"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Friday, September 16, 2016

MAONO SABA YA WILLIAM BRANHAM

Mfululizo wa maono saba alioonyeshwa ndugu William Branham kabla ya kurudi kwa BWANA YESU KRISTO mara ya pili, mnamo juni 1933 alipokuwa akifanya ibada zake huko Meigs Marekani, Maono haya yalimjia kwa mfululizo wa mwambatano wa yote saba kwa pamoja.

ONO LA KWANZA:
Aliona kwamba utawala wa kimabavu wa ITALIA ukiongozwa na Benito Mussoulini, angevamia nchi ya Ethiopia na kulingana na ile sauti iliyokuwa inasema  naye katika ono kwamba Ethiopia ''ingeanguka kwenye miguu yake (yani mussoulini) hata hivyo ile sauti aliyoisikia ndugu Branham iliendelea kutabiri mwisho mbaya wa yule mtawala wa kimabavu (Musoulini) kwani yeye angekufa kifo cha aibu na watu wake mwenyewe wangemtemea mate..''Ono hilo lilikuja kutimia kama lilivyo''.

.
(Mussoulini wa pili kushoto, akiwa ameuawa july 25, 1943 kwa kifo cha aibu cha kutundikwa kama mnyama sawasawa na ono aliloonyeshwa  ndugu Branham).

ONO LA PILI:
Ono lililofuata alionyeshwa Amerika ingeburutwa katika vita ya dunia dhidi ya Ujerumani, ambavyo vingeongozwa na raia wa Austria ADOLF HITLER.(ono hilo lilimtajia mpaka jina la kiongozi huyo) ile sauti aliyoisikia pia iliendelea kusema kwamba hivi vita vya kutisha vingemwangusha Hitler nae angefikia mwisho usioeleweka.Katika hili ono Branham alionyeshwa mstari wa Siegfried ambayo idadi kubwa ya uhai wa waamerika ingelipia,huenda ikawa vyema kutamka hapa kuwa ono linalohusiana na hii vita lilibashiri kuwa Raisi Roosevelt angetangaza vita dhidi ya ujerumani na kwa kufanya hivyo angechaguliwa kwa ajili ya kipindi cha nne.


(kiongozi wa mabavu wa ujerumani baada ya kushindwa katika vita ya pili ya dunia mwaka 1945, alikufa katika kifo kisichoeleweka sawasawa na ono aliloliona ndugu Branham)

ONO LA TATU:
Sehemu ya tatu ya ono ilionyesha kuwa ingawa kulikuweko na ITIKADI tatu kipindi kile yaani ufashisti,unazi na ukomunisti ulimwenguni; kuwa zile mbili za kwanza yaani Ufasisti na Unazi zingekuwa si chochote ila ule Ukomunisti ungepata nguvu na kuzishinda hizo nyingine mbili. Ile sauti ilimshauri kuweka jicho lake juu ya Urusi kuhusika kwa baadae kwani Ufasisti na Unazi ungeishia kuwa Ukomunisti


(na ilikuja kutokea kama ilivyo katika historia na ile sauti aliyoisikia ikimwambia aiangalie Urusi kwa wakati ule ilikuwa bado ni USSR kwamba itakuja kuwa na madhara siku za baadaye)

ONO LA NNE:
Sehemu ya nne ya ono ilitabiri baada ya vita kutakuwa na maendeleo makubwa ya teknologia hili lilionyeshwa kwa mfano wa gari lenye umbo la YAI likiwa na paa la plastiki likitembea kwenye barabara kuu zilizo nzuri likiongozwa na kifaa maalum cha 'remoti' kilicho mbali na gari lenyewe (gari hilo halikuonyesha kuwa na usukani ndani yake,na watu walikuwako ndani ya hilo gari wakicheza mchezo kama wa drafti).


