"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Thursday, December 28, 2017

UFUNUO 14

Kama tunavyofahamu baada ya wakati wa mataifa kuisha yaani unyakuo kupita itakuwa imebaki miaka 7 tu mpaka dunia kuisha, ndani ya hicho kipindi kifupi Mungu atakuwa anashughulika na Taifa la Israeli, na kuwatia muhuri wale wayahudi 144,000 kama tunavyosoma katika sura ya 7 ya kitabu cha Ufunuo, kwahiyo ile miaka mitatu na nusu ya kwanza itakuwa ni injili kwa wayahudi na ile miaka mitatu na nusu ya mwisho itakuwa ni wakati wa ile DHIKI KUU.

Tukiendelea na ufunuo sura ya 14 ambayo ni mwendelezo wa habari ya wale wayahudi 144000 waliotiwa muhuri na Mungu, kama haujapitia sura ya 7, unaweza ukaanzana nayo kwa kufuata link hii kisha ndio tuendelee na sura hii ya 14 >>>>>

Ufunuo 14:1-5" Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
2 Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao;
3 na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi.
4 Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.
5 Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.

Hapa tunaona wale wayahudi 144000 wakionekana wakiwa na mwanakondoo juu ya mlima Sayuni ikifunua nafasi za hawa wateule wa Mungu mbele za YESU KRISTO,katika utawala unaokuja wa miaka 1000, watakapomiliki na kutawala na YESU katika mlima Sayuni (yaani Yerusalemu), pia hawa wanaonekana ni bikira ikiwa na maana kwamba hawajajitia unajisi wowote na mafundisho ya dini za uongo,

Na pia kama tunavyoona walijifunza wimbo mpya ambao ni wao tu waliouweza kuuimba, sasa huu wimbo unamaana kuwa ni "furaha ya Roho Mtakatifu", kama vile sisi wakristo tunapompokea Kristo na Bwana anapotuokoa na kutupa pumziko pale tunapomfurahia na kumshukuru wimbo mpya wa Mungu unazalika ndani ya mioyo yetu ambao hakuna mwingine anayeweza kuuimba isipokuwa mwenye Roho wa Mungu kama sisi

..Daudi alisema katika Zaburi 40:1 "Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.
2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
3 AKATIA WIMBO MPYA KINYWANI MWANGU, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana ".

Kwahiyo hawa 144000 baada ya kutiwa muhuri wa Mungu kwa kupokea Roho Mtakatifu na kupata ufunuo kwamba mwokozi wao anaishi na ndiye atakayekuja kuwapigania wimbo mpya utazaliwa ndani ya mioyo yao ambao hakuna mwingine yoyote atakayeweza kujifunza isipokuwa wao,

Na pia kumbuka watu hawa hawakuwa mbinguni, bali ni hapa hapa duniani, ukisoma kwa makini utaona sio wale 144000 ndio waliokuwa mbinguni mbele ya kiti cha enzi wakiimba hapana bali ni sauti ilisikiwa mbinguni wakiimba na hawa si wengine zaidi ya malaika, na ndio wale 144000 walionekena wakijifunza wimbo ule. Hivyo hawa 144000 hawakunyakuliwa mbinguni, bali watakuwa hapa hapa duniani.

INJILI YA MILELE:

Tukiendelea.. Ufunuo 14:6-13" 6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
8 Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.
9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,
10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.
12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.

Katika mistari hii tunaona baada ya wale 144,000 kutiwa muhuri, na Bwana akiwaweka mbali na yule mnyama watafunguliwa pia na mlango wa kuhubiri INJILI YA MILELE. Na ndio wale malaika watatu tunaona wakiruka katikati ya mbingu wakihubiri injili ya milele juu yao wakaao juu ya nchi, kumbuka Mungu hajawahi kutumia malaika kuhubiri injili duniani, siku zote huwa anawatumia wanadamu, biblia inasema malaika ni roho zitumikazo kuwahudumia watakatifu(waebrania 1:14). Hivyo watakaozihubiri hizi jumbe za wa hawa malaika warukao ni wale wayahudi 144000.

Kumbuka Injili tuliyonayo sasa ni Matendo 2:38 "...Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu ". Injili hii ni ya kuwafanya watu kuwa wakristo lakini INJILI YA MILELE ni kwa watu wote na inayojulikana na watu wote, kwamfano inajulikana kuwa ushoga ni kosa,usagaji, kuua ni kosa, kuzini, kutukana,ufiraji, kuzini na wanyama,kufanya maasi ni kosa, dhamiri ya mtu ikimshuhudia kabisa kuwa anachokifanya sio sahihi bila hata kuhubiriwa n.k. ni injili ambayo kwa ufupi hahiitaji biblia kuijua, inajulikana na watu wote wenye dini na wasio na dini. Hiyo ni hofu ya Mungu ambayo ipo kwa kila mwanadamu.

Kwahiyo INJILI hii ya MILELE itahubiriwa tena kwa mara ya mwisho kwa wanadamu wote waliopo ulimwenguni wanaotenda maasi ili mtu asiwe na udhuru wa kusema sijasikia, kwa maana kwa wakati huo maasi yatakuwa ni mengi sana duniani kama tunavyoyaona leo...

Warumi 1:18 "Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
19 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana YAMEKUWA DHAHIRI NDANI YAO , kwa maana Mungu aliwadhihirishia.
20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, UWEZA WAKE WA MILELE NA UUNGU WAKE; hata wasiwe na udhuru; ........
32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao. "
Hivyo injili hii ya MILELE itagusa makundi yote hata wasiokuwa na dini, kwasababu ni mambo yaliyodhahiri ambayo yanajulikana na kila mtu.

Malaika wa pili akafuAata akisema “8 Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.”

Hawa watu 144000 baada ya kupokea ufunuo wa Mungu kuwa anayetawala dunia nzima na dini zote ni mpinga-kristo (PAPA) na jinsi kanisa Katoliki lilivyohusika kuwaua watakatifu wengi na litakapokwenda kuishia, kwamba Mungu ameshalihukumu hivyo watahubiri ujumbe wao katika dunia nzima, hukumu ya Babeli mkuu.

Tukiendelea mstari wa 9-11 tunasoma “9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,
10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.”

Sasa hili ni onyo la mwisho litakalohubiriwa kwa watu wote, kwamba mtu yoyote atakayemsujudia yule mnyama na sanamu yake (yaani Kushirikiana na Kanisa Katoliki na mafundisho yake au kuwa mshirika wa umoja wa madhehebu) au kuipokea chapa katika mkono wake au katika kipaji cha uso wake, atashiriki mapigo yote ya Mungu yanatakayofuata huko mbeleni.

