"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Thursday, October 26, 2017

ZIFAHAMU NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE SABA.

Tangu kipindi cha Bwana Wetu Yesu Kristo kuondoka duniani mpaka sasa imepita miaka takribani elfu mbili na katika hichi kipindi cha miaka hii elfu mbili kanisa limekuwa likipitia katika vipindi tofauti tofauti saba vinavyoitwa NYAKATI SABA ZA KANISA, kulingana na kitabu cha..
Ufunuo 1:12-20" Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;
15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.
 Ufunuo huu alipewa Yohana na Bwana Yesu alipokuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, akionyeshwa jinsi kanisa litakavyokuja kupitia katika siku za mwisho. Leo hii si rahisi sana kuona kitabu cha ufunuo kikiguswa au kuelezewa katika kanisa, na shetani hataki watu wafahamu siri zilizoandikwa katika hiki kitabu maana ndio kinaelezea hatma ya mambo yote ikiwemo na shetani mwenyewe. Kwahiyo ndugu fungua moyo wako ujifunze na Mungu akusaidie unapoenda kusoma ujue ni wakati gani tunaishi na jinsi Bwana Yesu alivyo mlangoni  kurudi kuliko hata unavyoweza kufikiri. Tafadhali pitia taratibu mpaka mwisho ili uelewe.


  • vile vinara saba vinavyozungumziwa ni makanisa saba tofauti tofauti ambayo yamepita tangu wakati wa Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani hadi wakati tunaoishi sasa.
  •  Na zile nyota saba ni malaika saba/wajumbe wa duniani(wanadamu 7 ambao Mungu aliwatia mafuta ) kupeleka ujumbe kwa hayo makanisa saba. Kila mjumbe kwa kanisa lake.







NYAKATI YA KWANZA:
Kanisa: Efeso
Malaika/Mjumbe: MTUME PAULO
kipindi cha kanisa: 53AD -170AD
Tabia ya kanisa: limeacha upendo wake wa kwanza,tangu wakati wa mauaji ya wakristo yaliyoongozwa na Nero mtawala wa Rumi hadi kifo cha mtume Yohana. Na kipindi hiki ndipo matendo ya wanikolai yalianza kuingia katika kanisa (mafundisho ya kipagani). kuanza kujichanga na ukristo. ufunuo 2:1-7
onyo kwa kanisa- litubu lirudi katika upendo wake wa kwanza, lililopoteza.
Thawabu: Yeye ashindaye atapewa kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani ya Mungu.

NYAKATI YA PILI;

Kanisa; Smirna
Malaika/Mjumbe;IRENIUS
kipindi cha kanisa: 170AD -312 AD
Tabia ya kanisa; Ni kanisa lilopitia dhiki nyingi kutoka katika utawala mkali wa Diocletian wa Rumi , watakatifu wengi waliuawa katika hichi kipindi kuliko kipindi chochote katika historia ya kanisa.walichinjwa wengi, na wengine kutupwa kwenye matundu ya simba na wanawake kukatwa matiti na kuachwa mbwa walambe damu zao, na ukatili mwingi sana wakristo walitendewa katika hichi kipindi lakini walistahimili dhiki zote hizi soma kitabu cha (Foxe's book of Martyr- kwenye archives zetu kinaelezea vizuri mauaji ya wakristo). Japo wakristo walikuwa maskini sana  Lakini Kristo aliwafariji kuwa wao ni  Matajiri. ufunuo 2:8-11
Thawabu; Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

NYAKATI YA TATU;
Kanisa ; Pergamo
Malaika/Mjumbe; MARTIN
Kipindi; 312AD -606AD
Tabia ya kanisa; Kanisa laingiliwa na mafundisho ya uongo zaidi, ambayo ndio yale matendo ya wanikolai sasa wakati huu yamegeuka kuwa mafundisho ya kidini. Ukristo ukaoana na upagani ukazaa Kanisa mama mfu Katoliki, katika baraza la Nikea AD 325 siasa na mafundisho ya miungu mitatu,ibada za sanamu na za wafu,sherehe na sikukuu za kipagani, ubatizo wa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, vyeo vya upapa n.k ndipo vilipochipukia. kwa mambo haya basi ikasababisha kanisa kuingia katika kipindi kirefu cha giza (Dark age). Ufunuo 2:12-17
Onyo kwa kanisa: litubu lirudi katika imani iliyoanzishwa na mitume wa Kristo
Thawabu; Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, ila yeye anayelipokea.

NYAKATI YA NNE:
Kanisa; Thiatira
Malaika/Mjumbe;COLUMBA
Kipindi; 606AD -1520AD
Tabia ya kanisa; Japo kanisa lilikuwa na juhudi na bidii katika kumtafuta Mungu, lakini bado lilikuwa na mafundisho ya yule mwanamke kahaba Yezebeli yaani mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Onyo; Litubu litoke katika mafundisho ya wanikolai. Ufunuo 2:18-29
Thawabu;Yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hata mwisho nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.

