"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Saturday, December 17, 2016

*******ZABURI 107 *******

Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele.
Walitangatanga jangwani katika njia ya nyika, hawakuona mji wa kukaa,waliona njaa,waliona na kiu, nafsi zao zilikuwa zikizimia ndani yao.
         “ wakamlilia BWANA katika dhiki zao, akawaponya na shida zao                                                           akawaongoza mpaka mji wa Kukaa.”     … Zab 107:2-9


Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti,wamefungwa katika taabu na chuma, kwasababu waliyaasi maneno ya MUNGU, wakalidharua shauri lake aliye juu, hata akawadhili moyo kwa taabu, wakajikwaa wala hawakuona msaidizi.
        “ Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, akawaponya na shida zao. Akayavunja Mafungo Yao.”  …zab 107:10-16

Wapumbavu kwasababu ya ukosaji wao, na kwasababu ya maovu yao, hujitesa nafsi zao zachukia kila namba ya chakula, wakayakaribia malango ya mauti.
           “ Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, akawaponya na shida zao. Hulituma neno lake, huwaponya. Huwatoa katika maangamizi   yao”…zab 107:17-22



Washukao baharini katika merikebu, wafanyao kazi zao katika maji mengi, hao huziona kazi za BWANA na maajabu yake vilindini. Wayumbayumba, wapepesuka kama mlevi, dhoruba na upepo mkali uwashikapo.
              “ Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, akawaponya na shida zao.  Naye akawaleta mpaka bandari waliyoitamani”…..zab 107:23-31


Akamweka mhitaji  juu mbali na mateso yake…’zab 107:41’
Aliye na hekima ayaangalie hayo; Na wazitafakari fadhili za BWANA, na maajabu yake kwa wanadamu…’zab 107:43’
Maana huishibisha nafsi yenye shauku, na nafsi yenye njaa huijaza mema..’zab 107:9’


“Ndugu mpendwa maneno yaliyosemwa hapo juu ni ya BWANA YESU KRISTO, akitupa tumaini kwa wote walio katika taabu za dhambi, shida na vifungo pamoja na magonjwa, waliokata tamaa kwa mateso ya shetani. Yeye BWANA peke yake ndiye awezaye kukuokoa haijalishi ni dhambi au shida ya namna gani uliyonayo mlilie yeye na hakika atakuokoa na utauona utukufu wake kwako.”
 
        “ Na ashukuriwe  BWANA YESU KRISTO kwa neema zake kwetu sisi wanadamu”
                                                                 *** AMEN***

No comments:

Post a Comment