"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Tuesday, January 2, 2018

MAELEZO JUU YA UFUNUO 15

Karibu tujifunze mwendelezo wa kitabu cha ufunuo, leo tukiendelea na sura ya 15;

Ufunuo 15:1-4 
1 Kisha nikaona ishara nyingine katika mbingu, iliyo kubwa, na ya ajabu; malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana Katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia.
2 Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.
3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.
4 Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.

Katika sura hii ya 15 tunaona Yohana akionyeshwa ishara nyingine kuu mbinguni kama vile alivyoonyeshwa kwenye ile sura ya 12 juu ya yule mwanamke aliyekuwa na utungu wa kuzaa ambaye tuliona anawakilisha taifa la Israeli, na ishara nyingine kuu aliyoonyeshwa mbinguni ni juu ya lile joka kubwa jekundu lililokuwa limejiandaa kummeza yule mtoto pindi atakapozaliwa, na huyu si mwingine zaidi ya shetani akipingana na YESU KRISTO na uzao wa Mungu.

Lakini katika sura hii ya 15 tunaona Yohana akionyeshwa ishara nyingine tena mbinguni iliyo kubwa na ya ajabu "malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia."

Hawa Malaika 7 wanaoonyeshwa hapa ndio wale watakaohusika katika kumimina vile vitasa 7 vya ghadhabu ya Mungu, kumbuka katika kipindi cha ile miaka mitatu na nusu ya mwisho kati ya ile saba, Mungu atamuhukumu yule KAHABA MKUU, (utawala wa mpinga-kristo chini ya Kanisa Katoliki ) kwa kupitia zile pembe 10 ambazo zitakuja kumchukia yule mwanamke na kumtowesha kabisa kama inavyoelezewa katika (ufunuo 16:10, pamoja na Ufunuo 17 & 18),

Sasa itakayofuata ni HUKUMU YA MATAIFA yote yaliyozini na huyu mwanamke kahaba Babeli mkuu, biblia inasema... Ufunuo 14:9-11" Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,
10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.

Hivyo hii HUKUMU YA MATAIFA itatekelezwa na Hawa malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho ambayo katika hayo ghadhabu ya Mungu itatimia, na mapigo haya tunayaona yakitekelezwa katika sura inayofuata ya 16.

Tukiendelea mstari wa 2-4 tunaona Yohana akiona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.

Hii bahari ya kioo iliyochanganyikana na moto inaonyesha watakatifu waliosafishwa kwa moto (yaani waliopitia dhiki kuu), ndio maana ile bahari imeonekana kama imechanganyikana na moto, kama vile tunavyoona kwenye ufunuo 4:6 bahari nyingine ya kioo mfano wa bilauri na sio ya moto. Kwahiyo hawa ni watakatifu waliotoka kwa yule mpinga-kristo.

Na pia ukiendelea kusoma utaona wameshinda kutoka kwa yule mnyama na sanamu yake na hesabu ya jina lake, hawa ndio waliokataa kushirikiana na yule mnyama hivyo iliwapasa kutoa maisha yao, kwa ushuhuda wa Yesu Kristo. Kumbuka wakati huo unyakuo utakuwa umeshapita yule mwanamwali mwerevu atakuwa ameshaondoka(kwenye unyakuo), amebaki yule mpumbavu (ukisoma Mathayo 25 utaona jambo hilo), hivyo kwasababu ya upumbavu wake wa kutokuwa na mafuta ya ziada kwa kujiweka tayari kumlaki Bwana wake wakati ajapo, aliachwa!, kumbuka tayari alikuwa ni mwanamwali wa Bwana isipokuwa alikuwa ni mpumbavu, hivyo itambidi akumbane na ghadhabu ya mpinga-kristo ambayo asingepaswa apitie.

Wakati unyakuo unapita sio watu wote watafahamu, utakuwa ni wa siri, na ni wachache tu watakaonyakuliwa wala hakutakuwa na ajali, wala mshtuko wowote duniani maana watakuwa ni wachache sana, Bwana Yesu alisema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na kama ilivyokuwa katika siku za luthu, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu, sasa jiulize? katika siku za Nuhu walipona watu wangapi? ni watu 8 kati ya mamilioni, siku za Luthu walipona wangapi? ni 3 kati ya mamilioni na Bwana Yesu anasema ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake. Je! na wewe utakuwa miongoni mwa hao wachache watakaokwenda na Bwana katika Karamu yake?..

Mstari unaofuata unasema .."3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa."

Hapo tunaona kuna aina mbili za nyimbo zikiimbwa 1) wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu ikiashiria watu wam Israeli watakaouawa kipindi hicho na mpinga-kristo kwa kukataa kumsujudia, 2) Wimbo wa mwana-kondoo ikifunua wakristo watakaouawa wakati wa dhiki kuu watakaokataa kuipokea ile chapa na kumsujudia. Kwahiyo hayo ni makundi mawili yatakayopitia dhiki kuu.

Tukiendelea mlango wa 15 kuanzia ule mstari wa 5 hadi wa 8 ambao ndio wa mwisho tunasoma habari ifuatayo.

Ufunuo 15:5-8
5 Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa;
6 na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung'aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.
7 Na mmoja wa wale wenye uhai wanne akawapa wale malaika saba vitasa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu, aliye hai hata milele na milele.
8 Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba ya wale a malaika saba.

Hapa tunaona hekalu la hema la ushuhuda mbinguni likifunguliwa na kujazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu ikiwa na maana kuwa ni hukumu ya Mungu, kumbuka popote palipo na hekalu la Mungu au hema ya ushuhuda utukufu wa Mungu huwa unashuka kama "wingu" kuashiria neema na rehema za Mungu mahali hapo aliposhukia lakini hapa tunaona hekalu limejaa "moshi" ikiashiria ghadhabu na hukumu ya Mungu, na kama vile inavyosema wala hakuna mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu mpaka yatimizwe yale mapigo ikionyesha kuwa mlango wa rehoema na neema mbaada ya haupo utakuwa umeshafungwa,

Na tunaona wale malaika saba walipewa vile vitasa 7 ili kumimina ghadhabu ya Mungu juu ya nchi ili kuleta mapigo yale yote Mungu aliyoyakusudia kwa wale wote waliomsujudia yule mnyama na kupokea chapa yake au hesabu ya jina lake. Katika kipindi hicho huruma Mungu haitakuwepo na watu wengi sana wataangamia. Kwa mwendelezo wa sura inayofuata ya 16 inayohusu juu ya ghadhabu ya Bwana ambayo ndio vile vitasa saba fuata link hii >>>
Ndugu tunaishi katika muda wa nyongeza, na KARAMU YA MWANAKONDOO imekaribia, na watakaoshiriki ni wale watakaokwenda katika UNYAKUO TU!. Wakati wateule wa Mungu wanapokea thawabu zao na kuwa wafalme na makuhani wa Mungu milele, wewe nafasi yako saa hiyo itakuwa wapi?,
wakati watakatifu wanafutwa machozi yao na Bwana YESU wewe utakuwepo wapi?. Huu ni wakati wa kutengeza taa zetu na kujiweka tayari kwenda kumlaki Bwana, huu sio wakati wa kuambiwa uumpe Bwana maisha yako bali ni wakati wa KUFANYA IMARA UTEULE WAKO NA WITO WAKO(2petro 1:10), vinginevyo utakuwa mwanamwali mpumbavu ambaye alibeba TAA pasipo mafuta ya ziada,

Kumbuka chapa ya mnyama imeshaanza kufanya kazi, na inaanzia ndani kisha ije nje Kumalizia! na hii inatenda kazi katika madhehebu yote yaliyofanya uzinzi na kanisa kahaba KATOLIKI, ni mara ngapi unaambiwa biblia inasema hivi, wewe unasema dhehebu letu haliamini hivyo?, ni mara ngapi unaulizwa wewe ni mkristo unajibu mimi ni wa-dhehebu fulani? Je unadhani ni ROHO MTAKATIFU ndiye aliyeleta hiyo migawanyiko? jibu ni hapana shetani ndiye aliyeleta hiyo migawanyiko, na bila kujua hilo dhehebu lako lina ushirika kamili na lile kanisa mama kahaba na ndio tunaona lile jina MAMA WA MAKAHABA limezaliwa huko. Sasa kwa dizaini hii utaachaje kushawishika kuipokea ile chapa?..umeshaipokea tayari moyoni mwako kilichobaki ni udhihirisho wa nje tu! ambao hauna tofauti na ule wa ndani. Biblia inasema tokeni kwake enyi watu wangu wala msishiriki dhambi zake, kutoka sio kwa miguu tu, bali kutoka moyoni kwanza kwa kubadilisha namna ya kumwabudu Mungu, Mungu ni ROHO nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli, na sio kwa kupitia sanamu, wala dhehebu wala papa wala bikira Mariamu, wala kwa mapokeo wala kwa mtu mwingine yoyote, bali katika roho na kweli (ndani ya YESU KRISTO).

Na pia Kumbuka kanisa tunaloishi sasa ni kanisa la mwisho linaloitwa LAODIKIA, na mjumbe wake ameshapita na ujumbe wetu tuliopewa na BWANA YESU KRISTO ni huu..

Ufunuo 3:15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. "

Umeona hapo?, hili ni kanisa vuguvugu, anasema ni heri uwe moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu, hivyo chagua moja,
Ufunuo 22:10" Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.

11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.
17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure. "

Amen!

No comments:

Post a Comment