NYAKATI YA TANO:
Kanisa; Sardi
Malaika/Mjumbe; MARTIN LUTHER
kipindi; 1520AD -1750AD
Tabia; Ni kanisa lililokuwa linarudi katika matengenezo kutoka katika mafundisho ya yule kahaba mkuu kanisa katoliki. lakini lilikuwa bado na Jina lililokufa, wakishikilia baadhi ya mafundisho ya kanisa mama katoliki, huku ndiko chimbuko la walutheri lilipoanzia.Ufunuo 3:1-6
Onyo: litubu, lirejee kwenye mafundisho ya mitume.
Thawabu; Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri Jina lake mbele za baba yangu na mbele ya malaika zake.

NYAKATI YA SITA;
Kanisa;Filadelfia
Malaika/Mjumbe; JOHN WESLEY
Kipindi; 1750AD -1906AD
Tabia; Ni kanisa lililosifiwa kwa matendo yake mema, lilifanikiwa kujua na kuyarekebisha mafundisho ya uongo Kristo alisema ''tazama nakupa walio wa sinagogi la shetani wasemao kwamba ni wayahudi nao sio, bali wasema uongo, tazama nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda''.ufunuo 3:7-13
Thawabu;Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu, huo Yesalemu mpya ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe lile jipya.

NYAKATI YA SABA;
Kanisa; Laodikia
Mjumbe;WILLIAM BRANHAM
Kipindi;1906- Unyakuo
Tabia; Ni kanisa ambalo sio baridi wala moto, bali ni vuguvugu, Kristo anasema ni heri lingekuwa moto au baridi, hii ndiyo hali ya kanisa tunaloishi sasa mimi na wewe, uvuguvugu mbaya umeingia katika kanisa, watu wanajiona kuwa wanamwabudu Mungu katika uzuri wao wa majengo ya kanisa, kwaya.na injili ya mafanikio, wakidhani kuwa hivyo yatosha tu kumjua Mungu kumbe hawajui wameshaingia katika udanganyifu wa shetani pasipo wao kujua, watu wanasema kuwa wanampenda Mungu na bado wanapenda mambo ya ulimwengu huu kama fashion za mitindo ya kisasa wanawake kuvalia mavazi ya nusu uchi, michezo, miziki, muvi, ponography, ulevi. anasa,uasherati,na shughuli za ulimwengu huu ambazo zinawasonga wengi hususani kwa kizazi hichi cha ubize, watu wanapata muda wa kufanya kazi sana, lakini muda wa kumtolea Mungu hawana na bado ni wakristo., huu ndio uvuguvugu Kristo anaouzungumzia kwa kanisa letu la Laodikia.Hapa Kristo anasema unajiona kuwa tajiri kumbe ni maskini na mnyonge na uchi na unamashaka na kipofu, jiulize ni hali gani ya kanisa tulilopo sasa. 

Na hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hili, na ndio linakaribia kuisha. jiulize umejiwekaje tayari kumpokea Bwana Yesu akirudi mara ya pili?. Mungu alimtuma mjumbe wake ndugu William Branham kulionya kanisa letu lirudi katika NENO na imani iliyohubiriwa na mitume pamoja na utakatifu.
Onyo; Kristo anasema kanisa liwe na bidii likatubu na kumgeukia Mungu.
Thawabu;Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na baba yangu katika kiti chake cha enzi. ufunuo 3:14-22

      

Watu wa Mungu hili ndilo kanisa la mwisho tunaloishi hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hapa, tunaishi katika wakati ambao Kristo yupo mlangoni kulichukua kanisa lake teule, JIULIZE! UMEKWISHA KUJIWEKA TAYARI KUMLAKI BWANA, TAA YAKO INAWAKA??UMEMPOKEA ROHO MTAKATIFU??YEYE ALIYE NA SIKIO, NA ALISIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA.



Mungu akubariki
MARAN ATHA!

Sunday, October 22, 2017

MAJI YA UZIMA.


Siku zote roho ya mwanadamu imejawa na KIU ya mambo mengi yahusuyo mema, kwa mfano KIU ya kupata FURAHA, kiu ya kuwa na AMANI, kiu ya UZIMA USIOKOMA,kiu ya kuwa na UPENDO kiu ya KUTENDA MEMA, kiu ya kutaka UTAKATIFU,  kiu ya kuwa MNYENYEKEVU na MVUMILIVU, kiu ya KUWA NA RAHA, kiu ya KUWA KARIBU NA MUNGU ..n.k..


