"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Monday, October 21, 2019

BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU.

Zaburi 23:1 "Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.  2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.  
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.  4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji"

Mchungaji ni tofauti kidogo na Mchungaji…Mfugaji anawafuga Wanyama nyumbani labda kwenye Boma au zizini na anawaletea chakula nyumbani. Wanyama wanakuwa hawana uhuru wa kwenda kutembea huko na kule kuchagua wenyewe aina za nyasi na kuruka ruka.

Lakini Mchungaji, ni mfugaji ambaye Wanyama wake wapo huru kuachiwa huku na kule kula watakacho…lakini wapo katika Ulinzi wa Mchungaji!...

Na sisi mbele za Kristo ni kondoo tulio huru…Tupo huru kwenda huko na kule, tupo huru katuachia tukae katikati ya uovu wa huu ulimwengu, …lakini tupo chini ya Ulinzi wa Mchungaji wetu Mkuu Yesu Kristo.

Ijapokuwa tutakwenda huku na huko, ijapokuwa tutakuwa tupo huru kuruka ruka na kupata mwanga wa jua, lakini siku zote jicho lake linatutazama..Hivyo hatutaogopa!

Kwasababu Gongo lake na fimbo yake vya tufariji, Fimbo yake ni kwaajili ya kumpiga adui.

Bwana ndiye jabali letu na ngome yetu Tumwogope nani?



MASWALI YALIYOULIZWA:

Saturday, October 12, 2019

MSHUNAMI

SWALI: Katika Biblia tunamsoma Mwanamke mmoja aliyeitwa Mshunami, ambaye alimsaidia Nabii Elisha sehemu ya malazi wakati wa huduma yake..Mwanamke huyu aliitwa Mshunami

2 Wafalme 4:12 "Akamwambia Gehazi mtumishi wake, Mwite yule Mshunami. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mbele yake. 13 Akamwambia, Sema naye sasa, Tazama, wewe umetutunza sana namna hii; utendewe nini basi? ..."
Sasa Swali Mshunami maana yake nini? 
JIBU: Ukisoma Mlango huo kuanzia juu kidogo, utaona kuwa Mshunami sio jina la mtu bali ni jina la sehemu..2 Wafalme 4:8 "Hata ikawa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo; naye akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula".
Kwahiyo Mshunami sio jina la Mtu, bali ni jina la mahali...Katika Israeli kulikuwa na mahali panapoitwa "SHENEMU" Kwahiyo mtu yeyote awe mwanamke au mwanamume kama ametokea sehemu hiyo basi aliitwa Mshunami...Ni sawa na nchi Tanzania, yeyote aliyetokea huko ataitwa Mtanzania.
Hivyo SHUNEMU ilikuwa ni Eneo la Israeli, lililokuwa urithi wa kabila la Isakari...Tunalithibitisha hilo katika kitabu cha...
Yoshua 19:17 "Kisha kura ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, maana, ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao.
18 Na mpaka wao ulifikilia Yezreeli, na Kesulothi, na Shunemu"
Na sio tu huyu mwanamke aliyemsaidia Nabii Elisha alitokea huko shunemu, kuna wanawake wengine pia biblia imerekodi walitokea huko huko shunemu...Mmoja wapo na Abishagi aliyeletwa kwa Mfalme Daudi
1 Wafalme 1:3 "Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.
4 Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua"
Mungu akubariki



Mada Nyinginezo





Friday, October 11, 2019

JE! MALAIKA WAPO WANGAPI?

Biblia haijataja kuna idadi gani ya Malaika walioko mbinguni...Lakini tukisoma Biblia tunaweza kujua au kupata picha kuwa kuna idadi kubwa kiasi gani ya Malaika walioko mbinguni..

Kama maandiko yanasema katika...
Mathayo 18:10 "Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni".
Mstari huo unatuonesha kwamba kila mtu aliyezaliwa mara ya Pili, anaye malaika wake akimlinda, akipeleka habari zake njema mbele za Mungu, na akimsaidia katika Kuishikilia Imani.

Sasa hebu fikiri endapo watu wote wangempa Kristo maisha yao, ina maana kila mtu angekuwa na angalau malaika mmoja.

