"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Tuesday, October 8, 2019

KUOTA UNAPEWA PESA.

Shalom, Ili upate uhasaha wa ndoto yako, na kuepuka kudanganywa na kila aina ya tafsiri mtu yeyote anayoweza kukuletea, awali ya yote unapaswa ufahamu ndoto yako inaangukia katika kundi lipi, yapo makundi makuu matatu ya ndoto,

Kundi la kwanza ni zile ndoto zinazotokana na Mungu, kundi la pili ni zile zinazotokana na adui(Shetani) na kundi la tatu ni zile zinazotokana na mtu mwenyewe,..Na hizi ndizo zinazootwa na watu mara kwa mara kila siku na kama mtu asipoweza kuzitambua atajikuta anahangaika nazo, na huku hazina maana yoyote ya kumsaidia, kwasababu ndoto za aina hii huja kutokana na shughuli anazozifanya kila siku au mazingira yanayomzungumka muda wote hivyo hizi huwa hazibebi  ujumbe wowote..Kwahiyo ni rahisi ubongo wake kuchukua yale matukio anayoyofanya kila siku na kuyatengenezea matukio yanayofanana na hayo katika ndoto usiku na kuota, ukijiona unaota hivyo basi puuzia ndoto hizo

Ikiwa unahitaji kufahamu kwa undani juu ya makundi haya basi pitia somo hili kwanza >>>> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?   kisha ndio tuendelee,
 Kwamfano ndoto za namna hii za kujiona unapewa pesa, utakuta mtu mmoja kazi yake kila siku ipo kwenye pesa kama vile benki au mfanyabiashara ambaye muda wote analipa na kulipwa pesa, hivyo kuota anapewa pesa linaweza kuwa ni jambo la kawaida kwake kutokea katika ndoto zake za kila siku, kwasababu ubongo ulishajiengenezea ulimwengu kama huo.
 
Lakini ikitokea umeota ndoto katika mazingira, ambayo hayaendani na wewe kupewa pesa, au umeota ndoto hiyo na ukaiona si ndoto ya kawaida, au ulikuwa katika maombi ya kumwomba Mungu kitu Fulani na imekuja na uzito Fulani hivi, au amani Fulani hivi, basi fahamu kuwa upo ujumbe unapaswa kujifunza ndani yake.
Kumbuka kibiblia Fedha inawakilisha chombo cha kuletea jawabu.
Mhubiri 10:19 “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote”.
Hivyo Mungu kukuonyesha katika ndoto, unapewa fedha, ni ishara kuwa amekupa jawabu la ombi lako, na hivi karibuni utapataji haja yako..Ila tilia maanani kitu kimoja hapo biblia inaposema, fedha huleta jawabu la mambo yote haimaanishi  kuwa inaleta majibu mpaka kwenye mambo ya rohoni hapana, fedha haiwezi kuleta uzima ndani ya mtu wala haiwezi kununua upendo..lakini kama ukichunguza hapo utaona mistari hiyo inalenga mambo ya mwilini..kama vile mambo ya karamu, nguo, chakula, nyumba, gari, biashara, ambavyo hivi kimsingi vinahudumiwa na fedha..
Na kama ukijiangalia ndio utagundua vitu vya aina hiyo hiyo ndio uliyokuwa unamwomba Mungu…

Hivyo ametumia ndoto ya fedha kama ishara ya kukuonyesha kuwa maombi yako ameyasikia,..Lakini usitazamie kuwa mtu anayemwomba Mungu mambo ya rohoni kama vile uzima wa milele, au Roho Mtakatifu, au nguvu za Mungu, ataonyeshwa ndoto za namna hiyo kama jibu la maombi yake hapana.. Mungu atamwonyesha Maono ya rohoni, pengine usishangae mtu kama huyo kuona maono ya mbinguni, au kukutana na malaika ndotoni, au kuisikia sauti ya Mungu ikisema naye, au kuota anahubiri au anafundishwa biblia n.k...

Lakini tukirudi kwenye hiyo ndoto ya pesa vile vile usitegemee sana kuwa atatumia njia hiyo hiyo uliyoiona kwamba kweli kuna mtu atakujana  kukupa wewe fedha hapana, inaweza ikawa hivyo au isiwe hivyo, anaweza  kutumia njia pengine ya kuirutubisha kazi yako unayoifanya sasa hivi ,au ukapata kibali mahali Fulani pengine kazini kwako, ambapo boss wako atakulipa vizuri zaidi kuliko sasa hivi, au ukapata mkopo wa kufanya biashara yako n.k. Hivyo kaa katika matarajio huku ukiulinda ukamilifu na utakatifu  katika kazi yako, ndipo Mungu ataitimiza ahadi yake juu yako. Lakini kama wewe upo nje ya Kristo ukaota ndoto kama hiyo, fahamu kuwa ni ishara mbaya nayo ni ishara ya upotevu zaidi..utakwenda kufanikiwa lakini ni ili upotee..
Mithali 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”.
Usisibirie udanganyifu wa mali au mafanikio vikuangamize..Mrudi Muumba wako mapema, tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi kwa Jina la YESU KRISTO ikiwa bado hukubatizwa kisha anza kumwangalia Mungu ili yeye atembee pamoja na wewe katika njia zako zote.

Ubarikiwe.
 
kwa mtiririko mzuri wa masomo na mafundisho mengi ya Neno la Mungu fungua website yetu hii https://wingulamashahidi.org

No comments:

Post a Comment