa n.k.
Haya ni machukizo mbele za Mungu,. Na hesabu ya hilo jina, kwa kirumi  ni 666. unaweza ukaona hesabu yake hapa chini.


kwahiyo kutiwa chapa katika mkono wa kuume au kwenye kipaji cha uso, ni kukubaliana na ule mfumo kichwani kwako,(hiyo ni kwenye kipaji cha uso) na kukubali kuutumia huo mfumo kama kitu cha kujipatia riziki au chakula (hiyo ni kwenye mkono wa kuume) tunafahamu kama vile mkono tunautumia kwa kula, kukubaliana na kitu, kusaini mikataba n,k  kwa wale watakaokubali kuuza na kununua ndio watapokea hiyo chapa (666). Kumbuka hii 666 ni namba inayomtambulisha mpingakristo na chapa yake, na sio chapa yenyewe. 

TAFUTA ROHO MTAKATIFU, EPUKA KAMBA NA UTAMBULISHO WA MADHEHEBU.

ukiulizwa wewe ni dhehebu gani, sema mimi ni mkristo usione haya Bwana Yesu alisema katika marko 8:38"Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu". Uvae ukristo umfuate Yesu usiuvae udhehebu utakupeleka jehanum.

Bwana Yesu anasema mathayo 16:24-26 "Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?."

Tubu ndugu mgeukie Mungu haya mambo yote, yatatokea kizazi tunachoishi sisi, unaona jinsi gani MPINGAKRISTO kashaweka mambo yake yote tayari, ni kutekeleza tu! mambo yaishe. YESU KRISTO YUPO MLANGO KURUDI, MUDA UMEENDA SANA KUSHINDA  UNAVYOFIKIRI.

MUNGU AKUBARIKI!

Monday, October 17, 2016

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

1Yohana 3:1 "Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye"
Katika maisha ya kila mmoja wetu, kuna ushuhuda ambao Mungu ameuandika.Bwana ameruhusu kila mtu apitie hatua mbili kuu muhimu maishani mwake nazo ni KUWA MTOTO, NA KUWA MZAZI( BABA/MAMA) Mungu hakuona vema mtu atokee tu duniani akiwa mtu mzima bali aliruhusu kwa makusudi kabisa mtu apitie hatua zote hizi mbili,ya kwanza awe mtoto, na kisha awe baba/mama,

Ili kusudi kwamba Mungu atakapojifunua kwetu kama Baba tuweze kumuelewa, kwa namna gani Baba ana nafasi yake katika maisha yetu kwakuwa tumeshayapitia hayo maishani ya kuwa na baba wa mwilini na kufahamu vizuri nafasi yake kwetu, ndio maana akasema ni pendo la namna gani alilotupa baba sisi kuitwa wana wa Mungu, kwasababu malaika hawajafananishwa na wana wa Mungu, kwakuwa hawajapitia njia tunazozipitia sisi wanadamu kama vile kuzaliwa na kuwa baba. Wao waliumbwa tu katika hali zao walizopo sasa Mtume Paulo alieleza wazi kabisa katika waebrania 1:5 "Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?" kwahiyo tunaona hapa malaika hawakuitwa wana wa Mungu, kwasababu hawajaumbiwa ile hali ya kuwa wana, wala kupitishwa katika maisha ya kuwa wana, biblia inasema wao ni roho zitumikazo ( waebrania 1:14 " Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?")

TABIA YA MWANA:
Kama sisi tumepewa neema hii kubwa ya kuitwa wana wa Mungu inatupasa sisi tufahamu jinsi Mwana anavyopaswa kuwa kwa Baba yake ili ampendeze Baba yake, inajulikana kuwa tabia ya mtoto yoyote mdogo hafikirii atakula nini wala atakunywa nini,wala atavaa nini, wala atalala wapi,wala hafikirii kesho itakuwaje, wala hafikirii kuhusu afya yake.Hizi ni tabia za watoto wote ikiwemo hata mimi na wewe tulivyokuwa watoto wadogo. Ujasiri huo wa maisha anao kwasababu anajua Baba yake yupo na ndiyo yeye anajukumu la kumlisha, kumvisha, kumnywesha,kuiangalia afya yake na kumlinda..mtoto haitaji kumweleza baba yake kuwa anaumwa ni jukumu la baba yake yeye kufahamu, mtoto hawezi kwenda kumsaidia baba yake kuleta chakula nyumbani hiyo haimuhusu mtoto kwasababu mtoto hayatambui hata hayo, na baba hachukizwi kumuona mtoto kuwa hivyo kwasababu anajua huyu ni mtoto tu, hawezi kufanya lolote.


Mtoto siku zote anaujasiri mkubwa sana kwa baba yake, kiasi cha kwamba anaona hakuna mtu mwingine yeyote anaweza akawa mkubwa kuliko baba yake, mtoto hana tabia ya kuweka kinyongo akiadhibiwa na baba yake baada ya muda mfupi ameshasahau, mtoto siku zote huwa anajishughulisha na vitu vidogo vidogo na huwa hatafuti ukubwa na ana tabia ya kupenda kukaa nyumbani na kuamini chochote atakachoambiwa na mzazi wake.

Na sisi kama wazazi tunachukuliana na watoto wetu na kuwapenda sana wakiwa katika hali kama hizo, tunawapenda pale tunapowaona watoto wetu wanavyojitoa kikamilifu kwetu,watiifu na wasio na kiburi, wanaojiachia kwetu..sidhani kama kuna mzazi yeyote anaweza akamchukia mtoto wake akiwa katika hali hiyo kwasababu anajua huyo ni mtoto tu hajiwezi na anahitaji uangalizi wote, na hakuna mzazi asiyemuhurumia mtoto wake, akimwona mtoto wake hana chakula yuko radhi alale njaa yeye ili mtoto wake ashibe, akimwona mtoto wake ana dalili tu ya kuumwa anamuhurumia na kumpeleka hospitali haraka sana.
JE! SI ZAIDI KWA BABA YETU ALIYE MBINGUNI??

kumbuka Mungu alitupitisha makusudi katika hatua hizi za kuwa mtoto au mzazi ili tumuelewe Mungu kama Baba yetu ana nafasi gani na umuhimu gani kwetu.

Kama Baba zetu wa mwilini wanaweza kututendea mema yote hayo, kutuangalia na kutuhudumia maisha yetu bure, kutuvisha,kutulisha, kutunywesha, kutupa malazi na kutupa afya pasipo kumlipa chochote si zaidi sana kwa Baba yetu aliye mbinguni?? 

Kuna mafundisho mengi ya uongo ya shetani na yanafundishwa hata na baadhi ya wanaojiita wahubiri wakisema Mungu wetu ni baba wa rohoni na kwamba yeye anatuhudumia tu kwa mambo ya rohoni na kwamba ya mwilini inatupasa tujihudumie wenyewe. Lakini biblia inasema waefeso 3:14-15 "
Kwa hiyo nampigia Baba magoti, ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa" Unaona hapo ni ubaba wote unaozungumziwa wa mbinguni na wa duniani sio tu wa mbinguni bali hata na wa duniani pia. Kwa namna ile ile uliyokuwa una mtegemea baba yako hapa duniani akulishe, akunyweshe, akuvishe, na akulinde na kukupa afya vivyo hivyo inakupasa umtegemee Mungu ambaye ni Baba yako hapa duniani kwa mahitaji yako yote ya mwilini na ya rohoni kwa kuwa ni baba wa rohoni pia.

Yesu Kristo alisema katika
mathayo 6:25-34 " Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake."


Neno hili shetani ameligeuza na kutoa tafsiri nyingi zinazopingana na maana ya maneno yaliyopo hapo juu.Maneno hayo Bwana Yesu aliyoyazungumza yana maana kama yalivyoandikwa, shetani anafahamu kuwa hii ni SIRI inayobeba uhusiano mkubwa kati ya Baba na Mwana, BWANA YESU anasema msisumbukie maisha yenu mle nini au mnywe nini kwamba baba yetu anajua kuwa hayo yote tunayahitaji, kama vile baba zetu wa mwilini tulivyokuwa watoto walikuwa wanajua yote kwamba tunahitaji kula na kunywa je! si zaidi kwa Baba yetu aliye mbinguni? embu jaribu kufikiri juu ya hilo ndugu kwa undani.Yesu Kristo alisema tujifunze kwa kunguru, hakusema tutazame wahubiri, mitume, waalimu n.k alisema tutazame kunguru, tujifunze jinsi wanavyokula, na kunywa, na kuishi hawapandi, hawavuni, hawana bima, hawana maghala lakini kila siku wana kula, kunguru anauwezo wa kuishi hadi miaka 80 na hajawahi kumeza kidonge katika maisha yake yote. Na maua ya mashambani hayafanyi ''KAZI'' lakini yanatoa harufu nzuri na rangi nzuri na kuuzwa kwa bei ghali kumbuka hayasogei hata inchi moja..Mungu ambaye ni baba yetu anasema "sisi si zaidi kuliko hao??"

