"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Wednesday, September 28, 2016

UBATIZO SAHIHI


Moja ya maagizo muhimu sana ambayo Bwana YESU KRISTO aliyatoa kwa kanisa ni ubatizo. Mengine yakiwemo kushiriki,kutawadhana miguu kwa wakristo,wanawake kufunika vichwa vyao wakati wa ibada.Kati ya hayo ubatizo ni muhimu sana kwa mwamini yeyote kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake.Lakini ubatizo huu shetani ameuharibu usifanyike ipasavyo kwa sababu anajua una madhara makubwa katika kumbadilisha mkristo.na hiyo ndiyo imekuwa kazi ya shetani tangu awali kuyapindisha maneno ya Mungu na kuzuia watu wasimfikie Mungu katika utimilifu wote,

Makanisa mengi leo hii yanabatiza watu au watoto wachanga kwa kuwanyunyuzia maji wakibatiza kwa jina la BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU kulingana na mathayo 28:19 "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu"..swali ni je! hili jina linatumiwa ipasavyo kubatizia?

Kwa kukosa Roho ya ufunuo na uelewa wa maandiko viongozi wengi wa dini wameacha kweli na kugeukia mafundisho ya kipagani na kuwafundisha watu uongo na kibaya zaidi wengi wao wanaujua ukweli lakini wanawaficha watu wasiujue ukweli kwa kuogopa kufukuzwa kwenye mashirika yao ya dini viongozi kama hawa ni watumishi wa shetani wale Kristo aliowazungumzia akisema  mathayo 23:13" ole wenu waandishi na mafarisayo, wanafki! kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamuingii wala wanaoingia hamwaachi waingie."

Tukirudi kwenye maandiko yohana 5:42-43 "walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.Mimi nimekuja kwa JINA LA BABA YANGU, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo." hapa tunaona dhahiri kabisa jina alilonalo Yesu ni jina la BABA yake. Kwa namna hiyo basi jina la baba yake ni Yesu.

Tukirudi tena kwenye maandiko yohana 14:26 Yesu Kristo alisema "lakini huyo msaidizi,huyo Roho mtakatifu ambaye baba atampeleka  KWA JINA LANGU, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."na  hapa tunaona Roho Mtakatifu alitolewa kwetu kwa jina la Bwana Yesu. kwahiyo hapa biblia inatufundisha dhahiri kabisa kuwa jina la Roho Mtakatifu ni Yesu.

Tukirudi tena kwenye maandiko tunaona kuwa Roho Mtakatifu ndiye Baba mathayo 1:20 "...Yusufu, mwana wa Daudi usihofu kumchukua Mariam mkeo maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu" kwahiyo Baba ndiye yule yule Roho na ndiye yule yule aliyechukua mwili na kuishi pamoja nasi kwahiyo hapa hatuoni 'utatu' wa aina yeyote ambao unahubiriwa leo hii na makanisa mengi.  Mungu ni mmoja tu!.

Kwahiyo jina la Baba ni Yesu na jina la Mwana ni Yesu na jina la Roho Mtakatifu ni Yesu; baba,mwana na roho ni vyeo na sio majina kwa mfano mtu anaweza akawa baba kwa mtoto wake,mume kwa mke wake,babu kwa mjukuu wake lakini jina lake anaweza akawa anaitwa Yohana na sio 'baba,mume au mjukuu' vivyo hivyo kwa Mungu.aliposema mkawabatize kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu alikuwa anazungumzia Jina la YESU KRISTO ambalo ndilo jina la baba na mwana na Roho Mtakatifu.

Katika biblia Wakristo na mitume wote walibatizwa na kubatiza kwa JINA LA YESU KRISTO na sio kwa JINA LA BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU. ubatizo huu wa uwongo ulikuja kuingizwa na kanisa katoliki katika baraza la Nikea mwaka 325 AD pale ukristo ulipochanganywa na upagani na ibada ya miungu mingi ya Roma.

Tukisoma matendo ya mitume 2:37-38 "Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao. wakamwambia Petro na mitume wengine , tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, tubuni mkabatizwa kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu."

Tukisoma tena  katika maandiko Filipo alipoenda Samaria na wale watu wa ule mji walipoiamini injili walibatizwa wote kwa jina lake Yesu Kristo matendo 8:12 " lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habati njema za ufalme wa Mungu na  JINA LAKE YESU KRISTO  wakabatizwa wanaume na wanawake"

Tukisoma tena matendo 8:14-17 " Na mitume walipokuwa Yerusalemu, waliposika ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu.wakawapelekea Petro na Yohana ambao waliposhuka wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila WAMEBATIZWA TU KWA JINA  LAKE BWANA YESU"

Tukisoma tena matendo 10:48  Petro alipokuwa nyumbani mwa Kornelio alisema maneno haya "Ni nani awezaye kuzuia maji,hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vilevile kama sisi? akaamuru WABATIZWE KWA JINA LAKE YESU KRISTO"

Tukisoma tena katika matendo 19:2-6  hapa Paulo akiwa Efeso alikutana na watu kadha wa kadha akawauliza." je! mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?, wakamjibu, la, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? wakasema, kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani Yesu. Waliposikia haya WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU"

Mitume wote hawa kuanzia Petro,Yohana,Filipo na mtume Paulo wote hawa walibatiza kwa jina la Yesu Kristo je? tuwaulize hawa viongozi wa dini wanaobatiza kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu wameutolea wapi??? na biblia inasema katika wakolosai 3:17 " na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote  katika Jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu baba kwa yeye"..hii ina maana tukiomba tunaomba kwa jina la Yesu,tukitoa pepo tunatoa kwa Jina la Yesu, tukiponya watu tunaponya kwa jina la Yesu,tukifufua wafu tunafufua kwa jina la Yesu na tukibatizwa tunabatizwa kwa jina la YESU biblia inasema kwenye matendo 4:12 "...kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo" na hakuna mahali popote katika biblia mtu alibatizwa kwa jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu

na maana ya neno ubatizo ni "kuzamishwa" na sio kunyunyuziwa, kwahiyo ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kwenye maji sawasawa na maandiko na hakuna mahali popote katika maandiko watoto wachanga wanabatizwa. Ubatizo ni pale mtu anapoona sababu ya yeye kutubu na kuoshwa dhambi zake ndipo anapoenda kubatizwa kwa jina la Yesu kwa ondoleo la dhambi zake.

