"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Wednesday, May 17, 2017

NDOA NA TALAKA:

Mathayo 19:3-8" Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? 4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 5 akasema, KWASABABU HIYO, MTU ATAMWACHA,BABAYE NA MAMAYE, ATAAMBATANA NA MKEWE; NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA;6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. BASI ALIOWAUNGANISHA MUNGU, MWANADAMU ASIWATENGANISHE. 7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? 8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. "


Hapa tunaona jambo la kuachana kwa mke na mume halimpendezi Mungu hata kidogo, kwasababu biblia inasema alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. Hivyo ndoa haipaswi kuvunjwa isipokuwa kwa sababu zifuatazo zilizohorodheshwa kwenye biblia; 

1) UASHERATI:

Biblia inasema kwenye mathayo 19:9" Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, ISIPOKUWA NI KWASABABU YA UASHERATI, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. ". 

Ikiwa mmojawapo kati ya wanandoa amefumaniwa katika uzinzi hapo biblia imeruhusu kumwacha mtu huyo, na kwenda kuoa au kuolewa na mtu mwingine, lakini kama ni kwasababu nyingine yoyote tofauti na uzinzi mfano kugombana, kuudhiana,  fitna, matatizo, shida, dhiki,magonjwa n.k. hapo biblia hairuhusu kuachana, na hata kama imetokea wameshindwa kulewana na kupelekea kuachana hairuhusiwi kwenda kuoa au kuolewa tena, Biblia inasema kila mmoja akae kama alivyo, ikiwa kama wakipatana wanaweza wakarudiana kinyume na hapo watakuwa wanafanya uzinzi.(marko 10:11-12) ,

 Biblia inasema 1wakoritho 7:10- 11" Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe".  

Hivyo basi ikiwa jambo kama hili limetokea mmojawapo kukamwatwa katika uzinzi ni vizuri ukajifunza kusamehe ili ndoa isivunjike, Mungu hapendi kuachana, kwasababu hata Bwana Yesu Kristo anatusamehe sisi mara nyingi pale tunapomfanyia uasherati wa kiroho, je! sisi hatupaswi kufanya zaidi?  lakini ikiwa huwezi kuvumilia  unaweza ukaivunja utakuwa hauna hatia biblia imeruhusu wewe kwenda kuoa au kuolewa na mtu mwingine.

2) IKIWA AMETAKA KUKUACHA KWA SABABU YA IMANI YAKO:

Kama imetokea mlifunga ndoa wakati wote hamjawa waamini, na wewe ukaja kuwa muamini angali ukiwa ndani ya hiyo ndoa, na mkeo/mumeo asitake kukubaliana na imani yako na akaamua kukuacha asiishi tena na wewe, katika hali kama hiyo biblia inaruhusu wewe kwenda kuoa/kuolewa na mtu mwingine lakini iwe katika BWANA TU!. Lakini kama ikitokea yule mtu katika hali yake ya kutokuamini anakubali kuishi na wewe hautakiwi kumuacha ukimuacha na kwenda kuoa/kuolewa na mtu mwingine utakuwa UNAFANYA UZINZI!
soma...1wakoritho 7:12-16 " Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. 13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. 14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu. 15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani. 16 Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo? ".

Kumbuka kuachana huku ni kwa wale tu! walioana kabla ya kuamini! Biblia haitoi ruhusu yoyote kwa wale walioamini kuachana isipokuwa kwa habari ya uasherati tu, na pia biblia hairuhusu mtu mwamini akaoe/kuolewa na mtu asiyeamini! Hilo ni kosa.

Hivyo basi kama maandiko yanavyosema waebrania 13:4" Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. ". Ni vizuri mtu unapoingia kwenye ndoa ujue ni jambo la kuheshimika na Mungu hapendezwi na wanandoa kuachana kwasababu yoyote ile! (malaki 2:16 ). Pale ndoa inapofungwa tu! Mungu anaachilia neema na baraka ya ziada tofauti na mtu ambaye hayupo kwenye ndoa, na pale ndoa inapovunjika kumbuka kuna hasara nyingi, ikiwemo kuzuia baraka za kiroho, watoto unawafanya kuwa kama yatima, unajirudisha nyuma na kuanza safari mwanzo hivyo basi ili kuyaepuka hayo kuwa mwaminifu kwa Bwana na kwa mke/mme wako. Na pia ufanye maamuzi sahihi katika kuchagua mwezi ikiwa kama bado haujaingia kwenye ndoa.

Mungu akubariki!

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 15


SWALI: Kuna andiko kwenye biblia ambapo Yakobo alimwibia kaka yake haki ya baraka kutoka kwa baba yake Isaka ambaye alikuwa haoni, Huku akisaidiwa na mama yake, je Mungu anaruhusu udanganyifu?.