Mathayo 18:3 " Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema, Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni."
Hapa tunaona Kristo anazungumzia aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni ni yule atakayejinyenyekeza kuwa kama mtoto mdogo. Unyenyekevu uliozungumziwa hapa ni maisha ya mtoto kwa baba yake, ni tabia ya mtoto kwa baba yake na sio kumpigia mtu magoti au kuonyesha utiifu fulani hapana. Kwetu sisi kujinyenyekeza kama watoto ni kujiweka/kujiachia kama watoto kwa baba yetu aliye mbinguni, na kuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni ni kuweza kuyashika na kuyaishi hayo maneno yote BWANA YESU aliyoyazungumza hapo juu kwenye mathayo 6:25-34.(huko ndio kujinyenyekeza kama mtoto) lakini kuwa na upako, au kuwa muhubiri mkubwa, au kuwavuta watu kwa Kristo au kuwa mchungaji au kuona maono au kuomba sana, au kufunga sana, au kwenda kanisani sana hakukufanyi wewe kuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. unapaswa uwe mtoto kwa Mungu(Baba wa mbinguni) kama vile mtoto alivyo kwa baba yake wa duniani.Hivyo ndivyo BWANA YESU KRISTO alivyokuwa hapa duniani kujiachia kwa baba yake wa mbinguni.

Uthibitisho mmoja wapo kuwa wewe umempokea Roho Mtakatifu ni wewe KUFANYIKA KUWA MWANA WA MUNGU yohana 1:12 "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;" na pia warumi 8 :14-16 inasema "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;"
Kwa hiyo uthibitisho kuwa wewe ni mtoto wa Mungu, ni Mungu kwako kuwa kila kitu na unamwona katika maisha yako akikuhudumia kwa mahitaji yote ya mwilini na ya rohoni( kumbuka! sio ya rohoni tu bali hata ya mwilini) hautasumbukia maisha kwasababu unaye baba, wewe sio yatima, baba yako atakuvisha, atakulisha, atakunywesha sikwambii wewe ufanye kazi akunyweshe hapana! ana njia zake mwenyewe, unaweza usifanye kazi kabisa wala kujishughulisha na jambo lolote na akakulisha na kukuvisha, unaweza usiwe na fedha hata kidogo na bado akakuvisha, akakulisha na akakuvisha, njia zake sio njia zetu, unaweza usiende hospitali kabisa na bado akakupa afya, BWANA YESU alisema Baba yetu anajua kabisa kuwa tunahitaji haya yote yaani tule, tunywe, tuvae, tulale, tuwe na afya, kasema mwenyewe kama yeye anaweza kuwafanyia hivyo ndege wa angani na maua ya kondeni je! sisi sio zaidi?? usimruhusu shetani autangue uhusiano wako wewe na Baba yako aliye mbinguni kwa kumwekea Mungu vikwazo na mipaka kwamba yeye hawezi kukuhudumia mpaka ufanye kazi..sipo kinyume na kazi, unaweza ukafanya kazi lakini Mungu hatumii hivyo tu kukuhudumia wewe...je! mtoto anafanya kazi?? jiulize hayo maswali..Mungu alitupitisha huko ili tujue nafasi ya baba kwa mtoto ni ipi?..usijaribu kumsaidia Mungu. Yeye ni Mungu tu na ni baba yako, kama wewe ulivyokuwa mtoto ulikuwa huwezi kuzichunguza njia za baba yako lakini ulikuwa una kula,ulikuwa hufikirii wala kuyasumbukia ya kesho wewe..kwanini leo ufikirie kesho?? BWANA YESU alisema msisumbukie ya kesho, kwa kuwa ya kesho itajisumbukia yenyewe..huko ndio kufanyika kuwa mwana na sio kudhania moyoni mwako kwamba wewe ni mwana wa Mungu wakati hujawahi kumuona Mungu kwako kama Baba, usidhani utakuwa kitu kule kwenye ufalme wa mbinguni, ni muhimu kuwa watoto kweli kweli kwa Baba yetu aliye mbinguni kama tulivyokuwa kwa baba zetu wa duniani.

Petro alipewa ufunuo mkubwa kuwa YESU KRISTO ni nani! ambao Bwana alimwambia Petro juu ya ufunuo huo atalijenga kanisa lake na milango ya kuzimu haitaiweza mathayo 16:18 "Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda."

Ufunuo huu Petro aliopewa sio wa Yesu Kristo kuwa ni Mungu, wala Yesu Kristo kama Mwokozi bali alipewa ufunuo kuwa yeye ndiye MWANA WA MUNGU aliye hai. Petro kwa kuona jinsi Kristo alivyokuwa anamtegemea baba yake kwa kila kitu, na jinsi baba yake alivyokuwa ana muhudumia kwa mambo yote, akatambua kuwa ule uhusiano ulikuwa ni wa kipekee kama vile wa BABA NA MTOTO WAKE. Hakukuwahi kutokea mtu yeyote katika torati au huko nyuma ambaye alishawahi kuwa na mahusiano ya kama baba na mtoto kwa Mungu, hiyo ilionekana kwa Yesu Kristo tu na ndio maana Petro alipewa ufunuo huo na Mungu jambo ambalo lilifichwa hata kwa baadhi ya mitume.

Sauti ilisikika kutoka mbinguni Yohana alipokuwa akibatiza na Yohana pekee yake ndiye aliyeusikia huo ufunuo mathayo 3:17 "na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye". Hapa Kristo hakushuhudiwa kama yeye ni Mungu au mfalme(ingawa Yesu Kristo alikuwa ni Mungu na Mwokozi) bali alishuhudiwa yeye kuwa ni Mwana wa Mungu . Sauti hii ilisikiwa pia na Petro, Yohana na Yakobo walipoenda mlimani na Bwana Yesu kusali mathayo 17 "Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye."
Chunguza tena maisha yako je! wewe ni kweli mwana halali au mwana haramu. mwana halali anaonekana kwa maisha yake anayoyaishi na uhusiano wake yeye na baba yake vilevile na mwana haramu anaonekana kwa maisha yake jinsi alivyo na mambo yake mwenyewe, hapendi kujishughulisha na mambo ya baba yake, asiyeweza kuadhibiwa anapokosea(kurudiwa), hamtegemei baba yake,

Je! Umepokea Roho Mtakatifu?? kama umepokea Roho wa Mungu atakushuhudia katika maisha yako kuwa wewe ni mtoto wa Mungu kwasababu maandiko ndivyo yanavyosema warumi 8 :14-16 inasema "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;"

MUNGU AKUBARIKI! 

Sunday, October 16, 2016

NGURUMO SABA

Katika kufunguliwa kwa mihuri saba, kwenye kile kitabu cha ufunuo, tunaona kuwa muhuri wa saba unatimia kabla ya muhuri wa sita, kwasababu muhuri wa sita unaelezea juu ya ile siku ya kuogofya ya Bwana, ambayo itakuja mwishoni baada ya ile dhiki kuu kuisha, Lakini muhuri wa saba unaelezea, mambo ya mwisho yatakayotokea kabla ya ujio wa pili wa Bwana Yesu Kristo kulichukua kanisa lake. Kwa ufupi muhuri wa kwanza, na wa pili, na wa tatu, na wa  nne, unaelezea jinsi roho ya mpinga kristo ilivyoanza kutembea katika kanisa la mataifa(ufunuo 6) kama inavyoonekana katika historia ya kanisa na tonaona pia zile Roho za wenye uhai wanne ambazo wakwanza alikuwa kama mfano wa simba, wapili mfano wa ndama, watatu mfano wa uso wa mwanadamu, na wanne mfano wa tai arukaye. Hizi ni Roho za Mungu zilizoachiwa kupambana na ile Roho ya mpinga kristo katika vipindi vya makanisa. Na muhuri wa tano unaelezea juu ya wayahudi waliouawa kipindi cha vita vya pili vya dunia(holocaust) chini ya utawala wa kimabavu wa Adolf Hitler wa ujerumani, inakadiriwa zaidi ya wayahudi milion 6 waliuawa. hizi ndizo zile roho zilizoonekana chini ya madhabahu kwenye ule muhuri wa tano ulipofunguliwa.(ufunuo 6:9)

Na leo tunauzungumzia ule muhuri wa saba, unaobeba zile ngurumo saba:

Tukisoma ufunuo 8:1" Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa." Muhuri huu ulipofunguliwa biblia inarekodi kulikuwa na ukimya mkubwa mbinguni kuonyesha kuwa tukio fulani kubwa linaenda kutokea. Na hili sio lingine zaidi ya Bwana wetu YESU KRISTO ,akinyanyuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, na kushuka kudai walio wake. zekaria 2:13"Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za Bwana; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu."

Jambo hili tunaendelea kuliona katika ile sura ya kumi.
 ufunuo 10 :1-8 "Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto. 2 Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi.
3 Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao.
4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.
5 Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni,
6 akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya; 7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.
8 Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Enenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi.
9 Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho kitakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali.
10 Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu.
11 Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi."


Malaika huyu mkuu mwenye nguvu aliyeshika kitabu kidogo aliyeonekana akishuka kutoka mbinguni sio mwingine bali ni BWANA YESU KRISTO, Na kile kitabu alichokishika  ndio kile kitabu kilichokuwa kimefungwa na ile mihuri saba, lakini sasa hapa kinaonekana kimefunguliwa.

