Luka 19: 37 “Hata alipokuwa amekaribia matelemko ya mlima wa Mizeituni, kundi zima la wanafunzi wake walianza kufurahi na kumsifu Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya matendo yote ya uwezo waliyoyaona,38 wakasema, Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana; amani mbinguni, na utukufu huko juu. 39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, uwakanye wanafunzi wako. 40 Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, MAWE YATAPIGA KELELE”.
Zamani nilijua kuwa Mimi nisipofanya kazi ya Mungu, basi
kazi ya Mungu itasimama katika eneo nililopo..Ndivyo nilivyokuwa nafikiri hivyo
kwa muda mrefu sana..Nilijua tunapoihubiri Injili ni kama tunamsaidia Mungu,
kwamba pasipo sisi kujitoa basi watu wengi hawataokolewa..Na ndivyo
nilivyofundishwa hata mimi.
Lakini namshukuru Mungu, nilikuja kuelewa zaidi ya
hapo…kwamba Mungu hasaidiwi kazi, wala hajalemewa na kazi, wala haitaji msaada
wowote kutoka kwa Mwanadamu…Mungu alipoiumba dunia na watu ndani yake,
hakuiweka pasipo mipango kama sisi wanadamu tunavyofanya kwamba tunafikia
mahali tunabanwa na majukumu yanayotuumiza kichwa mpaka wakati mwingine
tunakata tama ya kuendelea..
Mungu hayupo hivyo, alipoumba kila kiumbe chini ya jua
alikwisha kiwekea sehemu yake katika dunia kwamba kitazaliwa wapi, kitahitaji
kiasi gani cha chakula mpaka kife, kitahitaji hewa ya ujazo kiasi gani n.k …Hayo
yote Mungu alishayaweka kabla hata ya hicho kiumbe kuzaliwa au kuwepo..
Kadhalilka na kila mwanadamu anayezaliwa chini ya Mbingu,
Bwana alishampangia azaliwe wapi, aishi miaka mingapi, ale chakula kiasi gani,
aokolewe wakati gani, afe wakati gani n.k Kwahiyo mwanadamu anapozaliwa ni kama
anakuja tu kutimiza maandiko kwa yale aliyoandikiwa.
Kwahivyo basi hakuna mwanadamau yoyote anayeweza kumsaidia
Mungu majukumu yake…Yeye mwenyewe anatenda kazi zake kama alivyopanga…Kama alipanga nchi ya Tanzania ifikie idadi ya
watu milioni 60 mpaka mwishoni mwa mwaka 2019..penda tusipende hiyo idadi
itafika tu!!..Hata kama mtu fulani akatae kuzaa watoto…hiyo haizuii idadi ile
kufika..Bwana atatumia wengine kufidia nafasi yake.
Kadhalika tunapokuja katika suala la watu kuokolewa..Bwana
Yesu alisema “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba
aliyenipeleka”..Sentensi hii inaonyesha kwanza wokovu ni wa kuchaguliwa..Sio
kila mtu tu anaweza kuupokea..Ni lazima uchaguliwe na kisha uitwe/uvutwe kwa
Bwana ndipo umfuate..ikiwa na maana kuwa kama mtu hajasikia mvuto wowote au
msukumo wowote ndani yake wa kwenda kumfuata au kumpokea Bwana Yesu huyo hawezi
kamwe kumwamini ni sawa na kumlazimisha
mtoto mdogo aliyezaliwa leo azungumze haitawezekana.
Kwahiyo kama Bwana amekusudia idadi fulani ya watu wamfuate yeye mwaka huu
katika mji fulani labda wa Dar es salaam, hakuna yoyote atakayeweza kupunguza
au kuongeza idadi hiyo..wala hakuna mtu yoyote atakayeweza kuisimamisha kazi
yake.
Atanyanyua watu wake (watumishi wake) wanawake kwa wanaume, vijana kwa wazee
labda tuchukue mfano watumishi 5,000 kwa mji wa Dar es salaam..atawatuma
wakaihubiri injili katika huo mji na endapo hao aliowatuma walipaswa wavune
idadi ya wale watu milioni 20 wale waliokusudiwa uzima wa milele, na ile idadi
ikatimia basi kazi yao itakuwa imeisha watapelekwa mji mwingine..Lakini mfano
endapo kati ya wale 5,000 waliotumwa 2,000 wakawa wavivu wasilete mazao..basi
Bwana atawanyang’anya ile kazi na kuwapa watu wengine lakini mwisho wa siku
ile idadi ya watu milioni 20
waliokusudiwa kuokolewa itatimia tu!..kwa vyovyote vile itatimia tu!
Wataondolewa wale wavivu watapewa wale wachapa kazi.
Kwahiyo ndugu huu sio wakati wa kufikiri kazi ya Mungu
itasimama endapo sisi (mimi na wewe) leo hii tukikataa kuitenda kazi..Hiyo
haitakuwa hasara kwa Mungu bali itakuwa ni hasara kwetu.. kwasababu Nafasi zetu
watapewa wengine walio na bidii kuliko sisi endapo tukizembea..Na sisi tutakosa
thawabu mbele za Mungu siku ile.