Kumbuka hapo kanisa litakuwa limeshaondoka, watanyakuliwa watu wachache sana wakati huo ulimwengu hautajua chochote, dhiki zote zitawakuta wale waliobaki duniani, je umeokolewa?. kama biblia inavyoendelea kusema.. “13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao. "

SHINIKIZO LA GHADHABU YA MUNGU:

14 Kisha nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali.
15 Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa sauti kuu yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa.
16 Na yeye aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu wake juu ya nchi, nchi ikavunwa.
17 Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali.
18 Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana.
19 Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.
20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili. "

Mistari wa 14-20 unaelezea maandalizi juu ya ile vita ya Harmagedoni, vitakavyopigwa Israeli, Hapa tunaona malaika akiwa ameshika mundu mkali na kuvuna mzabibu wa nchi kuashiria maovu ya wanadamu yamefikia kilele, kikombe cha ghadhabu ya Mungu kimejaa wakati wa rehema hakuna tena, kinachofuata ni hasira ya Mungu kumwagwa juu ya nchi, na ndio maana unaona zile zabibu zikatupwa katika lile shinikizo kubwa la ghadhabu ya Mungu na damu ikatoka pale mpaka kwenye hatamu za farasi kwa mwendo wa maili 200, kumbuka farasi anawakilisha vifaa vya kijeshi, hii ni picha halisi inayoonyesha jinsi hiyo vita itakavyokuwa ya kumwagika damu nyingi hayo yatatimia katika kumiminwa kile kitasa cha sita kati ya vile saba vya ghadhabu ya Mungu..

Ufunuo 16:12-16"
12 Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.
Pia Ufunuo 19:11-16 Inasema..."11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.
15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, NAYE ANAKANYAGA SHINIKIZO LA MVINYO LA GHADHABU YA HASIRA YA MUNGU MWENYEZI .
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA."

Hii itakuwa ni vita ya mwisho mabilioni ya watu watakufa, na baada ya kumiminwa kile kitasa cha mwisho cha saba mwisho wa dunia utakuwa umefika. Kwa maelezo marefu juu ya vitasa 7 fuata link hii >>>> 

Hivyo ndugu kumbuka shetani hapendi ukifahamu kitabu cha UFUNUO kwasababu anajua siku ukiyajua mambo ya kutisha yanayokuja huko mbeleni utatubu na kuishi maisha ya uangalifu hapa duniani, yeye anachotaka ujue ni kuwa dunia itadumu milele na ni raha tu siku zote lakini biblia usisahau inasema 1wathesalonike 5:3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. "

Huu ni wakati wa jioni sana BWANA YESU yupo mlangoni kurudi kulinyakua kanisa lake je! na wewe utakuwa miongoni mwa wale watakaokwenda naye? Ni mara ngapi umesikia injili ubadilike lakini bado unaabudu sanamu, unapenda mambo ya ulimwengu huu zaidi ya Mungu , unavaa vimini, unapaka lipstick, unazini, mlevi, msengenyaji, mtukanaji,? Injili hiyo halitadumu milele, upo wakati mlango wa neema utafungwa hapo ndipo Bwana Yesu anasema kutakuwa na kilio na kusaga meno.

Mpe Bwana maisha yako leo uokolewe.

Mungu akubariki.

Wednesday, December 27, 2017

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 20

SWALI 1:  kumekuwa na mjadala mkubwa kati ya wakristo kuhusu suala la sabato,Wapo,wanaosema j2 na pia wapo wa jmosi..je! ni wapi walio sahihi?


JIBU:Neno la Mungu linasema Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa wamwabudu katika roho na kweli. Wakristo hawahesabiwi haki mbele za Mungu katika siku, miezi au miaka ya kuabudia, aidha uabudu j2, j3, jmosi au j5 huo ni utaratibu wako tu! haimuongezei mtu chochote katika uhusiano wake na Mungu. Biblia inasema..

wagalatia 4:9 "Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka. "

Na Pia inasema tena.....

Wakolosai 2:16 "Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO;  mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

Hivyo Maana ya NENO sabato ni "pumziko", na pumziko kwa wakristo lipo rohoni, na Yesu ndiye BWANA wa sabato hivyo ukimpata YESU umepata SABATO au "pumziko la rohoni" na ndio maana anasema.. mathayo 11:28

"28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami NITAWAPUMZISHA.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. "

Kwahiyo wanaoabudu jmosi, au j2 au j3 hawafanyi makosa, ni utaratibu wao tu, kwa mfano tunasoma katika biblia wakristo wakwanza waliiteua siku ya kwanza ya juma ( yaani JUMAPILI) kwa ajili ya kukusanyika na kufanya changizo pamoja na kumega mkate,soma  matendo 20:7 pia 1wakoritho 16:1-2, kwahiyo sio shida kwa mantiki hiyo  lakini ibada halisi ipo rohoni na Mungu anaabudiwa katika roho na kweli, na sio katika siku maalumu au miezi au miaka bali ni kila saa na kila wakati.


 SWALI 2:Mpendwa habari katika mambo yanayo niumiza sana kichwa ni suala KUZIMU ,hivi kuzimu wanaishi watu au kukaa na je Watu hupata mateso? zipo shuhuda nyingi zinazo nigusa moyo wangu kuhusu kuzimu.
JIBU: Kuzimu ipo, na ni sehemu iliyo halisi kabisa...
Mtu anapokufa katika dhambi (yaani haujaoshwa dhambi zake kwa damu ya YESU KRISTO)..mtu anaenda  moja kwa moja kuzimu/jehanum, huko kuna mateso mengi sana, mtu huyo atakaa huko akingojea ufufuo wa wafu, ambao utakuja baada ya ule utawala wa YESU KRISTO wa miaka 1000 kuisha ambapo wafu wote watafufuliwa na kuhukumiwa mbele ya kile kiti cheupe cha Hukumu..
Ufunuo 20: 12 "Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto".

Ukisoma pia Yohana 5:28 BWANA YESU aliyasema maneno hayo.." Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu. "

Unaona wale wanaotenda mabaya wote watafufuliwa kwa ufufuo wa hukumu, hivyo baada ya kuhukumiwa kulingana na matendo yao ndipo watakapotupwa kwenye lile ZIWA LA MOTO atakapokuwepo shetani na malaika zake, lenye mateso mengi kuliko jehanum. ni kama tu vile mtu anapokamatwa na hatia anawekwa kwanza mahabusu kwa muda fulani akisubiria kupandishwa mahakamani, sasa akishahukumiwa mahakamani kulingana na makosa yake ndipo anapopelekwa magereza kutumikia makosa yake. na ndivyo itakavyokuwa kwa waovu wote walioikataa neema ya msalaba wa Bwana YESU KRISTO watakapokufa sasa hivi wataenda kuzimu kwenye vifungo na mateso, wakingojea hukumu ya mwanakondoo kisha baadaye watatupwa kwenye lile ziwa la moto.

Lakini wanaokufa sasa katika haki, wanapelekwa mahali panapoitwa  "Paradiso" . Paradiso ni mahali panapofanana na mbinguni,lakini sio mbinguni, ni mahali pa raha, wanawekwa humo kwa muda fulani wakingojea ufufuo wa wenye haki, atakapokuja Bwana mawinguni, watafufuliwa na kuvaa miili ya utukufu na kuungana na watakatifu walio hai na kwa pamoja kwenda na Bwana mbinguni kwenye karamu ya mwana kondoo.