JIBU: Haki ya mzaliwa wa kwanza Esau aliitoa kihalali kwa kumuapia ndugu yake pale alipokuwa na njaa. Jambo la Yakobo na mama yake kudanganya ni matokeo ya Esau kutoa kibali mwenyewe, lakini kama asingeuza haki yake, Mungu asingeruhusu hayo yatokee angesimama na kumpigania ili ule UONGO wa Yakobo na mama yake usifanikiwe, Lakini kwasababu tayari alikuwa ameshaiuza ulinzi wa Mungu ulimtoka,kwahiyo baraka ya mzaliwa wa kwanza ikaenda kwa Yakobo, na hata kama wasingetumia uongo Mungu angechipusha  njia yoyote ile ili tu Yakobo abarikiwe. 
Hivyo Mungu aliruhusu uongo umvae Yakobo na mama yake, uwe kama njia ya kumpatia Yakobo haki ya mzaliwa wa kwanza, jambo kama hilo tunaweza pia tukaliona kwenye kitabu cha 1 wafalme 22:19-23, pale Mungu alipokusudia kumuua Mfalme Ahabu kwasababu ya maovu yake, akaruhusu pepo la uongo liende kumdanganya yeye kwa kupitia wale manabii wake 400, ili aende vitani akauawe, tunaona hao manabii wake 400 ambao mwanzoni walikuwa wanaona maono sahihi, na kumtabiria mambo ya kweli kutoka kwa Mungu lakini wakaingiwa na hayo mapepo wote wakamtabiria Ahabu uongo kuwa atashinda vitani naye akaamini lakini alivyokwenda kupigana akaishia kufa: 
 Tusome 1wafalme 22:19-23 " Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto. 20 BWANA AKASEMA, NI NANI ATAKAYEMDANGANYA AHABU, ili akwee Ramoth-Gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. 21 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. 22 Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo. 23 Basi angalia, Bwana ametia pepo wa uongo kinywani mwa manabii wako hawa wote; naye Bwana amenena mabaya juu yako. "..... 
Unaona mfano huo hapo juu, na kwa namna hiyo hiyo roho ya uongo ilimwingia Yakobo na mama yake kumdanganya Isaka, lakini amri ilitoka kwa Bwana kwasababu moyo wa Esau haukuwa mkamilifu mbele zake, ili makusudi yake yatimie.

SWALI 2: Kuna andiko linasema MUSA aliwahi kuua mtu huko Misri na kukimbilia nchi nyingine, pia Mungu akamchagua kuongoza taifa la Israeli kutoka misri kwenda nchi ya ahadi, je Mungu anaruhusu kuua?.


JIBU:  Musa alipokuwa Misri alikuwa hamjui Mungu bado, alikuwa ni pagani akiabudu miungu ya kimisri, hajasafishwa bado matendo yake ya kipagani, yeye alijaribu kutaka kuwaokoa wana wa israeli kwa njia zake za kisiasa na kiburi cha ujuzi wa kimisri aliokuwa ameupata katika jumba la Farao, lakini Mungu hatendi kazi hivyo ndio maana tunaona Mungu alimpeleka jangwani kumnyenyekeza kwa muda wa miaka 40, Na aliporudi tunaona hakuua tena alikuwa mtu mwingine, biblia inasema Musa alikuja kuwa mtu MPOLE kuliko watu wote DUNIANI (Hesabu 13:3" Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. "). 
Unaona Mungu hafanyi kazi na watu wenye kiburi na WAUAJI,Kwahiyo Mungu alianza kutembea na Musa baada ya ile miaka 40 lakini kabla ya hapo Musa alikuwa anajiamulia mambo yake mwenyewe alikuwa ni hodari katika maneno biblia inasema (matendo 7:22 "Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo. "), lakini baada ya kunyenyekezwa tunaona akimwambia Mungu yeye sio mnenaji (Kutoka 4:10" Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito." ).

Tuesday, May 16, 2017

MTU MWENYE KUSITA-SITA KATIKA MAWAZO MAWILI.

 YAKOBO 1:5-8"  Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. 
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. 
7 MAANA MTU KAMA YULE ASIDHANI,YA KUWA ATAPOKEA KITU KWA BWANA. 
8 MTU WA NIA MBILI HUSITA-SITA KATIKA NJIA ZAKE ZOTE."


Mtu akishakuwa mkristo vita kubwa anayoanza kupitia ni katika AKILI, shetani anahamisha vita vyake kutoka katika mambo ya nje, kwenda katika mambo ya ndani kwa kusudi moja tu, la kumfanya mtu huyo alitilie SHAKA Neno la Mungu!, kwa kumletea mashaka asiuamini wokovu wake jambo linalompelekea mtu kama huyo kuwa katika hali ya KUSITA KWENYE MAWAZO MAWILI.
Shetani anafahamu kuwa mtu atakapoliamini Neno la Mungu kwa asilimia zote pasipo mashaka atapata anachokitafuta, sasa hapo shetani ndipo anapoanza kuwinda imani ya huyo mtu kwa kumletea mashaka moyoni mwake. Tunaona mfano mtu kama Petro alianza kutembea vizuri juu ya maji lakini alipoanza kutia shaka tu akaanza kuzama. Kwahiyo silaha kubwa shetani anayoitumia kwa mkristo ni kumletea mashaka asiliamini Neno la Mungu aendelee kubaki katika hali ya kusita-sita asipokee kitu chochote kutoka kwa Bwana. Mbinu hii shetani alitoka nayo tangu Edeni pale Hawa aliporuhusu wazo la shetani la kutilia mashaka NENO la Mungu, na kula tunda ikapelekea mauti jambo ambalo linaendelea mpaka sasa. KULITILIA MASHAKA NENO LA MAUNGU!.

  Kwamfano Neno la Mungu limeahidi "wakutanikapo wawili au watatu kwa jina lake yeye atakuwepo katikati yao". Lakini shetani atamletea mtu huyo wazo kwenye akili yake likisema : {...Aah! hilo haliwezekani, Mungu yupo mbinguni hawezi kuwepo hapa katikati yetu,hawezi kuwepo sehemu kama hii, sisi ni wachafu kama sivyo mbona hatumuhisi....}.  Sasa mtu huyo akidhani kuwa hilo wazo ni la kwake, kumbe hajui linatoka kwa yule mwovu..kwasababu shetani amemletea hilo wazo likianza na "mimi.. mimi.. mimi". Halianzi kama shetani anamwambia mtu huyo bali linakuja kama vile yeye huyo mtu ndio analiwaza hilo wazo. Hivyo inakuwa ni ngumu kwa mtu kama huyo kutambua mawazo ya shetani ni yapi na yake ni yapi. Kwasababu hiyo basi shetani anafanikiwa kumwacha katika hali ya kusita-sita na mwisho wa siku hapokei chochote kutoka kwa Mungu kwasababu Mungu hakai katika mashaka, yeye ni wa kuaminiwa tu!.