Hivyo mbingu haiwezi kuwa na watenda kazi wachache wa kutuhudumia sisi kiasi kwamba kuna wanadamu wanaweza kukosa Malaika wa kuwahudumia. (Malaika wa Mungu watakaa mbali nasi endapo tu tutakuwa tunajitia unajisi na dhambi), lakini sio kwamba kuna idadi ndogo....Kwahiyo kama wanadamu duniani leo tupo Bilioni 7, basi Malaika ni wengi zaidi ya hiyo idadi...Hivyo unaweza kuona ni jeshi kubwa kiasi gani lililopo mbinguni.

Na Biblia pia inaonesha wazi kwamba inawezekana mtu kutembea na Malaika zaidi ya mmoja.. Soma (2Wafalme 6:16-17).

Mada Nyinginezo:






Tembelea  WWW.WINGULA MASHAHIDI.ORG kwa masomo zaidi

Tuesday, October 8, 2019

KUOTA UNASAFIRI.

Napendelea kabla mtu hajakimbilia kutafuta tafsiri ya ndoto yake, ni vizuri kwanza apate  elimu juu  ya aina za ndoto, hiyo itamsaidia kujua ndoto yake inaangukia katika kundi la aina gani, hivyo atapata wepesi wa kuweza yeye mwenyewe kuzitafsiri ndoto pasipo hata kutegemea msaada wa mtu mwingine.

Ikiwa utapenda kujua aina hizi za ndoto bofya hapa >>  NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?   ukishamaliza kusoma kisha tuendelee…
Sasa kama ndoto yako sio ile inayotokana na shughuli za kila siku au mazingira yanayokuzunguka na unaiota mara kwa mara, basi fahamu kuwa kuna jambo Mungu anazungumza na wewe hapo zingatia sana..Biblia inasema..
Ayubu 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,”
Mungu anakukumbusha kuwa upo safarini hapa duniani, kwamba kila jambo unalolifanya ukumbuke kuwa upo safarini hakuna chochote utashikamana nacho hapa duniani milele,..Na kama tunavyojua safarini, hata mkishuka kupumzika pengine kula au kujisaidia basi  ni dakika chache tu 10 au 15 basi safari inaendelea, hakuna muda wa kuzurura zurura au kuanza kujihangaisha na mambo ya hapo mlipokuwa mnapita, utakuwa ni mjinga kama utawaza kuwekeza eneo hilo, au kwenda kufanya shughuli hapo, gari litaondoka na kukuacha, na mwisho wa siku kule ulipokuwa unatazamia kwenda hutafika..

Hivyo Mungu kukuonyesha hivyo ni kukuonya usiangalie sana mambo ya ulimwengu huu yanayopita bali angalia vya kule mbele vinavyodumu na ukumbuke kuwa upo safarini, inamaanisha kuwa kwa namna moja au nyingine ulishawahi kuyatazama mambo ya kule, ishi kama maisha ya mpitaji, kwasababu watu wote wa Mungu ndivyo wanavyoishi..
Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.”
Hivyo angalia ni vitu gani vinavyokusonga katika maisha yako, Je! Ni shughuli za ulimwengu huu mpaka hauna muda na Mungu? Je! Ni tamaa ya mambo ya ulimwenguni huu, Je ni anasa? Biblia inasema:
1Petro 2:11 “Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.”
Hivyo Fahamu kuwa Mungu anakupenda na ndio maana amekuonyesha ndoto za namna hiyo, basi usipuuzie sauti yake, anza sasa kumtazama YESU ikiwa bado upo mbali naye, Unachopaswa kufanya ni kutubu sasa mkabidhi yeye maisha yako upya, nenda kabatizwe kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, kisha yeye mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu…nawe utakuwa na uhakika wa kuwa salama katika safari yako fupi iliyobakia hapa duniani… Aidha kama utakuwa upo tayari ndani ya Kristo na unajihisi huna kando lolote basi fahamu kuwa Mungu anataka uzidi kuiangalia safari yako zaidi kuliko kitu kingine chochote, kwasababu ipo thawabu kubwa amekuandalia mbele.
Ubarikiwe.


kwa mtiririko mzuri wa masomo na mafundisho mengi ya Neno la Mungu fungua website yetu hii https://wingulamashahidi.org