Na aliposhuka akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari na wa kushoto juu ya nchi, naye akalia kwa sauti kuu kama simba angurumavyo, na alipolia zile NGURUMO SABA, zikatoa sauti zao. Lakini hapa tunaona alipolia kwa sauti kuu, ile sauti iliambatana na sauti ya zile NGURUMO SABA. Hivyo basi tunaona hizi ngurumo saba zinabeba sauti ya BWANA zenye ujumbe unaohusiana na kile kitabu alichokuwa amekishika.

 Katikati ya waaminio wengi wa ujumbe wa malaki 4, kumekuwa na mgawanyiko mkubwa,na kutengeneza makundi mawili makubwa. Kuna kundi linaloamini kuwa ngurumo saba zimeshafunuliwa, na kuna kundi lingine linaloamini kuwa ngurumo saba bado hazijafunuliwa. katika kundi linaloamini kuwa ngurumo saba zimeshafunuliwa limegawanyika tena katika vikundi vikundi, kuna wanaoamini ngurumo saba ni ufunuo wa ile mihuri saba, kuna wengine wanaoamini kuwa ngurumo saba ni, zile hatua saba za kimo cha mtu mkamilifu 2petro 1:5-7. kuna wengine wanaamini ngurumo saba ni yale maono saba ya William Branham alioonyeshwa kabla ya kurudi kwa pili kwa BWANA YESU KRISTO, na wengine wanaamini ngurumo saba ni zile huduma tano zilizowekwa kulijenga kanisa waefeso 4.. n.k. Na kundi linaloamini kuwa ngurumo saba bado hazijafunuliwa wapo wanaoamini kuwa ngurumo saba ni watu 7 kabla ya unyakuo, na wapo wanaoamini kuwa ngurumo saba zitafunuliwa mara baada ya unyakuo kupita.

Ni wazi kabisa ndugu Branham alisema kuwa ufunuo sura ya kumi inazungumzia kuja kwa Bwana YESU KRISTO, 
kwenye kitabu cha ufunuo wa mihuri saba-William Branham { muhuri wa kwanza, pg 12, march 1963 William Branham alisema "Na ndipo kunakuja Ngurumo saba za siri ambazo hata hazijaandikwa kamwe. Hiyo ni kweli. Nami naamini ya kwamba, kupitia Ngurumo hizo Saba, zitafunuliwa katika siku za mwisho ili kumkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya kupata imani ya kunyakuliwa. Kwa sababu, ile tuliyo nayo sasa hivi, ha_hatungeweza kufanya jambo hilo. Kuna jambo fulani. Hatuna budi kupiga hatua mbele zaidi. Sisi, hatuwezi kupata imani ya kutosha kwa ajili ya uponyaji wa Kiungu, ni vigumu. Lazima tuwe na imani ya kutosha kubadilishwa, katika dakika moja, na kunyakuliwa tutoke katika dunia hii."

mahali pengine alisema,
{kwenye Muhuri wa tatu, pg 25, march 1963 "Bi-Bibi arusi hajawa na uamsho bado. Mnaona? Hakujakuwako na uamsho humo, hakujakuwako na madhihirisho ya Mungu kumwamsha Bibi-arusi bado. Mnaona? Tunautarajia huo sasa. Itahitaji hizo Ngurumo Saba zisizojulikana kule nyuma, kumwamsha Yeye tena, unaona. Naam. Yeye atazituma. Aliliahidi."

Ikiwa kama ngurumo saba zilishafunuliwa ni dhahiri kuwa tungekuwa tumeshapata imani ya kwenda kwenye unyakuo, Nabii alihubiri kuwa hizo ngurumo saba zitakapolia zitampa bibi-arusi imani ya kwenda kwenye unyakuo. Hivyo tunaona kuwa mawazo ya kusema kuwa ngurumo saba zimeshafunuliwa hayana uhalisia wowote wa kimaandiko.

Ngurumo saba ni hatua ya mwisho ya UAMSHO ya kumpa bibi arusi imani ya kwenda kwenye unyakuo, kwahiyo ninakubaliana na wanaosema kuwa hizi NGURUMO SABA NI WATU SABA, ambao Mungu ataenda kuwanyanyua katika kipindi hichi cha mwisho, watakaohubiri siri zile ambazo Yohana aliambiwa asiziandike, watahubiri mambo ambayo hayajarekodiwa kwenye biblia mahali popote, na kama vile zile nyota saba za makanisa saba ni watu saba, vivyo hivyo ngurumo saba zitakuwa watu saba, ambao watatoa jumbe zao tofauti tofauti kwa wakati mmoja, Na hawa watu saba watakapotoa sauti zao zitasikika duniani kote na itakuwa ni kwa muda mfupi, watakaopata ulewa wa jumbe hizo ni bibi arusi tu, aliyekwisha kujiweka tayari kwa kuuamini ujumbe wa malaki 4(yaani kupokea Roho Mtakatifu huko ndiko kuuamini ujumbe wa malaki4) lakini kwa waliobakia hizo jumbe zitasikika  kwao kuwa kama ushuhuda tu, kwahiyo injili itakayohubiriwa haitakuwa ya kuwavuta watu kwa Kristo tena, Bali ya kumpa bibi arusi imani ya kwenda kwenye unyakuo.

baada ya ngurumo 7 kutoa sauti zao ambao ni watu 7, Mungu atakaowanyanyua wakati wa mwisho kuzungumza siri zilizopo katika kile kitabu kidogo kilichobeba siri za ukombozi wa mwanadamu. Lakini tunaona pia hapo kwenye mstari wa 8 Yohana alipewa kile kitabu akile, hapa Yohana anawakilisha bibi arusi wa kristo, na alipokila kile kitabu ambacho kilikuwa kitamu mdomoni mwake bali kichungu tumboni mwake, maana yake ni  kwamba ule ufunuo atakaoupata kutoka katika kile kitabu ambacho kitahubiriwa na zile ngurumo 7 utakuwa ni mzuri kuusikia lakini utakuwa ni mgumu kuupokea na kuuhubiri. kwahiyo kama tunavyoona kwenye mstari wa 10 yohana (alinawakilisha bibi arusi) alivyoambiwa imempasa atoe tena unabii juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi, hii inamaana bibi arusi baada ya kuupokea ujumbe wa zile ngurumo 7, Roho kuu ya Mungu ya uvivuo itawajilia na ndio watakaopeleka injili duniani kote kwa mara nyingine tena, kwa udhihirisho mkuu wa nguvu za Mungu kwa namna ambayo haijawahi kutokea kabla ili kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, hapo ndipo ule mwisho utakapokuja(mathayo 24:14). Kwahiyo kuna uamsho mkuu unakuja mbeleni utakaopita dunia yote.

Ndugu umeona hatua tuliyopo sasa, ni wakati wa jioni, Kristo alisema ufunuo 22:11 "Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. " Hizo ngurumo saba zitakapotoa sauti zao Ndugu yangu kutakuwa hakuna muda tena, kitakuwa ni kipindi cha check-in process, pale wale wanawali wapumbavu watakapoona bwana arusi anakuja, na kuanza kwenda kutafuta mafuta, na waliporudi walikuta wenzao wameshaingia karamuni na ndivyo itakavyokuwa wakati huo zile ngurumo saba zitakapotoa sauti zao, kumbuka ni wale tu wenye Roho Mtakatifu ndio watakaoweza kupokea na kuzielewa jumbe hizo zitakapotelewa, lakini wewe unayejiita mwamini hauna Roho Mtakatifu na unalifahamu hilo unaishi maisha yasiyofanana na ukristo, siku hiyo itakukuta itakujia kama mwivi, wakati wewe umeshtuka na kuanza kwenda kutafuta mafuta wakati huo wenzako watakuwa wameshaondoka wapo mbinguni.
mimi sitaki kubaki sijui wewe ndugu yangu??.

Tafuta ROHO MTAKATIFU sasa, kabla hayo mambo hayajatokea maana yapo mlangoni, Nabii (William Branham) ameshakuja, katoa ujumbe wake kaondoka, ni jukumu lako wewe sasa kutafuta Roho Mtakatifu, ambao ndio muhuri wa Mungu, PASIPO HUYO HAKUNA UNYAKUO.

MUNGU AKUBARIKI....

Wednesday, October 12, 2016

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA

Mungu amekuwa akizungumza na wanadamu kwa njia tofauti tofauti na kwa wakati tofauti tofauti, 
Katika historia ya kanisa ujumbe Mungu alioutoa kwa kanisa la kwanza sio sawa na ujumbe alioutoa kwa kanisa la pili..na wala sio sawa na ujumbe alioutoa kwa kanisa la mwisho. Mungu anaongea kulingana na wakati, ni muhimu sana kulitambua hilo. Kwa mfano wakati ulipotimia wa Mungu kumleta mwana wake katika agano jipya watu wengi ikiwemo waalimu wa torati na mafarisayo hawakuweza kuiamini injili yake kwasababu hawakuuelewa ujumbe wa saa yao, walishikilia torati ya Musa lakini walisahau kuwa Musa alisema ''atakuja nabii mwingine kama mimi mwaminini yeye'', Lakini waliukataa ujumbe wa Yesu Kristo wakabaki kushikilia mapokeo yao.

