Tukisoma injili ya Mathayo 21:2-7, tunaona Bwana akiwaambia wanafunzi wake maneno haya:“2 Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona PUNDA AMEFUNGWA, NA MWANA-PUNDA PAMOJA NAYE; wafungueni mniletee.3 Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka.4 Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,5 Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda.6 Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru,7 wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake.”
*** Lakini tukirudi kusoma kwenye
Injili ile ya Marko na Luka utaona waandishi wale wanamtaja mnyama mmoja tu
kana kwamba hakukuwa na mwingine pamoja naye kwamfano tukisoma ile injili ya
Luka 19:30 inatuambia ..
“30 akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa.31 Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji.32 Na wale waliotumwa wakaenda wakaona kama alivyowaambia.33 Na walipokuwa wakimfungua mwana-punda, wenyewe waliwaambia, Mbona mnamfungua mwana-punda?34 Wakasema, Bwana ana haja naye.35 Wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana-punda, wakampandisha Yesu.36 Na alipokuwa akienda walitandaza nguo zao njiani”.
Unaona? Ni rahisi kusema maandiko
yanajichanganya, lakini si kweli maandiko yapo sawa siku zote, embu jaribu
kuwazia mfano huu, watu wawili walioshuhudia ajali iliyotokea mpanda wiki 2
zilizopita waliitwa kituo cha polisi ili kutoa taarifa ya tukio lilivyotokea..Mmojawapo
akasema: niliona fuso iliyobeba mizigo ikienda moja kwa moja kuivaa gari ndogo
ya abiria, na ghafla nilichokiona ni watu wakitoa nje ya vioo, wakirushwa huko
na huko na wengine wakipondwa vibaya na ile fuso iliyokuja kulala juu ya lile
gari la abiria hivyo ikapelekea kusitokee abiria yoyote aliyepona.,. Lakini
shahidi wa pili naye alipoitwa atoe taarifa zake alisema, niliona gari kubwa
likiwa katika mwendo wa kasi sana likitokea upande wa juu, lakini ghafla
pikipiki ikakatiza mbele yake, na yule dereva alipokuwa katika harakati za
kuikwepa pikipiki ile, alijikuta anaacha njia yake na kuingia upande wa pili na
hapo ndipo alipokutana na lile gari dogo la abiria na kusababisha ajali.
Sasa kama ukiangalia mfano huo
utaona mtu wa kwanza hakutoa habari za mwendesha pikipiki, yeye alitoa hasa
maelezo ya ajali ilivyotokea lakini wapili alizungumzia zaidi chanzo cha ajali
kuliko ajali ilivyokuwa, lakini hiyo haiwafanyi mashahidi wale wawili kuwa
waongo kwasababu maelezo yanayotofautiana, wala hauufanyi ushuhuda wao
kujichanganya.
Na ndivyo ilivyo katika habari hii
ya punda, kulikuwa na sababu Mungu kuruhusu waandishi hao watoe taarifa kwa
jinsi tofauti ili atufundishe sisi kitu..Ni kweli kabisa punda aliyechukuliwa
pale hakuwa punda mmoja, Bwana aliwaagiza mitume wake wamlete Punda,akiwa na
mtoto wake, japo shabaha yake ilikuwa ni Yule mtoto wa punda, na sio Yule punda
mkubwa na ndio maana waandishi wale wengine hawakusumbuka kueleza habari za
wote isipokuwa yule mwana-punda tu peke yake kwasababu yeye ndio ilikuwa
shabaha kubwa katika habari ile , lakini tukisoma huku kwingine kumbe Bwana
hakuona vema aende peke yake, bali pamoja na mama yake..
Hiyo ni kutupa sisi picha zaidi, juu
ya mazingira yaliyokuwa yanamzunguka mwana-punda yule, kutuonyesha ni jinsi
gani yule mwana-punda alivyokuwa bado ni mdogo, bado ni mchanga hawezi pengine
kwenda mahali popote peke yake bila mama yake,hajafikia hatua bado ya kutumia
katika utumishi wowote, bado ananyonya, hivyo alihitaji msaada mkubwa sana wa
mama yake pembeni au kama si msaada basi alihitaji walau faraja ya mamaye.
Biblia inatuambia alikuwa bado
hajakomaa kuweza kubeba mizigo wala kupandwa na mtu yeyote.
Bado alikuwa ni mchanga kabisa,
lakini ndiye huyo Bwana aliyemuhitaji. Tunaweza kujiuliza ni Kwanini Yesu
hakumwonea huruma walau angempanda mama yake, Yule mtoto apumzike pembeni mwa
mamae…Lakini hilo halikuwa chaguo lake mambo yalikuwa kinyume chake..
