"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Tuesday, October 17, 2017

TOKENI KWAKE ENYI WATU WANGU: Part 2

 Kanisa Katoliki na Majina ya makufuru.:

Mnamo disemba 27,2015 Huko Vatican Basilica, Jumapili katika sherehe ya familia takatifu ya Yosefu, Maria na Yesu Papa  alipokuwa akihubiri juu ya malezi na familia kwa kulinganisha na Familia nyingine katika biblia. Katikati ya mazungumzo yake kwa kutumia mfano wa familia ya Bwana Yesu alisema maneno yafuatayo,  fuatilie kwa makini.

"...........Mwishoni mwa safari ya (Yerusalemu wakati Kristo alipokuwa na miaka kumi na mbili). Yesu Alirudi Nazareti na alikuwa mtiifu kwa wazazi wake(luka 2:51). Hii inaweza ikawa picha nzuri kwa mafundisho ya familia zetu. Safari haiishii tu pale tunapofikia malengo yetu, bali pale tunaporejea manyumbani na kuendelea na maisha yetu ya kila siku, tukiyatendea kazi matunda ya kiroho ya tulichokipata. Tunajua jambo alilolifanya Yesu wakati ule, BADALA YA KURUDI NYUMBANI NA FAMILIA YAKE, YEYE ALIBAKI YERUSALEMU HEKALUNI, IKASABABISHA MATATIZO MAKUBWA KWA MARIAMU NA YUSUFU AMBAO HAWAKUWEZA KUMPATA. KWA "GHASIA HII NDOGO" YESU PENGINE ANGEPASWA AOMBE MSAMAHA KWA WAZAZI WAKE. Injili haizungumzii hilo lakini ninaamini tunaweza tukalidhania hivyo............"

Kwa mwanzo na mwisho wa mahubiri yake fuatilia link hii. Pia unaweza ukaitazama video chini.

https://w2.vatican.va/content/francesco/en/homilies/2015/documents/papa-francesco_20151227_omelia-santa-famiglia.html
Tukifuatilia kwa umakini tunaona Papa Francis anajaribu kuonyesha kuwa Bwana YESU alikuwa na makosa na kitendo alichokionyesha cha kuwaacha wazazi wake hakikuwa sawa na hivyo angepaswa atubu.

Lakini biblia inatufundisha kuwa BWANA alikuwa ni mkamilifu na hakuwa na hatia wala dhambi yoyote (Waebrania 4:15) isitoshe yeye ni MUNGU,na tangu lini Mungu akamkosea mwanadamu?. lakini Jambo ambalo Papa alikuwa anataka  kulionyesha ni  kuwa Mariam alikuwa mkamilifu kuliko BWANA YESU Na ndio maana Mariamu kwao anasimama kama mpatanishi kati ya sisi na Mungu kama YESU.

Kiongozi wa namna hii angali akijua analolifanya anawafundisha na wengine hivyo. Swali ni je! ikiwa kiongozi anafundisha hivi hali ya kiroho ya kondoo anaowachunga itakuwaje? Ndugu kimbia ibada za sanamu mgeukie Mungu na sio dhehebu.

Ufunuo 18:4" Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. "

Amen!.

No comments:

Post a Comment