Katika hichi kipindi cha siku za mwisho tunaona kuwa yote yaliyotabiriwa na BWANA YESU KRISTO yanaenda kutimia, Licha ya kwamba Bwana kumtuma mjumbe wake(William Branham) kutuamsha kujiweka tayari kwa ajili ya kumlaki Bwana mawinguni tunaona pia Mungu amekuwa akizungumza na sisi kwa kupitia maumbile ya ulimwengu (nature) kutufundisha na kututhibitishia kuwa nyakati hizi tunazoishi ni za mwisho.

Kwa mfano maendeleo makubwa ya teknolojia tunayoyaona sasa hivi yana hubiri dhahiri injili ya kuja kwa BWANA YESU KRISTO. Baadhi ya hayo ni:

TEKNOLOJIA YA SIMU YA MKONONI NA MITANDAO:
Leo hii sio jambo la kushangaza kuona mtu mmoja anawasiliana na mwingine aliye taifa la mbali maelfu ya maili, kwa sekunde tu!, watu wanaweza wakaonana na kuzungumza kwa mfumo wa video (yaani video chat), watu wanaweza kupelekeana taarifa na habari kwa mfumo wa televisheni ndani ya dakika chache tu na dunia nzima ikapata habari ya mambo yanayoendelea ulimwenguni, teknolojia imefanikiwa kuifanya dunia kuwa kama kijiji. Mungu kayaruhusu haya yote kutokea kwa kasi kubwa katika karne hii ya 20 na ya 21 ili kutufundisha na sisi watoto wa Mungu ya kuwa katika kipindi chetu cha mwisho mawasiliano yetu na Mungu yanapaswa yawe makubwa kuliko vipindi vyote vya nyuma vilivyotutangulia, tunajua kwa dunia ya sasa kuwa na chombo cha mawasiliano (kama simu) ni muhimu kwa ajili ya kujuzana habari sana sana kwa matukio ya gafla, pasipo hicho hauwezi kuendana na jamii/maisha ya sasa vivyo hivyo na sisi kama wana wa Mungu tumefika wakati ambao kila mtu anapaswa awe na Roho Mtakatifu kama chombo chake cha mawasiliano katika hichi kipindi cha uovu na mafundisho ya uwongo kuenea kila mahali, Leo hii mtu anaweza kutafuta ukweli wa jambo fulani kwa kutumia mtandao (internet) na sisi pia kama wana wa Mungu tunahitaji Roho Mtakatifu kutufundisha na kutuongoza katika kweli yote, na kama vile zamani ujumbe ni lazima upelekwe na mtu fulani(mjumbe) lakini sasahivi mjumbe haitajiki tena kwasababu kuna simu ambazo zimerahisisha mambo kupata habari kwa haraka vivyo hivyo katika wakati wetu tunaoishi sasa hivi Mungu alishawapeleka wajumbe wengi sasa tupo katika hatua ya sisi kuwasiliana na Mungu moja kwa moja mjumbe haitajiki tena kama kuna Roho Mtakatifu. Yeremia 31:33 " Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena". Tumeona hapa katika hizi siku za mwisho ni muhimu kuwa na Roho Mtakatifu kukufundisha ndani yako binafsi na kukuongoza katika kweli yote, maana saa tunayoishi ni ya hatari manabii wa uwongo waliotabiriwa na mafundisho mengi ya uwongo yameenea kila mahali hichi ndicho kile kipindi Bwana alichosema mathayo 24:23-26 "Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki".Ni wakati wa kutafuta uhusiano wako binafsi na Mungu, leo hii ukitaka kumwita mtu kwa haraka mahali fulani mbali ni lazima umpigie simu, kama hana simu basi hawezi kujua kama unamhitaji kwa wakati huo, vivyo hivyo usipokuwa na Roho wa Mungu hutaweza kufahamu wakati utakapoitwa haraka kwenda kumlaki Bwana mawinguni, watakaoenda ni wale tu wenye mahusiano na mawasiliano mazuri na Mungu.



TEKNOLOJIA YA NDEGE:
Kwa vizazi vya nyuma suala la mtu kupaa hewani lilikuwa ni jambo lisilowezekana lakini sasa mtu kusafiri kwenda kwenye magimba ya nje ya dunia limekuwa ni jambo la kawaida kwa kutumia roketi, hii inatufundisha kuwa kama sayansi imefanikiwa kufanya hivi, na sisi wakristo tunaomngojea Bwana wakati wetu wa kupaa mawinguni umekaribia, kama vile wanasayansi walivyokuwa wakitafiti kwa miaka na miaka huko nyuma ni jinsi gani wangeweza kuruka juu hewani na kufika kwenye magimba mengine nje ya dunia na kufanikiwa katika kizazi hichi baada ya kutaabika kwa muda mrefu, inatufundisha sisi wana wa Mungu kuwa ndege yetu ya kwenda mbinguni imeshaandaliwa na iko tayari katika hichi kizazi chetu baada ya kusubiria kwa muda mrefu, na kama vile mtu akitaka kusafiri kwa ndege ni lazima awe na tiketi naye amekata mapema(booking) vivyo hivyo na sisi tunapaswa sasa hivi kuwa na Roho Mtakatifu kama tiketi yetu ya kuingia katika ndege hiyo ya mbinguni na tunapaswa tu-book mapema kabla ya ndege kuondoka ili tuwe na uhakika wa safari yetu kabla nafasi hazijajaa.



Jiulize ewe ndugu..simu yako ni ipi?? kama hapo ulipo hukosi kuwa na simu mfukoni na unajua kabisa katika dunia ya sasa usipokuwa na simu hauwezi kuendana na jamii inayokuzunguka lakini hutaki kuwa na simu ya roho ambayo ni Roho Mtakatifu unatazamia nini hapo??..jibu ni dhahiri kwamba unategemea siku ile ikujie gafla kama mtego unasavyo..wakati wengine wakiwa na Roho wa Mungu akizungumza nao katika hichi hichi kizazi unachoishi wewe wakijiweka tayari kuchukuliwa juu wewe utakuwa huna habari...habari itakufikia baadae wakati wakristo wa kweli wameshaondoka kwasababu huna simu yako mwenyewe (Roho Mtakatifu) ingekupasa upigiwe simu ya kuondoka lakini kwasababu huna Roho Mtakatifu utasubiria uletewe habari kwasababu hiyo basi itakupasa uingie katika ile dhiki kuu..mimi binafsi nisingependa kubaki kwenye dhiki kuu sijui wewe??

Na je! tiketi yako ni nini??..kumbuka ndege ipo tayari na ina nafasi chache tu (limited number of seats) na kumbuka ndege sio gari uende saa hiyo hiyo na kupanda uondoke, ina process hivyo inahitaji booking mapema, wanashauri walau ukate tiketi wiki moja au mbili kabla kwa uhakika wa safari yako, na katika siku ya safari unapaswa ufike airport masaa 3 kabla kwa ajili ya hatua ya makaguzi (check-in process) usipozingatia hivi vigezo huwezi kusafiri. Vivyohivyo katika safari yetu ya kwenda mbinguni ndege yetu ipo tayari hatua tuliyopo sasa ni ya booking kwa ajili ya kupata nafasi katika sehemu ya ufalme, na hatua hii inakaribia kumalizika unatakiwa uwe na tiketi yako mkononi (Roho Mtakatifu) nafasi zinaenda kujaa, na zikishajaa hatua itakayofuatia ya makaguzi(check- in) ni kwa wale tu walio na tiketi zao wengine wasio na tiketi haitawahusu, na hatua zote hizi zinafanyika tukiwa hapahapa duniani kabla ya kwenda kupanda ndege yetu ya kwenda mbinguni.

Tukumbuke Mungu karuhusu haya mabadiliko makubwa ya teknolojia yatokee katika kizazi chetu ili sisi tujifunze, tusipojifunza yatakuja kutuhukumu katika siku ile ya Bwana..Je! hauoni ni wakati gani huu wa hatari tunaouishi??..na bado unaendelea kuupenda ulimwengu kuliko kumpenda Mungu, unakuwa mwasherati wakati Mungu anasema "hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu" unatazamiaje Roho wa Mungu aje juu yako, una kuwa mlevi, vuguvugu haueleweki wewe ni mkristo au ni nani, una kuwa msengenyaji, unajichanganya na watu waovu wa ulimwengu huu hao ndio rafiki zako wakati biblia inasema 'msifungwe nira pamoja na wasio amini" una kaa na watu wenye mizaha, maneno machafu yanatoka midomoni mwako na bado unajiita mkristo, unavaa mavazi yasiyo na heshima na kufanana na wanawake wa ulimwengu huu, huna muda wa kusoma neno na kusali na kuomba lakini unapata muda mwingi wa kuchati kwenye mitandao katika vitu visivyokuwa na maana, shetani amekupofusha akikudanganya kwamba wewe ni bibi arusi wa Kristo na kwamba yote ni sawa, lakini jua jambo moja katika kizazi hichi hichi unachoishi wewe kuna wakristo kweli kweli ulimwenguni kote waliojazwa Roho Mtakatifu wanaushinda ulimwengu katika mazingira kama hayo hayo yakwako unayoishi wewe na watatuhukumu maana biblia inasema 'watakatifu ndio watakaoouhukumu ulimwengu' umehubiriwa injili kila siku unaisikia bado unaishi maisha unayoishi sasa.Kristo alisema ''itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yako?'' mambo ya ulimwengu huu yanakusonga mpaka unashindwa kuwa mkristo kama unavyopaswa uwe,

Tubu! badilika muda umeenda kuliko tunavyodhani mambo yote yameshakuwa tayari, huu sio wakati tena wa sisi kumngojea Bwana bali Bwana ndiye anayetungojea sisi.

