"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Sunday, March 25, 2018

HOSANA JUU MBINGUNI


.Hosana ni neno la kiebrania likiwa na maana OKOA SASA”...Siku kama ya leo miaka karibia 2000 iliyopita maneno haya yalitamkwa kwa MWOKOZI wetu YESU KRISTO alipokuwa anaingia Yerusalemu, pale watu wote wakubwa kwa wadogo kwa furaha walipotandika mavazi yao na matawi ya miti ili mfalme apite, wakiimbakwa kwa nguvu HOSANA! HOSANA! JUU MBINGUNI…ikiwa na maana okoa sasa! Okoa sasa mwana wa Daudi.

Mathayo 21:1-11
1 Hata walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia,
2 Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye; wafungueni mniletee.
3 Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka.
4 Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,
5 Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, MPOLE, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda.
6 Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru,
7 wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake.
8 Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani.
9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, HOSANA, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; HOSANA JUU MBINGUNI.
10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?
11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, YESU, wa Nazareti ya Galilaya.”

 

Nawe pia leo usimwache apite imba kwa imani moyoni mwako kwa furaha HOSANA!...naye atakutoa katika vifungo hivyo vya dhambi kama hujampokea, naye atakuponya na magonjwa yote yanayokusumbua. Naye atapindua kazi zote za Yule mwovu zilizopandwa maishani mwako, kama alivyopindua zile meza za wale wafanyabiashara katika nyumba ya Mungu alipoingia Yerusalemu, hiyo ilikuwa baada ya kushangaliwa na kuimbiwa sana.…Na wewe pia ni nyumba ya Mungu. Mwimbie Bwana kwa shangwe..naye atakurehemu…

Haleluya..Hosana. YESU ndiye MFALME wetu.

No comments:

Post a Comment