"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Monday, October 3, 2016

UNAWEZA UKAULIZA SWALI LOLOTE HAPA

5 comments:

 1. Bro :
  Shalom naomba kujua wale wakristo watakapitia dhiki kuu na kuuawa ktk dhiki ile watafufuliwa lini? je watakuwepo pia ktk utawala wa miaka 1000?

  ReplyDelete
  Replies
  1. shalom!..wale wakristo watakao uliwa na mpinga kristo katika dhiki kuu (wale wasioipokea chapa ya manyama) watafufuliwa na kuhukumiwa kisha wataingia katika ule utawala wa miaka 1000 pamoja na kristo ukisoma ufunuo 20:4 " Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu"....na sio tu wakristo watakaofufuliwa bali pia na wayahudi watakaouawa katika kipindi cha dhiki kuu.

   Delete
 2. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
  Replies
  1. ok. nashukuru kwa jibu lkn hata hivyo bado nina swali jingine. je; hukumu sasa zitakuwepo za aina mbili au? Maana unasema watafufuliwa kisha wahumumiwe na watawale na Kristo miaka 1000 lakini kwa mujibu wa biblia utawala wa miaka 1000 ni kabla ya hukumu ya kile kiti cha enzi sasa inakuwaje hawa wahukumiwe kabla ya utawaka wa miaka 1000?

   Delete
  2. Kuna Hukumu kuu tatu za Mungu mwenyezi..HUKUMU YA KWANZA:..Ni hukumu ya watakatifu watakaoenda mbinguni, hukumu hii siyo ya kulaumiwa wala ya adhabu, bali ni ya thawabu, kila mtakatifu atalipwa kulingana na kazi aliyoifanya ya injili akiwa hapa duniani, 2wakorintho 5:10 "Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya." pia warumi 14:12 "Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu." tunaona hapa paulo alikuwa hazungumzi na watu wasioamini bali na wakristo....HUKUMU YA PILI: Hii itakuwa baada ya mwisho wa ile siku kuu ya Bwana baada ya ile dhiki kuu, itawahusisha wale wakristo walioachwa katika unyakuo, wasioipokea ile chapa ya mnyama, na kuuawa na mpinga kristo. kulingana na ufunuo 20:4..na mathayo 25:31-46, Kristo atakapowatenganisha kondoo na mbuzi....HUKUMU YA TATU:..itakuwa baada ya mwisho wa ule utawala wa miaka 1000 pale Kristo atakapokaa katika kiti cha enzi cheupe kuwahukumu mataifa ukisoma ufunuo 20:11-15 "Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao." Hii itakuwa ni hukumu ya mataifa kwa wale wingine wote waliobaki watahukumiwa kulingana na matendo yao. Na wale wote walioipokea chapa ya mnyama watahukumiwa kuona sababu ya kuenda katika ziwa la moto.

   Delete