"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Sunday, October 22, 2017

MAJI YA UZIMA.


Siku zote roho ya mwanadamu imejawa na KIU ya mambo mengi yahusuyo mema, kwa mfano KIU ya kupata FURAHA, kiu ya kuwa na AMANI, kiu ya UZIMA USIOKOMA,kiu ya kuwa na UPENDO kiu ya KUTENDA MEMA, kiu ya kutaka UTAKATIFU,  kiu ya kuwa MNYENYEKEVU na MVUMILIVU, kiu ya KUWA NA RAHA, kiu ya KUWA KARIBU NA MUNGU ..n.k..


Lakini wengi wanatafuta njia za kuzikata kiu hizi kwa njia nyingi tofauti tofauti za kibinadamu. wengine wanatafuta RAHA kwa kufanya anasa, wengine wanatafuta AMANI kwa kunywa pombe, wengine wanatafuta FURAHA kwa kupata mali, wengine wanatafuta UZIMA WA MILELE kwa waganga na wapiga ramli, wengine wanatafuta UPENDO kwa kulaghai, wengine wanatafuta UHURU kwa kuua n.k..


Lakini ni dhahiri kuwa njia zote hizo ni batili, yaani aidha hazikati kabisa au zinakata kiu kwa muda tu! baada ya hapo tatizo linarudi  palepale..Lakini kuna habari njema, ya mmoja tu anayeweza kuikata kiu yako moja kwa moja isikuwepo tena naye si mwingine zaidi ya BWANA YESU. 


Kwa yeye utapata Raha nafsini mwako, furaha isiyokoma, amani, upendo, unyenyekevu, upole, utakatifu, kujua kumcha Mungu, na uzima wa milele n.k..Hivyo nakushauri Mkaribishe moyoni mwako na hakika ataikata KIU yako, usiipuuzie sauti yake ikuitapo . kwa maana maandiko yanasema:


Yohana 7:37-38 "Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, YESU akasimama, akapaza sauti yake akisema, MTU AKIONA KIU, NA AJE KWANGU ANYWE. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake". 

 
Yohana 4:13-14 "Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. 


Mungu akubariki.

No comments:

Post a Comment