Ewe ndugu Mkristo epuka mapokeo ambayo Yesu aliyaita "chachu ya mafarisayo" penda kuujua ukweli ndugu mpendwa na ubadilike na umuombe Roho wa Mungu akuongoze katika kweli yote usipende mtu yeyote achezee hatima yako ya maisha ya milele, uuchunge wokovu wako kuliko kitu chochote kile,Mpende Mungu, upende kuujua ukweli,ipende biblia..Mwulize mchungaji wako kwa upendo kabisa kwanini anayafanya hayo huku anaujua ukweli na kama haujui mwambie abadilike aendane na kweli ya Mungu inavyosema kulingana na maandiko.

Kama hujabatizwa au umebatizwa katika ubatizo usio sahihi ni vema ukabatizwa tena kwa jina la YESU KRISTO kwa ondoleo la dhambi zako kwani ubatizo sahihi ni muhimu sana..ukitaka kubatizwa tafuta kanisa lolote wanaoamini katika ubatizo sahihi tulioutaja hapo  juu au unaweza ukawasiliana nasi tukakuelekeza kanisa linalo amini katika ubatizo sahihi.

email.watakatifuwasikuzamwisho@gmail.com
 Mungu akubariki
 Shalom!


                                                           Tazama hii video


         (ubatizo sahihi wa kuzamishwa na KWA JINA LA YESU KRISTO)  

USHUHUDA WA RICK JONYER

Rick Jonyer katika kitabu chake maarufu ulimwenguni kinachojulikana kama THE FINAL QUEST, kikielezea jinsi alivyochukuliwa na Bwana Yesu Kristo katika maono mbinguni, katika hicho kitabu alielezwa mambo mengi ikiwemo vita kubwa ya kiroho inayoendelea katika ukristo leo, alionyeshwa silaha shetani anazozitumia kuwaangusha wakristo, vitu kama wivu, hasira, chuki kutokuwa na UPENDO, n.k miongoni mwa wakristo, vinawafanya wasisonge mbele,washindwe vita. alionyeshwa pia thawabu tofauti tofauti wanazopewa wakristo  kulingana na mambo wanayoyafanya wakiwa duniani,aliambiwa mambo mengine mengi ya kumtia Mkristo moyo kuwa na bidii na kushinda vita vilivyo mbele yake. Ni kitabu chenye mhamsho mkubwa kwa Mkristo yeyote.

katika ukurasa wa 42 wa kitabu hichi, kinaeleza jinsi alivyochukuliwa mbinguni na kupelekwa mbele ya viti vya enzi na kumwona mtu ambaye alishawahi kumsikia alipokuwa duniani.. na hapa nanukuu maneno yake...

"na niliposikia hayo maneno, nilijisikia kuangalia moja ya viti vya enzi vilivyokaribu nami. ghafla nikamwona mtu ninayemfahamu. Alikuwa ni muinjilisti maarufu nilipokuwa mtoto mdogo, na watu wengi walimwona kwamba ni mtu aliyetembea na nguvu za Mungu nyingi zaidi ya mtu yeyote tangu kuwepo kwa kanisa la kwanza. nilishawahi kusoma habari zake na nilishawahi kusikiliza mahubiri yake,  ilikuwa ni ngumu kutokuguswa na unyenyekevu wake, na upendo wake kwa Bwana na kwa watu.Hata hivyo nilidhani mafundisho yake yalikuwa na makosa. Nilishangaa lakini hata hivyo nilipata unafuu kumwona akiwa ameketi kwenye kiti cha enzi kikuu.nilivutiwa sana na unyenyekevu wake na upendo wake ambao bado unatoka kwake. na nikamuliza Bwana kama ninaweza kuongea na huyu mtu, kwa jinsi ninavyoona Bwana anavyompenda. lakini Bwana aliniashiria niendelee kutembea mbele, hakuniruhusu kuzungumza na yule muinjilisti.
Bwana alisema ; "nilikuwa ninataka umuone wewe akiwa hapa", Na kuiona nafasi aliyonayo hapa pamoja nami, Kuna mengi ya wewe kujua kuhusu yeye. ALIKUWA NI  MJUMBE KWA KANISA LANGU LA MWISHO, na kanisa halikumsikiliza kwa sababu ambayo utakuja kuijua muda utakapofika. Alianguka kwenye kuvunjwa moyo na upotevu kwa muda na ujumbe wake ukapindishwa. Lakini utarejeshwa tena, pamoja na jumbe nilizowapa wengine ambazo zimepindishwa......."

Rick Jonyer alieleza jinsi alivyokutana na WILLIAM BRANHAM. kwenye maono aliyoonyeshwa na Bwana Yesu Kristo mwenyewe, leo hii Bwana kamthibitisha mjumbe wake. Rick Jonyer aliambiwa akiandike kitabu hiki na kukipeleka duniani kote.
waebr.12:1" Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, Na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu"

je? umempokea Kristo katika maisha yako. Umejazwa Roho Mtakatifu
Umeuamini ujumbe wa wakati huu wa mwisho?
Kristo Bwana wetu yupo mlangoni..."fanya imara kuitwa kwako, na uteule wako"
soma kitabu hichi hapa >>>>download




Monday, September 26, 2016

MVUTO WA TATU!

Bwana  wetu Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani, huduma yake iligawanyika katika sehemu kuu tatu.
ya kwanza:  huduma ya uponyaji, ishara na miujiza
ya pili: kueleza siri za mioyo ya watu, kama vile kwa yule mwanamke msamaria,
ya tatu: kuhubiri neno la Baba yake.

ndugu William Branham alifundishwa na malaika wa Bwana jinsi ya kuvua samaki WAKUBWA kutoka kwenye maji, na yule malaika alimwambia ni kwa namna hiyo hiyo Bwana Yesu Kristo aliitumia kuwavuta watu wake kwake kutoka kwenye dhambi alipokuwa hapa duniani

MVUTO WA KWANZA:
alielezwa kuwa baada ya kuweka mnofu wa kuwavutia samaki kwenye ndoano na kuitupa ndoano  majini baada ya muda kidogo utaivuta juu, wale samaki wadogo wataiona na kuifuata na kuizingira ila wale wakubwa watasogea tu karibu na tukio kuhakikisha kama ni chakula halisi, huo ndio mvuto wa kwanza.