(teknologia hii inaonekana sasa katika kizazi chetu cha sasa ambacho kwa kipindi cha mwaka 1933 ilionekana kama ni kitu kisichowezekana)

ONO LA TANO:
Sehemu ya tano ya ono ilihusisha hali ya mwanamke wa ulimwengu, katika ono hili inaonyesha kutokea mmomonyoko mkubwa sana wa maadili kwa wanawake kwa kasi kubwa, kutokana na ndugu Branham alivyosema wanawake walivyoanza kutafuta haki zao za kujiingiza katika masuala ya kiulimwengu kwa njia ya kura, ndipo hapo walipoanza kuvaa mavazi ambayo yanaonyesha miili yao kuchagua kuvaa mavazi ya wanaume na kukata nywele zao na hatimaye lile ono lilimwonyesha yule mwanamke akiwa uchi kabisa na kujifunika na kipande kidogo tu takribani chenye ukubwa wa jani la mtini. na ile hadhi yake yule mwanamke ikawa na thamani ndogo mno, kuharibika kwa mwenendo wa wote wenye mwili kukaja juu ya dunia na kuambatana na upotofu uliopo  duniani

 (tofauti kati ya wanawake wa karne ya ishirini mwanzoni kurudi nyuma na wa karne ya ishirini na moja)

ONO LA SITA:
Sehemu  ya sita ya ono ndugu Branham alionyeshwa mwanamke mrembo sana akitokea katika taifa la Marekani akivalia mavazi ya kifahari na akapewa mamlaka makuu, alionekana ni mzuri kwa umbo lakini kulikuweko na ugumu kumhusu huyo mwanamke ambao hauelezeki, kwajinsi alivyoonekana alikua mkatili sana, mwovu na mwerevu. alitawala nchi kwa mamlaka yake naye alikuwa na mamlaka kamili juu ya watu,(katika ono hili ndugu Branham alibashiri kuwa mwanamke huyu angeweza kuwa mwanamke halisi au kwamba huyu mwanamke anawakilisha mfano wa shirika fulani la kidini linalohusishwa na maandiko kwa mfano Kanisa Katoliki,(kama katika ufunuo 17 inavyosema ) ingawa ile sauti haikunena kumwelezea zaidi huyo mwanamke alikuwa ni nani,yeye alijisikia tu moyoni mwake kusema kuwa huyu mwanamke anaweza kuwa anawakilisha kuinuka kwa kanisa katoliki la kirumi.


(kutokana na ono la ndugu Branham, inawezekana pia ikawa ni mwanamke halisi ananyanyuka katika Taifa la Marekani kama tunavyoona sasa au ikawa ni kanisa katoliki au mwanamke mwingine ambaye hajaja bado). Tunangoja tuone muda utaeleza yote.

ONO LA SABA:
Sehemu ya saba ya ono;ile sauti iliyokuwa inasema nae katika ono ikamwambia kwa mara nyingine atazame na alipogeuka akaona kukawa na mshindo mkubwa ukaipasua nchi yote na kuiacha nchi ya America ikifuka moshi, vurugu ya maangamizi kwa kadiri ambavyo jicho lingeona hapakuwepo na chochote isipokuwa mashimo, mabaki ya vifusi yakifuka moshi na hakuna mwanadamu aliyeonekana, baada ya hapo yale maono yakaondoka



(hivi ndivyoMarekani itakavyokuja kuwa siku za usoni).

  kutokana na maono haya makuu ambayo yamekuwa na madhara makubwa katika kizazi chetu hichi tunachoishi tunaona kuwa matano kati ya hayo 7 yamekwisha tokea kama yalivyo na mawili yaliyobaki yapo mbioni kutimia. hii inatukumbusha wakristo tujue ni wakati upi tunaishi tazama Bwana ameshakwisha kutuonya mbele, dalili zote katika maandiko zimekwisha timia KRISTO yupo mlangoni kurudi,

je! umemwamini KRISTO?.
Umebatizwa katika ubatizo wa kweli kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako? nao ni ubatizo wa kuzamishwa  kwenye maji na ni kwa JINA LAKE YESU KRISTO?.
Umepokea ROHO MTAKATIFU?


kumbuka kama maandiko yanavyosema katika warumi 8:9 wale wote wasio na Roho wa Kristo hao sio wake. je! wewe una Roho wa Kristo? ndugu mpendwa fikiria hilo. na ujue kabisa kuna hukumu inakuja huko mbele. na kila mtu atatoa hesabu ya mambo yake yote aliyoyafanya hapa duniani.
fikiria juu ya hayo na uchukue maamuzi sasa muda umeenda kushinda tunavyodhani.
Mungu akubariki.

MARAN ATHA!

3 comments: