"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Tuesday, October 8, 2019

KUOTA UNAKIMBIZWA..


Moja kwa moja ndoto kama hii inatoka kwa Yule mwovu, kukimbizwa kwa namna yoyote ile, iwe ni mtu anakukimbiza, au mnyama, ni ndoto kutoka kwa mwovu…Sikuzote kitu kinachokimbizwa ni kitu kilicho dhaifu, cha kuwindwa ili kiliwe, swala anakimbizwa na simba, ni kwasababu yeye ni dhaifu, lakini kitu chenye ujasiri kamwe hakikimbizwi,

Ukijiona unakimbizwa fahamu kabisa moja kwa moja kuwa wewe ni dhaifu rohoni, na hiyo  ni kutokana na kuwa upo nje ya Kristo au kama upo basi hauijatambua mamlaka uliyonayo ndani ya Kristo kwa uchanga wako wa kiroho au kwa uzembe wako wa kutokujishughulisha na mambo ya Mungu..
Mithali 28:1 Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.
Hivyo mrudie Mungu wako kama bado haujaokoka, Tubu ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na uwe kwa Jina la Yesu Kristo, ili upate ondoleo la dhambi zake. Au kama tayari ulikuwa ndani ya Kristo na ulikuwa unayumba yumba huu ni wakati wako sasa kusimama imara.
Kisha anza kujifunza biblia kwa bidii, na pia tafuta kanisa la kiroho la kwenda kujifunzia Neno la Mungu, ili likae kwa wingi ndani yako, upate kujua nafasi uliyonayo katika Kristo. Mpaka siku moja na wewe uote unamkimbiza shetani.
2Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)”
Usipuuzie ndoto hizo, kwasababu shetani kweli anakuwinda akumeze…Fanya uamuzi wa busara kumgeukia Mungu.

Ubarikiwe.


kwa mtiririko mzuri wa masomo na mafundisho mengi ya Neno la Mungu fungua website yetu hii https://wingulamashahidi.org

No comments:

Post a Comment