Lakini wengi wanatafuta njia za kuzikata kiu hizi kwa njia nyingi tofauti tofauti za kibinadamu. wengine wanatafuta RAHA kwa kufanya anasa, wengine wanatafuta AMANI kwa kunywa pombe, wengine wanatafuta FURAHA kwa kupata mali, wengine wanatafuta UZIMA WA MILELE kwa waganga na wapiga ramli, wengine wanatafuta UPENDO kwa kulaghai, wengine wanatafuta UHURU kwa kuua n.k..


Lakini ni dhahiri kuwa njia zote hizo ni batili, yaani aidha hazikati kabisa au zinakata kiu kwa muda tu! baada ya hapo tatizo linarudi  palepale..Lakini kuna habari njema, ya mmoja tu anayeweza kuikata kiu yako moja kwa moja isikuwepo tena naye si mwingine zaidi ya BWANA YESU. 


Kwa yeye utapata Raha nafsini mwako, furaha isiyokoma, amani, upendo, unyenyekevu, upole, utakatifu, kujua kumcha Mungu, na uzima wa milele n.k..Hivyo nakushauri Mkaribishe moyoni mwako na hakika ataikata KIU yako, usiipuuzie sauti yake ikuitapo . kwa maana maandiko yanasema:


Yohana 7:37-38 "Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, YESU akasimama, akapaza sauti yake akisema, MTU AKIONA KIU, NA AJE KWANGU ANYWE. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake". 

 
Yohana 4:13-14 "Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. 


Mungu akubariki.

EDENI YA SHETANI:


Pale Edeni Mungu alimweka Adamu na Hawa, Na kwa muda wote waliokuwepo bustanini Biblia inatuambia walikuwa UCHI na hawakujitambua kuwa wako vile, lakini baada ya dhambi kuingia ndipo walipojijua kuwa wapo uchi. Hii ina maana gani?.

Hapo mwanzo Mungu alipowaumba Mungu aliwawekea "UTAJI MTAKATIFU" katika macho yao ambao ungewafanya wasijue dhambi na ule utaji ulikuwa si kingine bali ni ROHO MTAKATIFU. Lakini tunajua walipoasi ule utaji ukaondoka hivyo Mungu akaamua kuwafanyia mavazi ya ngozi ili kuwasitiri.

Lakini Shetani naye tangu ule wakati alianza kutengeneza EDENI yake kidogo kidogo, awarudishe watu katika kuwa UCHI tena na kuwavua mavazi ambayo Mungu aliwavisha.
 Takribani Miaka elfu sita sasa tangu Adamu kuumbwa imepita na shetani amekuwa akiimarisha hii edeni yake kwa kuwatia watu "UTAJI WAKE MCHAFU" wa kuwafanya watu waishi na wasijione kuwa wako uchi na wenye dhambi. Hii  ni hatari sana.

Miaka ya zamani kwa kweli mwanamke kutembea amevaa suruali barabarani alikuwa anajulikana kama KAHABA, Lakini sasa hivi zimekuwa ni nguo rasmi kuendea kila mahali mpaka kwenye nyumba za ibada, na sasa imevuka zaidi ya hapo vimini na nguo zinazoonyesha maungo yote wazi ni jambo la kawaida kuliona na  hata haliwashangazi watu tena..Huoni kama ni "UTAJI" wa shetani huo umewavaa watu hata pasipo wao kujua??. na wanaume pia wanaonyesha maumbile yao wakiwa na nguo za ndani tu!. Leo hii wanaume na wanawake wanatembea uchi wa mnyama barabarani pasipo aibu yoyote.

Edeni hii ya shetani inaanzia katika roho. Tunaona kanisa la kwanza lililoanza na Mitume lilikuwa na ule UTAJI wa ROHO MTAKATIFU, Ikiwa na maana kazi zake zote zilitendeka katika uvuvio wa Roho wa Mungu na usafi lakini sasa hivi katika kanisa hili la mwisho tunaloishi  ule utaji wote umeondoka kilichobakia ni utaji wa shetani unaomfanya mtu awe VUGUVUGU na asijijue, utakuta mwanamke anaingia kanisani nusu uchi na asijione kuwa yupo uchi, mwanamume ni mzinzi lakini anajiona yeye yupo sawa tu mbele za Mungu, mtu ni mlevi na anajiona yeye ni mkristo aliyesafi, mwanaume anafuga rasta na kujiona hana hatia, utakuta mkristo anaabudu sanamu na asione shida yoyote angali biblia inasema usijifanyie sanamu ya kuchonga usiisujudie wala kuiabudu, mtu kaokoka ni msengenyaji na hata hasikii kuhukumiwa nafsini mwake juu ya hilo analolifanya.n.k.
Ni dhahiri kabisa tunaishi katika kanisa la mwisho linaloitwa, LAODIKIA na ujumbe wetu tuliopewa na BWANA ni huu..

