Shalom! shalom!, karibu tuongeze
maarifa katika mambo yetu yahusuyo wokovu wetu hapa duniani. Wengi wanadhani
mtu akiingia tu katika wokovu basi, akili yake huwa inafutwa na kugeuzwa kuwa
kitu kingine cha kimbinguni, Na hivyo vitu kama wivu, hasira, ghadhabu, visasi,
vinyongo, chuki, huzuni, hofu, vinakuwa vimeondoka kabisa ndani ya huyo mu, Na
ikionekana kuwa havijaondoka basi huyo mtu bado hajafanyika kiumbe kipya.
Mimi hapo nyuma niliomuomba sana
Mungu aniondolee hivyo vitu ndani yangu, kwasababu nilikuwa ninachukia
ninapoona hasira inakuja ndani yangu na mimi ni mkristo, wakati mwingine hofu
Fulani,.hayo yalinifanya nijione kama bado sijawa mkristo. Lakini baada ya
kuona ninaomba sana viondoke bila ya kuona mafanikio yoyote, ndipo Mungu akanifumbua
macho yangu ya ndani nikaona…
Nikaja kugundua kuwa nilikuwa ninamuomba
Mungu aniondolee vitu ambavyo ameniumbia ndani yangu, na kama hiyo haitoshi,
yeye mwenyewe anavyo...Nikafiria nikasema ni kweli ukitafakari utaona Mungu
anao wivu, amejitaja mwenyewe kuwa yeye ni Mungu mwenye wivu (Kutoka 20),
amejitaja kuwa yeye ni Mungu mlipiza kisasi, amejitaja yeye ni Mungu mwenye
hasira nyingi na ghadhabu, isitoshe amejionyesha sehemu nyingi kuwa anahuzunika
wakati mwingine,..Sasa kama hivyo vitu vipo ndani yake kwanini mimi nimwombe
aniondolee?..Na yeye katuumba sisi kwa mfano wake, biblia inasema hivyo.
Kiuhalisia vitu hivi Mungu
hakuviumba kwa ubaya ndani yake na ndani ya watu wake, bali ni kwa nia njema
kabisa na ya Upendo. Embu jaribu kufikiria kama mtu asingekuwa na wivu hata
kidogo kwa mpenzi wake, inamaanisha kuwa hata angemwona mtu mwingine anam-baka
mke wake, asingeshuhulika kufanya lolote angemwacha tu, kwasababu ndani yake
hakuna chembe chembe za wivu, ambazo hizo zingemsaidia kumpigania mke wake
asifanyiwe kitendo kama kile..
Jaribu pia kufikiria kama mtu
asingekuwa na hofu ndani yake, angeweza hata kwenda kuchukua kisu na kumchoma
mtu mwingine, au angeweza hata kwenda kusimama juu ya ghorofa refu na kujitupa
chini, kwasababu ndani yake hakuna hofu ya kuogopa chochote, unadhani tungekuwa
na madhara mengi na makubwa kiasi gani duniani?. Jamii zetu zingesimamaje?
Au fikiria ungekuwa hauna hasira
hata kidogo ungekuwa wewe ni wa kuonewa au kuudhiwa tu kila saa, au
unadhulumiwa haki yako, lakini kama mtu akiona umekasirika, ataogopa na kuacha
kile alichokuwa anakifanya kwasababu anajua akiendelea madhara yoyote yanaweza
kumtokea..Hivyo unaona hasira hapo inasimama kama ulinzi kwa mtu asionewe au
asidhulumiwe au asiudhiwe.
Vivyo hivyo na vitu kama ukali, na
vinginevyo. Ni mambo ambayo Mungu ametuumbia ndani yetu, ili yatumikie katika
mahali papasapo,..Lakini leo hii ni kwanini tunaona , Wivu ni kitu kibaya,
hasira ni kitu kibaya, kisasi ni kitu kibaya, chuki ni kitu kibaya, kinyongo ni
kitu kibaya….Ni kwasababu tunavitumia mahali ambapo Mungu hakutaka vitumike na
ndio hapo vinaonekana kuwa ni vitu vibaya visivyofaa kuonekana ndani ya mtu
yeyote.
Embu tuangalie mfano wa wivu mzuri,
Tuchukulie mfano wa Bwana wetu Yesu, yeye kuna wakati alishikwa na WIVU wa
kushindwa kuvumilia mpaka kufikia hatua ya kuleta madhara na vurugu..Hayo
yalitokea pale alipokwenda Hekaluni na kukuta watu wanafanya biashara mahali
ambapo pangepaswa pawe mahali pa Ibada…ndipo tuona akapindua mezi zile na
kuwachapa wale waliokuwa wanafanya biashara mule ndani. ..Mpaka wanafunzi wake
wakakumbuka kuwa iliandikwa hivyo (Yohana 2:17 ….Wivu wa nyumba yako utanila.).