1 Wathesalonike 4: 15 "Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele."


SWALI 3:Mtumishi nakuomba unipe majibu ya haya maswali, 1).Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli?  2).Mkristo wa Kweli Anaruhusiwa Kunywa Pombe/kuvuta sigara? 3).Ubatizo Wa Mkristo Wa Kweli Ni Wa Namna Gani?


JIBU:1) Hakuna tatizo lolote kula nyama ya nguruwe au chakula chochote ambacho mtu anaweza kukipokea kwa shukrani mbele za Mungu...biblia inasema viumbe vyote vimetakaswa na Mungu, Tukisoma  1Timotheo 4:1-5 inasema.. "Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru WAJIEPUSHE NA VYAKULA, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. "

Hivyo vyakula vyote ni halali lakini biblia inasema tule kwa IMANI, ila tukila kwa mashaka ni dhambi, na pia biblia inasema anayekula asimuhukumu asiyekula, wala asiyekula asimuhukumu anayekula, haupaswi kumkwaza mwenzako kwa ujuzi wako, ukimkosea mwenzako kisa hali nguruwe ni sawa na kumkosea Kristo mwenyewe 1wakorintho 8:13 inasema "Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu."....."8 Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu.
Na pia tukisoma warumi 14:14 -17 "Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.
15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.
17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.

2) Mkristo wa kweli haruhusiwi kunywa pombe wala kuvuta sigara wala kuuharibu mwili wake kwa namna yoyote ikiwemo kuchora alama kwenye miili, kwasababu biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, hivyo hekalu la Mungu lazima liwe ni safi,

3) Kuhusu ubatizo, ubatizo sahihi kulingana na maandiko ni wa kuzamishwa katika maji mengi, na inapaswa iwe ni kwa JINA LA YESU KRISTO, na sio kwa jina la BABA na Mwana na Roho Mtakatifu, kama inafanyika kimakosa na makanisa mengi, kwa ufafanuzi mrefu kuhusu UBATIZO SAHIHI fuata link hii.>>>https://wingulamashahidiwakristo.blogspot.com/2016/09/ubatizo-sahihi_28.html#links
SWALI 4: Kuna aina ngapi za ubatizo?

JIBU: Kuna aina 3 za ubatizo kulingana na maandiko ,wa kwanza ni-ubatizo wa maji, wapili ni ubatizo wa Roho mtakatifu, na watatu ni ubatizo wa moto (Mathayo 3:11)....huu ubatizo wa moto unafuata baada ya kupokea Roho mtakatifu ambapo Mungu anampitisha mtu katika majaribu mbalimbali  ili kuiweka imara imani yake huyo mtu, ndio usishangae mtu akishakuwa mkristo kuanza kukutana na changamoto mbalimbali mfano kutengwa na marafiki,au ndugu, kudhihakiwa imani yako, wakati mwingine mipango yako ya mwanzo yote inavurugika, wakati mwingine misiba, dhahabu ili ing'ae lazima ipitishwe kwenye moto, na sisi tunafananishwa na dhahabu safi mbele za Mungu, na pia Bwana Yesu alisema Marko 9:49" Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto". ...sasa huo ndio ubatizo wa moto Mungu anaompitisha mtu ili kuuondoa uovu na kumnyenyekeza mbele zake na kumweka katika njia ya kusudi lake..lakini ni kwa muda tu, Mungu akishakwisha kukutengeneza anakufanya uwe chombo bora kwa kazi yake.


SWALI 5:  BWANA YESU asifiwe! Naomba kuuuliza swali.
Hivi ni kweli kwamba, ukimuombea mtu aliye uawa na wachawi anaweza kurudi tena??? Na Je, utakitambuaje kifo halisi au cha kiini macho????

 
JIBU: Mchawi anapokuua ni sawasawa na mtu yeyote anavyoweza kukuua wewe, au jambazi kumuua mtu asiyekuwa na hatia..wote wanao uwezo wa kusababisha kifo halisi  kwa mtu

Lakini kuna vifo vingine vinaonekana kama ni vifo halisi lakini kumbe sio, unakuta huyo mtu bado anaishi sehemu nyingine hajafa, watu wanawaita misukule n.k sasa hawa hawajafa bali wamehamishwa tu, na wanaweza kurudishwa kwa njia ya maombi kwa jina la Yesu.
Na pia kuhusu namna ya kutambua kama ni kifo halisi au kiini macho hayo ni mambo ya rohoni ambayo Bwana anaweza akakufunulia au asikufunulie, na kama hujafunuliwa na BWANA lakini wewe ukahisi tu, jambo ni moja tu, kuomba kwa imani maana biblia inasema yote yanawezekana kwa yeye aaminiye ..hapo haijalishi amechukuliwa kwa kiini macho au amekufa kifo halisi, atarudi tu!..lakini hayo yote yanafanyika kwa imani, vinginevyo hakuna lolote litakalotokea.

Ubarikiwe na BWANA YESU.

Wednesday, December 20, 2017

KITABU CHA UFUNUO: SURA YA 17

Karibu tujifunze kitabu cha Ufunuo leo tukiwa katika mwendelezo wetu wa sura ya 17, Biblia inasema...


Ufunuo 17:1-6"
1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.


Tukirudi nyuma kidogo kwenye ile sura ya 13, tunamwona yule mnyama aliyetoka baharini mwenye vichwa saba na pembe 10, akielezewa, jambo hilo hilo tunaliona tena katika hii sura ya 17 mnyama yule yule mwenye vichwa 7 na pembe 10 na majina ya makufuru ametokea tena, isipokuwa hapa katika sura hii ya 17 tunaona kuna jambo lingine limeongezeka; anaonekana MWANAMKE  AKIWA AMEKETI JUU YAKE. Kwahiyo msisitizo mkubwa katika sura hii ni juu ya huyo mwanamke aliyepambwa kwa dhahabu, lulu na vito vya thamani aliyeketi juu ya huyo mnyama.

Sasa mwanamke huyu ni nani?


Mwanamke katika biblia anawakilisha KANISA, Sisi wakristo tunatambulika kama BIBI-ARUSI wa KRISTO,(2Wakoritho 11:2 Paulo anasema "..Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo BIKIRA SAFI. ") Na pia..
Ufunuo 19:7 inasema.." Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na MKEWE amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing'arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.  Pia Taifa la Israeli Bwana alilitambua kama MKE WAKE" [soma ezekieli16:1-63, ezekieli 23] utaona jambo hilo. Hivyo mahali popote Mungu anapozungumza juu ya kundi la watu wake huwa analifananisha na mwanamke.

