"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Friday, February 1, 2019

NI JAMBO LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?

Luka 18:1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.
4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?.
8 Nawaambia, atawapatia haki upesi;
Shalom! Mwana/binti wa Mungu, karibu tuyachunguze maandiko, natumai leo utajifunza jambo jipya litakalotusaidia katika maisha yako ya maombi..Embu jaribu kufikiria mfano huu watoto wawili mapacha wamemfuata baba yao tajiri kwa faragha na kumwomba awapatie kitu..mmoja kamwambia baba nimeona suruali nzuri dukani naomba uninunulie, na mwingine akasema baba nimeona ndege kubwa inapita angani, naomba uninunulie na mimi niwe na ya kwangu niendeshe..We unadhani maombi ya nani yatakuwa ya kwanza kujibiwa kwa haraka zaidi ya mwingine?..Ni wazi kuwa aliyeomba nguo inawezaka isipite hata siku awe ameshatimiziwa haja yake..Lakini huyo mwingine japo aliomba na mwenzake katika muda mmoja, japo walisikiwa wote katika muda mmoja, japo baba yao aliwahidi wote kuwapa walivyoviomba, lakini majibu ya huyu wa pili, yanaweza yasije kwa wakati alioutarajia, inaweza kumgharimu mambo mengi sana, ikiwemo muda, na maisha.

Na hiyo ni kwasababu gani?. Ni kwasababu jambo aliloliomba lina uzito mkubwa zaidi kuliko la Yule mwingine. Sasa japo baba yake alikuwa anao uwezo wa kumnunulia ndege hata wiki ile ile, lakini alijua kuwa kwa utoto wake hawezi bado kuendesha ndege, hana maarifa ya kutosha kwa alichokiomba, ni sharti kwanza aende shule, akasome masomo magumu ya sayansi,na Jeografia, kisha akajaribiwe katika vituo vingi vya ndege ndogo, na ndio baadaye sana pengine hata baada ya miaka 20 baada ya kufudhu madarasa hayo ndipo baba yake amnunulie ndege yake mwenyewe, aliyomwomba. Hivyo jambo atakalohakikisha baba kwa wakati huo ni kumwezesha kwa kumpeleka katika shule zenye mafunzo hayo, na kumkazania awe chini ya waalimu wazuri, na kusoma vitabu vingi, n.k. ili aweze kufikia malengo yake.
  
Vivyo hivyo na sisi, Bwana YESU alituambia imetupasa tumwombe Mungu sikuzote wala tusikate tamaa..Ukiona hujapata majibu ya maombi yako leo, haimaanishi kuwa Mungu hajayasikia, au Mungu anapenda kukuona una msumbua sumbua, kila siku kumpigia magoti hapana, jua kuwa majibu ya maombi yanatofautiana kulingana na hitaji lililopelekwa kwa Mungu.

Mungu huwa anamakusudi yake kufanya hivyo, na ndio wakati mwingine utaona unamwomba Mungu akufanyie kitu Fulani, utashangaa hata hujamaliza kuomba jambo hilo lilishatendeka zamani, na wakati huo huo pengine umekuwa ukimwomba Mungu hitaji fulani kwa muda mrefu lakini bado hujaona matokeo yoyote..Fahamu kuwa hilo uliloliomba lina uzito mkubwa mbele za Mungu kuliko lile la kwanza, na hivyo kabla hujalipokea linahitaji maandalizi kwanza.

Pengine wewe ni mgonjwa, na umeshamwomba Bwana kwa muda sasa pengine miaka akuponye ugonjwa wako lakini huoni dalili yoyote ya huo ugonjwa kuondoka, na wakati huo huo ukitazama unaona wengine wanakuja na matatizo makubwa hata zaidi ya ulionanayo na wanapokea miujiza yao saa ile ile, na wewe unajiuliza mimi nina ninamakosa gani?..

Ndugu jambo hilo lisikufanye kujiona kuwa Mungu hakuoni, au anapenda uendelee kuteseka.Fahamu kuwa wote wawili alishawasikia wakati mmoja mlipo mwomba, na wote wawili alishaanza kuwajibu maombi yetu tangu wakati ule ule mlipomwomba…Isipokuwa Mungu anajua njia nzuri zaidi ya sisi kutupatia hitaji la ombi letu kuliko sisi tunavyofikiri,Hivyo ukiona hakuna matokeo yoyote leo wala kesho zidi kufurahi kwasababu ombi lako wewe limeonekana kuwa na faida kubwa zaidi mbeleni kuliko lile la mwingin, kwanza kwako mwenyewe, na pia katika ufalme wa Mungu.

