"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Monday, September 30, 2019

MWANZO WA UTUNGU.

Mwanzo wa Utungu maana yake, sio mwisho wa Utungu...Bwana aliposema katika Mathayo 24:7 " Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali. 8  Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu".  Alimaanisha kuwa ndio utakuwa mwanzo wa Matetemeko na vita, kwahiyo Kwa kipindi chote kabla ya Kurudi Kwa Kristo vita vitakuwepo vingi, ndio maana kila kukicha tetesi za vita, na vita vya dunia tayari vimeshapiganwa zaidi ya mara mbili...kadhalika na matetemeko ya ardhi yamekuwepo mengi... mengine makubwa na yanayoanzia katikati ya sakafu ya bahari.

Lakini hiyo pia inamaanisha kuwa siku utungu utakapoisha na hatua ya kuzaa mtoto itakapofika ndipo maumivu yatakapoongezeka zaidi...ule utungu unajizidisha mara nyingi zaidi ingawa kwa kipindi kifupi..

Na siku za Mwisho wa Utungu wa huu ulimwengu, maumivu yatazidi mara nyingi zaidi, Vita vitaongezeka zaidi ingawa kwa muda mfupi, kadhalika Matetemeko yataongezeka ingawa kwa muda mfupi.

Vita vya kwanza na vya pili viliitetemesha dunia, lakini hivyo vyote si kitu dhidi ya Vita ya tatu ya dunia itakayokuja ya HARMAGEDON...Kadhalika matetemeko ya Tsunami na mengine si kitu dhidi ya Matetemeko ya Nchi yatakayokuja yatakayohamisha visiwa na Milima.

Bado tupo kipindi cha Utungu, muda mfupi sana ulimwengu utaingia kipindi cha Kuzaa, siku hizo watakatifu watakuwa wameshanyakuliwa.

Je utakuwepo kwenye unyakuo?..Umempa Bwana Yesu maisha yako, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na Kwa Jina la YESU KRISTO?


Ubarikiwe.

Bofya hapa kwa masomo zaidi ya Biblia >>> WWW.WINGULAMASHAHIDI.ORG


Saturday, September 14, 2019

TANGAZO


⇛Shalom!, tunapenda kutoa taarifa kuwa, kuanzia sasa, ukurasa wetu wa "mafundisho" utakuwa unapatikana katika website yetu hii  

WWW.WINGULAMASHAHIDI.ORGMasomo yote mapya yatakuwa yanapatikana katika tovuti yetu hapo juu au Bofya Hapa chini Kukupeleka moja kwa moja kwenye ukurasa wetu huo