  Tuchukue mfano mwingine, Neno la Mungu linasema."Kwa kupigwa kwake sisi tumepona". Hivyo Mtu akiwa mgonjwa atakapojaribu tu kulitafakari hili NENO limfae kwa ajili ya uponyaji wake, wazo lingine litamjia kwa haraka kichwani mwake,..{....Aaah! Hivi ni kweli inawezakana, hii inahitaji mtu mwenye upako sana, au mtakatifu sana, mimi nimemkosea sana Mungu hawezi kunisamehe wala kunisikia....} .Kwahiyo mtu huyu anadhani kuwa mawazo hayo ni yeye kayatengeneza kumbe hajui ni shetani ndiye aliyemtengenezea na kuyapandikiza kwenye Akili yake pasipo mtu huyo kujua, Na kama ilivyo ada  shetani anamletea hilo wazo lianze na neno "mimi,.. mimi". Hivyo basi mashaka hayo yakishaingia ndani ya moyo wake yanamsababishia mtu huyo asipokee uponyaji wake. Shetani anakuwa amemshinda.

  Mfano mwingine, Bwana Yesu alisema Marko 11:24"  Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. ". Hapa utamkuta mtu yupo katika kusali na kupeleka mahitaji yake binafsi mbele za Mungu. akiwa katikati ya kusali wazo linamjia,{..."Aah! Hivi kweli Mungu atajibu maombi yangu, Mungu lazima atakuwa hapendezwi na mimi!. Ili anisikie ingenipasa nifunge kwanza wiki tatu, Aaah! acha tu niombe anaweza akanijibu"....}..Unaona hapo hilo neno "anaweza".tayari ni mashaka hayo hana uhakika na anachokiomba akidhani kuwa hayo ni mawazo aliyoyatengeneza yeye, kumbe ni mawazo ya shetani kayatupa kwenye akili yake, na kumfanya mtu huyo kuwa katika hali ya kusita-sita hivyo hawezi kupokea chochote kutoka kwa Mungu, Kwasababu shetani anajua tu! atakapoliamini hilo NENO kwa asilimia zote, pasipo kutilia shaka kwa namna yoyote, Atapokea chochote anachokiomba.


Tazama hichi kisa hapa chini, jinsi mtu huyu alivyompa Kristo maisha yake, siku ya jumatatu, lakini angalia shetani alivyoanza kuiwinda imani yake, na kumpelekea kuwa MTU WA KUSITA-SITA KATIKA MAWAZO MAWILI.


 
   Siku ya jumanne anaanza kujifunza Neno la Mungu...


 ..Siku ya jumatano anautilia mashaka wokovu wake...


...Alhamisi anajihisi hajaokoka na kurudia kumpa Kristo tena maisha yake...



NAMNA YA KUSHINDA HALI HIYO:
Wazo lolote linalokuja katika kichwa chako linalokufanya ulitilie shaka NENO la Mungu, lipinge na kulikataa kwa JINA LA YESU kwasababu hayo sio mawazo yako bali ni ya shetani ameyaelekeza kwako ili usipokee kitu kutoka kwa Mungu kwasababu Mungu anasema katika Yakobo 1:7-8 "Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. 
8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.". Hivyo basi  Rudisha mawazo yako na sema ndani ya moyo wako "maneno ya Mungu, ni kweli na hakika". yashikile hayo hayo pasipo kujihukumu mwenyewe. Na kwa kufanya hivyo shetani atakukimbia na kukufanya kuwa mshindi siku zote na kupokea Ahadi za Mungu. Usiruhusu mawazo yoyote ya kulichunguza NENO la Mungu kuwa linafanyaje fanyaje kazi, siku zote njia za Mungu hazichunguziki wewe AMINI tu!. Hayo mengine mwachie yeye, amesema kwa kupigwa kwake tumepona! amini hilo NENO kila siku litamke,sema moyoni mwako Mungu siku zote hawezi kusema uongo! usitafute kujua litafanyaje fanyaje kazi, itaonekana kuwa hakuna matumaini! lakini wewe liamini tu na utashangaa unapokea uponyaji wako. NENO la Mungu linasema "yote yawezekana kwake yeye aaminiye".Kwahiyo ukiwa katika sala unaomba jambo lolote amini umelipokea. usianze kusita-sita, au kujiuliza uliza au kutafuta njia mbadala,wewe mwamini Mungu lishikilie hilo neno, nalo litatokea kama lilivyo usitazame muda hata kama litachelewa lakini litakuja tu! wewe liamini tu usiruhusu mawazo mengine yoyote ya shetani ya mashaka kuingia ndani yako. Pambana shetani hapo ndipo anapofanyia vita na hakuna vita vigumu kama hivyo, Tutamshinda shetani tu pale tutakapokuwa na NENO ndani yetu na kuliamini asilimia mia, lakini tukiwa watu wa mashaka kama maandiko yanavyosema TUSITAZAMIE KUPOKEA KITU CHOCHOTE KUTOKA KWA BWANA.


       ......Hapa yule mtu anatambua uongo wa shetani na anachukua hatua..




.....mwishoni wokovu wake unakuwa thabiti usiokuwa na mashaka.......

Mungu akubariki!