Ufunuo 3:14 "Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 Nayajua matendo yako, YA KUWA HU BARIDI WALA HU MOTO; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 KWA KUWA WASEMA, MIMI NI TAJIRI, NIMEJITAJIRISHA, WALA SINA HAJA YA KITU; NAWE HUJUI YA KUWA WEWE U MNYONGE, MWENYE MASHAKA, NA MASKINI, NA KIPOFU NA UCHI.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. "

Kama unavyoona sisi tunaambiwa  tunajiona kuwa ni matajiri kumbe ni maskini na tu "UCHI"
Ni uthibitisho kabisa kuwa huu ni UTAJI WA SHETANI umelifunika kanisa hili la mwisho. Tunaishi nyakati za hatari tubu. mpokee ROHO MTAKATIFU  huo ndio muhuri wa Mungu utakaotuokoa sisi katika kizazi hichi cha mwisho. kumbuka pasipo Roho Mtakatifu hakuna unyakuo, Umeamua kumfuata Bwana mfuate kweli kweli na kama umeamua kumfuata shetani mfuate kweli kweli usiwe vuguvugu.

Tazama video chini, ujionee mwenyewe ulimwengu tunaoishi ulipofikia na jinsi Edeni hi ya shetani ilipofikia ili ujue tunaishi katika nyakati za hatari watu kutembea uchi barabarani si ajabu tena..Na kama vile shetani alivyoiharibu Edeni ya Mungu vivyo hivyo na ya kwake imeandaliwa kwa ajili ya uharibifu ambao upo karibu kutokea.




Mungu akubariki.

Saturday, October 21, 2017

KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA...TUBU UMGEUKIE MUNGU

Kumbukumbu 22:5" Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako".
Na bado Isitoshe  BWANA anawapelekea watu wake kuwaonya lakini bado wanadhihaki na kuziba masikio yako wasisikie




Warumi 1:18-28" Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.
 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;.......Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo,..................
Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.


Tunahitaji uthibitisho gani tena kuwa tunaishi katika siku za mwisho nyakati za hatari kama hizi?? JE! umeokolewa,..umempa KRISTO maisha yako? umeoupokea ujumbe wa wakati huu aliouleta Mungu kupitia mjumbe wake ndugu William Marrion Branham wa kanisa la saba na la mwisho ?.

Kama hujafanya hivyo ndugu ni vema ukamgeukia BWANA kabla mlango haujafungwa...

Mungu akubariki.

              Nukuu za ndugu William Branham.                                                                                               

" Kaka au Dada, kama Yesu aliomba kwa bidii, inatupasaye sisi kuomba kwa bidii?. Kama Kristo, Mungu wa mbinguni aliyeuva mwili aliomba kwa bidii, je! inatupasaje sisi wenye dhambi tunaookolewa kwa neema,? omba kwa bidii..kama ule uamuzi ulimfanya mwana wa Mungu kukata tamaa, itakuwaje mimi na wewe? tunapaswa tulie hasaa! 

 (Ujumbe : Kukata tamaa 63-0901      UK 28) William Marrion Branham



"Mtu hawezi kuwa katika hali yake ya kawaida mpaka awe amezaliwa mara ya pili. Katika moyo wake ni mnyama mpaka atakapokuwa amezaliwa na Roho wa Mungu, Hapo roho ya asili itakapoondolewa na kuruhusu Roho ya Mungu kuingia na kutawala, ambayo itamwongoza na kumpeleka katika nuru na kuijua kweli yote. Hiyo ni sawa. Na kama mtu hatafanya hivyo, na asipojua ya kuwa amefungwa na malango ya kuzimu, kuna shida ndani yake.


(Ujumbe : Why 60-0309)" 
William Marrion Branham

Tuesday, October 17, 2017

TOKENI KWAKE ENYI WATU WANGU: Part 2

 Kanisa Katoliki na Majina ya makufuru.:

Mnamo disemba 27,2015 Huko Vatican Basilica, Jumapili katika sherehe ya familia takatifu ya Yosefu, Maria na Yesu Papa  alipokuwa akihubiri juu ya malezi na familia kwa kulinganisha na Familia nyingine katika biblia. Katikati ya mazungumzo yake kwa kutumia mfano wa familia ya Bwana Yesu alisema maneno yafuatayo,  fuatilie kwa makini.

"...........Mwishoni mwa safari ya (Yerusalemu wakati Kristo alipokuwa na miaka kumi na mbili). Yesu Alirudi Nazareti na alikuwa mtiifu kwa wazazi wake(luka 2:51). Hii inaweza ikawa picha nzuri kwa mafundisho ya familia zetu. Safari haiishii tu pale tunapofikia malengo yetu, bali pale tunaporejea manyumbani na kuendelea na maisha yetu ya kila siku, tukiyatendea kazi matunda ya kiroho ya tulichokipata. Tunajua jambo alilolifanya Yesu wakati ule, BADALA YA KURUDI NYUMBANI NA FAMILIA YAKE, YEYE ALIBAKI YERUSALEMU HEKALUNI, IKASABABISHA MATATIZO MAKUBWA KWA MARIAMU NA YUSUFU AMBAO HAWAKUWEZA KUMPATA. KWA "GHASIA HII NDOGO" YESU PENGINE ANGEPASWA AOMBE MSAMAHA KWA WAZAZI WAKE. Injili haizungumzii hilo lakini ninaamini tunaweza tukalidhania hivyo............"