TAFUTA ROHO MTAKATIFU MAANA HUO NDIO MUHURI WA MUNGU!

Mungu akubariki.

Tuesday, October 11, 2016

THE DAY OF OUR REDEMPTION IS NEAR!!

Nations are breaking, Israel's awaking,
The signs that the bible foretold,
The gentile days numbered with, 
Horrors encumbered; Eternity soon
will unfold.

Chorus:
The day of redemption is near,
Men's hearts are failing for fear,
Be filled with the spirit, your
lamps trimmed, and burn,
Look up! Your redemption is near.

The fig tree is growing; Jerusalem's 
restoring, Her national life, Long 
dethroned, Today she is calling, her
latter rain is falling; Return O dispersed
to your own.

Heaven's power are shaking, and 
many are mistaking God's meaning 
to be of the sky; God's church is the power
that is shaking this hour; The day
of redemption is nigh.

False prophets are lying. God's truth, 
they are denying, That Jesus the Christ
is our GOD; Though this generation,
spurns God's revelation, We'll walk
where the apostles have trod.



Monday, October 10, 2016

UWEZA WA BWANA YESU KRISTO KATIKATI YETU SISI WANADAMU



Jinsi rehema za MUNGU zilivyo nyingi kwetu..huwatuma malaika zake kutuangalia sisi usiku na mchana, na kutuokoa kutoka katika matatizo yetu pale tunapoliitia jina la lake. ASHUKURIWE BWANA WETU YESU KRISTO MILELE NA MILELE AMINA..

JUMA LA 70 LA DANIELI

Kabla hatujaliangalia juma la 70 hebu tufahamu kwa ufupi haya majuma 70 ni yapi?

Tukisoma Danieli

9:24-27 "24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. 25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.
27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu"

Katika lugha ya biblia juma moja linawakilisha miaka 7.Hivyo majuma 70 ni sawasawa na 7*70=490

kwahiyo miaka 490 imeamuriwa kwa watu wake,sasa hawa watu wake wanaozungumziwa hapa ni wayahudi na sio watu wa mataifa. Majuma haya sabini yalianza kuhesabiwa baada tu ya danieli kupokea hayo maono.

MAJUMA 7 YA KWANZA:
Majuma 7 ya kwanza ambayo ni miaka 49 Danieli aliambiwa Yerusalemu utajengwa tena upya na njia zake kuu katika kipindi cha taabu na shida. katika hichi kipindi Hekalu la pili lilijengwa upya na kumalizika ndani ya hii miaka 49 ya kwanza baada ya kutoka uamishoni babeli.

MAJUMA 62:
Haya yalianza kuhesabiwa pale tu baada ya hekalu kumalizika kujengwa ndani ya yale majuma 7 ya kwanza. katika haya majuma 62 yaani miaka 434 ikishakwisha masihi yaani YESU KRISTO atakatiliwa mbali. Mpaka hapo majuma 69 yatakuwa yameisha. kwahiyo masihi yaani Yesu Kristo atakuwa ameshazaliwa na mwisho wa hilo juma la 69 yaani 62+7=69, atakatiliwa mbali, hili lilitokea pale alipopelekwa kalvari.AD 33

JUMA 1 LA MWISHO:
Majuma 69 yalipoisha Mungu aliacha kushughulika na wayahudi na neema ikahamia kwa mataifa kwasababu wayahudi walimkataa Masihi wao,kwahiyo kikaanza kipindi cha mataifa ambacho mpaka sasa tunaendelea nacho takribani miaka 2000 sasa. Na Neema itakaporudi Israeli ndipo juma moja la mwisho litakapoanza kuhesabiwa tena yaani miaka 7 ya mwisho, kutimiza majuma sabini.  majuma haya 70 yaliamuriwa kwa watu wa Daniel yaani wayahudi na sio pamoja na watu wa mataifa. Na katikati ya hili juma la mwisho yaani miaka mitatu na nusu ya kwanza injili itapelekwa Israeli, na katika miaka mitatu na nusu ya mwisho mpinga kristo atavunja agano atakaloingia na wayahudi na kukomesha sadaka na dhabihu na ndipo ile dhiki kuu itakapoanza.

MTAZAMO AMBAO SIO SAHIHI 
Kuhusu juma la mwisho la 70, watu wengi waaminio wa ujumbe wa William Branham wananukuu baadhi ya sehemu alizohubiri katika vitabu vya ujumbe, mfano katika kitabu cha "ufunuo wa mihuri saba" katika zamu ya maswali na majibu, alisema  kuwa lile juma la 70 lilishaanza na BWANA YESU alishalitimiza nusu ya juma hilo alipokuwa duniani katika ile miaka mitatu na nusu ya kwanza aliyohubiri ulimwenguni.na miaka mitatu na nusu iliyobaki itatimizwa baada tu ya kanisa kunyakuliwa.

Lakini pia tukinukuu ndugu William Branhama alichofundisha katika kitabu cha "LILE JUMA LA 70 LA DANIELI"  agosti 6 mwaka 1961 alisema kuwa lile juma la sabini litaanza baada tu ya utimilifu wa mataifa(yaani kanisa kwenda kwenye unyakuo) na itabaki miaka 7 ambapo  miaka mitatu na nusu ya kwanza injili itapelekwa Israeli na wale manabii wawili wa ufunuo 11 na mitatu na nusu ya mwisho itakuwa ni wakati wa ile dhiki kuu baada ya mpinga kristo kulivunja lile agano atakaloingia na wayahudi.

Hapa tunaona kuwa ndugu Branham alizungumza vitu viwili tofauti vinavyoonekana kama kupingana..sasa tuchukue lipi tuache lipi???. Je! ni ujumbe unashida?? hapana ni watu wasioulewa ujumbe na kushikilia vipengele vya vitabu tuu pasipo kuomba msaada wa Roho Mtakatifu ndio wanaoufanya ujumbe usieleweke, Hata ndugu William Branham alisema  mwenyewe "biblia ndio muongozo wangu" na pia alisema "hata mimi nikizungumza neno lolote kinyume na biblia usilichukue" Mambo mengi aliyoyazungumza nabii alipewa na BWANA ila sio yote aliyokuwa anazungumza yalikuwa ni "HIVI ASEMA BWANA".. ni mara ngapi tuliona akikiri kuwa mambo mengine hafahamu, anayefahamu kila kitu na asiyekosea ni BWANA YESU KRISTO peke yake. Aleluya.!
.Ni dhahiri kabisa tunajua kuwa NENO LA MUNGU haliwezi kujichanganya Mungu aliyaruhusu haya makusudi ili kutupima sisi kama tumelielewa NENO na kama kweli tunampenda BWANA YESU, na kurejeza kila kitu kwenye NENO lake 
Sasa ili kuondoa huo mkanganyiko inatupasa kurudi kwenye biblia tuangalie inasemaje na sio kuangalia vitabu vinasemaje, vitabu vinapaswa kuturudisha kwenye NENO na sio NENO liturudishe kwenye vitabu. Ni jukumu letu sisi kuhakiki kila neno linalosemwa na mtu yeyote kwa NENO na nabii mwenyewe ndivyo alivyotufundisha wote. Nabii hakumvumilia wala kumuonea haya mtu yeyote anayetoa mapokeo yake nje ya neno.
Biblia inasema danieli 9:26 " Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji" Hapa tunaona dhahiri Masihi atakatiliwa mbali mara baada ya majuma 62  kukamilika, kukamilisha majuma 69 yaani (7+62=69) kuisha, na sio baada ya majuma 62.5 yaani(7+62.5=69.5).unaona biblia inasema baada ya yale majuma 69 kuisha ndipo masihi atakapokatiliwa mbali.

 Na huyo mkuu atakayekuja baada ya Masihi kukatiliwa mbali atakuwa ni mpinga kristo naye atafanya agano na watu wengi katika juma moja yaani miaka 7. na nusu ya juma hilo atalivunja hilo agano na kuikomesha sadaka na dhabihu, kumbuka Masihi na mkuu atakayekuja ni watu wawili tofauti.chukizo la uharibifu ni mpinga kristo atakapoingia lile agano na israeli.

Tukisema masihi ni sawa na mkuu wa watu atakayekuja tutakuwa hatujaielewa biblia vizuri kwasababu, maandiko yanasema watu wa huyo mkuu atakayekuja ndio watakoutekeza mji, na tunafahamu katika historia warumi ndio waliouteketeza mji 70AD kutimiza ule unabii Bwana Yesu aliousema mtakapouna mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi mjue uharibifu wake umefika.(luka 21:20). hivyo sio watu wa Yesu Kristo(yaani wayahudi) walioteketeza mji bali ni watu(warumi), wa yule "mkuu atakayekuja" yaani mpinga kristo. ambaye kwa kipindi hicho alikuwa bado hajaja lakini baadaye atakuja na kuingia agano na wayahudi katika lile juma moja la mwisho lililobaki.