Saturday, May 13, 2017

KITABU CHA UZIMA


Ufunuo 20:11-15" Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na VITABU VIKAFUNGULIWA; na KITABU KINGINE KIKAFUNGULIWA, AMBACHO NI CHA UZIMA; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa KATIKA VILE VITABU, sawasawa na MATENDO YAO. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 NA IWAPO MTU YEYOTE HAKUONEKANA AMEANDIKWA, KATIKA KITABU CHA UZIMA, ALITUPWA KATIKA LILE ZIWA LA MOTO."

Amina! Tukifuatilia mistari hiyo hapo juu tunaona katika ile siku ya mwisho ya Hukumu Bwana Yesu atakapoketi kuwahukumu wanadamu katika kiti chake cheupe, kutakuwa na ina kuu mbili za vitabu: KITABU CHA UZIMA na VITABU VINGINE,. Hapo unaona kitabu cha uzima kinaonekana ni kimoja tu!. Lakini pia kuna vitabu vingine, ikiashiria ni vingi, kwa ufupi  tuvichunguze hivi vitabu ni vitabu gani;



1) KITABU CHA UZIMA:
Kitabu cha uzima kama kinavyojielezea ni kitabu kinachoelezea UZIMA, kama vile kitabu cha hesabati kinaelezea njia za hesabu, kitabu cha jeografia kinaelezea masuala ya kijeografia vivyo hivyo na vitabu vingine vyote. Na tunafahamu vitabu huwa vinagawanyika katika kurasa mbali mbali. Lakini tunaona vitabu vyote hivi tulivyonavyo duniani vinatueleza tu kanuni na mbinu za mambo mengi yahusuyo ulimwengu huu, na tunaona hakuna kitabu chochote ulimwenguni kilichoweza kuelezea UZIMA wa mwanadamu isipokuwa BIBLIA TU!. Kwahiyo kitabu cha uzima kinachozungumziwa hapo ni BIBLIA ambalo ni NENO LA MUNGU.

2) VITABU VINGINE
Tunaona biblia imevitaja kuwa ni vingi, hivi navyo  vinaelezea habari fulani na sio nyingine zaidi ya wanadamu kulingana na biblia inavyosema. Hivi ni VITABU vya wanadamu na kila mwanadamu anacho cha kwake, kikimwelezea maisha yake jinsi alivyoishi hapa duniani kwa muda wote aliopewa hapa duniani kuanzia kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Na hivi navyo vina ukurasa, ambazo ni hatua unazopitia hapa duniani, Lakini hivi vitabu vyote havina uzima ndani yake, kitabu cha UZIMA ni kimoja tu, na ndio maana hivi vyote vinakitegemea hicho kitabu cha UZIMA kutoa hatma ya mwanadamu.
Kwahiyo kile kitabu cha UZIMA kinaelezea kanuni na taratibu za mwadamu anavyopaswa aishi hapa duniani ili aupate huo uzima uliondikwa ndani yake, hivyo basi kama wanadamu tunaoandika vitabu vya maisha yetu tunapaswa tuviandike vifanane na kile kitabu cha UZIMA yaani BIBLIA, kuanzia utoto wetu mpaka kuondoka kwetu duniani vitabu vyetu vinatakiwa vifanane na Kitabu cha UZIMA, na huko ndiko KUONEKANA KWA  MAJINA YETU KATIKA KITABU CHA UZIMA. 

Hivyo ndugu kitabu chako unakiandikaje? angalia muda unavyokimbia! usiseme nitampokea Kristo au nitaishi maisha matakatifu nifikisha umri fulani au nikishapata kitu fulani. Jua mpaka sasa kitabu chako kinaendelea kuandikwa na ndivyo kurasa zinavyozidi kufunguka na kufunga, muda unavyozidi kwenda ghafla utajikuta kitabu chako kimefungwa kinasubiriwa kufunguliwa kwenye ILE SIKU YA HUKUMU. 

Na siku ile ya Hukumu kitabu cha UZIMA kitafunguliwa na cha kwako pia kitafunguliwa, vitalinganishwa, kama vinafanana au la! '"HUKO NDIKO KUHAKIKIWA JINA LAKO". Kama Jina lako halikuonekana inamaanisha kitabu chako (maisha yako), Hayaendani na kile kitabu cha UZIMA  (yaani Biblia, NENO LA MUNGU). Hivyo basi kwa kuwa hauna UZIMA ndani yako sehemu yako itakuwa katika lile ziwa liwakalo Moto na kibiriti.

Kama mkristo maisha yetu kila siku tunapaswa tuyalinganishe maisha yetu na biblia, je! tukifanyacho kinaendana na kitabu cha uzima?. unafahamu kabisa waasherati, wazinzi, walevi, watukanaji, waabudu masanamu, waongo, wasengenyaji, mashoga, wasagaji, wavutaji sigara, wafanyaji wa mustarbation, watazamaji wa pornography, waizi, mafisadi,waendaji kwa waganga na wapiga ramli, wala rushwa, wauaji, nk, watu wa dizaini hii maisha yao yapo mbali na kile kitabu cha UZIMA, unategemea vipi uonekane katika kile kitabu, kumbuka majina yanayozungumziwa pale sio John, Yohana au Mary bali ni maisha yako  Jihakiki ndugu komboa wakati siku hizi ni za mwisho. soma. Ufunuo 21:27 " Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo."

Siku zote Kitabu hakiandikwi katika siku moja, ili kitabu chako kifanane na kile cha UZIMA Sio hatua ya siku moja bali ya maisha yako ya kila siku, usiishi maisha ya kuidharau injili leo ukasema siku moja nitamgeukia Mungu, usijinganye kile kitabu haukifananishi ndani ya siku moja inahitaji maisha. Bwana YESU alisema Luka 9:23" Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake KILA SIKU, anifuate. " Unaona sio siku moja.
Maombi yangu ni wewe umgeukie Mungu. Anza kukiandika kitabu chako vizuri katika muda wako wa maisha uliobakiza hapa duniani, kila siku kifananishe kitabu chako na kitabu cha UZIMA ili siku ile ikifika JINA LAKO LIONEKANE. UIEPUKE HUKUMU.