Kwa mwanzo na mwisho wa mahubiri yake fuatilia link hii. Pia unaweza ukaitazama video chini.

https://w2.vatican.va/content/francesco/en/homilies/2015/documents/papa-francesco_20151227_omelia-santa-famiglia.html




Tukifuatilia kwa umakini tunaona Papa Francis anajaribu kuonyesha kuwa Bwana YESU alikuwa na makosa na kitendo alichokionyesha cha kuwaacha wazazi wake hakikuwa sawa na hivyo angepaswa atubu.

Lakini biblia inatufundisha kuwa BWANA alikuwa ni mkamilifu na hakuwa na hatia wala dhambi yoyote (Waebrania 4:15) isitoshe yeye ni MUNGU,na tangu lini Mungu akamkosea mwanadamu?. lakini Jambo ambalo Papa alikuwa anataka  kulionyesha ni  kuwa Mariam alikuwa mkamilifu kuliko BWANA YESU Na ndio maana Mariamu kwao anasimama kama mpatanishi kati ya sisi na Mungu kama YESU.

Kiongozi wa namna hii angali akijua analolifanya anawafundisha na wengine hivyo. Swali ni je! ikiwa kiongozi anafundisha hivi hali ya kiroho ya kondoo anaowachunga itakuwaje? Ndugu kimbia ibada za sanamu mgeukie Mungu na sio dhehebu.

Ufunuo 18:4" Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. "

Amen!.

Monday, October 16, 2017

TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU: Part 1


Majina ya makufuru na Kanisa Katoliki:

Wakati mikesha ya Pasaka inadhaniwa kuwa ni siku muhimu ya kukumbuka ushindi tulioupata  kwa njia ya BWANA wetu YESU KRISTO pale Kalvari, wengine wanaitumia kuwakosesha watu  wadhaifu wa imani na cha ajabu na kusikitisha zaidi shetani amenyanyua viongozi hawa wanaojiita ni wa dini ili kuwapotosha watu wasiomjua Mungu na sio tu kupotosha bali  na  kulikufuru Jina la Mungu mwenyezi (YESU KRISTO). Si ajabu biblia imewataja katika


   2Wakoritho 11:13" Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. "

Kanisa Katoliki limekuwa na SALA maalumu inayosomwa  kila "EASTER" (Mkesha wa Pasaka), inayohudhuriwa na viongozi wote wa kanisa hilo ikiwemo PAPA, Hii Ni MISA maalumu inayoandaliwa kwa kusudi maalumu la kumtukuza "SHETANI/LUCIFER" na kumkufuru Bwana wetu YESU KRISTO.

Misa hii haifanyiki kwa siri, ni jambo lililowazi la kila mtu kuona, sala hiyo huwa inaimbwa katika lugha ya kilatini, tazama video chini ujionee na hii ndiyo tafsiri ya maneno yake:


" Lucifer uangazaye nuru yako kwa wanadamu 
..O Lucifer usiyeweza kushindwa.
..KRISTO NI MWANA WAKO
..Aliyepanda kutoka kuzimu
         ..Aliyeangaza nuru yake ya amani, na anaishi na anatawala
..Ulimwengu pasipo mwisho."





Unaweza ukajionea mwenyewe jinsi sala hiyo inavyomtaja shetani/Lucifer kuwa ni MUNGU na YESU KRISTO ni mwana wake. Hivyo baba wa Yesu ni shetani..JE! HAYA SI MAKUFURU?..
Ufunuo 18:4 inasema "...... TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU!, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. "

Ndugu ikiwa unampenda Bwana hautashiriki uovu huo wa mwokozi wako kuitwa mwana wa shetani,na kwamba shetani ni Mungu, ikimbie dini hii ya uongo na inayowapeleka wengi kuzimu wakidhani wanamwabudu Mungu kumbe ni ibilisi. Iokoe roho yako toka katika mifumo ya dini na madhehebu mwangalie Bwana Yesu maana yeye ndiye njia, kweli na uzima mtu hatofika kwa BABA Isipokuwa kwa njia yake yeye tu!

Amina.