MVUTO WA PILI:
baada ya muda tena kidogo utaivuta ndoano juu tena ila isitoke yote, na wale samaki wadogo waliokuwa wameizunguka ndoano, watakimbia lakini wale samaki wakubwa, watakikaribia na kukila na kunaswa,

MVUTO WA TATU:
baada ya wale samaki wakubwa kunaswa katika mvuto wa pili sasa ni wakati wa kumalizia mvuto wa mwisho.na huu ndio wa kumtoa samaki nje ya maji.

sasa kanisa la Mungu lipo katika mvuto wa tatu ambao ni NENO LA MUNGU, kuandaliwa kwenda kwenye unyakuo, ishara na miujiza haviwezi kutukamilisha hivyo vyote vilikuwa vinatuandaa kwa ajili ya mvuto wa tatu, ambao ni kusikia neno la Mungu,
 tunawashauri wakristo wayatazame mafundisho haya, yameelezea vizuri zaidi kuhusu MVUTO WA TATU,



MUNGU AKUBARIKI





Sunday, September 25, 2016

HUYU NDIYE MFALME WETU NA MUNGU WETU

TUNAMPENDA SANA!


ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO


Papa kiongozi wa kanisa katoliki duniani alipokuwa akihutubia mbele ya maelfu ya watu juni 25, 2014 St. Peter's Square vatican akisema:
  •     katika ukristo hakuna hilo suala kama kumtafuta Kristo peke yako
  •     Mkristo yeyote ni lazima awe mshirika wa kanisa fulani 
  •     papa aliendelea kusema kwamba kuwa na mahusiano binafsi na Kristo, kwa kujaribu kufanya              hivyo ni hatari kubwa na yenye madhara
  •      papa alisema kwa mkristo yeyote jina lake la kwanza liwe la kwake na la pili liwe la kanisa kwa           mfano wewe unaitwa Maiko hivyo wewe utaitwa Maiko Mkatoliki, au Joseph Mlutheri n.k

    Mafundisho haya yanapingana na biblia ni mafundisho ya mpinga kristo,kulingana na ufunuo 17:5.."katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa kwa siri, BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI" katika maandiko mwanamke anawakilisha kanisa,kwa hiyo mwanamke huyu aliyezungumziwa hapa ni kanisa-kahaba,inamaanisha ni kanisa lililochanganya mafundisho ya neno la Mungu na ibada za sanamu  hivyo limemwacha Mungu na kumwabudu shetani ndio maana likafananishwa na mwanamke kahaba na kanisa hili sio lingine zaidi ya kanisa katoliki,
 hivyo basi tunaona hapa sio tu kahaba bali pia ni mama wa makahaba,amezaa mabinti ambao ni makahaba kama yeye, nao ni madhehebu yote na mashirika yote ya dini yaliyoiacha kweli ya neno la Mungu na kugeukia mafundisho kama ya mama yao ya kipagani.Leo hii tunaona makanisa yote ulimwenguni yanaungana na kanisa mama yaani katoliki, na kuiunda ile CHAPA YA MNYAMA,ambayo pasipo hiyo huwezi kuuza wala kununua katika kile kipindi cha dhiki kuu,itafika wakati kila mkristo itampasa asajiliwe  katika dhehebu lake kwa yeye kutambulika kama ni mkristo vinginevyo hautaweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa,wala kufanya kazi yeyote usipokuwa na hiyo chapa ya mnyama ambayo ni..(utambulisho wako wa kidini au dhehebu lako) pia hautaruhusiwa kuabudu kwa uhuru kama unavyoabudu leo,..kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ataingia katika ile dhiki kuu.
    Na kwa jinsi tunavyoiona dunia ya leo vitendo vya ugaidi vimekithiri kutokana na itikadi kali za kidini, shetani ameunyanyua uislamu kuvuruga amani ya dunia kwa kigezo cha itikadi kali za dini,hivyo basi leo dunia inatafuta mtu wa kuleta amani naye ni lazima awe mtu wa dini ili amalize hili tatazo. na yupo mmoja tu duniani sasa anayekubalika na dini zote naye ni PAPA ambaye anajulikana kama mtu wa amani (man of peace) kiongozi wa kanisa katoliki, baadaye atapewa nguvu na dunia ili maandiko ya daniel 11:21 yatimie "Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza", ataleta ustaarabu mpya wa dunia wa kuleta amani (NEW WORLD ORDER). hapo ndipo itakapompasa kila mtu asajiliwe kulingana na shirika lake la dini na dhehebu lake, kwa dhumuni la kuwatambua watu wote, na kukomesha ugaidi, wengi wataliona kuwa ni jambo zuri bila kujua kuwa ndio wanaipokea ile chapa ya mnyama, lakini baadhi ya wale wakristo waliobaki wasiokwenda katika unyakuo hawatakubali kusajiliwa katika madhehebu ya dini, kwasababu watajua kuwa hiyo ndio ile chapa ya mnyama 666 ndani yake, ni hao tu watakao pitia dhiki kuu wakisingiziwa kuwa wao ndio waondoa amani na magaidi, kwa kutokutaka kusajiliwa kwenye dini zao, watakataliwa na watu wote, hawataweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa mahali popote, na mwishoni yule mnyama  atawauwa wote akiwa na roho ya mpingakristo

Mkristo leo hii anayedai kutafuta uhusiano binafsi na Mungu kulingana na papa alivyosema ni "hatari na yenye madhara" hii ni roho ya mpinga Kristo inatenda kazi ndani ya papa ikizungumza maneno haya ya makufuru...dhumuni kubwa ni kuizuia Roho ya Mungu ndani ya watu kutenda  kazi kwa sababu Roho ya Mungu aliachiwa kwa dhumuni moja tu kutuongoza katika kuijua kweli yote.. na pia yeremia 31:34.." Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana;....

Mtu ataijua kweli tu akiwa na Roho Mtakatifu na wala sio kwa kuwa mshirika wa kanisa lolote...biblia inasema  warumi 8:9 "..lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo sio wake."....warumi 8:14.."kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu" ...na wala sio wanaoongozwa na kanisa.

(yohana 14:6 inasema "mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi." hivyo basi hatumfikii Baba kwa njia ya kanisa lolote,wala kwa njia ya kiongozi yoyote wa dini, wala kwa njia ya papa,wala kwa ukatoliki,wala kwa uanglikana,ulutheri,upentekoste,usabato, u-endtime,ubranhamite n.k
  Ukweli ni kwamba KUTOKUWA NA MAHUSIANO BINAFSI NA YESU KRISTO NI HATARI NA YENYE MADHARA MAKUBWA.....

MARAN ATHA!


