Mwanafunzi
mmoja mwerevu akajibu Ndio ninaweza kwani ni wazi kuwa mmojawapo alikuwa na
mwamvuli na mwingine hakuwa nao.
Mwingine
akasimama kwa furaha na kusema hapana mmoja alipita pembezoni mwa majengo na
mwingine barabarani, hivyo Yule wa barabarani ni lazima alilowesha na mvua.
Mwingine
akasema, inawezekana mmoja alivaa koti la mvua, na mwingine hakuwa nalo hivyo
Yule mwenzake ni wazi kuwa alilowanishwa na mvua.
Kila mwanafunzi
alisema la kwake, na ndipo mwalimu akasema ninyi wote mmepeleka mawazo
yenu, “ kwa wale watu wawili tu kana kwa ndio hao peke yao walikuokuwa kwenye hiyo sentensi”..Lakini
sentensi inasema “mtu mmoja hakunyeshewa”..Hivyo inawezekana wote wawili
walinyeshewa na mvua lakini kulikuwa na mwingine aliyekuwa anapita katika njia
hiyo, au yupo kwenye gari lake hakunyeshewa.
Wanafunzi wote
wakaingiwa na aibu kwa kulijibu juu juu tu bila ya kufikiria kwa undani.
Ndio maana Bwana Yesu alisisitiza
akituambia “Luka 8: 18 “JIANGALIENI BASI JINSI MSIKIAVYO; kwa kuwa mwenye kitu
atapewa, na yule asiye na kitu atanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa
nacho.”
Kwani kama tukiwaangalia hao wanafunzi
inawezekana kabisa ni kweli majibu yao yalikuwa ni sahihi, lakini kwa mwalimu
wao hayakuwa sahihi.
Unaona kauli
hiyo ya Bwana anayosema, ‘hata kile ambacho mtu anadhaniwa kuwa anacho,
atanyanganywa’, pale mtu anapojihisi anajua kila andiko, hivyo hakuna haja ya
kuhubiriwa na huku anaona kabisa maisha yake hayaakisi kwa namna yoyote maisha
ya Kristo. Mtu kama huyo atanyang’anywa hata kile anachodhani anakijua.
Tunaona Maneno
hayo Bwana Yesu aliyatamka baada ya kutoa ule mfano wa mpanzi, akisema kuwa
wale wote ambao mbegu zao ziliangukia katika miiba,na wengine barabarani, na wengine,na
kwenye miamba na wengine kwenye udongo
mzuri, wote hao WALISIKIA NENO LA MUNGU kwa wakati mmoja, Ni neno lile lile
walilisikia la habari ya Yesu mwokozi, wala hakuna aliyehubiriwa zaidi ya
mwingine, lakini viwango vya kusikia vilitofautiana kati ya mmoja na mwingine
na ndio maana utaona wengine waliishia njiani, wengine, kwenye miamba, na
wengine kwenye udongo mzuri..
Lakini tujiulize
Yule aliyeishia kwenye udongo mzuri yeye alisikiaje sikiaje tofauti na wengine
mpaka kufikia kuzaa hata 60 mpaka 100, sikio lake lilikuwa ni la namna gani?
Embu tusoma
kidogo huo kisha tutapata majibu.
Luka 8:10 “Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, iliwakiona wasione, na wakisikia wasielewe.11 Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu.12 Wale wa karibu na njia NDIO WASIKIAO, kisha hujaIbilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao,wasije wakaamini na kuokoka.13 Na wale penye mwamba ndio wale ambao WASIKIAPO hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.14 Na zilizoanguka penye miiba ni WALE WALIOSIKIA, na katika kuenenda kwao husongwa nashughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lolote.15 Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao KWA UNYOFU NA WEMA WA MIOYO YAO HULISIKIA neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.16 Hakuna mtu ambaye akiisha washa taa huifunika kwa chombo, au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuona nuru yake.17 Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kutokea wazi.18 JIANGALIENI BASI JINSI MSIKIAVYO; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kituatanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.”
Unaona hapo, wale waliofanikiwa
kufika kwenye udongo mzuri, Bwana Yesu anasema KWA UNYOFU, na KWA WEMA hulililisikia
na KULISHIKA, kwa KUVUMILIA.