Saturday, October 14, 2017

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?:


Karibu tuongeze maarifa katika Neno la Mungu,


Tukisoma kwenye biblia kitabu cha warumi 4 tunaona mtume Paulo anasisitiza kuwa mtu hahesabiwi haki mbele za Mungu kwa matendo yake bali kwa Imani, lakini tukisoma tena katika kitabu cha Yakobo 2, Yakobo anasisitiza kuwa mtu hahesabiwi haki kwa Imani tu, bali pia na kwa matendo. Tunaona sentensi hizi mbili zinaonekana kama kupingana, Lakini je! Biblia kweli inajipinga au ni sisi uelewa wetu ndio unaojipinga??..tuichambue mistari hii miwili kwa undani kidogo..


1) Warumi 4:1-6


"1 Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili?
2 KWA MAANA IKIWA IBRAHIMU ALIHESABIWA HAKI KWA AJILI YA MATENDO YAKE, ANALO LA KUJISIFIA, LAKINI SI MBELE ZA MUNGU.

3 Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.
4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.
5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.
6 Kama vile Daudi anenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,.

Ni dhahiri kuwa hapa mtume Paulo alipokuwa anazungumzia MATENDO, alikuwa analenga matendo yatokanayo na sheria  ya kwamba hakuna mwanadamu yoyote anaweza akasimama mbele za Mungu kwa matendo yake kuwa ni mema au amestahili kumkaribia Mungu. Kwa mfano mtu kusema nimestahili kwenda mbinguni kwa matendo yangu mazuri, mimi sio mwasherati, sio mwizi, sio mtukanaji, sio mlevi, sio mwongo, sio mwuuaji n.k. kwa kusimamia vigezo kama hivyo hakuonekana hata mmoja aliyeweza kumpendeza Mungu isipokuwa mmoja tu naye ni BWANA wetu YESU KRISTO! wengine wote kama biblia inavyotaja kuanzia Adamu mpaka mwanadamu wa mwisho atakayekuja duniani Mungu alishawaona wote tangu mwanzo kuwa wamepungukiwa na utukufu wake,

 Warumi 3:23" kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; " na ukisoma pia Zaburi 14:2-3 inasema " Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja." .Hivyo hii inadhihirisha kabisa hakuna hata mmoja atapata kibali mbele za Mungu kwa matendo yake mazuri.


 lakini swali ni je! kama sio kwa matendo, basi mtu atapata kibali mbele za Mungu kwa njia gani tena??..


Ukiendelea kusoma mbele tunasoma mtume Paulo anasema ni kwa njia moja tu tunaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu nayo ni njia ya kumwamini BWANA YESU KRISTO tu!. Ndio njia pekee inayotupa sisi kupata kibali mbele za Mungu, kwa namna hiyo basi tunayo haki ya kuwa na uzima wa milele, kwenda mbinguni, kubarikiwa kwasababu tumemwamini mwana wa Mungu YESU KRISTO na sio kwa matendo mema tuyatendayo. Kumbuka zipo dini nyingi zenye watu ambao wanatenda matendo mema lakini je! wanao uzima wa milele ndani yao? utakuta ni wema kweli wanatoa zaka, wanasaidia maskini, sio waasherati, sio  walevi n.k. lakini bado Mungu hawatambui hao. Lakini sababu ni moja tu, hawajamwamini mwana wa Mungu ili aziondoe dhambi zao. Kwahiyo tunaona hapo jambo kuu Mungu analolitazama ni wewe kumwamini mwana wa Mungu, na ukishamwamini (yaani kumpa maisha yako) ndipo ROHO wake MTAKATIFU anakutakasa na kukufanya uishi maisha matakatifu ya kumpendeza.

2). Lakini tukirudi kusoma kitabu cha Yakobo 2:21-26 


"21 JE! BABA YETU IBRAHIMU HAKUHESABIWA KUWA ANA HAKI KWA MATENDO, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?
22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.
23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

Katika kifungu kile cha kwanza ukiangalia kwa undani utaona kuwa mtume Paulo alikuwa anazungumzia juu ya MATENDO YATOKANAYO NA SHERIA. Lakini hapa Yakobo hazungumzii habari ya matendo yatokanayo na sheria bali ni MATENDO YATOKANAYO NA IMANI.. hivyo ni vitu viwili tofauti. 



MFANO WA MATENDO YATOKANAYO NA IMANI: 

Kwamfano: Mtu amepimwa na daktari na kuambiwa kuwa anaugonjwa wa kisukari, na hatakiwi kula vyakula vyenye asili ya sukari na wanga. lakini mtu yule akilishikilia lile Neno kwenye biblia Mathayo 8:17 linalosema " ....Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu. " Na kuliamini na kuamua kuchukua hatua na kusema mimi ni mzima na sio mgonjwa kwasababu yeye alishayatwaa madhaifu yetu, na kusimama na kutembea kama mtu mzima asiyeumwa na kula vyakula vyote hata vya sukari na wanga ingawa daktari alimkataza, akiamini kuwa amepona kwa NENO lile atapokea uponyaji wake. sasa  kitendo cha yeye kuchukua hatua ya kuishi kama mtu mzima ambaye haumwi japo ni mgonjwa na kula vile vyakula alivyoambiwa asile hicho ndicho kinachoitwa MATENDO YA IMANI Yakobo aliyoyazungumzia..