Saturday, September 24, 2016

JEHANAM IPO HAPA CHINI YA DUNIA!!

video hii fupi inaelezea jinsi wanasayansi wa Urusi, huko Siberia walivyokuwa wakifanya utafiti wao wa miamba umbali wa km 4.4 chini ya ardhi na cha ajabu na cha kushangaza badala ya kusikia sauti za miamba walisikia sauti za watu wengi wanaume kwa wanawake wakilia kwa uchungu mwingi.. jambo hili ni kweli na limethibitishwa na wanasayansi wa taifa lile.. JEHANAM IPO KWELI!
tazama hii video hapa chini na uone sababu ya kuachana na injili za mafanikio ya ulimwengu huu, na kutafuta utakatifu , ukijua kabisa hukumu inakuja mbeleni.


MARAN ATHA!

Thursday, September 22, 2016

MAHOJIANA YA NDUGU WILLIAM BRANHAM- kiswahili

Ndugu Branham akitoa ushuhuda mfupi juu ya maisha yake, jinsi alivyotembelewa na malaika wa Bwana akiwa na umri wa miaka 37, na kupewa huduma ile kuu, kama jinsi tulivyoiona Bwana alivyoweza kumtumia kwa ishara na miujiza mingi sana ambayo haijawahi kutokea katika historia ya kizazi chetu,pamoja na ujumbe wa kuwarejesha watu katika imani ya mababa(PENTECOSTAL FAITH), Na ujumbe wa kumuandaa bibi-arusi wa kristo kwenda kwenye unyakuo. tazama video hii imeongezewa tafsiri kwa lugha ya kiswahili( swahili subtitle).


Monday, September 19, 2016

WAKRISTO KATIKA DHIKI.



Ona jinsi wakristo wa kwanza walivyopitia dhiki nyingi katika kuipigania imani, chini ya utawala wa kipagani wa rumi. wakristo waliliwa na simba, walisulibishwa, walitiwa magerezani, walichomwa moto, waliburutwa, wakubwa kwa wadogo wazee kwa vijana, waume kwa wake kwa ajili ya kuisimamia imani.
Kizazi hiki chetu kibaya kimezungukwa na wingu hili lote la mashahidi.

TUTAWEZAJE KUPONA TUSIPOUTHAMINI WOKOVU MKUU NAMNA HII?

MARAN ATHA.

KITABU CHA DHIKI ZA WAKRISTO- Foxe's book of martyr





kusoma kitabu bonyeza hapa chini.>>>>>download

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

Tangu kipindi cha Bwana Wetu Yesu Kristo kuondoka duniani mpaka sasa imepita miaka takribani elfu mbili na katika hichi kipindi cha miaka hii elfu mbili kanisa limekuwa likipitia katika vipindi tofauti tofauti saba vinavyoitwa NYAKATI SABA ZA KANISA, kulingana na kitabu cha..
Ufunuo 1:12-20" Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;
15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.
 Ufunuo huu alipewa Yohana na Bwana Yesu alipokuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, akionyeshwa jinsi kanisa litakavyokuja kupitia katika siku za mwisho. Leo hii si rahisi sana kuona kitabu cha ufunuo kikiguswa au kuelezewa katika kanisa, na shetani hataki watu wafahamu siri zilizoandikwa katika hiki kitabu maana ndio kinaelezea hatma ya mambo yote ikiwemo na shetani mwenyewe. Kwahiyo ndugu fungua moyo wako ujifunze na Mungu akusaidie unapoenda kusoma ujue ni wakati gani tunaishi na jinsi Bwana Yesu alivyo mlangoni  kurudi kuliko hata unavyoweza kufikiri. Tafadhali pitia taratibu mpaka mwisho ili uelewe.


  • vile vinara saba vinavyozungumziwa ni makanisa saba tofauti tofauti ambayo yamepita tangu wakati wa Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani hadi wakati tunaoishi sasa.
  •  Na zile nyota saba ni malaika saba/wajumbe wa duniani(wanadamu 7 ambao Mungu aliwatia mafuta ) kupeleka ujumbe kwa hayo makanisa saba. Kila mjumbe kwa kanisa lake.







NYAKATI YA KWANZA:
Kanisa: Efeso
Malaika/Mjumbe: MTUME PAULO
kipindi cha kanisa: 53AD -170AD
Tabia ya kanisa: limeacha upendo wake wa kwanza,tangu wakati wa mauaji ya wakristo yaliyoongozwa na Nero mtawala wa Rumi hadi kifo cha mtume Yohana. Na kipindi hiki ndipo matendo ya wanikolai yalianza kuingia katika kanisa (mafundisho ya kipagani). kuanza kujichanga na ukristo. ufunuo 2:1-7
onyo kwa kanisa- litubu lirudi katika upendo wake wa kwanza, lililopoteza.
Thawabu: Yeye ashindaye atapewa kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani ya Mungu.

NYAKATI YA PILI;

Kanisa; Smirna
Malaika/Mjumbe;IRENIUS
kipindi cha kanisa: 170AD -312 AD
Tabia ya kanisa; Ni kanisa lilopitia dhiki nyingi kutoka katika utawala mkali wa Diocletian wa Rumi , watakatifu wengi waliuawa katika hichi kipindi kuliko kipindi chochote katika historia ya kanisa.walichinjwa wengi, na wengine kutupwa kwenye matundu ya simba na wanawake kukatwa matiti na kuachwa mbwa walambe damu zao, na ukatili mwingi sana wakristo walitendewa katika hichi kipindi lakini walistahimili dhiki zote hizi soma kitabu cha (Foxe's book of Martyr- kwenye archives zetu kinaelezea vizuri mauaji ya wakristo). Japo wakristo walikuwa maskini sana  Lakini Kristo aliwafariji kuwa wao ni  Matajiri. ufunuo 2:8-11
Thawabu; Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

NYAKATI YA TATU;
Kanisa ; Pergamo
Malaika/Mjumbe; MARTIN
Kipindi; 312AD -606AD
Tabia ya kanisa; Kanisa laingiliwa na mafundisho ya uongo zaidi, ambayo ndio yale matendo ya wanikolai sasa wakati huu yamegeuka kuwa mafundisho ya kidini. Ukristo ukaoana na upagani ukazaa Kanisa mama mfu Katoliki, katika baraza la Nikea AD 325 siasa na mafundisho ya miungu mitatu,ibada za sanamu na za wafu,sherehe na sikukuu za kipagani, ubatizo wa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, vyeo vya upapa n.k ndipo vilipochipukia. kwa mambo haya basi ikasababisha kanisa kuingia katika kipindi kirefu cha giza (Dark age). Ufunuo 2:12-17
Onyo kwa kanisa: litubu lirudi katika imani iliyoanzishwa na mitume wa Kristo
Thawabu; Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, ila yeye anayelipokea.