Kwahiyo kulingana na NENO juma la sabini litaanza baada tu ya injili kumalizika kwa mataifa na ndivyo hata nabii alivyohubiri katika ujumbe aliofundisha agosti 6 mwaka 1961"LILE JUMA LA SABINI LA DANIELI". Hivyo mtazamo unaosema kuwa Bwana Yesu alishakamilisha nusu ya juma akiwa hapa duniani sio sahihi.

2 petro 1:10 "Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo."


Mungu akubariki!

Sunday, October 9, 2016

JINSI SHETANI ALIVYOINGIA KATIKA UJUMBE WA MALAKI 4:5-6

Watu wengi, sana sana waamini wa ujumbe wa ndugu William Branham wameshindwa kuulewa ujumbe huu wa thamani Mungu aliotupa una maana gani. Kwa uelewa wao wa kawaida umewafanya hata wale wasio waamini wa ujumbe huu kuona kama ni kikundi fulani cha occult au kikundi kinachomwabudu mtu. Shetani amenyanyua watu wasiokuwa na Roho Mtakatifu ili kuuchafua ujumbe na uonekane kama haufai. Lakini hila za yule mwovu hazitadumu.Lakini Bwana anaurejesha upya.

Roho hii ya shetani imeingia kwa wanaojiita waumini wengi na kumtukuza Nabii zaidi ya BWANA WETU YESU KRISTO aliyetufia msalabani. Nabii alikuwa mtu wa Mungu mnyenyekevu, aliyewarudisha watu kwa Kristo wala hakumwambia mtu yeyote, amwabudu au amkuze kushinda YESU KRISTO.Lakini baadhi ya watu shetani aliowanyanyua wameiingia katika ujumbe huu wa saa na kumwabudu Mtu, zaidi ya BWANA WETU YESU KRISTO.kiasi cha kwamba hata watu wasioamini wanashindwa kuvutiwa na ujumbe. Kumbuka wakatoliki wana picha ya Bikira Mariam wakidhani wanamuheshimu Mariam, Hawakujua kuwa Mariam alimtumikia Yesu, kwa kuwa hawakuitambua huduma ya Mariam. leo hii wanamwabudu Mariam ambazo ni ibada za sanamu. Vivyo hivyo baadhi ya waamini wa ujumbe huu, wanafahamu zaidi juu ya nabii na familia yake na picha zake kuliko wanavyomjua BWANA YESU KRISTO wakidhani ndio wanamheshimu nabii wamesahau kuwa wameiga hayo kutoka kwa mama yao Katoliki. kuwa na picha sio vibaya lakini tunaposahau ujumbe aliouleta nabii zinageuka kuwa ibada za sanamu. Mkristo yeyote anapaswa kulielewa hilo.

William Branham alikuja kuturejesha sisi kwa KRISTO YESU,( ndio kiini cha ujumbe wake) lakini watu wamemwacha Bwana aliye mwokozi wetu na kumhubiri nabii,

Biblia imeachwa kusomwa na kuhubiriwa, badala yake ni vitabu tu vya ujumbe vinavyohubiriwa makanisani. kitu ambacho nabii hakukiagiza wala kukifundisha, ndugu William Branham alisema " Hata mimi mwenyewe nikifundisha jambo lolote kinyume na biblia, usilichukue hilo"

Na shetani pia ameingia katika ujumbe hata kufikia hatua ya watu kumuabudu Nabii kama Mungu, wengine wanabatiza kwa jina la William Marrion Branham na sio kwa jina la BWANA YESU KRISTO tena.Hii ni roho ya mpinga kristo ikitenda kazi ndani ya ujumbe.



Kumbuka sio mambo yote ndugu William Branham aliyoyasema ni 'HIVI ASEMA BWANA"..Lakini kuna baadhi ya watu wanahubiri kwamba kila neno ndugu Branham alilosema ni HIVI ASEMA BWANA. na kuwafundisha watu washikilie tu masomo ya kwenye vitabu, wakisema hayo tu yanatosha siri za Mungu zote zimeshafichuliwa ndani yake. Pia Utakatifu, karama za rohoni na ubatizo wa ROHO MTAKATIFU hazihubiriwi tena. Na wengine wao hawaamini tena katika kusambaza injili.

Biblia ndio kitabu pekee cha ukombozi wa mwanadamu, chenye pumzi ya Bwana na BWANA YESU KRISTO ndiye mtunzi wa hicho kitabu. hatujaokolewa kwa damu ya mwanadamu yeyote, wala mtume yeyote, wala nabii yeyote wala malaika yeyote. Hawa wote ni watumishi wanaoturudisha kwa Bwana, na sio sisi tuwageuze wao waichukue nafasi ya BWANA YESU KRISTO. hizo ni ibada za sanamu, na za wafu ambazo zinafanywa pia na kanisa Katoliki. Kuwaabudu watakatifu na Jeshi la mbinguni. wakidhani wanawatii manabii wa Mungu. Kumbe wanamwabudu shetani mwenyewe bila wao kujijua.

Hivyo ndugu ikiwa wewe ni mwamini wa ujumbe huu wa malaki 4. Ni vizuri kutambua kuwa ujumbe huu unamaana gani, na unakuelekeza wewe wapi? ukishakwisha kuuelewa utaona sababu ya wewe kumpenda BWANA YESU KRISTO na kumwabudu YEYE PEKE YAKE , na kuifanya biblia kuwa ni mwongozo wako,sio vitabu vya ujumbe, vile viwe kukurudisha wewe katika neno lakini sio viwe litrujia yako. na pia kuona sababu ya wewe kutokupingana na KWELI, Kama hautaweza kufanya hivyo basi ujue kabisa haujauelewa wala haupo kwenye ujumbe. Haijalishi una picha ngapi za nabii, au umesoma vitabu vingapi vya nabii, au unamuheshimu nabii kiasi gani au unahudhuria kanisani mara ngapi.

Naamini Mungu atakubadilisha na kukupa uelewa zaidi juu ya ujumbe wa ndugu. William Branham unamaana gani.


Mungu akubariki.

Friday, October 7, 2016

UNYAKUO

Imekuwa ikijulikana na wengi kuwa unyakuo utakuwa ni tendo la ghafla. kufumba na kufumbua mamilioni ya watu watatoweka, watu watakuwa wakikimbia mabarabarani, ulimwengu mzima utataharuki, ndege zitaanguka, ajali nyingi zitatokea duniani, amani itapotea ghafla na watu watakuwa wakilia na kuomboleza, wakimwona mpinga-kristo akipanda kutoka kuzimu kuleta uharibifu duniani kote. Lakini Je! ni kweli unyakuo utakuwa kwa namna hiyo kulingana na maandiko?. Tukisoma;

1wathesalonike 4:16-17 "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na MWALIKO, na SAUTI YA MALAIKA MKUU, na PARAPANDA YA MUNGU; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele".

Tukiyachunguza haya maandiko hapa juu tunaona kuwa kuna hatua tofauti tatu zitakazoambata na kuja kwa Bwana Yesu kulichukua kanisa lake: Hatua ya kwanza: Bwana atashuka kutoka mbinguni na 'MWALIKO'.na hatua Ya pili: Bwana atashuka na 'SAUTI YA MALAIKA MKUU'..na hatua Ya tatu: Bwana atashuka na 'PARAPANDA YA MUNGU'. Hii inaashiria kwamba kuja kwa Bwana kutakuwa ni kwa hatua za kufuatwa.na sio ghafla tu kama inavyodhaniwa. Tunapaswa tuzitambue tambue ili tusiwe gizani kwa jinsi siku zinavyokaribia, Hebu tuzitazame hizi hatua tatu kwa undani zaidi.

HATUA YA KWANZA:

Biblia inasema 1wathesalonike 4:16 "Bwana atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko" sasa hili neno “mwaliko” kama linavyozungumziwa hapo halimaanishi ule mwaliko wa kama mtu anaalikwa kwenye sherehe fulani hapana! Bali inamaanisha Kilele za nguvu zinazoambatana na nderemo na vifijo kuashiria kuwa mtu fulani wa kipekee anakaribia kuwasili mfano,Raisi, Bwana arusi n.k,... Hii ni kwa kusudi la kumfanya mtu anayemngojea kujiweka tayari kumlaki atakapofika langoni mwake, ili isiwe ghafla ghafla.

Hivyo Tukisoma kwenye tafsiri nyingine za biblia, mfano ile biblia ya kiingereza KJV inatuambia..
''For the Lord himself shall descend from heaven with a SHOUT, with the voice of the archangel, and with the trump of God: and the dead in Christ shall rise first:"

Sasa Hapo neon 'Shout' linamaanisha ni kupaza sauti kuu za kelele kwa nguvu, ili kumfanya mlengwa aamke au awe makini kujianda na tukio linalokwenda kutokea mbele.