Ni kwanini kama tukitazama leo hii
mtu anahubiriwa injili kila siku, lakini inaonekana haina manufaa, miaka
inapita haonyeshi badiliko lolote, si kwamba Neno alilohubiriwa linatofauti na
la Yule aliyempokea Kristo na kusimama katika Imani, hakuna tofauti yoyote,
isipokuwa huyu wa pili Aliangalia jinsi asikiavyo, alizingatia kwa unyofu wa
moyo, na kwa wema wote kutokulidondosha hilo aliloambiwa, alilishika na kwenda
kulitafakari, na hivyo kwa kufanya vile Mungu akamfunulia akili zake za rohoni
kujua maana zaidi ya kile alichokisikia..na
ndicho hicho kilichompa nguvu ya kuchukua uamuzi wa kumwishia Bwana mpaka sasa.
Na kwa kuwa hakutaka kulichukulia
suala hilo juu juu tu, bali kwa hofu akijua kuwa siku moja atasimama hukumuni
na kutoa hesabu ya yote aliyoyasikia, alijishusha na kutii, hivyo Mungu akampa
neema zaidi ya kumwelewa yeye kama alivyotaka amwelewe, na kwa jinsi alivyozidi
kuendelea kulipalilia lile Neno ndani yake, ndivyo kidogo kidogo Mungu akamjalia
kuzaa matunda mengi baadaye. Anaongezewa na vya ziada kwasababu alizingatia kuangalia
jinsi anavyosikia.
Inawezekana Injili ya Kristo haijawa
na manufaa yoyote kwako kwa miaka mingi, ni kwasababu hauyachukulii maneno ya
Mungu katika unyofu wote, unayaona kama ni siasa, na maneno ya kawaida tu, umekuwa
ukiyachukulia juu juu tu, na hivyo Mungu amekuacha uendelee kuyasikia lakini usiyaelewa, uyaone tu lakini
usiyatambue. Lakini leo hii Mungu amekupa neema ya kuliambua hilo ufanye tena
upya maisha yako.
Itakufaidia nini uupate ulimwengu
mzima kisha upate hasara ya nafsi yako?, Embu chagua jambo la msingi kwanza
kumtii Mungu uokolewe na hayo mengi yaje huko mbeleni kama yatakuwa na muhimu,
okoa roho yako kwanza, Sikia Neno la Mungu leo na ulipokee kwa weupe wa moyo
kwa mara nyingine tena, ili Bwana akapate kukufunua akili yako uanze kuona uzuri
wa wokovu, ili baadaye ukamzalie matunda.
Ikiwa utakuwa tayari kutubu, basi
fanya hivyo kwa kudhamiria kabisa kutoka moyoni mwako, kwamba kuanzia leo
utazingatia kutii kile Mungu anachosema na wewe, kuacha maisha ya dhambi na
baada ya kutubu kwako unapaswa ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa
katika maji mengi na uwe kwa jina la YESU KRISTO ili upate ondoleo la dhambi
zako(Matendo 2:38),, kumbuka ubatizo wa vichanga sio wa kimaandiko, kadhalika
ubatizo wa kwa jina la Baba na Mwana, na Roho Mtakatifu sio sahihi kwani
umetafsiriwa isivyopaswa kwasababu walioubatizia huo hawakuzingatia JINSI
WASIKIAVYO…Ubatizo wa kwa jina la YESU KRISTO ndio wa kimaandiko, na ndio
uliotumiwa na mitume wote katika kubatizia kwenye biblia. Soma (Matendo 2:38,
8:16, 10:48, 19:5) utayathibitisha hayo mwenyewe.
Hivyo ukiyakamilisha hayo, basi
Bwana mwenyewe kuanzia huo wakati atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu
atakayekuongoza katika kweli yote. Na hapo utakuwa umeshazaliwa mara ya pili. Ni
Wengi wanaosema wameokolewa lakini hawazingatii vigezo vya wokovu vilivyotolewa
na Bwana Yesu. Ubatizo sahihi ni muhimu kwa mtu yoyote anayedai amemwamini
Kristo. Hivyo fanya hima ukabatizwe tena, kama ulibatizwa ukiwa mtoto au kama
hukuwahi kubatizwa kabisa.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa
wengine. Na Mungu atakubariki.
No comments:
Post a Comment