NYAKATI YA NNE:
Kanisa; Thiatira
Malaika/Mjumbe;COLUMBA
Kipindi; 606AD -1520AD
Tabia ya kanisa; Japo kanisa lilikuwa na juhudi na bidii katika kumtafuta Mungu, lakini bado lilikuwa na mafundisho ya yule mwanamke kahaba Yezebeli yaani mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Onyo; Litubu litoke katika mafundisho ya wanikolai. Ufunuo 2:18-29
Thawabu;Yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hata mwisho nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.

NYAKATI YA TANO:
Kanisa; Sardi
Malaika/Mjumbe; MARTIN LUTHER
kipindi; 1520AD -1750AD
Tabia; Ni kanisa lililokuwa linarudi katika matengenezo kutoka katika mafundisho ya yule kahaba mkuu kanisa katoliki. lakini lilikuwa bado na Jina lililokufa, wakishikilia baadhi ya mafundisho ya kanisa mama katoliki, huku ndiko chimbuko la walutheri lilipoanzia.Ufunuo 3:1-6
Onyo: litubu, lirejee kwenye mafundisho ya mitume.
Thawabu; Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri Jina lake mbele za baba yangu na mbele ya malaika zake.

NYAKATI YA SITA;
Kanisa;Filadelfia
Malaika/Mjumbe; JOHN WESLEY
Kipindi; 1750AD -1906AD
Tabia; Ni kanisa lililosifiwa kwa matendo yake mema, lilifanikiwa kujua na kuyarekebisha mafundisho ya uongo Kristo alisema ''tazama nakupa walio wa sinagogi la shetani wasemao kwamba ni wayahudi nao sio, bali wasema uongo, tazama nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda''.ufunuo 3:7-13
Thawabu;Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu, huo Yesalemu mpya ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe lile jipya.

NYAKATI YA SABA;
Kanisa; Laodikia
Mjumbe;WILLIAM BRANHAM
Kipindi;1906- Unyakuo
Tabia; Ni kanisa ambalo sio baridi wala moto, bali ni vuguvugu, Kristo anasema ni heri lingekuwa moto au baridi, hii ndiyo hali ya kanisa tunaloishi sasa mimi na wewe, uvuguvugu mbaya umeingia katika kanisa, watu wanajiona kuwa wanamwabudu Mungu katika uzuri wao wa majengo ya kanisa, kwaya.na injili ya mafanikio, wakidhani kuwa hivyo yatosha tu kumjua Mungu kumbe hawajui wameshaingia katika udanganyifu wa shetani pasipo wao kujua, watu wanasema kuwa wanampenda Mungu na bado wanapenda mambo ya ulimwengu huu kama fashion za mitindo ya kisasa wanawake kuvalia mavazi ya nusu uchi, michezo, miziki, muvi, ponography, ulevi. anasa,uasherati,na shughuli za ulimwengu huu ambazo zinawasonga wengi hususani kwa kizazi hichi cha ubize, watu wanapata muda wa kufanya kazi sana, lakini muda wa kumtolea Mungu hawana na bado ni wakristo., huu ndio uvuguvugu Kristo anaouzungumzia kwa kanisa letu la Laodikia.Hapa Kristo anasema unajiona kuwa tajiri kumbe ni maskini na mnyonge na uchi na unamashaka na kipofu, jiulize ni hali gani ya kanisa tulilopo sasa. 

Na hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hili, na ndio linakaribia kuisha. jiulize umejiwekaje tayari kumpokea Bwana Yesu akirudi mara ya pili?. Mungu alimtuma mjumbe wake ndugu William Branham kulionya kanisa letu lirudi katika NENO na imani iliyohubiriwa na mitume pamoja na utakatifu.
Onyo; Kristo anasema kanisa liwe na bidii likatubu na kumgeukia Mungu.
Thawabu;Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na baba yangu katika kiti chake cha enzi. ufunuo 3:14-22

      

Watu wa Mungu hili ndilo kanisa la mwisho tunaloishi hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hapa, tunaishi katika wakati ambao Kristo yupo mlangoni kulichukua kanisa lake teule, JIULIZE! UMEKWISHA KUJIWEKA TAYARI KUMLAKI BWANA, TAA YAKO INAWAKA??UMEMPOKEA ROHO MTAKATIFU??YEYE ALIYE NA SIKIO, NA ALISIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA.



Mungu akubariki
MARAN ATHA!

Sunday, September 18, 2016

KIMBIA! KIMBIA! KIMBIA!

Makanisa yanayohubiri injili ya mafanikio tu. Na kukwambia kuwa uthibitisho wa Mungu kuwa yupo na wewe, ni kuwa tajiri ...JIHADHARI NA HILO KANISA!

Makanisa yasiyohubiri toba ya msamaha na kuwafanya watu wajione ni kawaida kuishi na dhambi zao...JIHADHARI!

Makanisa yanayochanganya NENO la Mungu na siasa na vikundi vya kijamii, jambo ambalo huwezi kutofautisha jukwaa la siasa na kanisa....JIHADHARI SANA!

Makanisa yasiyohubiri utakatifu na kufundisha watu ukweli kulingana na Biblia...KUWA MWANGALIFU NA HILO KANISA..

Makanisa yanayohubiri ujumbe wa kutoa tu, na kuacha mafundisho ya adili kama upendo, utakatifu na imani,,,,JIHADHARI KWAUSALAMA WA MAISHA YAKO YA MILELE.

Kanisa lisilokufundisha wala kugusia kujiandaa kwenda katika unyakuo...KUWA MAKINI!

Kanisa lisiloruhusu karama za Roho kufanya kazi, kama uponyaji wa kiungu, unabii, lugha, miujiza n.k. jua hilo kanisa limekufa au lipo karibuni kufa. JIHADHARI NDUGU!











