"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Friday, December 1, 2017

JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?


Waefeso 1 : 4 " Kama vile alivyotuchagua katika yeye KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na urathi wa mapenzi yake."

Mambo yote tunayoyaona sasa katika ulimwengu yalikuwa yameshakusudiwa yawepo kabla hata ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, hakuna lolote linalotokea kwa bahati mbaya ambalo Mungu hakulijua, Kuna swali watu wengi wanauliza je! Mungu anafahamu mtu kabla hajazaliwa kwamba atakuja kwenda mbinguni au kuzimu?? Jibu ni ndiyo anafahamu!..Ni lazima ajue hayo yote ili awe Mungu..na kuna wengine wanauliza kama ni hivyo basi kwanini aumbe wengine angali anajua mwisho wao utakuwa ni kuzimu?? Jibu ni kwamba ewe mwanadamu wewe ni nani umuulize Muumba wako, kwanini chombo hichi unakifanya hivi na kile unakifanya vile? Hatuwezi kushindana na kusudi la Mungu Akili za Mungu hazichunguziki wala njia zake hazitafutikani.

Mtume Paulo alisema katika warumi 9:20 kwamba vipo vyombo Mungu aliviumba vya ghadhabu kwa ajili ya uharibifu tunaona kama vile Farao,Yezebeli,Balaamu,n.k. na vipo vingine aliviumba kwa ajili ya heshima mfano Musa, Ayubu,Ibrahimu n.k.

Hivyo basi tukivitazama hivi vyombo vya heshima Mungu alivyovichagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu na kuvitengenezea njia ya kupitia mpaka vitakapofikia ule utukufu wa Mungu alioukusudia juu yao. Na ndio maana alisema katika..

Warumi 8:28-30" Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, WALE WALIOITWA KWA KUSUDI LAKE.
29. MAANA WALE ALIOWAJUA TANGU ASILI, ALIWACHAGUA TANGU ASILI WAFANANISHWE NA MFANO WA MWANA WAKE, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.
30. Na wale aliowachagua tangu asili hao AKAWAITA, na wale aliowaita, hao AKAWAHESABIA HAKI; na wale aliowahesabia haki, hao AKAWATUKUZA.

Unaona hapo kuna hatua za kufuata kwa kile chombo cha heshima kilichoteuliwa na Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili kifikie utukufu wake uliokusudiwa. Sasa Baada ya kuchaguliwa tangu asili zipo hatua TATU za kufuata 1) KUITWA, 2) KUHESABIWA HAKI, 3) KUTUKUZWA. Embu tuzitazame kwa ufupi hizi hatua.

1) KUITWA:

Waliochaguliwa na Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ni lazima waisikie sauti ya Mungu inapolia masikioni mwao.Kumbuka na sio watu wote wataisikia hiyo sauti, bali ni wale tu Mungu aliowachagua tangu asili,. Bwana Yesu aliwaambia makutano hivi wale waliomtilia shaka kwamba yeye hajatumwa na Mungu kuwaokoa wanadamu alisema hivi..Yohana 6:43" ...Msinung'unike ninyi kwa ninyi. HAKUNA MTU AWEZAYE KUJA KWANGU, ASIPOVUTWA NA BABA ALIYENIPELEKA; nami nitamfufua siku ya mwisho" kwahiyo unaona ni lazima uvutwe kwanza.

Mahali pengine Yesu aliwaambia hao hao mafarisayo alisema..Yohana 10:26" Lakini ninyi hamsadiki, kwasababu HAMMO miongoni mwa kondoo wangu. KONDOO WANGU WAISIKIA SAUTI YANGU; NAMI NAWAJUA NAO WANIFUATA. NAMI NAWAPA UZIMA WA MILELE; WALA HAWATAPOTEA KAMWE.

Umeona hapo tena walio wa Kristo wataisikia sauti yake tu!, haihitaji kuwa bembeleza sana, kwani ile mbegu ya nuru Mungu alishaiweka ndani yao tangu asili, wakisikia tu, saa hiyo hiyo wanabadilika na kumfuata Kristo katika hali zote. Jiulize ni kwasababu gani mafarisayo na masadukayo pamoja na dini zao zote walishindwa kumwamini YESU KRISTO jibu ni rahisi kwasababu hawakuwa miongoni mwa kondoo wake aliowachagua tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, lakini tunaona wale watu wasiokuwa na elimu, wavuvi, wakina Petro walimkubali YESU pasipo maswali mengi au shuku shuku nyingi ni kwasababu gani? ni kwasababu walikuwa ni miongoni mwa wale aliowachaguliwa tangu asili.
 