Ukikataa leo kuwashuhudia wengine habari njema za wokovu
usidhani umeathiri kazi ya Mungu kwa vyovyote vile..Kazi ya Mungu itafanyika tu
na watu wale waliokusudiwa kuokolewa wataokolewa..Bwana alipotuambia tuenende
ulimwenguni kote tukahubiri injili kwa kila kiumbe sio kwa faida yake yeye..Ni
kwa faida yetu sisi, Hatutumi ili tukamsaidie kazi yake hapana! Yeye
hasaidiwi..katutuma ili tukapate faida sisi sio yeye..
Wewe usipoihubiri injili mtaani kwako, mjini kwako au nchini
kwako. Kazi ya Bwana haitasimama, Mungu atanyanyua mwingine na kumleta hapo
mjini kwako, au nchini kwako kuitangaza habari yake na wale waliokusudiwa
kuokolewa wataokolewa tu!..lakini utakuwa umejizuiliwa thawabu yako mwenyewe..
Wewe ukikataa kuichangia kazi ya Mungu mahali ulipo,
usifikiri itasimama kwa vyovyote vile.. Hapana Mungu hasaidiwi kazi wala
hategemei mfuko wa mtu hata kidogo..atanyanyua wengine kutoka mahali pengine
watakaoipalilia ile kazi…Anapotushauri
tumtolee yeye sio kwa faida yake
yeye bali ni kwa faida yetu sisi..Yeye tayari ana kila kitu..sasa ana haja na
nini tena? Dunia yote ni yake sasa ni nini tutamwongezea yeye??
Anapokuambia umtafute yeye, au umtegemee yeye..sio kwamba
yeye ana uhaba wa watu au wa sifa, au anahitaji sana utukufu..hapana ndugu anao
mabilioni ya malaika watakatifu huko mbinguni wanaomsifu usiku na
mchana…anakuambia umsifu wewe kwa faida yako?? Sio kwa faida yake..
Ni sawa na mtu mwenye kampuni kubwa tajiri lililoendelea
sana na lenye wafanyakazi wengi wanaojitosheleza, na akamwona mtu maskini na
kwa huruma zake akaona ampatie nafasi ya kazi kwenye lile kampuni, sasa sio
kwamba kampa ajira kwa sababu anaupungufu wa faida kwenye kampuni lake hapana
bali kampa ajira kwasababu amemuhurumia yule maskini na anataka na yeye apate
kitu..lakini endapo yule maskini akikataa ile nafasi basi hasara haitakuwa kwa
yule mwajiri bali kwake yeye kwasababu yeye tayari anao wafanyakazi wengi
wanaojitosheleza....Na kwetu sisi katika kumtumikia Baba yetu wa mbinguni ndio
ivyo hivyo.
Ndio maana mahali fulani Bwana Yesu alipokuwa anaingia
Yerusalemu aliwaambia mafarisayo maneno yale..
“ 39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, uwakanye wanafunzi wako. Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, MAWE YATAPIGA KELELE”.
Umeona! Hapo…Bwana alikuwa anataka kuwaonyesha kuwa sio
kwamba Mungu ni maskini wa sifa..kwamba pasipo wao kumsifu yeye basi ndio hana sifa mahali pengine..hapana hata
mawe yatapiga kelele endapo wao wakinyamaza.
Kama Mtume Paulo alivyosema pia kwa uwezo wa Roho…2 Timotheo
2: 13 “Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa.
Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe”.
Kwahiyo tukiyafahamu hayo ni wakati wa kumtumikia Mungu kwa
Nguvu zote..kwa talanta tulizopewa..tukijua kuwa ni kwa faida yetu, kwasababu
siku ile inakuja katika Mbingu mpya na nchi mpya..ambapo Bwana hatakuwa na
upendeleo kule..Kila mtu atakuwa na nafasi yake kule, kulingana na talanta
alizozifanyia kazi hapa duniani.. Katika mbingu mpya na nchi mpya watakuwepo
wafalme, na watu wakawaida, nafasi mtu atakayokuwa nayo kule ndio itakuwa yake
hiyo milele..Kwahiyo tujitahidi tupige mbio tukiyatazamia mambo yale yanayokuja
kama vile Mtume Paulo alivyokuwa anayatazamia..
Ufunuo 22: 10 “Akaniambia, Usiyatie
muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.
11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye
uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu
na azidi kutakaswa.
12 TAZAMA, NAJA UPESI, NA UJIRA WANGU U PAMOJA NAMI,
KUMLIPA KILA MTU KAMA KAZI YAKE ILIVYO.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza
na wa mwisho.
14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo
mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”.
Tukaze mwendo, tumtumikie Bwana katika nafasi alizotuweka,
naye atatuhifadhi kwa reema zake.
Bwana akubariki.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.
No comments:
Post a Comment