 


USHUHUDA

ushuhuda wa dada aliyekuwa amechukuliwa mume wake na mwanamke mchawi akiachwa bila kitu peke yake na mumewe akiwa ameondoka na watoto wake 4, na kumuacha katika hali ya umaskini na ufukara kiasi ambacho ilimfanya akose hata mahali pa kulala, isipokuwa katika sehemu za mabaraza ya maduka wakati wa usiku akingojea yafungwe. Lakini alipomwomba BWANA, BWANA YESU  akasikia kilio chake, na siku moja alipokuwa kanisani kwenye ibada Mungu alimfunulia nabii mmoja miongoni mwa watumishi, na kumweleza dada huyu matatizo yake yote, usiku huo huo Bwana alimtoa katika umaskini wake wote, na kumgeuza kuwa milionea na kupata makazi  mapya na Bwana kumuahidia kurudi kwa mume wake na watoto wake. Tazama video hapo chini...

JINA LA BWANA LIBARIKIWE KWA FADHILI ZAKE KWETU SISI WANADAMU!


Saturday, September 17, 2016

MAWASILIANO

Kwa mawasiliano

Ndugu.  DEVIS JULIUS,
Ndugu.  DENIS JULIUS.


email. watakatifuwasikuzamwisho@gmail.com.


+255789001312
+ 255693036618


 Mungu akubariki sana..






Kanisa la Bride Assembly- nigeria.




mahubiri ya ndugu Moses Alu, wa kanisa la Bride assembly Nigeria. Kwa neema za Mungu alizotupa tumetazama mafundisho mengi ya kanisa hili na tumeona kwa sehemu kubwa yanaendana na kweli ya biblia kwa yeyote atakayesikiliza ayatazame pia kwa neno na yatamsaidia kupata kuijua ile kweli zaidi. ujumbe unaofundishwa ni : ''KWA NINI SISI SIO MADHEHEBU'' au kwa kiingereza WHY WE ARE NOT A DENOMINATION;
 Mungu akubariki.!

WINGU LA MASHAHIDI WA KRISTO NA MJUMBE WA MUNGU, NDUGU WILLIAM BRANHAM

Blogu hii imeanzishwa mahususi kwa kusambaza ujumbe wa siku za mwisho kwa BIBI ARUSI safi wa  YESU KRISTO waliokwisha wekwa tayari kwenda katika unyakuo. Hatufangamani na dhehebu lolote wala shirika lolote la kidini, ila tunawakaribisha Wakristo Wote ulimwenguni wenye kumpenda Bwana. Tunaamini Biblia kuwa ni kitabu pekee kitakatifu kilichoshushwa na Mungu kumwongoza mwanadamu,na hivyo misingi ya mafundisho yetu yote unakitegemea hicho.

pia tunaamini kulingana na  malaki 4:5 kama inavyosema " angalieni nitawapelekea Eliya Nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogfya. Naye ataigeuza mioyo ya Baba iwaelekee watoto wao na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana."

kama Mungu alivyoahidi angemtua Eliya nabii. ambaye kulingana na maandiko tunafahamu Yohana mbatizaji aliyatimiza hayo maandiko kwa sehemu "A"( Yaani kuja kabla ya ile siku KUU YA BWANA) ambaye yeye alitangulia kuja kwake Kristo kwa mara ya kwanza kwa kusudi la kuigeuza Mioyo ya Baba iwaelekee Watoto. hii inamaanisha kwamba Yohana alihubiri injili ya kuwarejeza waalimu wa sheria na marabi wa torati ili waiamini injili ya Kristo ambayo baadaye ilikuja kuhubiriwa na wana wa pentecoste yaani Mitume wa Yesu Kristo.Lakini hawakumpokea kuwa kama nabii wa Bwana bali walimkataa kama maandiko yanavyosema.

Lakini ile sehemu 'B' ya maandiko ambayo inasema Eliya atakuja kabla haijaja ile siku ya KUOGOFYA , yaani ile siku ya kutisha ya Mungu Mwenyezi. hapa Eliya atakuja tena ili kuigeuza mioyo ya Watoto iwaelekee Baba zao.kumbuka Yohana mbatizaji alikuja kuigeuza Mioyo ya Baba iwaelekee wana lakini sasa huyu atakuja kuigeuza mioyo ya Watoto iwaelekee Baba zao. katika siku za mwisho ambazo ndizo tunazoishi sasa. Na watoto wanaozungumziwa hapo ni sisi tunaoishi sasa katika nyakati hizi za mwisho, na mababa ni Mitume wa Kristo wa kanisa la kwanza ambao mafundisho yao ni biblia ambayo ndio msingi wa Ukristo wa kweli.

hivyo basi Eliya huyu wa mwisho alioahidiwa ni kwa kazi moja tu ya kuturudisha sisi katika Ukristo wa biblia ambao kwa muda mwingi kama tunavyosoma katika historia ya ukristo uliingiliwa na mafundisho ya uongo nayo ni mafundisho ya mpinga Kristo ambayo kwenye ufunuo 2:6 "Kristo ameyakemea kama mafundisho ya wanikolai" ambayo leo hii tunaweza tukayaona katika kanisa la Kristo.

hivyo basi Eliya wa kwanza alitangulia kuja kwa kwanza kwa Kristo, na katika siku hizi za mwisho Mungu alimtuma ndugu WILLIAM MARRION BRANHAM kama Eliya  kwa kuliandaa kanisa kwa ajili ya kuja kwa pili kwa Kristo,na ujumbe Mkuu Bwana aliompa ni kuwarudisha watu kwenye ukristo wa kimaandiko yaani biblia na kulingana na ufunuo 18:4.''.....tokeni kwake enyi watu wangu msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake."..huu ndio ujumbe wa bibi arusi safi wa  Kristo wa wakati huu wa mwisho.  .


(katika eneo hili la mto Ohoi karibu na barabara ya Spring jeffersonville Marekani ndugu Branham alipokuwa akibatiza mnamo juni 1933 picha hii ilipopigwa  hapo ndipo aliposikia sauti  ikisema "kama Yohana mbatizaji alivyotangulia kule kuja kwa kwanza kwa Kristo, wewe nawe utatangulia kuja kwake kwa pili"..na mwanga mkubwa ulitokea mahali pale ulioambatana na hiyo sauti na maelfu ya watu waliohudhuria waliuona huo mwanga, na magazeti mengi pia siku uliyofuata yalitangaza jambo hilo kuu la kustaabisha"


(Nguzo ya moto ilionekana juu ya kichwa cha ndugu William branham alipokuwa akihubiri huko houston texas, Marekani, januari 1950. nguzo hiyo ilionekana miongoni mwa mamia ya watu na kuchukuliwa katika picha kama inavyoonekana hapo juu, nguzo hii hii ndiyo iliyomtokea alipokuwa akibatiza kwenye ibada yake ya ubatizo katika mto ohio huko indiana na sauti ilisikika katika hiyo nguzo ya moto ikisema ''kama yohana mbatizaji alivyotangulia kule kuja kwa kwanza kwa Kristo wewe nawe utakutangulia kuja kwake kwa pili" sauti hii pia ilisikiwa na watu wengi walio hudhuria mahali pale.

