"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Friday, October 13, 2017

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 19

SWALI 1: Naomba ufafanuzi wa huu mstari; 1Wakoritho 15:29 "Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, KWANINI KUBATIZWA KWA AJILI YAO? . Kulingana na mstari huu inaonekana ni sahihi wale wanaobatiza kwa ajili ya wafu au kuwaombea, hawakosei?.

JIBU: 
Ni vema Tukiisoma habari hiyo kuanzia juu mstari wa 12-14 ili tupate picha sahihi 

" 12 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?
13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka;
14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.
15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.
Tunaona habari hii katika kanisa lililokuwa Koritho kulikuwa na shida ya baadhi ya watu waliokuwa wanajiita waumini wasioamini kuwa kuna kiyama ya wafu, na bado wengine  walikuwa wanaendelea kushikilia imani  ya kubatiza kwa ajili ya wafu. Mambo hayo yalikuwa yanafanywa na hawa wakoritho kama ilivyoelezewa na mwandishi mmoja wa historia aitwaye st.John Chrysostom wa karne ya nne, Achbishop; kwamba kulikuwa na utaratibu wa mtu ambaye amekufa kabla ya kuamini na hajabatizwa ili kwamba mtu huyo aweze kwenda mbinguni ni lazima mtu mwingine aliye hai ajitokeze na kubatizwa kwa niaba yake, ilikuwa wanafanya kumchukua mtu mzima na kumficha chini ya kitanda cha yule marehemu, kisha kuhani anakuja na kumwongelesha yule maiti ikiwa kama yupo tayari kubatizwa au la na kama hatajibu yule mtu aliyelala chini yake atamjibu kuhani kwa niaba ya yule maiti kisha atakwenda kubatizwa, na kwa kufanya hivyo atakuwa amemkomboa yule mtu aliyekufa kutoka katika adhabu ya milele. 


Lakini kwanini mtume Paulo alinukuu hilo?
Ukiendelea mpaka mstari wa 29” utakutana na jambo hili.."Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, KWANINI KUBATIZWA KWA AJILI YAO? . “
 
Jambo hili mtume Paulo alilizungumzia kwa kutaka kuwakumbusha wale wasioamini kuwa kuna kiyama cha wafu kuwa kama hawaamini hivyo kwanini wanabatiza mtu kwa ajili ya mfu? ikiwa hakuna kiyama cha wafu. maana kama hawaamini ingewapasa wasifanye hivyo maana kwa kufanya kitendo hicho ni dhahiri kuwa wanaamini  kwamba kuna maisha baada ya kufa. je! hawaoni kama wanajichanganya wao wenyewe? ..Hiyo ndiyo sababu ya mtume Paulo kuandika hivyo. 
Lakini Mtume Paulo hakumaanisha yeye au wakristo walikuwa wanafanya hicho kitendo cha kubatiza kwa niaba ya wafu bali ni wengine ndio maana alitumia neno “WENYE”.
Na sio tu jambo hilo potofu la kubatiza kwa ajili ya wafu lilikuwepo kwenye makanisa bali pia imani nyingine potofu kama ya kusema " siku ya Bwana imeshakuja" N.K. zilikuwa zikihubiriwa katikati ya makanisa ya Mungu (soma 2timotheo 2:18, 2wathesalonike 2:2).
 
Leo hii imani kama hizi zimeasilishwa pia katika Kanisa Katoliki, likishikilia mistari hii kuthibitisha fundisho la (wakristo kupitia "toharani /purgatory ") ikiwa na maana kuwa mkristo aliyekufa katika dhambi na hajakamilishwa katika neema anakwenda mahali pa mateso ya muda kwa ajili ya utakaso wa dhambi zake kisha akishatakasika anaweza kwenda mbinguni, hivyo basi muda wa kuendelea kukaa katika hiyo sehemu ya mateso inaweza ikafupishwa kwa kutegemea maombi au sala za walio hai wakimwombea. Jambo ambalo sio sahihi Biblia inasema mwanadamu ameandikiwa kufa mara moja na baada ya kufa ni hukumu (waebrania 9:27), kumuombea mtu aliyekufa, au kubatizwa kwa ajili yake ni moja ya mafundisho potofu ya kuwafanya watu waendelee kustarehe katika dhambi wakiamini kwamba hata wakifa katika dhambi watakuwa na nafasi ya pili ya kusafishwa, usidanganyike hizo ni elimu za shetani wakiyapindua maandiko kuthibitisha uongo wao biblia pia inasema  1 timotheo 4:1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, WAKISIKILIZA ROHO ZIDANGANYAZO, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; “.

SWALI 2:
Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?.


JIBU: Neno Malkia wa mbinguni limeonekana mara mbili katika biblia  
1).Yeremia 7:18-20 ”Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi. “ na  baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.” Je! Watu hawa wanikasirisha mimi? Asema Bwana; hawajikasirishi nafsi zao, na kuzitia haya nyuso zao wenyewe?Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.  
2). Yeremia 44:17-23” Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.
18 Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa.
19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko, waume zetu wasipokuwapo?
20 Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake, yaani, watu wote waliompa jibu lile, akisema,
21 Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! Bwana hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake?
22 Hata Bwana asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.
23 Kwa sababu mmefukiza uvumba, na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya Bwana, wala hamkuitii sauti ya Bwana, wala hamkwenda katika torati yake, wala katika amri zake, wala katika shuhuda yake; ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo. “
 
Tunaona habari hizo zote mbili zinaelezea juu ya miungu ya kipagani iliyowasababishia Israeli kuingia matatizoni kwa kwenda kuifukuzia uvumba na kumbuka haina uhusiano wowote na ukristo, kwahiyo mbinguni Mungu anapoishi hakuna malkia, biblia inamtaja MFALME TU!, Naye ni mmoja na si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA yeye peke yake. Hivyo Mariamu sio malkia wa mbinguni, alikuwa ni mwanamke kama wanawake wengine waliokuwa wanamcha Mungu na kupewa neema ya kumzaa Bwana Yesu, lakini hilo halina uhusiano wowote na yeye kuwa malkia, desturi za kuabudu miungu wake ni za kipagani na zilikuwepo tangu zamani AShtorethi mungu mke alikuwa anaabudiwa zamani zile na ndiye aliyekuwa anajulikana kama malkia wa mbinguni. 

Kanisa katoliki ndilo lililobeba tamaduni hizi za kipagani kumwabudu Mariamu na kuwa kama kipatanishi kati yetu na Mungu ambayo ni machukizo makubwa mbele za Mungu.


Bwana akubariki!

No comments:

Post a Comment