Tunasoma kwenye biblia, wakati Fulani Lazaro, aliugua sana, pengine alikuwa na ugonjwa uliokuwa unamsumbua kwa muda mrefu, labda tuseme kwasasa kisukari na wakati huo huo biblia inatuambia alikuwa ni rafiki wa karibu sana na YESU, alitembea na Yesu sehemu nyingi, pamoja naye hata katika mikutano ya uponyaji alikuwa pamoja na Bwana, aliweza kushuhudia jinsi watu wengi walivyokuwa wanaponywa kimiujiza. Lakini yeye alikuwa bado na ugonjwa wake, mpaka ilipofikia wakati hali imekuwa mbaya sana sasa hawezi hata kutoka kitandani mwake,

Hivyo akapeleka watu kwa Bwana aje upesi kumwombea walau atoke kitandani..Lakini Bwana alipopata taarifa zile, hakwenda popote, jiulize ni kwanini Bwana hakuondoka haraka haraka na kwenda Huko kumwangalia rafiki yake kipenzi, badala yake akabaki pale pale siku nyingine mbili..

Tengeneza picha wale watu waliompelekea Yesu taarifa, wakati wanarudi njiani walikuwa wanawaza nini vichwani mwao?, pengine walisema, huyu alikuwa anampenda Lazaro kweli?, au alikuwa anaonyesha unafki tu!, haiwezekani rafiki yake yupo ICU mahutihuti, na yeye yupo buzy na watu wengine hata asiowajua, rafiki yake anaumwa tangu siku nyingi kwanini asimponye yeye kwanza.? Lakini Yesu alisubiri mpaka mauti ilipomkuta..Ndipo sasa akaondoka aende kumtembelea rafiki yake..Tunasoma.

Yohana 11.17 “Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne.
18 Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi;
19 na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao.
20 Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani.
21 Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.
22 Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa.
23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka.
24 Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.
25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
27 Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.
28 Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita.
29 Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea.
30 Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo pale pale alipomlaki Martha.
31 Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko.
32 Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.
33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,
34 akasema, Mmemweka wapi?Wakamwambia, Bwana, njoo utazame.
35 Yesu akalia machozi.
36 Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda.
37 Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?
38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.
39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.
40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?
41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake".

Unaona hapo? Hata baadhi ya makutano waanza kudhihaki wakisema aliweza kuwaponya wengine kwanini alishindwa kumzuia huyu asife?..Lakini habari yote tunaijua, ule muujiza uliotokea pale, baada ya Lazaro kufufuliwa, Israeli yote Ilimtazama Kristo kwa jicho lingine, mpaka watoto wadogo wakawa wanamwimbia mabarabarani wakisema Hosana! na Mafarisayo na Masadukayo kuona vile sasa Israeli yote inakwenda kumgeukia ndipo walipopanga shauri la kumwua sio tu Yesu peke yake bali pia Lazaro kwasababu kwa ushuhuda wake aliwafanya watu wengi wamgeukie Mungu..Embu fikiria Lazaro alikufa na ugonjwa wake usiotibika, lakini sasa anafufuka bila ugonjwa wowote..alikufa pasipo umaarufu, lakini sasa anafufuka na umaarufu mkubwa.

Sasa angalia njia za Mungu zilivyo za ajabu, hata leo hii sikiliza shuhuda ambazo zinawajenga watu kuwafanya hata wakate shauri kumgeukia Mungu, utagundua kuwa shuhuda zao sio zile zilizokuja kwa majibu ya haraka, haraka mwingine atakwambia madaktari walithibitisha kuwa mapigo ya moyo yamesimama kabisa, lakini baadaye akaja kuamka, na kuwa mzima, n.k.
Hivyo ndugu Bwana anaposema imetupasa kumwomba Mungu bila kukata tamaa, haimaanishi kuwa Mungu anatupuuzia kama Yule kadhi dhalimu alivyokuwa anafanya hapana, Bali ni kwamba ametusikia na hivyo anatuandalia ushuhuda ulio bora zaidi kwetu sisi na kwa ajili ya ufalme wake. Unachopaswa kufanya ni kuzidi kumshukuru yeye kila wakati na kukaa katika uwepo wake bila kukata tamaa, haijalishi hali yako itakuwa enaendelea kuwa mbaya kiasi gani, jua tu hakuna dhara lolote litakalokutokea..Endelea tu kukaa uweponi mwake maombi yako yalishasikiwa tangu siku ya kwanza ulipoomba, Hivyo hiyo hali unayopitia sasa ni matokeo ya yale maombi.