Ili tuelewe vizuri juu ya maneno haya na jinsi mwaliko ulivyo, tupitie baadhi ya vipengele vya maandiko, kama tunavyosoma mfano wa wale wanawali kumi. Katika Mathayo 25, tunasoma…

Mathayo 25:1-13" 1 Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.
3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;
4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.
5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.
6 Lakini usiku wa manane, PAKAWA NA KELELE, Haya, bwana arusi; TOKENI MWENDE MKUMLAKI.
7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.
10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa. "

Hivyo turudi katika kizazi hichi tuishicho, sote tunajua kuwa kuja kwa Bwana wetu YESU KRISTO kumefananishwa na wale wanawali kumi waliokuwa wakingoja kumlaki Bwana wao atakapokuja waende naye arusini, Na tunaona ilipofika usiku wa manane wote waliishiwa nguvu, na kusinzia kwa kuona Bwana wao anakawia kwa kungojea sana, Lakini ghafla usiku ule ule pakawa na ''KELELE kubwa ikisema Tazama! Bwana arusi anakuja''.

Kwahiyo kitendo kile cha zile kelele kuwaamsha hawa wanawali 10 kutoka usingizini huo ndio ule 'Mwaliko' unaozungumziwa pale kwenye ( 1wathesalonike 4:16-17). ambapo biblia inasema, Bwana atashuka pamoja na mwaliko… ni kwa dhumuni la kumwamsha bibi arusi ili ajiweke tayari kwa kwenda kumlaki Bwana wake. Na kama huo mwaliko usingepita kwanza hakuna mwanawali yoyote angeweza kutambua kuja kwa Bwana wake, wote ingewajia kama mwivi, Hivyo jambo hili kutangulia ni mahususi ili kumfanya aamke usingizini na kuaacha mambo yake anayoyafanya yote aanze kuiweka taa yake sawa, kwasababu muda waliokuwa wanauongojea umewasili.

Lakini Hatua hii ilianzia wapi katika kanisa?

Kanisa lilipokuwa limelala katika vipindi vyote vya nyuma baada ya roho ya mpinga Kristo kuliharibu, na kulipindua kama tunavyosoma katika historia ya ukristo jinsi kanisa lilivyopitia katika kipindi kirefu cha giza, na jinsi lilivyoingia katika mafundisho ya upotofu pale ukristo ulipooana na upagani na kuendelea hivyo kwa muda mrefu sana wa mamia ya miaka..Sasa muda wote huo ulikuwa ni muda kanisa lilikuwa limelala, Lakini ulipofika wakati wa Bwana kushuka kulijilia kanisa lake tena, hakuja ghafla, kwasababu hakuna ambaye angestahili kwenda naye, alianza kwanza na kutanguliza Mwaliko wake, ni ujumbe wa kumwamsha kwanza bibi arusi kutoka usingizini yaani (mwaliko) na kumfanya aiweke tayari taa yake na ahakikishe pia inayo mafuta ya ziada (mafuta ni Roho Mtakatifu na mafuta ya ziada ni ufunuo wa Roho wa Mungu).

kwahiyo huu MWALIKO ni UAMSHO wa Roho ambao unatangaza ujio wa Bwana Yesu kulichukua kanisa lake na watu wajiweke tayari kumpokea Bwana wao. Kama tulivyoona katika

(Mathayo 25:6..na ilipofika usiku wa manane pakawa na ''KELELE Bwana arusi anakuja''). Sasa huu mwaliko ulianza na Martin Luther mjumbe wa kanisa la tano, ukaendelea hivyo hivyo na John Wesley mjumbe wa kanisa la sita, Na mwisho Bwana aliutoa tena kwa kupitia mjumbe wa kanisa la saba William Branham,.. Kumbuka sauti hiyo ya mwaliko ilianza kusikika kutoka mbali, na ilivyokuwa inazidi kukaribia ndivyo ilivyozidi kuwa kubwa zaidi, Hivyo sauti ya mwaliko wa kanisa hili la mwisho la Laodikia ni kali, kuliko ilivyokuwa kwa kanisa la tano au la sita. Kwasababu Bwana yupo mlango kufika amtwae Yule mwanawali mwerevu aliyeitii sauti ya mwaliko. Kumbuka ndugu Ujumbe tulionao sasahivi ni KUTOKA kabisa katika mifumo ya dini na madhehebu na kuishi maisha ya utakatifu, Ni kuishi kama mtu anayemngojea Bwana wake, Huko ndiko kuzitengeneza Taa zetu.

Luka 12: 35 “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA;
36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, ATAKAPORUDI KUTOKA ARUSINI, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
38 Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao”.

Unaona hapo?..MWALIKO wa kuja kwa Bwana ulishaanza tangu wakati wa kanisa la tano, na la sita, na unaendelea na la saba. Ulianza na Martin Luther, kwa ujumbe wa kuwahubiria watu watoke, kutoka katika ile dini ya uongo(Katoliki). Ndipo kuanzia huo wakati bibi-arusi wa kweli wakaanza kuzitengeneza TAA zao, lakini cha kusikitisha ni baadhi yao hawakuwa na mafuta ya kuwatosha ya ziada (Ufunuo wa Roho),kuwawezesha kudumu katika hayo mpaka Bwana wao atakapokuja, hivyo kilichowatokea ni wao kudumu katika dhehebu linaloitwa Lutherani, hawamruhusu tena Roho wa Mungu kufanya kazi ndani yao, wakawa wametosheka na mapokeo yao tu, hawakujua kuwa inawapasa wapige hatua nyingine katika kumjua Mungu,..[Wanadamu tumeumbiwa kukua kila siku, katika mambo yote, kadhalika na mambo ya rohoni ukiona hukui jua tu kuna tatizo mahali Fulani.]

Kadhalika John Wesley mjumbe wa kanisa la sita naye pia aliutangaza ule mwaliko kwa nguvu zaidi kuliko Luther wengi walitengeneza taa zao lakini ulipofika wakajitengenezea dini na kusababisha taa zao nao kuzima, na katika kanisa la mwisho la Laodikia Bwana alimnyanyua mjumbe wake tena Ndugu. William Branham na sauti kubwa na ya mwisho ya mwaliko kuwaambia watu watoke wakamlaki Bwana wao maana ameshafika na muda umekwisha, sasa bibi-arusi wa kweli atatoka katika hili kanisa la mwisho kwa kutii sauti ya mtumishi wake na kwenda katika hatua inayofuata yaani ya “sauti ya Malaika Mkuu”, lakini pia kama makanisa mengine ya nyuma yalivyomzimisha Roho kwa kujiundia madhehebu kadhalika na katika kanisa hii la Mwisho wapo waliojiundia dhehebu, na kujiita wa-Branhamu, kama tu wafuasi wa Luther walivyojiita wa-luther, kadhalika na kundi hili pia halitafika katika hatua inayofuata ya sauti ya malaika mkuu, kundi hili litaishia njiani, kwasababu limemzimisha Roho, kumbuka Bwana hajawahi kuleta dhehebu lolote, Bwana huwa analeta UAMSHO kama ilivyotokea siku ya Pentekoste, madhehebu yote ni mifumo ya wanadamu inayodai kumtafuta Mungu lakini ndani yake imejaa mapokeo ya wanadamu na dogma zinazochukua nafasi ya Roho Mtakatifu, na kumzimisha kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba anaonekana mwanadamu au mapokeo zaidi ya YESU KRISTO Mungu wetu,na ndio maana Bwana kayakataa.

Hizi ni nyakati za mwisho, utafika wakati utatamani sekundi moja ya kuwa mtakatifu utakosa, siku hiyo utakapogundua kuwa umeachwa, leo unahubiriwa tunaishi katika siku za mwisho unadhihaki unasema Bwana Yesu hawezi kurudi kizazi hiki,bado sana, ni kweli hatujui siku wala saa lakini alitupa majira ya kuja kwake na dalili zote zinaonyesha kuwa tunaishi katika kizazi ambacho tukashuhudia kuja kwa pili kwa Yesu Kristo. Kwahiyo kama hautaweza kuitikia hii sauti ya MWALIKO kwa kujiweka tayari kumpokea Bwana sasa kama mwokozi wako, na kwa kupokea Roho Mtakatifu na kuishi maisha yampendezayo Mungu ya utakatifu sawa sawa na NENO na sio sawasawa na dhehebu lako au dini yako, hautawezi kuendelea hatua inayofuata, na wala hautaijua, utafanana na wale wanawali wapumbavu waliokosa mafuta katika taa zao. Tunaishi katika wakati wa matenganisho, Bwana anawatenga wanawali werevu kutoka katika wanawali wapumbavu, anatenga magugu na ngano, magugu atawatuma watu (manabii wa uongo) wayafunge matita matita (madhehebu) na ngano atawatuma watumishi wake wayakusanye(kwa ajili ya unyakuo) ghalani mwake. Je! Wewe upo kundi gani?

HATUA YA PILI:

1 wathesalonike 4:16 "BWANA ATASHUKA NA SAUTI YA MALAIKA MKUU"
Hii ni hatua ya pili na itawahusu tu wale waliokwisha kuisikia sauti ya mwaliko(yaani wanawali werevu), wale ambao wamekwisha weka taa zao tayari wakiwa na mafuta ya ziada ambayo ni Roho Mtakatifu na Roho ya ufunuo (ya kutaka kumjua Mungu zaidi na zaidi pasipo kumzimisha ndani yao) hawa ndio wale wanawali wenye busara. 
 
Tunapaswa tujiulize hii sauti ya Malaika Mkuu ni ipi??
Tukisoma Katika kitabu cha..
 
ufunuo 10:1-7 " Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto. 2 Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi.
3 Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao.
4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.
5 Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni,
6 akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya;
7 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii."