Mungu akubariki!

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 14

SWALI 1: Mathayo 6:7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.Nisaidie ninaweza kuomba vipi nikaonekana kuwa sijapayuka payuka mbele za Mungu?

JIBU:Mungu akubariki ndugu, mstari huo ukiangalia kwenye tafsiri nyingine hilo neno "kupayuka-payuka" halimaanishi kama "kupaza sauti kwa nguvu," kama watu wengi wanavyodhani, hapana bali linamaanisha "KURUDIA-RUDIA" maneno yale yale, Hilo la kupaza sauti kwa nguvu mstari wake ni ule wa juu yake kabla ya huu unaosema "Mathayo 6: 5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Na ndipo sasa mstari unaofuata unasema...

7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. "

Hivyo watu wanao rudia-rudia maneno, kwa mfano watu  dini nyingine na watu wanaosali rozari na sala za bikira mariamu wanafahamu,huwa wanarudia maneno yale yale kwa muda mrefu hata masaa na masaa wakidhani kuwa kwa kufanya vile Mungu atasikia dua zao. Hizo ni desturi za kipagani ndio maana tumeonywa tusifanane na hao. kwahiyo tunapoenda mbele za Mungu tuwe na malengo, tutoe hoja zetu zote, kisha zikishaisha, basi, tushukuru tuondoke Tukiamini kuwa Mungu kashatusikia na sio kuanza kurudia rudia tena kile tulichokiomba kana kwamba Mungu hasikii,. kwa ufupi usiweke mfumo fulani unaoonyesha mrudio rudio katika kusali, kuwa huru mbele za Mungu ndivyo Sala zako zitakavyokuwa na thamani mbele za Mungu.

SWALI 2: Katika ule mfano wa wanawali kumi Bwana Yesu alioutoa katika mathayo 25, wanawali werevu walikuwa na mafuta katika taa zao pamoja na mafuta ya ziada lakini wale wapumbavu walikuwa na mafuta lakini hawana ya ziada. swali ni je! Haya mafuta ya ziada ni nini?


JIBU: Kama inavyoeleza wote walikuwa ni wanawali ikiwa na maana wote  ni wakristo wanaomngojea Bwana. Na yale mafuta waliokuwa nayo wote ni "Roho Mtakatifu". Lakini wengine walionekana kuwa na mafuta ya ziada, na wengine hawana.Hii inafunua aina mbili za wakristo watakaokuwepo siku za mwisho,
 AINA YA KWANZA: Hawa ni wale wakristo werevu waliopokea Roho Mtakatifu na kuruhusu Roho wa Mungu kufanya kazi ndani yao kwa kutaka kujifunza na kuendelea kupokea mafunuo ya Roho wa Mungu mpaka kufikia utimilifu, mtu wa dizaini hii kila siku anakuwa tayari kujifunza jambo jipya, hivyo anahama kutoka utukufu hadi utukufu kila siku kiu na bidii ya kuendelea kumjua Mungu inaongezeka, hafungwi na mifumo fulani ya dini au dhehebu, bali Neno la Mungu ndio taa yake, Hivyo basi Mungu anamfungulia mlango wa kufahamu mafunuo ya ziada (ile mana iliyofichwa, ufunuo 2:17) kutokana na jitihada yake ya kumtafuta Mungu hivyo basi inamfanya yeye kuwa watofauti na wakristo wengine. Kwahiyo hata Bwana atakapokuja atakuwa na NURU ya kwenda kumlaki hatakuwa gizani. 

AINA YA PILI: Hawa ni wale  wakristo wapumbavu ambao walishapokea Roho Mtakatifu (ambayo ndio yale mafuta kwenye taa zao) lakini sasa baada ya kupokea Roho wa Mungu wanamzimisha ndani kwa kutomruhusu tena aendelee kuwafundisha mambo mapya. kwasababu kazi ya Roho Mtakatifu ni kukuongoza katika kuijua kweli yote, soma Yohana 16:13" Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. ". Kwahiyo aina hii ya wakristo wanakuwa wameridhika na hali walionayo na mafundisho ya dini zao au madhehebu yao tu, hawataki kujifunza jambo jipya na wakiambiwa hata kama linatoka kwa Mungu hawatataka kusikia, kiu na bidii ya kuendelea kumjua Mungu hawana wanaridhika na mafundisho ya madhehebu yao tu. Hivyo basi wakati Bwana atakapokuja hawatakuwa na NURU ya kumtambua na kwenda kumlaki.  

Kwahiyo kama wewe ni mkristo fahamu jambo moja Mungu mpaka leo anatenda kazi anaongea, anatoa mafunuo mapya, anaonya, anawapasha watu habari ya mambo yajayo, na anawapa wale tu wanaompenda na kumtafuta kwa bidii na kutaka kuufahamu ukweli hao ndio atakaowafunulia, Ndugu fahamu tu UNYAKUO hautakuwa SIRI kwa watu wote, wale wapumbavu ndio hawatajua siku ya kuondoka, lakini wenye mafuta ya ziada watajua. Kwahiyo ukiwa kama mkristo kwa ulimwengu tunaoishi leo mtafute Bwana kwa moyo wako wote aendelee kujifunua kwako ili siku ile isikujie kama mwivi. kwahiyo usiwatazame hao wakristo wapumbavu wewe kuwa mwerevu kwa kumruhusu Roho Mtakatifu kuendelea kufanya kazi ndani yako.
SWALI 3:  Naomba kuuliza..ni nani anayetawala dunia kati ya Mungu na shetani? Na kama ni Mungu anayetawala kwa nini kuna matukio ya kutisha kama ajali mbaya za magari,ndege,mafuriko kama ya Japan kama Mungu ndiye anayetawala kwanini hayazuii anaacha yanaua watu??? Na ukisoma mathayo 4:1 na kuendelea unasoma shetani anamwambia Yesu dunia ni Mali yake, nataka kufahamu pia je! Kuna  tofauti gani kati ya dunia na ulimwengu nisaidie?