Lakini hapa tunaona mwanamke mwingine ametokea ambaye anaonekana ni KAHABA,  amelewa kwa DAMU za watakatifu na za mashahidi wa YESU, na tena wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.  Na katika kipaji cha uso wake ana jina limeandikwa, la SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

Hivyo tunaona tabia ya huyu mwanamke (ambaye anawakilisha KANISA fulani) kuwa ni KAHABA, Na kama tunavyofahamu kanisa la KRISTO haliwezi kuwa kahaba, kwasababu ni BIKIRA SAFI, na haliwezi kuua watakatifu wa Mungu, kwasababu lenyewe ni TAKATIFU, Hivyo hili Kanisa haliwezi kuwa lingine zaidi ya KANISA KATOLIKI chini ya uongozi wa PAPA.

Kwanini ni Kanisa  KATOLIKI na si kitu kingine?


Tunajua siku zote shetani anatabia ya kuunda "copy" inayofanana na ya Mungu ili aabudiwe kirahisi, au kudanganya watu kirahisi, vinginevyo asingeweza kupata wengi, ili noti feki iweze kufanya kazi ni lazima ifanane sana na orijino, shetani anataka kuabudiwa kama Mungu hivyo atatumia njia zote zinazofanana na za Mungu  ili apate wafuasi wengi. Na ndio maana Mungu alikataza Mtu kutengeneza mfano wa Kitu chochote kama Mungu ili kukiabudu kwasababu mtu anaweza akadhani anamwabudu Mungu kumbe anamwabudu shetani mwenyewe kwa kivuli cha ile sanamu pasipo kujua.ZIKIMBIE IBADA ZA SANAMU. Mimi sipo kinyume na wakatoliki, wala siwahukumu ndugu zangu wakatoliki, bali nipo kinyume na mifumo ya kanisa Katoliki kwasababu Mungu alishaihukumu, na kupiga mbiu watu wake watoke huko wasishiriki mapigo yake!.

Sasa mpango wa Mungu aliouunda tangu awali ni kumleta "MTU" atakayesimama kwa niaba yake ili kuwakomboa wanadamu (VICAR) katika dhambi zao hivyo akamleta mwanae anayeitwa YESU KRISTO, ambaye kwetu sisi ni Mungu mwenyewe katika mwili..shetani kuona hivyo akaanza kuiga kwa kumtengeneza mtu wake (VICAR), ambaye naye atasimama kwa niaba yake hapa duniani, na akampa jina lililo maarufu (VICARIUS FILII DEI) yaani tafsiri yake,  ni "Badala ya mwana wa Mungu duniani", hivyo huyu mtu wake anasimama hapa duniani badala ya mwana wa Mungu (yaani YESU KRISTO), na  shetani akamvika uwezo wake bandia kwamba na yeye anaweza kusamehe dhambi duniani kama vile BWANA WETU YESU KRISTO alivyo na uwezo wa kusamehe dhambi.
Na kama vile Mungu alivyounda kanisa lake takatifu kwa kupitia BWANA YESU KRISTO, ambalo ndilo linaloitwa BIBI-ARUSI safi, vivyo hivyo shetani naye alilitengeneza Kanisa lake kwa kupitia huyu (VICARIUS FILII DEII) yaani PAPA, Kutimiza kusudi lake la kutaka kuabudiwa na kupeleka watu kuzimu na hilo KANISA  ndilo KAHABA, Na si lingine zaidi ya KANISA KATOLIKI. 

Na tunajua Kanisa la Kristo safi linaongozwa na ROHO MTAKATIFU kwa kupitia zile huduma na karama za roho, yaani mitume, manabii,wachungaji, wainjilisti na waalimu lakini hili kanisa kahaba na lenyewe limevuviwa vyeo vya uongozi  kama Upapa, Ukadinali, upadre, paroko, ukasisi n.k.
Kwahiyo unaweza ukaona ni jinsi gani cha uongo kinavyofanana na cha ukweli, na watu wengi wamepofushwa macho na shetani wakidhani kuwa wanamwabudu Mungu hapo kumbe ni shetani.

Na ni kwasababu gani ni kahaba?


Ni kahaba kwasababu biblia inasema wafalme wa nchi wamezini naye nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo wa usherati wake, si ajabu Kanisa hili lina nguvu nyingi katika mataifa mengi kwa utajiri wake kwa jinsi linavyotoa misaada na miradi mingi ya kimaendeleo na ya kijamii, linajenga mashule na mahospitali linatoa misaada ya majanga na kusapoti siasa za nchi, linafanya hivi kwa lengo moja tu! kupumbaza mataifa na wafalme wa nchi ili kuwalewesha kwa kupenyeza mafundisho na itikadi zake za uongo kwa watu ambazo zipo nje ya MANENO MATAKATIFU YA MUNGU.

Na ndio maana tunaona mwanamke huyu ana jina limeandikwa kwa SIRI katika kipaji cha uso wake "BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA, NA MACHUKIZO YA NCHI"..Umeona hapo, jina lake lipo katika SIRI, hivyo inahitaji HEKIMA kumtambua, kwasababu shetani huwa hafanyi vitu vyake kwa wazi wazi, anatumia kivuli cha "orijino" ili kuwadanganya watu.

Ni BABELI mkuu kwasababu tafsiri yenyewe ya neno BABELI ni "MACHAFUKO", Hivyo Mji wa Babeli ndio ulikuwa chimbuko la machafuko yote, ibada za kipagani za kuabudu miungu mingi na uchawi ndipo zilipozaliwa, Nimrodi akiwa muasisi wa mji ule na mke wake Semiramis pamoja na mtoto wao Tamuzi, waliabudiwa kama miungu, ndipo baadaye Waroma wakaja kutohoa mfumo huo wa kuabudu miungi mingi, na sio ajabu tunaona baadaye wakaja kumweka Yosefu kama Nimrodi, Semiramis kama Mariam na Tamuz kama mtoto YESU ili kutimiza matakwa yao ya ibada zao za sanamu ambazo walikuwa nazo tangu zamani, kwakweli haya ni machafuko makubwa sana katika KANISA LA KRISTO.

Na mji huu huu wa Babeli baadaye ndio uliohusika kuutesa na kuuchukua uzao wa Mungu (ISRAELI) mateka, sasa hii ilikuwa ni Babeli ya mwilini iliyolichukuwa Taifa la Israeli mateka sasa hii iliyopo leo ni  BABELI YA ROHONI(ambayo ni kanisa Katoliki ) inawachukua wakristo wengi mateka kwa kuwafanya waabudu miungu mingine mbali na YAHWE  YESU KRISTO MUNGU WETU. 

Lakini Biblia inasema hakika BABELI HII ya sasa itaangushwa tu! kama ilivyoangushwa ile ya kwanza ya mwilini. Nadhani kuanzia hapo utakuwa umeanza kupata picha ni kwanini mwanamke yule anajulikana kama BABELI MKUU. Sasa tuone ni kwa nini anaitwa "MAMA WA MAKAHABA".