2) KUHESABIWA HAKI.

Mtu anahesabiwa haki kwa kumwamini YESU KRISTO katika uweza wa Damu yake inayoondoa dhambi, kumbuka wale wote walio wake baada ya kuitikia wito wao wenyewe watataka kuuliza tufanyeje?? Hapo ndipo Bwana atakapowaongoza katika hatua inayofuata ya kuufanya imara WITO wao na UTEULE wao (2Petro 1:10). Hapo ndipo mtu anapoutafuta ubatizo wa MAJI na wa ROHO MTAKATIFU..

Tunaona ile siku ya Pentekoste Petro baada ya kuwashuhudia wale makutano walio kusanyika waliamini ..tusome Matendo 2:37-38" Waliposikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia, TUBUNI, MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote WATAKAOITWA, na Bwana Mungu wetu WAMJIE."

Kwahiyo unaona hapo? ili uhesabiwe haki lazima ukabatizwe katika ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. kumbuka hakuna ubatizo wa watoto wadogo, wala hakuna ubatizo wa kunyunyuziwa maji, unapaswa UKAZAMISHWE, na ubatizwe kwa JINA LA YESU KRISTO kulingana na maandiko, hata mimi nilinyunyuziwa nilipokuwa mchanga lakini baada ya kufahamu ubatizo sahihi kulingana na maandiko ilinipasa nikarudie tena. Kisha baada ya hilo una AHADI YA ROHO MTAKATIFU, na ni vizuri kujua kuwa ahadi hii si kwa ajili ya kila mtu(hata kafiri) bali ni kwa wale watakaoitwa na Bwana wamjie. Naamini nawewe ni mmoja wapo wa walioitwa.

3) KUTUKUZWA.

Baada ya kupokea Roho Mtakatifu ambao ndio muhuri wa Mungu (Efeso 4:30). Kitu kilichotiwa muhuri maana yake ni kimehakikiwa na kuonekana kimekamilika. Hivyo mtu anapopokea Roho Mtakatifu anakuwa ametiwa muhuri na Mungu mpaka ile siku ya ukombozi. Kumbuka Kupokea Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni zaidi ya kunena kwa lugha, kunena kwa lugha ni karama sio watu wote wanaweza wakanena, ni kama vile sio watu wote wanaweza wakawa manabii, au wainjilisti, vivyo hivyo mtu anaweza akapokea Roho Mtakatifu na asinene kwa lugha, bali karama nyingine ikajidhihirisha, na pia wapo ambao wananena kwa lugha na hawajapokea Roho Mtakatifu. Kwahiyo kipimo cha kwamba umepokea Roho Mtakatifu sio karama uliyonayo bali ni maisha matakatifu unayoishi baada ya kumpokea Roho.

Hivyo baada ya kukamilishwa kwa kubatizwa na Roho Mtakatifu tunasubiria siku ya ukombozi wetu( yaani siku ya kutukuzwa) kwenda mbinguni, siku tutakapovaa miili ya utukufu na kuwa kama BWANA YESU KRISTO alivyo sasa.

Kwahiyo ndugu tathimini maisha yako, je! unavyoishi leo hii ni miongoni mwa wale kondoo wake aliowachagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu? au vile vyombo vya ghadhabu vilivyowekwa kwa ajili ya uharibifu??..Kumbuka kuna makundi mawili tu, ni aidha kondoo au mbuzi, umeitikia wito au hujaitikia wito, umechaguliwa au haujachaguliwa, ni wa mbinguni au ni wa kuzimu? jibu lipo moyoni mwako. Je! upo katika hizo hatua? kwamaana biblia inasema wale wote wasio na Roho wa Kristo hao sio wake (warumi 8:9).

2 Timotheo 2:19 " Lakini msingi wa Mungu ulioimara umesimama, wenye MUHURI HII, BWANA ANAWAJUA WALIO WAKE. NA TENA, KILA ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AACHE UOVU.
20. Basi katika nyumba nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.
21. Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima kilichosafishwa, kimfaacho BWANA, KIMETENGENEZWA KWA KILA KAZI ILIYO NJEMA.

AMEN!

Maombi yangu ndugu ni uchague kufanyika chombo cha heshima. Muda umeenda kuliko unavyodhani Bwana yupo mlangoni kurudi.

Mungu akubariki.

No comments:

Post a Comment