"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Wednesday, May 17, 2017

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 15


SWALI: Kuna andiko kwenye biblia ambapo Yakobo alimwibia kaka yake haki ya baraka kutoka kwa baba yake Isaka ambaye alikuwa haoni, Huku akisaidiwa na mama yake, je Mungu anaruhusu udanganyifu?.


JIBU: Haki ya mzaliwa wa kwanza Esau aliitoa kihalali kwa kumuapia ndugu yake pale alipokuwa na njaa. Jambo la Yakobo na mama yake kudanganya ni matokeo ya Esau kutoa kibali mwenyewe, lakini kama asingeuza haki yake, Mungu asingeruhusu hayo yatokee angesimama na kumpigania ili ule UONGO wa Yakobo na mama yake usifanikiwe, Lakini kwasababu tayari alikuwa ameshaiuza ulinzi wa Mungu ulimtoka,kwahiyo baraka ya mzaliwa wa kwanza ikaenda kwa Yakobo, na hata kama wasingetumia uongo Mungu angechipusha  njia yoyote ile ili tu Yakobo abarikiwe. 
Hivyo Mungu aliruhusu uongo umvae Yakobo na mama yake, uwe kama njia ya kumpatia Yakobo haki ya mzaliwa wa kwanza, jambo kama hilo tunaweza pia tukaliona kwenye kitabu cha 1 wafalme 22:19-23, pale Mungu alipokusudia kumuua Mfalme Ahabu kwasababu ya maovu yake, akaruhusu pepo la uongo liende kumdanganya yeye kwa kupitia wale manabii wake 400, ili aende vitani akauawe, tunaona hao manabii wake 400 ambao mwanzoni walikuwa wanaona maono sahihi, na kumtabiria mambo ya kweli kutoka kwa Mungu lakini wakaingiwa na hayo mapepo wote wakamtabiria Ahabu uongo kuwa atashinda vitani naye akaamini lakini alivyokwenda kupigana akaishia kufa: 
 Tusome 1wafalme 22:19-23 " Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto. 20 BWANA AKASEMA, NI NANI ATAKAYEMDANGANYA AHABU, ili akwee Ramoth-Gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. 21 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. 22 Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo. 23 Basi angalia, Bwana ametia pepo wa uongo kinywani mwa manabii wako hawa wote; naye Bwana amenena mabaya juu yako. "..... 
Unaona mfano huo hapo juu, na kwa namna hiyo hiyo roho ya uongo ilimwingia Yakobo na mama yake kumdanganya Isaka, lakini amri ilitoka kwa Bwana kwasababu moyo wa Esau haukuwa mkamilifu mbele zake, ili makusudi yake yatimie.

SWALI 2: Kuna andiko linasema MUSA aliwahi kuua mtu huko Misri na kukimbilia nchi nyingine, pia Mungu akamchagua kuongoza taifa la Israeli kutoka misri kwenda nchi ya ahadi, je Mungu anaruhusu kuua?.


JIBU:  Musa alipokuwa Misri alikuwa hamjui Mungu bado, alikuwa ni pagani akiabudu miungu ya kimisri, hajasafishwa bado matendo yake ya kipagani, yeye alijaribu kutaka kuwaokoa wana wa israeli kwa njia zake za kisiasa na kiburi cha ujuzi wa kimisri aliokuwa ameupata katika jumba la Farao, lakini Mungu hatendi kazi hivyo ndio maana tunaona Mungu alimpeleka jangwani kumnyenyekeza kwa muda wa miaka 40, Na aliporudi tunaona hakuua tena alikuwa mtu mwingine, biblia inasema Musa alikuja kuwa mtu MPOLE kuliko watu wote DUNIANI (Hesabu 13:3" Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. "). 
Unaona Mungu hafanyi kazi na watu wenye kiburi na WAUAJI,Kwahiyo Mungu alianza kutembea na Musa baada ya ile miaka 40 lakini kabla ya hapo Musa alikuwa anajiamulia mambo yake mwenyewe alikuwa ni hodari katika maneno biblia inasema (matendo 7:22 "Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo. "), lakini baada ya kunyenyekezwa tunaona akimwambia Mungu yeye sio mnenaji (Kutoka 4:10" Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito." ).

No comments:

Post a Comment