Ni Mama wa makahaba kwasababu amezaa wabinti ambao nao pia ni makahaba kama yeye na si mengine zaidi ya madhehebu yote yanayoshirikiana naye, wale waliokuwa wanajiita ma-protestants mwanzo  sasa hivi hawapo hivyo tena, wanashirikiana naye kwa namna zote. Kanisa Katoliki limefanikiwa kuwalewesha na kuwavuta tena kwake, lutheran imeshaungana na katoliki rasmi, pamoja na madhehebu mengine mengi,na ndio maana linaitwa "KANISA MAMA". Sasa ni rahisi kuelewa hapo kwanini ni "MAMA WA MAKAHABA"..Kwasababu yeye ameshakuwa kanisa mama, na mabinti wake wameshafuata mifumo yake ya ibada zisizotokana na NENO la Mungu.
Na ni kwanini ni "Mama wa Machukizo ya nchi"?.

Hili kanisa lenyewe ndio linalohusika na machukizo yote ya nchi yanayovuta ghadhabu yote ya Mungu juu ya nchi, kama ya kuwauwa watakatifu wa Mungu, kimwili na kiroho, kwa ibada zake za sanamu, kanisa hili limeua zaidi ya wakristo milioni 68 katika historia hiyo ni idadi kubwa sana, hata Bwana YESU  alishatabiri juu yao alisema..Yohana 16:1-3"Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania KILA MTU AWAUAYE YA KUWA ANAMTOLEA MUNGU IBADA. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. " 

Hiyo ndio sababu ya yule mwanamke kuonekana amelewa kwa damu za watakatifu ..Haya yote ni machukizo makuu mbele za Mungu, na yule  mpinga-kristo atakayetokea huko ndiye atakayelisimamisha lile CHUKIZO LA UHARIBIFU lililotabiriwa na nabii Daneli na BWANA wetu YESU KRISTO, ndio  maana anajulikana kama "MAMA WA MACHUKIZO YA NCHI".


SIRI YA YULE MNYAMA.Tukiendelea Ufunuo 17:7-18 "
7 Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi.
8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.
9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.
10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.
11 Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.
12 Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
13 Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.
14 Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
15 Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.
16 Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto.
17 Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.
18 Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi. "

Hapa pia tunaona Yohana anaonyeshwa siri ya yule mnyama ambaye ndio yule yule aliyeonyeshwa katika ile sura ya 13 ambaye ana vichwa 7 na pembe 10, isipokuwa hapa zile pembe 10 zinaonanekana hazina vilemba ikiwa na maana hazijapokea ufalme bado, na ndio maana tukisoma mstari wa 12 inasema watakuja kupokea ufalme(yaani kuvikwa vilemba) saa moja na yule mnyama.

Kumbuka vile vichwa saba, ni FALME 7, ambazo shetani alizikalia kuutesa au kutaka kuungamiza kabisa uzao wa Mungu, ambazo ni 1) MISRI   2)ASHURU  3)BABELI   4)UMEDI & UAJEMI  5) UYUNANI   6)  RUMI-ya-KIPAGANI   7) RUMI-ya KIPAPA...


kwa maelezo marefu juu ya huyu mnyama kama anavyoonekana kwenye sura 13 fuata link hii.>>> https://wingulamashahidiwakristo.blogspot.com/2017/12/maelezo-juu-ya-ufunuo-13.html#links

Lakini tunaona hapo wakati Yohana anaonyeshwa maono hayo aliona watano wameshakwisha anguka, na mmoja yupo na mwingine hajaja bado. Kumbuka wakati ule Yohana anapewa haya maono  AD 90 ,utawala uliokuwa unaitawala dunia wakati ule  ni RUMI ya kipagani, kwahiyo zile tawala tano za kwanza zilikuwa  zimeshapita yaani Misri, Ashuru, Babeli, Umedi&uajemi pamoja na Uyunani. Hivyo ule wa Urumi ndio uliokuwepo na ndio ule uliomsulibisha KRISTO.

Na kama alivyoambiwa mmoja bado hajaja(ambaye ni wa 7), Na kwamba atakapokuja itampasa akae muda mchache, sasa  huo  si mwingine bali ni ule utawala wa RUMI ya kidini chini ya upapa ulioongoza dunia nzima kuanzia kile kipindi cha karne ya 4, ni ule ule tu wa RUMI sema hapa umegeuka ukawa wa kidini chini ya upapa.

Tukiendelea kusoma mstari wa 11 inasema.." Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.".Hivyo tunaona mnyama mwingine wa 8 anajitokeza hapo, lakini biblia inasema huyu wa 8 ndio yule yule wa 7, hii ikiwa na maana kuwa ni kile kile kichwa cha saba isipokuwa kimebadilisha taswira, kwasababu yule mnyama tayari anavyo vichwa saba hawezi akawa tena na vichwa nane,

Na huyu mnyama wa 8 biblia inasema ambaye alikuwako naye hayupo naye anaenda kwenye uharibifu, tukirudi kwenye historia tunamwona  huyu mnyama (ambaye ndio kile kichwa cha 7 -Rumi ya kidini chini ya Upapa wa Kanisa Katoliki) ulikuwa na nguvu kipindi kile cha utawala wake, lakini baadaye ulikuja kutiwa jeraha la mauti na wale wanamatengezo, hivyo nguvu zake za kutawala dunia nzima zilikufa, lakini tunaona lile jeraha lilianza kupona tena, kuanzia kile kipindi cha vita vya pili vya dunia mpaka leo linaendelea kupona, utakapofika wakati atakaporejeshewa nguvu zake tena alizopoteza ndipo atakapoingia katika UHARIBIFU, naye ataitawala dunia kwa kipindi kifupi cha miaka mitatu na nusu ndio kile kipindi cha dhiki kuu, ndio maana biblia inasema alikuwepo naye hayupo, naye anajiandaa kwenda kwenye uharibifu. Kwasababu hapo mwanzo alishawahi kutawala na atakuja kutawala tena.

Sasa Zile pembe 10 za yule mnyama ambayo ni yale mataifa 10 ya ULAYA(EU), Biblia inasema  yatakuja kupata nguvu wakati mmoja na yule mnyama. Na haya ndiyo mpinga-kristo PAPA atakayoyatumia kuwatesa wale ambao hawataipokea chapa ya mnyama katika kile kipindi cha dhiki kuu.

Lakini mstari 16 tunaona jambo lingine.." Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto." 

Mwisho wa yote baada ya dhiki kuu kukaribia kuisha yale mataifa 10 ya Ulaya yatagundua kuwa utawala wa mpinga-kristo(PAPA) Chini ya kanisa katoliki hauna manufaa yoyote wala haujasaidia chochote kutimiza matakwa yao, na suluhu zao za AMANI, sasa kwa pamoja yatamchukia yule mwanamke(yaani PAPA) na Makao yake VATICAN  na kumwangamiza kabisa, hiyo ndio HUKUMU ya YULE KAHABA MKUU kama mstari wa kwanza unavyosema.

" Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;"


Huo utakuwa ndio mwisho wa Utawala wa Upapa na Kanisa Katoliki, kwasababu makao makuu yake VATICAN yatakuwa yameshateketezwa, hukumu hii imeelezewa kwa urefu kwenye SURA YA 18, jinsi Babeli ulivyoanguka na kuwa ukiwa mfano wa ile Babeli ya kwanza ilivyokuwa.

Baada ya huyu mwanamke Babeli mkuu kuhukumiwa, sasa mstari wa 14 unasema. zile pembe 10 (yaani yale mataifa ya ulaya)" ndio yatafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu." Kumbuka hii itakuwa ndio ile vita ya MUNGU MWENYEZI yaani "HARMAGEDONI"  inayozungumziwa kwenye ufunuo 16:16.Ufunuo 18:1-5"
1 Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. "

Hivyo ndugu unaona ni HATARI! gani  iliyo mbele yetu?, ni wazi kabisa muda umeshaisha Yule mnyama siku yoyote anaingia katika uharibifu, kumbuka wakati huo kanisa ambaye ni BIBI-ARUSI safi atakuwa ameshanyakuliwa, bibi-arusi asiyeabudu sanamu, bibi-arusi aliyebikira kwa NENO tu na sio pamoja na mapokeo mengine yaliyo nje na NENO LA MUNGU Kama kusali Rosari na ibada za wafu. Bibi-arusi Anayemwabudu Mungu katika Roho na kweli  sio katika mifumo ya ki-DINI  na ya-kimadhehebu, Bibi-arusi aliyepokea kweli ubatizo wa Roho Mtakatifu, na kama tunavyofahamu asili ya bibi-arusi ni kuvaa vazi refu la kujisitiri, je! na wewe mwanamke mavazi yako ni ya kujisitiri?, Utakuwa mkristo na bado uwe  kahaba kwa mavazi unayovaa? kumbuka fashion zote ni dhambi! lipstic,vimini, wigy,suruali, wanja nk. vitakupeleka kuzimu mwanamke.
BWANA YESU ANASEMA...


12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, NA HAO WAABUDUO SANAMU, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.
17 NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO!  Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.

TUBU ANGALI MUDA UPO.


Mungu akubariki.

Monday, December 18, 2017

MAELEZO JUU YA UFUNUO 13


Tukisoma kitabu cha Ufunuo mlango wa 13 tunaona kuna wanyama wawili wanaozungumziwa pale; wa kwanza akiwa ni yule mwenye vichwa saba na pembe 10 aliyetoka baharini na wa pili ni yule aliyekuwa mfano wa mwanakondoo mwenye pembe 2 akitoka katika nchi.

Kwa ufupi tuwatazame hawa wanyama wanawakilisha nini na wanachukua nafasi gani katika siku hizi za mwisho:

MNYAMA WA KWANZA:

Ufunuo 13:1-5" Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
9 Mtu akiwa na sikio na asikie.
10 Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu. "Hapa tunamwona huyu mnyama akiwa na vichwa saba na pembe 10, na juu ya zile pembe zake ana vilemba 10, sasa hivi vichwa 7 inafahamika vinawakilisha ngome/mamlaka ambazo shetani alizikalia na kuzitumia kupambana na kuuharibu uzao wa Mungu hapa duniani tangu taifa la Israeli lilipoundwa. Na tawala hizi tunaweza tukaziona katika biblia nazo ni 1) MISRI   2) ASHURU, 3) BABELI 4) UMEDI & UAJEMI   5) UYUNANI   6) RUMI   7) RUMI -KIDINI.


Lakini Yohana alimwona yule mnyama akiwa na PEMBE 10 katika kichwa chake, kumbuka zile pembe 10 hazikuwa zimesambaa juu ya vichwa vyote saba kama inavyofikiriwa na watu wengi, bali zote 10 Yohana alizoziona zilikuwa juu ya kichwa KIMOJA TU! na sio kingine zaidi ya kile kichwa cha saba. Kwahiyo kile kichwa cha saba ndicho Yohana alichokikazia macho kwasababu kilikuwa ni tofauti na vingine vyote.


Hivyo zile pembe 10 kulingana na maono aliofunuliwa Danieli juu ya ile sanamu ya Nebukadneza alioiona yenye miguu ya chuma na nyayo zenye vidole 10 zilizochanganyikana nusu chuma, nusu udongo, kama inavyojulikana ile miguu ya chuma ni utawala wa RUMI na vile vidole ni utawala wa RUMI uliokuja kugawanyika na kuwa yale mataifa kumi ya ULAYA wakati ule ambayo yalikuwa bado hayana nguvu kwasababu yalikuwa bado hayajavikwa vilemba(CROWNS). Hivyo vile vidole 10 ndio zile pembe 10 zinazoonekana juu ya yule mnyama na ni mataifa 10 yaliyopo katika umoja wa ULAYA (EU), na kama tunavyoona sasa kwa huyu mnyama zile pembe 10 zimetiwa VILEMBA inaashiria kuwa utakuja wakati haya mataifa yanayounda umoja wa ulaya yatapewa nguvu ya utawala na yule mnyama kutenda kusudi la kuwaua watakatifu katika kipindi cha ile miaka mitatu na nusu ya mwisho ya dhiki kuu.


Leo hii tunaona umoja wa ulaya unaundwa na mataifa zaidi ya 10, lakini yatakuja kuishia kuwa 10 tu ili kutimiza unabii wa kwenye biblia na yapo mbioni kuvikwa vilemba( yaani kupewa utawala wa dunia) yakiwa chini ya yule mnyama ( RUMI) chini ya utawala wa PAPA ambaye ndiye mpinga-kristo biblia inayomwitwa "mtu wa kuasi", mwana wa uharibifu ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.(2Thesalonike 2). Leo hii bado hayana nguvu kwasababu Danieli alionyeshwa kuwa vile vidole kumi nusu yake vitakuwa na nguvu na nusu yake vitakuwa vimevunjika ndivyo ilivyo sasa hivi Umoja wa ulaya hauna nguvu sana, lakini utakuja kupata nguvu duniani kote ili kutimiza kusudi la yule mnyama(mpinga-kristo)