JIBU:
Dunia yote ni ya Mungu ukisoma;



 Zaburi 24: 1-2 "1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.
2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. "



Na pia Bwana Yesu Kristo baada ya kufufuka kwake aliwaambia wanafunzi wake

 mathayo 28:18"Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. "



Kwahiyo kwa maandiko hayo tunaona kabisa kuwa dunia yote inamilikiwa na Mungu na wala sio shetani, lakini "dunia sio ulimwengu". Huu ulimwengu ndio mali ya shetani na ndio yeye anayeumiliki na kitakachokuja kuteketezwa sio dunia bali ni ulimwengu huu mbovu wa shetani ambao ni milki yake aliyojijengea..


Tofauti kati ya dunia na ulimwengu ni hii;

  • Dunia ni vitu vyote vya asili na vya kijeografia unavyoviona  kama vile mabara, bahari, miti, milima, hewa, ardhi, mito,mabonde, visiwa,anga, n.k.

  • Na Ulimwengu ni ustaarabu uliobuniwa na aidha Mungu au shetani ili kuifanya dunia iwe na mantiki paonekane kama ni mahali pa kuishi. mfano. elimu, burudani, miziki, utawala, uchumi, mahakama,Milki, fahari, uchukuzi, mawasiliano,  n.k. Haya yote ni mambo yaliyobuniwa kuipa dunia muonekano unaoleta maana. Na ndio maana kwenye mathayo 4 shetani alimwambia Bwana Yesu nitakupa ULIMWENGU na fahari yake ukianguka kunisujudia.

Kwahiyo dunia itadumu siku zote, lakini ustaarabu uliowekwa na shetani (yaani ulimwengu )utaangamizwa utabaki tu ule uliowekwa na Mungu, na hata hivyo 99% ya ustarabu uliopo duniani leo hii unakaliwa na shetani na ndio maana siku ya Bwana itaharibu ustaarabu wote wa shetani na kuleta ustaarabu mpya wa Kristo hapa duniani huo ndio utakaodumu milele na  utakaokuwa ni ule utawala wa miaka 1000 ufunuo 19 & 20.


Na sababu ya Mungu kuruhusu mambo mabaya kutokea kama ajali, vimbunga, mafuriko ni kwasababu ya mambo maovu ya huu ulimwengu yaliyopo kama umwagaji damu, rushwa, uasherati, ulevi, uaribifu wa mazingira, ushoga, vita, n.k. mambo kama haya ardhi haiwezi ikavumilia, yanaiharibu  dunia na kupelekea gadhabu ya Mungu kumwaga juu ya nchi.
Tujitahidi tujiepushe na mambo ya ulimwengu huu yanayopita..Tuyatazame yaliyo juu.


Mungu akubariki

Ukiwa na swali, lolote unaweza ukatutumia, kwa neema za Bwana tutalijibu na kukutumia. Weka jina lako, na swali lako, tutakutumia kwa njia ile unayoitaka. (inbox, e-mail, whatsapp).

Sunday, May 7, 2017

MPINGA-KRISTO


Vita kubwa inayoendelea duniani leo ni vita kati ya MUNGU na SHETANI. Mungu anatafuta roho za watu vile vile shetani naye anawinda roho za watu. Hizi roho mbili zimekuwa zikipingana siku zote tangu ulimwengu ulipoanza kukaliwa na wanadamu. 

Lakini baada ya mwanadamu kuanguka Mungu alitumia njia zote kwa Roho wake kumvuta kwake tena, mwishoni akaona vema kumleta mwanawe mpendwa YESU KRISTO kwa dhumuni moja tu! kutupatanisha sisi na Mungu, ili katika yeye sisi sote tuokolewe. 

Vivyo hivyo shetani naye, kwa kuona hivyo kwa roho yake ya uovu, alitumia njia zake zote za kuweza kumtoa mwanadamu katika kusudi la Mungu na kumvuta kwake, jambo hili lilianza tangu Edeni, tunaona shetani jinsi alivyomtumia Nyoka kumdanganya Hawa ili aipate roho yake. Hivyo basi ulipofika wakati alipoona Mungu amemleta mwokozi katika mwili yaani YESU KRISTO na kuwavuta wengi kwa BABA, yeye naye alianza mipango ya kumwandaa mtu mmoja ambaye atakuwa na kazi maalumu ya kuwavuta watu kwake na kwenda kinyume na huyo mmoja Mungu aliyemteua (yaani YESU KRISTO). Sasa mwana huyu wa shetani ndiye anayeitwa MPINGA-KRISTO.

Kumbuka vita vya kwanza kabla ya Kristo kuja vilikuwa ni roho kwa roho (yaani Roho wa Mungu dhidi ya roho ya shetani), lakini vita vya mwisho ni MTU dhidi ya MTU (yaani YESU KRISTO dhidi ya MPINGA-KRISTO).

Wakristo wengi wanapokosa shabaha ni pale wanaposhindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani na MPINGA-KRISTO ni nani?. Ukishindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani huwezi kumfahamu MPINGA-KRISTO ni nani.