Huyu Malaika mwenye nguvu anayezungumziwa hapa akishuka kutoka mbinguni ni BWANA YESU KRISTO, kumbuka neno malaika maana yake ni “mjumbe” na Bwana Yesu anajulikana kama “mjumbe wa Agano” Malaki 3: 1 “Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule MJUMBE WA AGANO mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi”.
 
Na hapa kwenye ufunuo anaonekana akiwa ameshika kitabu kidogo, na hichi kitabu si kingine zaidi ya kitabu cha ukombozi wa mwanadamu, ndio kile kilichokuwa kimetiwa mihuri saba, Ufunuo 6 na tunasoma pia aliapa “hakutakuwa na wakati baada ya hapa” kuashiria kuwa muda utakuwa umeisha wakati atakapokuwa anazungumza, tunaona pia alipolia kwa sauti kuu kama simba angurumavyo zile NGURUMO SABA zikatoa sauti zao ambazo Yohana aliambiwa asiziandike, hizo ni siri ambazo hazijarekodiwa mahali popote katika biblia ni siri zitakazokuja kufichuliwa katika hatua hii ya pili, na ni kwa ajili tu ya kumpa bibi arusi imani ya kwenda katika unyakuo.

Kwahiyo hii ya SAUTI YA MALAIKA MKUU ni siri ya zile ngurumo saba, ambazo zitakuja kuhubiriwa kwa bibi-arusi aliyeko ulimwenguni kote,Hizi ngurumo saba zitakapotoa sauti zao ndipo bibi arusi atapata imani kamili ya kwenda kwenye unyakuo, katika uamsho huu yatahubiriwa mambo ambayo hayajaandikwa katika biblia, haimaanishi kwamba yatapingana na biblia hapana bali ni mambo ambayo hayajarekodiwa katika biblia yatakuwa ni ufunuo wa mambo mapya mahususi tu kwa wale wakristo ambao wameitikia wito wa sauti ya mwaliko.Uamsho huo hautakuwa wa watu wote wa dunia nzima, hapana bali utakuwa ni wa kikundi kidogo sana Bwana alichokipa neema kuvuka hatua ya kwanza ya mwaliko.
 
Mungu alikuwa na makusudi kwanini alimwambia Yohana asiziandike zile ngurumo saba kwa wakati ule, ni kwa sababu maalumu zije zifunuliwe kipindi cha siku za mwisho katika hatua hii ya pili,kwa bibi arusi wa Kristo aliyewekwa tayari, ni siri zilizoandikwa katika kile kitabu kidogo kilichokuwa kimeshikwa na yule malaika mkuu(Yesu Kristo). Wakati huo hizo ngurumo zitakapokuwa zinatoa sauti zao, hawa wengine hawatafahamu chochote, kwao wataona kama ni imani mpya imezuka duniani..Lakini walio na Roho Mtakatifu kweli kweli watafahamu kwa uweza wake, kutaambatana na maagizo ya kufuata mahususi kwa bibi-arusi wa Kweli.

kwahiyo hiyo Huyu MALAIKA MKUU tuliyemsoma kwenye 1Thesalonike 4:16 , ndiye huyo tunayemwona katika kitabu cha ufunuo sura ya kumi aliyetoa zile ngurumo saba. Na si mwingine zaidi ya Bwana Yesu Kristo.
 
HATUA YA TATU:
Hatua hii ni ya mwisho na inahusu PARAPANDA YA MUNGU .Tukisoma 1wathesalonike 4:16" Inasema..Bwana atashuka na parapanda ya Mungu. nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele"

Hii ni sauti ya parapanda ya YESU kwa wafu kwa ajili ya ufufuo, hapa ndipo wafu watakapoisikia sauti ya Mungu ikiwaita huko waliko nao watafufuka na kuivaa miili ya utukufu na kuungana pamoja na wale walio hai na kwenda kumlaki Bwana mawinguni, kama vile Lazaro alivyoisikia sauti ya Bwana ilipomwambia njoo huku nje Yohana 11:43 naye akafufuka. ndivyo itakavyokuwa kwa wafu waliokufa katika Kristo siku ile watakapoisikia sauti ya parapanda ya mwisho.

Yohana 5:25 Inasema.. "Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai." 
 
Hii ndio hatua ya mwisho na sisi tulio hai miili yetu itabadilika kufumba na kufumbua na kuungana na waliofufuliwa kwenda mbinguni kwa BWANA WETU YESU KRISTO.
 
Na sio wakristo wote watanyakuliwa bali wale tu walioitikia mwaliko, na sauti ya malaika Mkuu, na hatua hii inafananishwa na “check-in procedures” katika safari za ndege.
 
Na kumbuka sio watu wote watafahamu kama unyakuo umepita watu wasiofahamu wataendelea na shughuli zao kama kawaida, itakuwa ni siri hakutatokea vurugu wala ajali mabarabarani, kama kukitokea vurugu mpinga-kristo atafanyaje kazi sasa hapo? Na nani atashawishika kupokea chapa ya mnyama? Ni dhahiri kuwa hakuna atakayeshawishika kwasababu watu wote watamjua mpinga-kristo amefika, na unyakuo hapo utakuwaje wa siri tena?? lakini siku hiyo wengi hawatamjua mpinga-kristo wala chapa yake kwasababu hatakuja akiwa na mapembe, atakuwa ni mtu anayeheshimika,na kukubalika na dunia, atakuja na kivuli cha amani, na atapendwa na wengi, na atakuwa ni mtu wa kidini, na anashika biblia, lakini ndani yake ni utendaji kazi wa shetani wenyewe, atawadanganya wengi waipokee ile chapa, na ni muhimu pia kufahamu namba 666 sio chapa ya mnyama, hilo ni jina la mnyama na sio chapa yake, chapa yake ni kitu kingine kabisa. Ikiwa namba 666 ndio chapa yake, watu wengi pia siku hiyo wataikataa, lakini siku hiyo mamilioni ya watu wataipokea kwasababu hawataijua, Hivyo ni kuwa makini sana na hizi nyakati.

Ndugu mpendwa ujue mpaka wakati huu tuliopo unyakuo umeshakwisha kuanza,na hatua ya kwanza ya mwaliko ndiyo tuliyopo sasa ni wakati wa kutengeneza taa zetu tuhakikishe tumepokea Roho Mtakatifu na tumeitikia vizuri UJUMBE WA SAA HII ambao ni KURUDI KATIKA UKRISTO WA BIBLIA na kutoka katika mifumo ya madhehebu ambayo yamewapofusha wengi macho na yamewasababishia wafanye uasherati na yule mama wa makahaba( ufunuo 17) ambalo ni kanisa la roman katholiki. Hivyo basi kwa kuitikia hivyo inatufanya sisi kuwa bikira safi waliotayari kumlaki Bwana.

Hatua inayofuata itakuwa ni zile Ngurumo saba na watakaoweza kuzipokea ni wale bikira safi tu na ndiyo hatua tunayoisubiria sasa na iko mbioni kutokea, uamsho mkubwa unakuja mbeleni, siri hizo hazitaweza kueleweka na mtu wa kawaida asiyekuwa na Roho wa Kristo.Kisha baada ya hapo ni parapanda ya mwisho ya kwenda kumlaki Bwana mawinguni wafu watafufuliwa na sisi tutaungana nao kwenda mbinguni ndio siku hiyo mmoja atatwaliwa na mmoja ataachwa, kama Elisha alivyotwaliwa na Eliya kuachwa kama Henoko alivyotwaliwa na Nuhu kuachwa. Ni kwasababu gani? Ni kwasababu Eliya alikuwa na ufunuo wa ziada zaidi ya Elisha, na kadhalika Henoko alimpendeza Mungu na alikuwa ana ufunuo wa ziada zaidi ya Nuhu, hivyo wakashuhudiwa kwamba hawataonja mauti ni bibi-arusi wa siku za mwisho aliyepita hatua ya kwanza, atashuhudiwa kuwa hatakufa hata atakapomwona Bwana akija mawinguni, kuja kwa Bwana kwake hakutakuwa siri, atajua siku atakapoondoka,

1 Wathesalonike 5: 1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.
8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu”.
 
je! bado unafanya mzaha na haya maisha katika hichi kipindi cha hatari tunachoishi sasa cha kuja kwa BWANA YESU KRISTO kwa mara ya pili,? bado unaupenda ulimwengu unaokwenda kuisha, unaendelea kuwa mwasherati, mlevi,mwongo,mwizi, una majivuno,mlafi,kusengenya, kuvaa vimini, mawigi na mahereni, na kupaka wanja, lipstick, na fashion?? Bado unaendelea kuwa mlevi,na mtazamaji pornography, bado unaendelea kuwa msagaji, mlawiti na mfanyaji masturbation? Bado unaendelea kuwa mtukanaji, Kuzimu! Ipo usidanganyike!Tafuta Roho Mtakatifu Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, Muda umeenda sana. Leo hii tubu kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi kwa jina la Yesu Kristo, kisha Bwana mwenyewe atakupa ahadi ya Roho Mtakatifu aliyowaahidia waitakayo.
 
Mungu akubariki sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine ili wapone na Mungu atakubariki.

Kwa mafundisho mengine mengi unaweza