Tukiendelea kusoma mstari wa tatu tunaona moja ya kichwa chake (ambacho ndio kile kichwa cha saba) kimetiwa jeraha la mauti nalo likapona. Kumbuka Rumi-ya kidini(UKATOLIKI) iliyokuwa chini ya UPAPA katika historia ilikuwa inatawala dunia nzima, na ilifanikiwa kupata nguvu dunani kote kiasi cha kwamba mtu yeyote aliyeonekana anakwenda kinyume na hiyo dini adhabu ilikuwa ni kifo tu, mamilioni ya wakristo waliouwa wote waliokataa kuisujudia miungu yao ya kipagani, jambo hili liliendelea na hii dini ilizidi kupata nguvu hadi kufikia karne ya 16 wakati wa matengenezo ya kanisa ambapo Mungu alianza kuwanyanyua watu wake kama Martin Luther ambaye alianza kufundisha watu "kuhesabiwa haki kwa imani" na kukosoa mafundisho potofu ya kanisa Katoliki lakini PAPA alipotaka kumuua mfalme wa Ujerumani alisimama kumuhifadhi Luther, ndipo watu wengi wakaanza kuacha hii dini ya uongo na kuligeukia NENO la Mungu hivyo Ukatoliki ukaanza kupungua nguvu, na wakati huo huo Mungu aliwanyanyua wengine kama Calvin, Zwingli, Knox n.k. ili kulitengeneza tena kanisa lililokuwa limeharibiwa na mafundisho ya uongo ya Kanisa katoliki.Hapo ndipo ulipokuwa mwanzo wa lile jeraha la yule mnyama lakini pigo hasa lilikuja karne ya 18 mwaka 1798 katika mapinduzi huko Ufaransa Jenerali Berthier alipeleka vikosi vyake Roma na kumng'oa PAPA katika utawala wake, akamchukua mateka pamoja na mali zake zote za dini yake, Hivyo ikapelekea dini ya kikatoliki iliyokuwa inatiisha dunia kuwa karibuni na kutoweka kabisa, hilo lilikuwa pigo kubwa sana lilofananishwa na jeraha la mauti lakini tunaona Biblia inasema lile JERAHA LA MAUTI lilipona,


 Je! Jeraha hili liliponaje na lilipona lini?.


Wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia, matatizo yalikuwa mengi duniani, uchumi ulishuka sana, mataifa ya ulaya yaliaanza kuanguka na kupoteza nguvu zao kutokana na athari ya vita, Hivyo kiu ya kutafuta amani duniani ikaongezeka kumbuka wakati huo huo Marekani ilianza kupata nguvu, na likiwa kama taifa la kikristo (protestant) lenye nguvu kubwa ya kiuchumi na kijeshi hivyo kwa kushirikiana na mataifa ya ulaya kwenye harakati za kutafuta amani, (isiyokuwa ya kivita) walianza kuutambua umuhimu wa PAPA Kwasababu alionekana kuwa ni mtu mwenye mvuto na anayekubalika na watu wengi duniani, hivyo mataifa mengi yakaanza kutuma mabalozi wake kwa papa ajihusishe na masuala ya AMANI YA DUNIA. Sasa kuanzia hapo jeraha lake la mauti likaanza kupona, wale ambao walikuwa wanafanya mageuzi kinyume chake(protestants) wakaanza kushirikiana nae tena, uprotestant ukabakia kuwa jina tu na ndio huko inapoundiwa ile sanamu ya mnyama nitakayoielezea zaidi mbeleni...Tukiendelea mstari 4 & 5, Tunaona lile joka ambaye ni Shetani mwenyewe alimpa nguvu yule mnyama naye akaanza kunena maneno makuu ya makufuru. Tukisoma pia kitabu cha Danieli alizungumziwa kama ile PEMBE ndogo iliyozuka na kungo'a wale wafalme watatu na kunena maneno ya makufuru Danieli 7:25 "Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. " Na huyu si mwingine zaidi ya mpinga-kristo ambaye ni PAPA,..Si ajabu PAPA leo anasimama "badala ya mwana wa Mungu duniani"..Vicarivs filii Dei, ..Papa leo amejivika uwezo wa kusaheme dhambi jambo ambalo BWANA YESU KRISTO mwenyewe ndiye anayeweza kulifanya ..haya yote ni maneno ya makufuru, na yapo mambo mengi zaidi ya hayo ambayo ni makufuru. Kumbuka ninaposema PAPA namaanisha kile "CHEO"..kwahiyo yeyote anayekikalia hicho cheo amejitwika cheo cha mpinga-kristo mwenyewe.


Na tunaona wakati wa mwisho atapewa uwezo wa kutenda kazi miezi 42, hii ni miaka mitatu na nusu, kati ya ile miaka saba ya mwisho ya lile juma la 70 la Danieli. Hichi kitakuwa kipindi cha DHIKI KUU, sasa hivi PAPA anaonekana kama mtu asiyekuwa na madhara yoyote, anakuja kwa njia ya kujipendekeza ili apate nguvu kiurahisi, kama kitabu cha Danieli kinavyomtabiri, leo hii duniani kote anajulikana kama "MTU WA AMANI", Ni mtu mwenye wafuasi wengi duniani, na aneyekubalika kuliko mwanasiasi yoyote duniani, dini nyingi zimeanza kuvutiwa naye, hata waislamu sasa wanamwona kama ni mtetezo wao mtu anayejali watu wote, PAPA anasema wote tunamwabudu Mungu mmoja ila kwa njia tofauti tofauti (yaani wakristo, waislamu wahindu, wabudha tunamwabudu Mungu mmoja), angali biblia inasema YESU ndiye njia pekee ya kumfikia Mungu, na cha ajabu umaarufu wake unaongozeka na watu wanamfurahia ili kutimiza ule unabii kwamba "watu wote ambao majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ndio watakaomsujudia." Na kumsujudia sio kumpigia magoti bali ni kukubaliana na mifumo yake na imani yake.


Ndugu yangu mpinga-kristo hatakuja na mapembe kichwani, akilazimisha watu wamwabudu, kumbuka biblia inasema shetani ana HEKIMA kuliko Danieli, na sehemu nyingine biblia inasema ile roho itataka kuwadanganya yamkini hata wateule. Siku zote anakuja kama malaika wa nuru, usitazamie kuwa mpinga-kristo atakuwa muislamu au muhindi au freemason, hapana ndugu yupo kanisani amebeba biblia na anafanya kampeni za amani duniani na watu wanamshangilia na kumbusu, biblia inasema hapo ndipo "PENYE HEKIMA " .

Kwahiyo inahitajika Hekima kumjua vinginevyo utachukuliwa na mafuriko yake kama wengi walivyochukuliwa huu ni wakati wa kuwa macho sana, jali maisha yako ya umilele yanayokuja. Chunguza maandiko kama watu wa Beroya, sio kila roho inayoshabikiwa na wengi unaipokea moyoni mwako kwasababu biblia inasema IPO NJIA IONEKANAYO KUWA NJEMA MACHONI PA WATU..LAKINI MWISHO WAKE NI UPOTEVU, na BWANA YESU alisema njia iendayo upotevuni ni PANA na wengi wanaiendea hiyo.


MNYAMA WA PILI:

Ufunuo 13:11-18"
11 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
13 Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.
14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.
15 Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita. "


Tunaona huyu mnyama wa pili ana pembe kama mwanakondoo, lakini sio mwanakondoo, na huyu anaonakana ametoka katika nchi na sio katika bahari na yeye hana vichwa saba Kama yule mnyama wa kwanza, ikiwa na maana kuwa utawala wake haukuanzia mbali kama yule mnyama wa kwanza bali ulizuka mwishoni. Hivyo huyu mnyama si mwingine zaidi ya MAREKANI. Ukiangalia katika ile nembo ya Marekani katika ile dola yao utaona yule tai akiwa ameshika mishale 13, ile piramidi kuna ngazi 13, kuna nyota 13 juu ya yule tai, matawi 13 ya ule mzeituni ulioshikwa ..nk. kila mahali 13..13... na taifa la Marekani linaonekana katika UFUNUO 13.


