"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Wednesday, October 2, 2019

HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA

Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.

Biblia inasema “Heri” heri maana yake “amebarikiwa yeye”…na inasema pia heri wafu wafao katika Bwana, ikiwa na maana kuwa sio kufa tu! bali kufa katika Bwana.. Wafu ambao hawajafa katika Bwana ni kinyume chake, kwamba Ole wao…

Sentensi hizo zinamaanisha kuwa kuna kitu kitafuata baada ya kifo, nacho si kingine zaidi ya hukumu! Na watakaokufa katika Kristo wanatumaini la kufufuliwa tena na kupewa uzima wa milele, na kupata raha isiyoisha..ndio maana wanaambiwa wana heri. hakuna kitu kinachofuata, isingesema heri wafu! bali ingesema heri walio hai!

Je! maisha yako umeyatengeneza kiasi kwamba, una uhakika, hata leo hii ukiondoka ulimwenguni! utakuwa na heri? Utayatengenezaje?..kwa matendo yako! kwasababu Matendo ya kila mtu yanamfuata popote aendapo! Majumba tukifa tutayaacha, magari tutayaacha, mali tutaziacha lakini matendo tunakwenda nayo huko ng’ambo ya pili. Hivyo sio kitu cha kukichukulia kiwepesi!

kumbuka hakutakuwa na nafasi ya pili baada ya kifo.

Waebrania 9:27 “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu”;
Mgeukie Bwana Yesu kikamilifu. Kimbilio letu na Tumaini letu

Maran atha!

No comments:

Post a Comment