Unaona hapo haki ya huyo mtu kuponywa haikutokana na matendo ya sheria (yaani utakatifu, kutokuwa mwasherati, au mlevi au mwizi n.k.). bali ni matendo yaliyotakana na kumwamini YESU KRISTO katika NENO lake ndio yaliyomponya. Na ndio jambo hilo hilo lililomtokea Ibrahimu pale alipomwamini Mungu na kumtoa mwanae kuwa dhabihu, kwahiyo kile kitendo cha yeye kumtoa mwanawe hayo ndiyo MATENDO yanayozungumziwa na Yakobo YA IMANI kwasababu hiyo basi ikampelekea yeye kupata haki mbele za Mungu. Unaona hapo haikuwa sababu ya yeye kutokuwa mwongo, au mlevi, au muuaji n.k. ndio kulimpa haki yeye ya kubarikiwa hapana bali ni kumwamini Mungu na kuiweka ile imani katika matendo. Kwasababu kama ingekuwa kwa usafi wake Mtume Paulo asingesema Ibrahimu hana la kujisifu mbele za Mungu.

Vivyo hivyo kwa mambo mengine yote kwamfano haki ya kuzungumza na Mungu, haki ya kuponywa magonjwa,  haki ya kubarikiwa, haki  ya kwenda mbinguni, haki ya karama za rohoni, haki ya kuwa mrithi, n.k. havitokani na MATENDO YA SHERIA bali MATENDO YA IMANI. Kwa sisi kumwamini YESU KRISTO katika Neno lake ndipo tunapopata vyote. Kwahiyo matendo yote mema ya sheria yanakuja baada ya kuwa ndani ya Kristo na hayo ndiyo yanayokupa uhakika kama upo ndani ya Kristo, ni kweli huwezi ukawa ni mkristo halafu bado ni mlevi, mwasherati, mwongo, mwizi n.k.. lakini jua katika hayo mtu hahesabiwi haki mbele za Mungu kama tukitaka tuhesabiwe katika hayo hakuna mtu atakayesimama mbele za Mungu.


Kumbuka Ibilisi anawinda IMANI yetu kwa Bwana pale tunapoiweka katika matendo na sio kingine, tunasamehewa dhambi kwa imani, tunaponywa kwa imani, maombi yetu yanajibiwa kwa imani, kila jambo tunapokea kwa Mungu kwa IMANI IPATIKANAYO KATIKA NENO LAKE. Lakini shetani anaenda kinyume kukufanya udhani utasamehewa dhambi kwasababu unashika amri kumi, au  kwa kufunga na kuomba sana ndio utapata haki ya kuponywa, n.k. Bwana amesema waebrania 10:38 " Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. "


Wagalatia 2:16 " hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki. "

Waefeso 2:8-9 "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;  wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. "

Bwana akubariki.


Friday, October 13, 2017

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 19

SWALI 1: Naomba ufafanuzi wa huu mstari; 1Wakoritho 15:29 "Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, KWANINI KUBATIZWA KWA AJILI YAO? . Kulingana na mstari huu inaonekana ni sahihi wale wanaobatiza kwa ajili ya wafu au kuwaombea, hawakosei?.

JIBU: 
Ni vema Tukiisoma habari hiyo kuanzia juu mstari wa 12-14 ili tupate picha sahihi 

" 12 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?
13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka;
14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.
15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.
Tunaona habari hii katika kanisa lililokuwa Koritho kulikuwa na shida ya baadhi ya watu waliokuwa wanajiita waumini wasioamini kuwa kuna kiyama ya wafu, na bado wengine  walikuwa wanaendelea kushikilia imani  ya kubatiza kwa ajili ya wafu. Mambo hayo yalikuwa yanafanywa na hawa wakoritho kama ilivyoelezewa na mwandishi mmoja wa historia aitwaye st.John Chrysostom wa karne ya nne, Achbishop; kwamba kulikuwa na utaratibu wa mtu ambaye amekufa kabla ya kuamini na hajabatizwa ili kwamba mtu huyo aweze kwenda mbinguni ni lazima mtu mwingine aliye hai ajitokeze na kubatizwa kwa niaba yake, ilikuwa wanafanya kumchukua mtu mzima na kumficha chini ya kitanda cha yule marehemu, kisha kuhani anakuja na kumwongelesha yule maiti ikiwa kama yupo tayari kubatizwa au la na kama hatajibu yule mtu aliyelala chini yake atamjibu kuhani kwa niaba ya yule maiti kisha atakwenda kubatizwa, na kwa kufanya hivyo atakuwa amemkomboa yule mtu aliyekufa kutoka katika adhabu ya milele. 


