"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Wednesday, September 28, 2016

USHUHUDA WA RICK JONYER

Rick Jonyer katika kitabu chake maarufu ulimwenguni kinachojulikana kama THE FINAL QUEST, kikielezea jinsi alivyochukuliwa na Bwana Yesu Kristo katika maono mbinguni, katika hicho kitabu alielezwa mambo mengi ikiwemo vita kubwa ya kiroho inayoendelea katika ukristo leo, alionyeshwa silaha shetani anazozitumia kuwaangusha wakristo, vitu kama wivu, hasira, chuki kutokuwa na UPENDO, n.k miongoni mwa wakristo, vinawafanya wasisonge mbele,washindwe vita. alionyeshwa pia thawabu tofauti tofauti wanazopewa wakristo  kulingana na mambo wanayoyafanya wakiwa duniani,aliambiwa mambo mengine mengi ya kumtia Mkristo moyo kuwa na bidii na kushinda vita vilivyo mbele yake. Ni kitabu chenye mhamsho mkubwa kwa Mkristo yeyote.

katika ukurasa wa 42 wa kitabu hichi, kinaeleza jinsi alivyochukuliwa mbinguni na kupelekwa mbele ya viti vya enzi na kumwona mtu ambaye alishawahi kumsikia alipokuwa duniani.. na hapa nanukuu maneno yake...

"na niliposikia hayo maneno, nilijisikia kuangalia moja ya viti vya enzi vilivyokaribu nami. ghafla nikamwona mtu ninayemfahamu. Alikuwa ni muinjilisti maarufu nilipokuwa mtoto mdogo, na watu wengi walimwona kwamba ni mtu aliyetembea na nguvu za Mungu nyingi zaidi ya mtu yeyote tangu kuwepo kwa kanisa la kwanza. nilishawahi kusoma habari zake na nilishawahi kusikiliza mahubiri yake,  ilikuwa ni ngumu kutokuguswa na unyenyekevu wake, na upendo wake kwa Bwana na kwa watu.Hata hivyo nilidhani mafundisho yake yalikuwa na makosa. Nilishangaa lakini hata hivyo nilipata unafuu kumwona akiwa ameketi kwenye kiti cha enzi kikuu.nilivutiwa sana na unyenyekevu wake na upendo wake ambao bado unatoka kwake. na nikamuliza Bwana kama ninaweza kuongea na huyu mtu, kwa jinsi ninavyoona Bwana anavyompenda. lakini Bwana aliniashiria niendelee kutembea mbele, hakuniruhusu kuzungumza na yule muinjilisti.
Bwana alisema ; "nilikuwa ninataka umuone wewe akiwa hapa", Na kuiona nafasi aliyonayo hapa pamoja nami, Kuna mengi ya wewe kujua kuhusu yeye. ALIKUWA NI  MJUMBE KWA KANISA LANGU LA MWISHO, na kanisa halikumsikiliza kwa sababu ambayo utakuja kuijua muda utakapofika. Alianguka kwenye kuvunjwa moyo na upotevu kwa muda na ujumbe wake ukapindishwa. Lakini utarejeshwa tena, pamoja na jumbe nilizowapa wengine ambazo zimepindishwa......."

Rick Jonyer alieleza jinsi alivyokutana na WILLIAM BRANHAM. kwenye maono aliyoonyeshwa na Bwana Yesu Kristo mwenyewe, leo hii Bwana kamthibitisha mjumbe wake. Rick Jonyer aliambiwa akiandike kitabu hiki na kukipeleka duniani kote.
waebr.12:1" Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, Na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu"

je? umempokea Kristo katika maisha yako. Umejazwa Roho Mtakatifu
Umeuamini ujumbe wa wakati huu wa mwisho?
Kristo Bwana wetu yupo mlangoni..."fanya imara kuitwa kwako, na uteule wako"
soma kitabu hichi hapa >>>>download
No comments:

Post a Comment