Hawa wote wawili waliandikwa kwenye NENO la Mungu katika "SIRI". Ikiwa na maana utendaji kazi wao ulihitaji "UFUNUO wa ROHO" Kuutambua. Embu kwa ufupi, tutazame siri iliyopo kwa YESU KRISTO ambayo ilikuwa imefichika kwa Muda mrefu na hata sasa baadhi ya watu bado imefichika machoni pao.

SIRI YA YESU KRISTO:

1 Timotheo 3:16 " Na bila shaka SIRI YA UTAUWA NI KUU. Mungu alidhihirishwa katika MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu."
Ukisoma hapo utaona kuwa jambo hili Mungu aliliweka liwe SIRI,na sio kitu cha wazi ya kwamba Yesu Kristo alikuwa ni MUNGU KATIKA MWILI. Yaani ni Roho ya Mungu ikitenda kazi katika mwili, lakini wengi hawakulijua hilo walimkataa na kumsulubisha,na hata leo wengi hawalifahamu hilo. maana Bwana Yesu alisema "Yohana 5:43  Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. " unaona huyo mwingine BWANA YESU aliyemzungumzia akija kwa jina lake mtampokea ni MPINGA-KRISTO mwenyewe..tusome tena mstari ufuatao

1 Wakoritho 2:6-8"  Walakini iko HEKIMA tusemayo KATI YA WAKAMILIFU; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; 7 bali twanena HEKIMA YA MUNGU KATIKA SIRI, ILE HEKIMA ILIYOFICHWA, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; 8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, WASINGALIMSULIBISHA BWANA WA UTUKUFU; ".
Kwa maandiko hayo hapo juu, hata leo watu katika mioyo yao wanamchukulia YESU KRISTO kama ni mtu wa kawaida kama walivyofanya watu wa kipindi kile, wanayadharau maneno yake sio kwa mdomo bali kwa matendo, lakini hawajui kuwa wanamkataa na kumsulibisha Mungu mwenyewe ambaye ni BWANA WA UTUKUFU,  kwa heshima aliitoa damu yake, imwagike kwa ajili ya dhambi zetu kutupatanisha sisi na yeye lakini bado leo hii unaichezea hii damu ya thamani, itafika wakati hii neema haitakuwepo tena.

SIRI YA MPINGA-KRISTO:

2 Wathesalonike 2:3 "Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; AKAFUNULIWA YULE MTU WA KUASI , MWANA WA UHARIBIFU; 4 YULE MPINGAMIZI, AJIINUAYE NAFSI YAKE JUU YA KILA KIITWACHO MUNGU AMA KUABUDIWA; hata yeye mwenyewe kuketi katika HEKALU LA MUNGU, AKIJIONYESHA NAFSI YAKE KANA KWAMBA YEYE NDIYE MUNGU. 5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo? 6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. 7 Maana "ILE SIRI YA KUASI" HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule ASI, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; 9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; 10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa." 
Ukisoma habari hiyo mstari wa saba inazungumzia SIRI YA KUASI ambayo inatenda kazi duniani, na hii siri ya kuasi inatenda kazi ndani ya yule ASI (ambaye ndio mpinga-kristo mwenyewe) kama maandiko yanavyomtaja kwenye mstari wa 9, kuwa "kutenda kwake kazi ni mfano wa kutenda kwake shetani mwenyewe". Kama tu vile SIRI YA UTAUWA ilivyokuwa inatenda kazi ndani ya YESU KRISTO, na kutenda kwake kazi Yesu kulikuwa ni mfano wa kutenda kwake Mungu mwenyewe vivyo hivyo na huyu (Mpinga-kristo) siri ya kuasi inatenda kazi ndani yake na  kutenda kwake kazi kutakuwa ni mfano wa shetani.

JE HUYU MPINGA-KRISTO NI NANI?
Baada ya shetani kuona kuwa hawezi kuwapata wanadamu wengi kwa kutaka wamwabudu moja kwa moja kama wanadamu wamwabuduvyo Mungu, aliamua kujibadilisha na kujifanya kuwa kama malaika wa Nuru (2Wakoritho 11:14), ili awapate wale wanaoonyesha dalili ya kuipenda Nuru. Kumbuka shetani hafanyi vita na watu wa ulimwengu huu, kwasababu hao alishawapata na siku zote wapo gizani, kwahiyo ili awapate wale wa nuruni ni lazima ajigeuze kuwa mfano wa malaika wa Nuru, vivyo hivyo na watumishi wake nao ni lazima wajigeuze kuwa kama watumishi wa nuru. Hapo ndipo penye vita vikali pale mbwa-mwitu anapokuja kwa vazi la kondoo. Hivyo inahitaji hekima ya Roho Mtakatifu kumtambua mpinga-kristo vinginevyo hawatakaa ufahamu adui yako yupo wapi na anatendaje kazi.

Ndugu kuna vikundi vingi vya kishetani na kichawi, vinavyosifika kama freemason, rotary clubs, iluminati, ku klux klan, brotherhood, n.k. vimekuwa vikiogopeka kana kwamba hivyo ndio makao makuu ya shetani, usidanganyike vikundi hivyo shetani anavitumia kuwadaka watu wasiokuwa wakristo na wakristo wachache wenye imani isiyothabiti kwasababu mkristo wa kweli yoyote hawezi kwenda kwa mganga na shetani analijua hilo, wala hawezi kujiunga kwenye mojawapo ya hivyo vikundi wala kupiga ramli, au kupunga-pepo, shetani anajua kabisa kama angetegemea njia hiyo tu, basi angewakosa wakristo wengi sana duniani. Anafahamu kuwa mkristo mahali pake pekee anajihisi atakutana na Mungu ni kanisani na ndiko huko huko anapowafuata wakristo.