Unaona huo ni mfano mzuri jinsi wivu
ulivyotumika jinsi ipasavyo. Lakini tujiulize ingekuwa na sisi tupo pale na
yeye je! Tungeshirikiana naye kufanya kile kitendo? Ni rahisi kusema
ndio.Lakini ikiwa leo hii tunaona Injili ya YESU KRISTO Bwana wetu inageuzwa na
kuwa taasisi za kibiashara, na hakuna chochote kinachotukuna ndani
yetu?..Badala yake wivu wetu unajidhihirisha katika mambo mengine yasiyokuwa na
umuhimu sana, pale tunapoona wanafanyazi wenzetu wanatuibia ofisini, ndio
tunakuwa na wivu, pale tunapoona mafisadi wanaaiibia nchi, wanapitisha magendo, ndio tunazungumza
mpaka mshipa ya shingo inatutoka, na kibaya zaidi pale tunapoona majirani zetu
wanafanikiwa, ndipo tunatafuta namna zote juu chini za kuwashusha ili
wasiendelee mbele …
Sasa kama wivu wa namna hii ndio
Mungu kaukataa, kama upo ndani yetu basi tujue umetumika isipovyopasa na hivyo
unahesabika kuwa ni dhambi mbele za Mungu..Nguvu hizo hizo unazotumia
kuhakikisha adui yako hafanikiwi kwanini usizipeleke mbele za Mungu wako
kuhakikisha adui yako MKUU shetani hafanikiwi na kazi zake mbovu?..Kwanini
tunaona kazi ya Mungu inachezewa na sisi tunakaa kimya, wachekeshaji wameingia
mpaka madhabahuni wanamfanyia Mungu dhihaka na sisi tunafurahi pamoja nao,..
Halikadhalika KISASI ni kitu chema
ambacho kimeumbwa ndani yetu ili kitimize kusudi Fulani..Na kusudi hilo si
lingine ziadi ya kumpiga shetani. Fikiria Ulipokuwa katika dhambi ulivyokuwa
unateseka na magonjwa, ulivyokuwa unateswa na nguvu za giza au mapepo au
wachawi au jinsi ulivyokuwa unakesha Disco na kupeteza muda mwingi na pesa
nyingi, hata kwa wiki mara mbili ukimwabudu shetani kule..Lakini sasa umekuwa
mkristo, kuna kitu Fulani ndani yako unapaswa ukihisi kitu kama kisasa
kumlipizia shetani kukupotezea muda wako, na kukutesa na mambo mabaya, Hivyo
sasa utahakikisha muda wako hata kwa wiki mara tatu unakeshsa katika kumsifu
Mungu na na katika kuomba nakuziharibu kazi za shetani katika kuwavuta watu kwa
Kristo..Hicho ndio kisasi Mungu anachokitafuta, ulikuwa unaimba nyimbo za
kidunia, sasa umeokoka ni wakati wa kumwimbia na kumsifu Mungu kwa nguvu zaidi
kulipiza kisasi kwa vile shetani alivyokutenda..
Ulikuwa ni msengenyaji na mmbea wa
kupelekea taarifa za watu kwa watu wengine mpaka mtaa wa tatu sasa umeokoka ni
wakati wa kutumia kipawa kilekile kimlipizia shetani kisasi kwa kusambaza
habari za Yesu kwa nguvu wa watu wengine zaidi ya pale ili kumkomesha shetani.
Hivyo ndio visasa ambavyo Mungu anavihitaji.
Vivyo hivyo tumeumbiwa hofu. Ulikuwa
unamwogopa shetani na wachawi kiasi kwamba hata wewe mwenyewe ulikwenda huko
huko kumwomba akupe hirizi kama kinga yako. Lakini sasa umeokoka, ile hofu
imerudi mahali ipasapo, itumie hiyo kumwogopa Mungu wako na sio adui yako
tena..kama Bwana Yesu alivyotuambia
Luka12:5 “Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.”
Hofu yako ikiwa kwa Mungu utaogopa
kwenda kuzini, utaogopa kutukutana, utaogopa kusema uongo, utaogopa kufanya
mambo maovu, kama haipo hautamjali Mungu
n.k.
Chuki iliyopo ndani yako, ndugu hiyo
Mungu hakukuumbia kwa ajili ya kuwachukia ndugu zako, ni wazi kuwa huwezi
kumwekea chuki mdogo wako au kaka yako au mama yako aliyekuzaa, utakuwa na
chuki sana na Yule ambaye uliyemwona akimchoma mdogo wako moto bila huruma.,
Vivyo hivyo chuki hasaa ya ki-Mungu ipo ndani yetu kumchukia SHETANI pamoja na
mapepo yake yote, na kazi zake zote, na sio wanadamu wenzetu ambayo hayo ndiyo
yamekuwa sababu ya ndugu zetu wengi mamilioni kuwepo kuzimu leo hii.. Na hivyo
kama hiyo chuki itatumika ndani yetu kisawasawa leo hii tutaweka mikakati
kabambe ya kumwangamiza shetani na kazi zake kwa KUHUBIRI INJILI YA YESU KRISTO
kwa watu wote.
Hivyo kwa kumalizia, ni maombi yangu
kuwa vipawa vyote na tabia zote Mungu alizizoweka ndani yako, usiruhusu shetani
azitumie vibaya kwa faida zake, bali badala yake, tuziteke zikaleta manufaa
makubwa katika ufalme wa mbinguni. Leo hii usimwombe Mungu akuondolee hasira
ndani yako, haitaondoka hiyo, ili uwe mfano wa Mungu lazima uwe nayo, badala
yake pale inapokuja basi ukumbuke lile Neno kuwa je! Mahali ninapoiachilia ni
mahali pafaapo, kama hapafai, moja kwa moja ikatae hiyo hali na yenyewe
itatulia,. Lakini ikiwa ni sehemu ifaayo yaani ni sehemu yenye manufaa kwa
ajili ya ufalme wa mbinguni na kumkandamiza shetani..basi usiizuie kwani hiyo
imevuviwa na Mungu kutimiza kusudi lake.
Ubarikiwe sana na Bwana Yesu.
No comments:
Post a Comment