SAFARI YA MSAFIRI- KISWAHILI

Filamu ambayo wengi wanaifahamu, yenye ujumbe mzuri unaomfaa Mkristo yeyote ambaye yuko katika safari yake ya kwenda mbinguni. kama biblia inavyosema (2 petro 2:11..wapenzi nawasihi kama WAPITAJI NA WASAFIRI ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho, muwe na mwenendo mzuri katika mataifa ili iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya,wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.)

Friday, September 16, 2016

HE CAME TO SET THE CAPTIVES FREE- BY REBECCA BROWN




Kitabu hichi kipo katika lugha ya kiingereza, tumeona tukiweke huku kwa yeyote atakayesoma kitamsaidia sana kujua hila za yule mwovu katika ulimwengu wa roho na shetani jinsi anavyowafunga watu, kwa kutumia vikundi vya kichawi (yaani occult groups) kama vile freemasons, brotherhood, sisters of light n.k. habari hii inamwelezea dada mmoja anayeitwa ELAINE Mmarekani jinsi Kristo alivyomkomboa kutoka katika kamba hizi za kuzimu akiwa kama malkia wa shetani mwenyewe, ameeleza mambo mengi mbalimbali jinsi shetani anavyowateka watu wengi kupitia miziki ya rocky, filamu za kutisha, sana sana kwa watoto wadogo, jinsi wachawi wanavyotumwa kuharibu mipango ya Mungu yao na mambo mengine mengi hivyo ni muhimu kukisoma utaona jinsi dada huyu mkristo REBEKA alivyotumiwa na YESU KRISTO kumtoa dada huyu katika kamba hizi za kuzimu kwa namna ya ajabu. kwa kujua zaidi soma kitabu hicho hapo chini.

Mungu akubariki!
download.>>>: He came to set the captives free

MAONO SABA YA WILLIAM BRANHAM

Mfululizo wa maono saba alioonyeshwa ndugu William Branham kabla ya kurudi kwa BWANA YESU KRISTO mara ya pili, mnamo juni 1933 alipokuwa akifanya ibada zake huko Meigs Marekani, Maono haya yalimjia kwa mfululizo wa mwambatano wa yote saba kwa pamoja.

ONO LA KWANZA:
Aliona kwamba utawala wa kimabavu wa ITALIA ukiongozwa na Benito Mussoulini, angevamia nchi ya Ethiopia na kulingana na ile sauti iliyokuwa inasema  naye katika ono kwamba Ethiopia ''ingeanguka kwenye miguu yake (yani mussoulini) hata hivyo ile sauti aliyoisikia ndugu Branham iliendelea kutabiri mwisho mbaya wa yule mtawala wa kimabavu (Musoulini) kwani yeye angekufa kifo cha aibu na watu wake mwenyewe wangemtemea mate..''Ono hilo lilikuja kutimia kama lilivyo''.

.
(Mussoulini wa pili kushoto, akiwa ameuawa july 25, 1943 kwa kifo cha aibu cha kutundikwa kama mnyama sawasawa na ono aliloonyeshwa  ndugu Branham).

ONO LA PILI:
Ono lililofuata alionyeshwa Amerika ingeburutwa katika vita ya dunia dhidi ya Ujerumani, ambavyo vingeongozwa na raia wa Austria ADOLF HITLER.(ono hilo lilimtajia mpaka jina la kiongozi huyo) ile sauti aliyoisikia pia iliendelea kusema kwamba hivi vita vya kutisha vingemwangusha Hitler nae angefikia mwisho usioeleweka.Katika hili ono Branham alionyeshwa mstari wa Siegfried ambayo idadi kubwa ya uhai wa waamerika ingelipia,huenda ikawa vyema kutamka hapa kuwa ono linalohusiana na hii vita lilibashiri kuwa Raisi Roosevelt angetangaza vita dhidi ya ujerumani na kwa kufanya hivyo angechaguliwa kwa ajili ya kipindi cha nne.


(kiongozi wa mabavu wa ujerumani baada ya kushindwa katika vita ya pili ya dunia mwaka 1945, alikufa katika kifo kisichoeleweka sawasawa na ono aliloliona ndugu Branham)

ONO LA TATU:
Sehemu ya tatu ya ono ilionyesha kuwa ingawa kulikuweko na ITIKADI tatu kipindi kile yaani ufashisti,unazi na ukomunisti ulimwenguni; kuwa zile mbili za kwanza yaani Ufasisti na Unazi zingekuwa si chochote ila ule Ukomunisti ungepata nguvu na kuzishinda hizo nyingine mbili. Ile sauti ilimshauri kuweka jicho lake juu ya Urusi kuhusika kwa baadae kwani Ufasisti na Unazi ungeishia kuwa Ukomunisti


(na ilikuja kutokea kama ilivyo katika historia na ile sauti aliyoisikia ikimwambia aiangalie Urusi kwa wakati ule ilikuwa bado ni USSR kwamba itakuja kuwa na madhara siku za baadaye)

ONO LA NNE:
Sehemu ya nne ya ono ilitabiri baada ya vita kutakuwa na maendeleo makubwa ya teknologia hili lilionyeshwa kwa mfano wa gari lenye umbo la YAI likiwa na paa la plastiki likitembea kwenye barabara kuu zilizo nzuri likiongozwa na kifaa maalum cha 'remoti' kilicho mbali na gari lenyewe (gari hilo halikuonyesha kuwa na usukani ndani yake,na watu walikuwako ndani ya hilo gari wakicheza mchezo kama wa drafti).


