Hii ni moja ya ndoto ambayo inaotwa na watu wengi sana, na hii huwa inachukua maumbile tofauti tofauti, wengine utakuta wanaota wanafanya mitihani na hawajajiandaa, wanachoshtukia tu ni wakati wa mtihani umefika, hakuna chochote walichofanya wanajiuliza siku zote alikuwa wapi…wengine wanaota wanafanya mtihani mgumu sana lakini wenzake wanaonekana wanafahamu cha kujaza yeye hajui, wengine wanaota kama walikatisha masomo wakaondoka, baadaye aliporudi muda umeshapita mitihani ya mwisho imekaribia, wengine wanaota wamerudi madarasa ya nyuma ambayo tayari wameshayavuka siku nyingi na ni lazima wayavuke ili waendelee na madarasa ya mbele, wengine wanaota wapo wanafundishwa, wengine wanapewa adhabu n.k.…
Na ndoto hizi huwa zinatesa sana, zinaweza kujirudia hata kila baada ya wiki au mwezi, au miezi kadhaa, inategemea na mtu na mtu, lakini ni ndoto ambazo haziachi kuja.
Biblia inasema..Ayubu 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.Mungu sikuzote huwa anapenda kutumia vitu vinavyotuzunguka kutufukishia sisi ujumbe fulani au kutufundisha, na ndio maana utaona Bwana Yesu alipokuwa anafundisha mifano yake yote alikuwa anatumia mambo ya kawaida tu yanatozunguka sikuzote ili kutufikishia sisi ujumbe na tuulewe utaona wakati mwingine alitumia mifano ya ndege, wanafanyabiashara, wafalme, harusi n.k…Hivyo na Mungu ili kukufikisha ujumbe wako wa wokovu huwa anapenda kutumia mfano wa kitu ambacho kimetukuka sana mbele yako, kitu chenye maana sana kwako ambacho ukikisoma anajua kabisa umekosa maisha na hicho si kingine zaidi ya ELIMU.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”
Kufunua kuwa Ipo elimu iliyokuu ambayo inafungua ufunguo sio tu wa maisha ya hapa bali pia wa maisha ya ulimwengu unaokuja, na hiyo si nyingine zaidi ya Elimu ya Ufalme wa Mbinguni..Mungu anakuonyesha hali yako ya kiroho ilivyo kupitia maisha yako ya shuleni, kama unavyojiona upo shuleni hujajiandaa, au mtihani ni mgumu basi katika roho ndivyo hivyo ulivyo.. kuwa upo nyuma, na unapaswa ushinde, yapo madarasa haujayavuka bado, upo pale pale kiroho umekwama, unatamani uendelee mbele unashindwa au unaona ni ngumu kwasababu bado hujayamaliza madarasa ya nyuma Mungu aliyokupa.
Hivyo unapaswa uongeze bidii yako kwa Mungu, ili ufike pale Mungu anapotaka kufika, ongeza kiwango chako cha maombi, jifunze Neno la Mungu sana, ishi maisha yanayompendeza Mungu, punguza muda wa kuihangaikia dunia, na ongeza muda wako wa kumtafuta Mungu, kwasababu yeye ndio ufunguo wa kweli wa maisha yako ndugu. Ukimpata Mungu umepata vyote.
Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”Hivyo ukiwa na bidii na Mungu akaridhika na wewe basi atakuvusha na kukupeleka katika kiwango kingine cha kiroho na kiufahamu. Kumbuka Mungu anakupenda na ndio maana anakuonyesha ndoto kama hizo, Hivyo usipuuzie ungeza bidii yako kwake.
Ubarikiwe.
kwa mtiririko mzuri wa masomo na mafundisho mengi ya Neno la
Mungu fungua website yetu hii https://wingulamashahidi.org
No comments:
Post a Comment