Kumbuka, shetani anatenda kazi katika SIRI, na ndiyo maana ikaitwa "SIRI YA UASI". na inatenda kazi ndani ya Kanisa la Mungu pale shetani anapovaa mavazi ya kondoo lakini ndani ni MBWA-MWITU(Hii ni SIRI). kuharibu roho za watu(wakristo wa kweli) na kuwapeleka kuzimu. Anatumia hila zake kuwafanya watu waone kama wanamwabudu Mungu, kumbe wanamwabudu yeye. Anaingia kanisani na kuwafanya watu wajione kuwa wapo katika njia sawa, lakini mwisho wake ni kuzimu,. Na anaowapeleka kuzimu kwa njia hii ni kubwa sana kuliko hata hizo njia nyingine ndogo ndogo kama uchawi, freemason n.k. HAPA NDIPO KRISTO ALIPOTUTILIA MSISITIZO KWAMBA "TUJIHADHARI NA MANABII WA UONGO, WANAOVAA MAVAZI YA KONDOO LAKINI NDANI NI MBWA-MWITU WAKALI"..Ndugu, Bwana hakutuonya tujihadhari na wachawi au wapiga-ramli, au freemason, au wapunga-pepo hilo ni jambo dogo sana ambalo kwa namna ya kawaida mkristo yoyote anaweza kujihadhari nayo. 

Baada ya shetani kujiingiza kwa siri kwenye kanisa la Mungu na kukomaa kwa muda mrefu, tunaona alianza kwa kuharibu mafundisho ya Mungu ya kweli na kupachika mafundisho ya kipagani kama ibada za wafu, ibada za miungu mitatu, kuongeza vitabu katika NENO la Mungu, Ibada za sanamu kanisani, kubariki pombe kanisani, na kupindisha maandiko na utaratibu uliokuwepo wa kanisa kwa kupotosha ubatizo sahihi wa maji, na wa Roho Mtakatifu, kwa kuua karama za roho, kuingiza siasa na vyeo katika kanisa visivyotakana na Mungu,kuua mafundisho ya uponyaji wa kiungu,  n.k.



 Kwa kuendelea hivyo alifanikiwa kutengeneza kanisa lake moja "MFU" lenye jina linalofanana na  lile kanisa la mwanzo la kweli lakini sio, watu wakidhani kuwa ndio lile kanisa la kwanza (la Mitume) kumbe wamepotea pasipo wao kujua ROHO MTAKATIFU ameshaondoka muda mrefu imebaki roho ya shetani ikitawala, Kwahiyo shetani akalipa jina hili kanisa lake akaliita UNIVERSAL CHURCH yaani KANISA LA ULIMWENGU (KANISA KATOLIKI). 

Na yeye(shetani) akiwa kama mungu wa hilo kanisa aliweka watumishi wake, Na akaweka cheo cha juu zaidi kabisa katika hilo kanisa ambacho ndio cheo kile cha UPAPA (hichi ndicho cheo cha MPINGA-KRISTO mwenyewe) kisimame kwa niaba yake duniani kama Yesu Kristo alivyosimama kwa niaba ya Mungu duniani. Tunafahamu katika historia chombo chake kiteule alichokitumia shetani kupambana na uzao wa Mungu ni KANISA KATOLIKI,na si kingine, lilifanikiwa kuua zaidi ya wakristo milioni 68, waliojaribu kuenda kinyume na mifumo yake ya kipagani. Na hadi leo kanisa hili linaendelea kuuwa watu wengi kiroho, kwa kudhani wanamwabudu Mungu kumbe wanamwabudu shetani katika hilo kanisa. Na litakuja kuuwa wengi zaidi katika kipindi cha ile dhiki kuu. HAYA NDIYO MALANGO YA KUZIMU.

Hivyo basi roho ya mpinga-kristo inakaa katika cheo cha UPAPA, kwahiyo mtu yeyote atakayekikalia hicho cheo atakuwa amekidhi vigezo vyote kuwa MPINGA-KRISTO. 
Injili iliyopo leo hii, kulingana na wakati tunaoishi sio injili tu ya kuwavuta watu kwa Kristo, kwasababu wengi wameshampokea Kristo lakini hawajui kuwa wanamwabudu shetani pasipo wao kujua katika madhehebu yao wakidhani kuwa wapo sawa kumbe hawapo sawa. Ndugu Mungu kashatoa laana juu ya kanisa Katoliki na madhehebu yote yasiyokaa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, (maana haya kwa pamoja ndiyo yanayounda ile chapa ya mnyama).  Kwa kufahamu zaidi kwa undani juu ya chapa ya mnyama unaweza kusoma soma tuliloliandika linaloitwa "CHAPA YA MNYAMA".

Haya ndiyo maneno ya Bwana mwenyewe.

Ufunuo 18:4-5"  Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE. 5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. "
Bwana anatuonya tutoke (sio kutoka kwa miguu bali kwa roho. Yaani kujihadhari na mafundisho yote yasiotoka na Mungu, ukiri ukristo wa biblia usiukiri udhehebu) Toka katika kamba za madhehebu, umwabudu Mungu katika roho na kweli kwasababu hayo yamefanya uasherati wa kiroho kwa kuchanganya NENO la Mungu na mafundisho ya kipagani hivyo Bwana ameyahukumu na yoyote atakayeshirikiana nayo atashiriki katika mapigo yake yote yaliyoandaliwa kwasababu yameshiriki katika kumwaga damu nyingi za watakatifu wa Mungu.