Ndugu/Kaka, kumbuka mahali ulipo,
katika udogo wako, katika uchanga wako wako uwe ni wa kimwili au wa kiroho
kiasi cha kwamba huwezi kuenenda mwenyewe bila kutegemea msaada wowote kwa
walio juu yako, hujawahi kutumika katika utumishi wa aina yoyote ile, lakini
Bwana anakuita umtumikie katika hali hiyo hiyo uliyopo, chini ya huyo huyo
kiongozi wako wa kiroho ambaye anakufundisha..Bwana anakuita ukamtumikie, hivyo
usikwamishwe na chochote, Bwana aliyemwita Yule ndiye anayekuita na wewe, (wote
wawili amewaita)….Yeye hana upendeleo wala jicho lake si kama macho yetu, haangalii
cheo, umaarufu wala uzoefu…
Lakini tukiurudi kwenye hiyo habari…kiukweli
hawezi kuwapanda wote wawili kwa wakati mmoja, bali amekuchagua wewe ULIYE MDOGO
UMTUMIKIE, Ili Yule mkubwa asimame pembeni yako kukufariji ,.. Bwana hawezi
kumtumia Yule kwa viwango vya sasa anavyovihitaji kwasababu kashatumika
tayari..Ni zamu yako sasa, leo hii wewe bado ni fresh, anakuhitaji sana katika
utumishi wake, wa kumtukuza yeye katika nyakati hizi za mwisho za kumalizia,
Mteule wa Bwana.
Umekuwa ukiwaangalia viongozi wako
kama kitu cha kurejea, ni jambo jema, sio jambo baya,umekuwa ukijiona hujafikia
bado viwango vya kutumika mbele za Mungu, mpaka utakapipitia pengine madarasa
Fulani au chuo fulani au hatua Fulani kama za mchungaji wako au mwalimu wako,
hiyo ni kweli kabisa, lakini Yesu amekuchagua wewe sasa katika udogo huo, ukamtukuzwe
katikati ya mataifa. Hivyo Ndivyo ilivyompendeza yeye…Bwana Yesu alisema hivi.
"Wakati ule Yesu akajibu,
akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya
uliwaficha wenye hekima na akili, UKAWAFUNULIA WATOTO WACHANGA. 26 Naam, Baba, KWA KUWA NDIVYO ILIVYOPENDEZA
MBELE ZAKO.(Mathayo 11:25).
Unaona? Hivyo ndugu ikiwa utausikia
ujumbe huu, ikiwa utasikia wito wa Mungu ndani yako, usikawie kawie, wala
kujiuliza uliza mara mbili eti mimi nafaa, au nitaweza?, ingia gharama ya
kumfuata Kristo, jitwike msalaba wako, umfuate sasa, neema hiyo haitadumu
milele juu yako ukichelewa chelewa shetani naye yupo pembeni kutaka kukutwika
mizigo yake, au akupande ili akutumie katika mambo yake maovu, na kama
unavyofahamu Kristo hatampanda punda Yule ambaye tayari kashatumiwa, wakati
ndio huu uusikiapo ujumbe huu.. chukua uamuzi sasa. Kwasababu yeye mwenyewe
alisema..
Mathayo 28:29 “JITIENI NIRA YANGU,
mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata
raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni
mwepesi.”
Sasa usisubiri shetani akutie nira
yake ngumu katika uchanga wako, huu ni wakati wa kusema mimi na YESU tumefunga
pingu za maisha milele..Na kuanzia sasa namaanisha kumfuata YESU katika hali
zote zitakazokuja mbele yangu. Na hakika atakuangazia wema wake kwa wakati wake
aliouweka juu yako..Kumbuka Punda Yule mdogo aliyekuwa akikaa mabandani tu na
kula majani, muda mfupi baadaye tunamwona akitembea juu ya red-carpet, Hiyo ni
kututhibitishia kuwa hakuna mtu yeyote aliyewahi kumtumikia Bwana akaja kujuta
maishani.
Na kumbuka leo Tarehe 14, mwazi huu
wa Nne ni sikukuu ya Mitende…wakristo wote duniani wanaadhimisha siku ile kuu
Bwana aliyoingia Yerusalemu huku akiwa amempanda mwana-punda…Hebu huyo
mwanapunda leo awe wewe…Mwambie Bwana nipo mimi, nitwae jinsi nilivyo, niwe
chombo chako, wewe Mfalme wa wafalme, Na hakika utauona wema wa Mungu kwa
viwango ambavyo havipo.
Marko 11: 7 “Wakamletea Yesu yule
mwana-punda, wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake.8 Watu wengi
wakatandaza mavazi yao njiani, na wengine matawi waliyoyakata mashambani.
9 Nao watu waliotangulia na wale
waliofuata wakapaza sauti, Hosana; ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana;
10 umebarikiwa na ufalme ujao, wa
baba yetu Daudi. HOSANA JUU MBINGUNI.”
Ni matumaini yangu, utafanya hivyo
sasa.
Bwana akubariki na Jina la BWANA
YESU libarikiwe daima.
Kwa mafundisho mengine ya ziada
tembelea website yetu |www wingulamashahidi org|, kuna masomo mengi kule
naamini utajifunza na kuinuliwa katika viwango vingine.
Pia usiache ku-“SHARE” ujumbe huu
kwa wengine na Bwana atakubariki.
No comments:
Post a Comment