Lakini kwanini mtume Paulo alinukuu hilo?
Ukiendelea mpaka mstari wa 29” utakutana na jambo hili.."Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, KWANINI KUBATIZWA KWA AJILI YAO? . “
 
Jambo hili mtume Paulo alilizungumzia kwa kutaka kuwakumbusha wale wasioamini kuwa kuna kiyama cha wafu kuwa kama hawaamini hivyo kwanini wanabatiza mtu kwa ajili ya mfu? ikiwa hakuna kiyama cha wafu. maana kama hawaamini ingewapasa wasifanye hivyo maana kwa kufanya kitendo hicho ni dhahiri kuwa wanaamini  kwamba kuna maisha baada ya kufa. je! hawaoni kama wanajichanganya wao wenyewe? ..Hiyo ndiyo sababu ya mtume Paulo kuandika hivyo. 
Lakini Mtume Paulo hakumaanisha yeye au wakristo walikuwa wanafanya hicho kitendo cha kubatiza kwa niaba ya wafu bali ni wengine ndio maana alitumia neno “WENYE”.
Na sio tu jambo hilo potofu la kubatiza kwa ajili ya wafu lilikuwepo kwenye makanisa bali pia imani nyingine potofu kama ya kusema " siku ya Bwana imeshakuja" N.K. zilikuwa zikihubiriwa katikati ya makanisa ya Mungu (soma 2timotheo 2:18, 2wathesalonike 2:2).
 
Leo hii imani kama hizi zimeasilishwa pia katika Kanisa Katoliki, likishikilia mistari hii kuthibitisha fundisho la (wakristo kupitia "toharani /purgatory ") ikiwa na maana kuwa mkristo aliyekufa katika dhambi na hajakamilishwa katika neema anakwenda mahali pa mateso ya muda kwa ajili ya utakaso wa dhambi zake kisha akishatakasika anaweza kwenda mbinguni, hivyo basi muda wa kuendelea kukaa katika hiyo sehemu ya mateso inaweza ikafupishwa kwa kutegemea maombi au sala za walio hai wakimwombea. Jambo ambalo sio sahihi Biblia inasema mwanadamu ameandikiwa kufa mara moja na baada ya kufa ni hukumu (waebrania 9:27), kumuombea mtu aliyekufa, au kubatizwa kwa ajili yake ni moja ya mafundisho potofu ya kuwafanya watu waendelee kustarehe katika dhambi wakiamini kwamba hata wakifa katika dhambi watakuwa na nafasi ya pili ya kusafishwa, usidanganyike hizo ni elimu za shetani wakiyapindua maandiko kuthibitisha uongo wao biblia pia inasema  1 timotheo 4:1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, WAKISIKILIZA ROHO ZIDANGANYAZO, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; “.

SWALI 2:
Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?.


JIBU: Neno Malkia wa mbinguni limeonekana mara mbili katika biblia  
1).Yeremia 7:18-20 ”Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi. “ na  baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.” Je! Watu hawa wanikasirisha mimi? Asema Bwana; hawajikasirishi nafsi zao, na kuzitia haya nyuso zao wenyewe?Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.  
2). Yeremia 44:17-23” Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.
18 Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa.
19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko, waume zetu wasipokuwapo?
20 Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake, yaani, watu wote waliompa jibu lile, akisema,
21 Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! Bwana hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake?
22 Hata Bwana asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.
23 Kwa sababu mmefukiza uvumba, na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya Bwana, wala hamkuitii sauti ya Bwana, wala hamkwenda katika torati yake, wala katika amri zake, wala katika shuhuda yake; ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo. “
 
Tunaona habari hizo zote mbili zinaelezea juu ya miungu ya kipagani iliyowasababishia Israeli kuingia matatizoni kwa kwenda kuifukuzia uvumba na kumbuka haina uhusiano wowote na ukristo, kwahiyo mbinguni Mungu anapoishi hakuna malkia, biblia inamtaja MFALME TU!, Naye ni mmoja na si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA yeye peke yake. Hivyo Mariamu sio malkia wa mbinguni, alikuwa ni mwanamke kama wanawake wengine waliokuwa wanamcha Mungu na kupewa neema ya kumzaa Bwana Yesu, lakini hilo halina uhusiano wowote na yeye kuwa malkia, desturi za kuabudu miungu wake ni za kipagani na zilikuwepo tangu zamani AShtorethi mungu mke alikuwa anaabudiwa zamani zile na ndiye aliyekuwa anajulikana kama malkia wa mbinguni. 

Kanisa katoliki ndilo lililobeba tamaduni hizi za kipagani kumwabudu Mariamu na kuwa kama kipatanishi kati yetu na Mungu ambayo ni machukizo makubwa mbele za Mungu.


Bwana akubariki!