Pia huyu mnyama alipewa uwezo wa kufanya watu wote wakaao duniani wamsujudie yule mnyama wa kwanza na kuunda ile SANAMU YA YULE MNYAMA.


Sasa Sanamu ya mnyama ni ipi?

Marekani kama taifa lilokuwa la kiprotestant ambalo hapo kwanza lilikuwa halishakamani wala halishirikiani na kanisa Katoliki kwa namna yoyote, lakini katika karne ya 20 baada ya vita ya pili Vya dunia liliacha njia ya kweli ya NENO LA MUNGU, na kurudi kuiga tabia za yule mnyama,kazi nzuri na juhudu zote zilizofanywa na wale wana-matengenezo zikawa ni bure, ni sawa na mbwa aliyerudia matapishi yake.


Baada ya kuibuka jopo kubwa la madhehebu ya kiprotestant duniani, viongozi wa madhehebu ya kimarekani walikutanika kwa agenda ya kutaka kuondoa tofauti katikati ya wakristo ili kufikia muafaka mmoja wa IMANI, ndipo walipounda BARAZA LA MAKANISA ULIMWENGUNI (World Council Of Churches), na NATIONAL COUNCIL OF CHURCHES , na ndio chimbuko la EKUMENE. (Ecumenical council)
Na Kanisa Katoliki likiwa kama washirika wao wa karibu wakiwasaadia.


Baraza hili la UMOJA WA MAKANISA liliazimu kuyarudia mambo yale yale ya ukahaba yaliyofanywa na kanisa Katoliki, Iimekuwa ni SHIRIKA LA KI-DINI, na Linasheria zake na itakadi zake ambazo zinaenda kinyume na mpango na NENO LA MUNGU. Kwahiyo UMOJA HUU ndio unaoitwa SANAMU YA MNYAMA..Kwasababu tabia zote zilizokuwa katika kanisa kahaba katoliki zipo nazo kule na hivi karibuni yule mnyama (America) ataenda kuipa PUMZI ILE SANAMU INENE, ili watu wote waiabudu, hii ikiwa na maana siku sio nyingi watu wote duniani watenda kulazimishwa kuwa washirika wa muunganiko wa hayo makanisa mtu yeyote atakayeonekana kwenda kinyume atauawa.

Na kama tunavyoona huyu mnyama wa pili (MAREKANI) anaweza kufanya ishara kubwa hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni, jambo hili linatupa picha nguvu za kijeshi walizonazo Marekani kama uwezo wa kushusha makombora makubwa ya vita kutoka angani mabomu ya atomic n.k.


Hili baraza la makanisa duniani sasa linafanikiwa kuzivuta dini zote ulimwenguni pamoja, ikiasisiwa na PAPA kiongozi wa kanisa katoliki duniani, itafika wakati kama hautakuwa mshirika wa dini au kanisa ambalo halijaunganishwa katika huu UMOJA WA MAKANISA NA DINI hutaweza kuuza wala kununua wala kuabudu, wala kuishi katika jamii,


Leo hii tunaona vitendo vya kigaidi na vya mauaji vikiongezeka, wanasiasa wameshindwa kuirejesha amani ya dunia, na matatizo yote yahusuyo amani yanatokana na mizozo ya kidini tunaweza kuona mambo yanayoendelea mashariki ya kati mfano Israeli, syria-kuna ISIS,Iraq, Lebanoni-kuna hezbolah, myanmar huko Asia kuna warohighya, sehemu za Afrika nchi kama Nigeria kuna Boko kuna haramu, Somalia-alshabaab, central Africa- antibalaka ..na makundi mengine mengi sana,. tunaona mizizi yote ya migogoro inaanzia katika DINI. Hivyo atahitajika mtu wa KIDINI mashuhuri kutatua migogoro ya kidini na sio wanasiasa au watu wa kijamii - Na huyu atakuwa si mwingine zaidi ya PAPA kwasababu yeye ndiye anayekubaliwa na dini zote pamoja na wafalme wote wa dunia.


Hivyo atapokwisha kupata nguvu, ataibua mfumo mmoja wa kutambua watu wote duniani kwa imani zao, kwa kivuli cha kuleta amani na kukomesha vitendo vya uvunjifu amani duniani kumbe nia yake itakuwa ni kuwateka watu wote duniani na kuwatia ile CHAPA YA MNYAMA. Wakati huo watu wengi duniani wataufurahia huo mfumo pasipo kujua ndio wanaipokea chapa hivyo. Wengi watasajiliwa katika madhehebu na dini zao zilizokuwa na ushirika huo wa UMOJA WA MAKANISA ULIMWENGU , Vitatumika vitu kama CHIPS, IDS, na utambulisho mwingine utakotengenezwa ili kuyafikia makundi yote, sasa wale watakaokaidi ndio watakaopitia dhiki kuu, hao ndio watakaoonekana magaidi na wavunjifu amani, kama sivyo kwanini wasikubali utambulisho huo mpya? na kumbuka watakuwa ni wachache sana watakaogundua kuwa ndio CHAPA YENYEWE ,Kwa maelezo marefu zaidi kuhusu chapa ya mnyama fuatilia link hii >>>
https://wingulamashahidiwakristo.blogspot.com/2016/10/chapa-ya-mnyama.html


Hivyo ndugu injili tuliyonayo sasa hivi inasema ..UFUNUO 18:4-5" Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU,MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, wala msipokee mapigo yake.Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. "


Ndugu toka katika mifumo ya madhehebu kwasababu yameshirikiana na yule mnyama(kanisa katoliki) kufanya ukahaba, na kuua watakatifu wa Mungu wengi, yeye anaitwa BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA ikiwa na maana kama yeye ni mama wa makahaba ni dhahiri kuwa anao mabinti na wao pia ni makahaba kama mama yao alivyo na hao mabinti sio wengine zaidi ya madhehebu yote yaliacha uongozo wa Roho mtakatifu na kuandamana na desturi za kanisa kahaba Katoliki, hivi karibuni tumesikia WALETHERANI wameungana rasmi wakatoliki.!! Biblia inasema TOKENI KWAKE ENYI WATU WANGU, kama ukishirikiana naye inamaanisha kwamba na wewe pia utashiriki mapigo yake ndivyo Mungu anavyokuchukulia.


Ufunuo 14:9 " Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. "


Bwana ametuita kuwa BIKIRA SAFI, na bikira tu ndiye atakayeingia katika karamu ya mwanakondoo, toka kwenye mifumo ya madhehebu umwabudu Mungu katika ROHO NA KWELI.


Mungu akubariki, na Mungu atusaidie katika safari yetu tuumalize mwendo salama

Amen.