Tukiyafahamu hayo, embu turudi sasa kwenye kiini cha somo letu kinachosema.. NI JAMBO GANI BWANA ANATAMANI SANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?..
Kama tulivyoona kila hitaji tunalomwomba Mungu hatupaswi kulikatia tamaa, iwe ni afya,iwe ni mafanikio, au chochote kile chema..Lakini lipo jambo ambalo Mungu analitamani kila mmoja wetu aliombe hilo usiku na mchana, awe na haja ya hilo siku zote za maisha yake..Ni jambo ambalo Mungu analiona ni KUU kuliko hitaji lolote tunaloweza kumwomba Mungu, ni jambo ambalo mtu akilipata basi ni sawa na Yule mtoto aliyemwomba baba yake ndege zaidi ya aliyemwomba nguo.
Jambo hilo Yesu alilifunua katika maombi maneno yanayofanana na yale yale tuliyosoma hapo juu..tusome:
Luka 10: 5 Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu,
6 kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake;
7 na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe?
8 Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.
9 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
10 Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
11 Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?
12 Au akimwomba yai, atampa nge?
13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni HATAZIDI SANA KUWAPA ROHO MTAKATIFU HAO WAMWOMBAO?.
Unaona hapo? HATAZIDI SANA KUWAPA ROHO MTAKATIFU HAO WAMWOMBAO?.Kwanini hakusema MALI,au AFYA, bali Roho Mtakatifu?..Ndugu kumbuka hii dunia isingekuwa hivi ilivyo kama Roho wa Mungu asingetua juu yake na kufanya uumbaji upya..Hata mtu yeyote anayesema amemwamini Yesu, hakumwamini hivi hivi kama hakuvutwa na Roho wa Mungu kwake (Yohana 6:44).. Hata leo hii anayesema amesimama, au anamtumikia Mungu, hafanyi hayo yote kama sio Roho wa Mungu amekufanya uwe hivyo. Roho wa Mungu ndio kila kitu kwenye maisha yetu..Ndio muhuri wa Mungu (waefeso 4:30), na ndio maana biblia inasema wale wote wasio na Roho wa Mungu hao sio wake (Warumi 8:9)..haijalishi utakuwa mwema kiasi gani…

Roho Mtakatifu ni karama ya bure kabisa, mtu anampokea pale tu anapoitii sauti yake na kumkaribisha ndani yake..Hii inakuja pale mtu anapokusudia kabisa kwa weupe wa moyo wake kutoka moyoni KUTUBU dhambi zake na kuacha maisha yake ya kale, kisha akaenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake kulingana na (Matendo 2:38). Basi kuanzia hapo mtu wa namna hiyo anakuwa ametiwa muhuri na Mungu kwa Roho wake mtakatifu..Lakini hiyo peke yake haitoshi,.Kumwamini tu, bila ya kumtamani ROHO MTAKATIFU katika maisha yako, hutafika mahali popote…Wengi wameishia hapo na ndio mwisho wa siku Roho Mtakatifu amezimika ndani yao.

Pindi tu unapompokea BWANA kuanzia huo wakati na kuendelea ni jukumu lako kumtamani Roho Mtakatifu awe pamoja nawe. Na ndio hapo linakuja hilo ombi kuu la Bwana, Akupe Roho mtakatifu, au kwa lugha rahisi tunaweza kusema AKUJAZE Roho Mtakatifu…Ulikuwa katika kipimo cha chini lakini sasa unataka AKUJAZE mpaka kwenye kipimo cha juu kabisa. Kumbuka Roho Mtakatifu sio kunena kwa lugha, ni jambo lingine, Na kwa jinsi utakavyozidi kuendelea kuomba bila kukata tamaa, basi ujue ndivyo unavyojijengea daraja zuri la Mungu kuyatawala maisha yako yote, na kuruhusu madarasa Fulani upitie kwa kukuandaa kwa kazi yake teule ya utumishi mwema..Kama tunavyoona ilivyokuwa kwa Yohana mbatizaji, ilivyokuwa kwa Bwana Yesu na ilivyokuwa kwa mitume wake..Wote walipokea Ujazo wa Roho Mtakatifu,lakini hiyo ilikuja kwa jinsi walivyotamani kipawa hicho tunaona baadaye walikuja kuvipokea, Roho mtakatifu aliposhuka juu yao na kuwatia mafuta ya utumishi, ndipo hapo Mungu alitembea nao kwa namna ya kipekee sana.

Hivyo ni maombi yangu, mimi na wewe kila siku na sisi tusikate tamaa kuomba Roho Mtakatifu..Leo unaweza usione matokeo yoyote, lakini jua tu ombi lako limesikiwa, na kama hujakata tamaa juu ya hilo unaendelea kulishikilia basi jua maisha unayopitia sasa ni maandalizi ya kazi ya huyo Roho atakayekuja juu yako baadaye.

Waefeso 5:17 “Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.18Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; BALI MJAZWE ROHO;”

Ubarikiwe sana.

“Share” ujumbe huu kwa wengine.

No comments:

Post a Comment