(teknologia hii inaonekana sasa katika kizazi chetu cha sasa ambacho kwa kipindi cha mwaka 1933 ilionekana kama ni kitu kisichowezekana)

ONO LA TANO:
Sehemu ya tano ya ono ilihusisha hali ya mwanamke wa ulimwengu, katika ono hili inaonyesha kutokea mmomonyoko mkubwa sana wa maadili kwa wanawake kwa kasi kubwa, kutokana na ndugu Branham alivyosema wanawake walivyoanza kutafuta haki zao za kujiingiza katika masuala ya kiulimwengu kwa njia ya kura, ndipo hapo walipoanza kuvaa mavazi ambayo yanaonyesha miili yao kuchagua kuvaa mavazi ya wanaume na kukata nywele zao na hatimaye lile ono lilimwonyesha yule mwanamke akiwa uchi kabisa na kujifunika na kipande kidogo tu takribani chenye ukubwa wa jani la mtini. na ile hadhi yake yule mwanamke ikawa na thamani ndogo mno, kuharibika kwa mwenendo wa wote wenye mwili kukaja juu ya dunia na kuambatana na upotofu uliopo  duniani

 (tofauti kati ya wanawake wa karne ya ishirini mwanzoni kurudi nyuma na wa karne ya ishirini na moja)

ONO LA SITA:
Sehemu  ya sita ya ono ndugu Branham alionyeshwa mwanamke mrembo sana akitokea katika taifa la Marekani akivalia mavazi ya kifahari na akapewa mamlaka makuu, alionekana ni mzuri kwa umbo lakini kulikuweko na ugumu kumhusu huyo mwanamke ambao hauelezeki, kwajinsi alivyoonekana alikua mkatili sana, mwovu na mwerevu. alitawala nchi kwa mamlaka yake naye alikuwa na mamlaka kamili juu ya watu,(katika ono hili ndugu Branham alibashiri kuwa mwanamke huyu angeweza kuwa mwanamke halisi au kwamba huyu mwanamke anawakilisha mfano wa shirika fulani la kidini linalohusishwa na maandiko kwa mfano Kanisa Katoliki,(kama katika ufunuo 17 inavyosema ) ingawa ile sauti haikunena kumwelezea zaidi huyo mwanamke alikuwa ni nani,yeye alijisikia tu moyoni mwake kusema kuwa huyu mwanamke anaweza kuwa anawakilisha kuinuka kwa kanisa katoliki la kirumi.


(kutokana na ono la ndugu Branham, inawezekana pia ikawa ni mwanamke halisi ananyanyuka katika Taifa la Marekani kama tunavyoona sasa au ikawa ni kanisa katoliki au mwanamke mwingine ambaye hajaja bado). Tunangoja tuone muda utaeleza yote.

ONO LA SABA:
Sehemu ya saba ya ono;ile sauti iliyokuwa inasema nae katika ono ikamwambia kwa mara nyingine atazame na alipogeuka akaona kukawa na mshindo mkubwa ukaipasua nchi yote na kuiacha nchi ya America ikifuka moshi, vurugu ya maangamizi kwa kadiri ambavyo jicho lingeona hapakuwepo na chochote isipokuwa mashimo, mabaki ya vifusi yakifuka moshi na hakuna mwanadamu aliyeonekana, baada ya hapo yale maono yakaondoka



(hivi ndivyoMarekani itakavyokuja kuwa siku za usoni).

  kutokana na maono haya makuu ambayo yamekuwa na madhara makubwa katika kizazi chetu hichi tunachoishi tunaona kuwa matano kati ya hayo 7 yamekwisha tokea kama yalivyo na mawili yaliyobaki yapo mbioni kutimia. hii inatukumbusha wakristo tujue ni wakati upi tunaishi tazama Bwana ameshakwisha kutuonya mbele, dalili zote katika maandiko zimekwisha timia KRISTO yupo mlangoni kurudi,

je! umemwamini KRISTO?.
Umebatizwa katika ubatizo wa kweli kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako? nao ni ubatizo wa kuzamishwa  kwenye maji na ni kwa JINA LAKE YESU KRISTO?.
Umepokea ROHO MTAKATIFU?


kumbuka kama maandiko yanavyosema katika warumi 8:9 wale wote wasio na Roho wa Kristo hao sio wake. je! wewe una Roho wa Kristo? ndugu mpendwa fikiria hilo. na ujue kabisa kuna hukumu inakuja huko mbele. na kila mtu atatoa hesabu ya mambo yake yote aliyoyafanya hapa duniani.
fikiria juu ya hayo na uchukue maamuzi sasa muda umeenda kushinda tunavyodhani.
Mungu akubariki.

MARAN ATHA!

Thursday, September 15, 2016

MIAKA 7 YA NEEMA


ujumbe aliopewa dada Nnenna wa Nigeria  na Bwana Yesu Kristo kwa kanisa duniani kote. katika ujumbe huu aliambiwa kanisa limepewa miaka saba ya neema(ya kumrudia Mungu). ambayo ilianza disemba 2014 na itaenda kuisha disemba 2021,katika kipindi hichi hapa katikati Bwana alimwambia atafanya kila namna kuwavuta watu wake kutoka katika madhehebu,dini,upagani n,k na kuwaleta katika nuru ya kweli ya ukristo, kanisa tukufu na katika ufunuo huo Bwana pia alimwambia baada ya hiyo miaka 7 kuisha jambo lolote linaweza kutokea, Na pia alimwambia katika wakati huu wa mwisho Bwana ana kitu cha kufanya na bara la Afrika, alimweleza pia matetemeko ya ardhi tuliyoyazoea kuyaona nchi za Asia sasa yanakuja Afrika ndani ya  kipindi cha mwaka 2016/2017. aliambiwa na mambo mengine mengi, tazama video na uyafahamu haya...

na unabii huu ni kweli kwani tumeshaanza kuona matetemeko makubwa ya ardhi kutokea hata katika nchi yetu ya tanzania na kuleta maafa makubwa na vifo vya watu.

je! swali tujiulize ni wakati gani huu tunaishi??? 
tuamke, muda umeenda kuliko tunavyodhani.

KRISTO YUPO MLANGONI KURUDI!!!!
"kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara KUITWA KWENU NA UTEULE WENU; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, mwokozi wetu YESU KRISTO..2pet 1:10"

WILLIAM MARRION BRANHAM

 

 Nguzo ya moto ilionekana juu ya kichwa cha ndugu William branham alipokuwa akihubiri huko houston texas, Marekani, januari 1950. nguzo hiyo ilionekana miongoni mwa mamia ya watu na kuchukuliwa katika picha kama inavyoonekana hapo juu, nguzo hii hii ndiyo iliyomtokea alipokuwa akibatiza kwenye ibada yake ya ubatizo katika mto ohio huko indiana na sauti ilisikika katika hiyo nguzo ya moto ikisema ''kama yohana mbatizaji alivyotangulia kule kuja kwa kwanza kwa Kristo wewe nawe utakutangulia kuja kwake kwa pili" sauti hii pia ilisikiwa na watu wengi walio hudhuria mahali pale.