"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Monday, December 12, 2016

MASWALI YALIYOULIZWA NA MAJIBU YAKE: SEHEMU YA KWANZA


SWALI 1: Je! watoto wadogo kubarikiwa na kwenda mafundisho ya kupokea kumunyo na kipaimara na kupewa vyeti ni sahihi kimaandiko?
 JIBU: Watoto wadogo kwenda kwenye mafundisho ya kupokea kipaimara na kumunyo hayo ni mapokeo ya kibinadamu na hayapo sehemu yoyote katika biblia, isipokuwa watoto wadogo wanawekewa mikono tu kama kuwekwa wakfu kwa Mungu..kama Bwana Yesu alivyowawekea mikono wale watoto walioletwa kwake na kuwabariki ukisoma mathayo 19:13-15( Ndipo akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea.
14 Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.
15 Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko.) na pia marko 10:13-16 inaelezea... na watoto hao kama ni kufundishwa wanapaswa kuwekwa chini ya mafundisho ya biblia tu na sio mafundisho ya mapokeo ya dini ambayo yanaishia kwenye kutoa vyeti na kumfanya mtoto aijue sana dini yake kuliko kumjua Kristo,suala ambalo halipo kwenye maandiko kwasababu Kristo hakutoa vyeti  pale alipowabariki wale watoto. Kwahiyo kufanya hivyo sio sahihi kulingana na maandiko.

SWALI 2: Je mtu aliye okoka anaruhusiwa kumiliki guest house au lodge ambayo ina Bar ndani yake na kutoa fungu la kumi kwa kupitia hiyo kazi? ...kwa mfano mimi nina rafiki yangu anafanya kazi kampuni ya TBL kazi ya kampuni hii ni kutengeneza na kuuza bia kama yalivyo makampuni mengine kama Serengeti nk. Huyu ndugu ni mlokole na jumapili bila shaka hutoa fungu la kumi na sadaka zingine pia ana cheo kanisani ..tunalisemaje hili?
JIBU: Kumiliki lodge yenye bar ni kosa..biblia inasema wazi  katika kumbukumbu 23:18 "usilete ujira wa kahaba wala mshahara wa mbwa katika nyumba ya Bwana, ni machukizo" na sio tu kazi ya bar, bali na hata kazi nyingine yoyote isiyokuwa halali mfano biashara ya madawa ya kulevya, ufisadi, ulanguzi,uuzaji pombe,wizi, kamari n.k usijaribu kufanya hivyo ukadhani Mungu ataziridhia sadaka zako hata kama unatoa nyingi kiasi gani au kwa moyo kiasi gani, kwa kufanya hivyo utakuwa unajichukulia laana badala ya baraka, ni machukizo mbele za BWANA, kutii ni bora kuliko dhabihu(1 Samweli 15:22) Mungu hadhihakiwi.
Kwahiyo kuhusu hiyo kazi anapaswa aache ..amwombe tu Mungu awe mwaminifu atampa kazi nyingine tena nzuri zaidi ya hiyo.. Mungu Alisema kuwa anajua tunayahitaji hayo yote mathayo 6:31-34 ''Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake''...kwahiyo asiwe na wasiwasi hilo suala amwachie Mungu.Hivyo mshauri atafute kazi nyingine inayompa Mungu utukufu.

SWALI 3; kuna tofauti gani kati ya vita vya Har magedoni na vita ya gogu na magogu?
JIBU:tofauti kati ya vita vya harmagedon na vita vya gogu na magogu ni hii...vita vya harmagedon vitapiganwa baada ya dhiki kuu kuisha ,hivi ni vita vya siku ile kuu ya Mungu mwenyezi ambapo mataifa yote yatakusanyika kupigana na Mwanakondoo lakini mwanakondoo atawaua kwa upanga unaotoka katika kinywa chake ufu19:15, ufu 16:14-16. na vita vya Gogu na Magogu vitapiganwa baada ya utawala wa miaka 1000 kuisha pale shetani atakapoachiliwa ayadanganye mataifa yote ukisoma ufu 20:8 inaelezea, na hivi vitakuwa sio vita kama vita kwasababu kabla hawajapigana na watakatifu moto utashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza wote....lakini pia kuna  vita nyingine inayozungumziwa katika ezekiel 38 ambayo itakuwa ni vita kati ya Israeli na baadhi ya mataifa hii itakitapiganwa kabla ya unyakuo kufika.Kwahiyo kulingana na unabii wa kibiblia kuna vita kuu tatu zinazokuja mbeleni, ya kwanza ni hiyo vita ya ezekiel 38-39 ambapo Mungu atajichukulia utukufu atakapowapigania Israeli dhidi ya maadui zake, vita ya pili itakuwa ni vita ya Harmagedon kama ilivyoelezewa hapo juu na vita ya tatu na ya mwisho itakuwa ni mwishoni mwa ule utawala wa miaka 1000 pale mataifa yote yatakapoizunguka kambi ya watakatifu.

 SWALI 4;Baada ya unyakuo nini kitatokea kwa waliobakia bila kwenda kwenye unyakuo? 
JIBU: Kwa wakristo watakaobaki wasiokwenda kwenye unyakuo wale wasiopokea chapa ya mnyama watapitia dhiki kuu na mpingakristo atawaua wote, na wote waliobakia ambao sio waamini yaani wale watakaopokea ile chapa ya mnyama wataingojea ile siku ya Bwana ya kuogofya iwakayo kama moto ambayo itakuja tu mara baada ya dhiki kuu kuisha mathayo 25:29 '' Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi'' katika hiyo siku ndipo Bwana atakapoimwaga ghadhabu yake na kisasi chake kwa mataifa yote ulimwenguni. ufu.6:16 ''Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?. Kwahiyo hayo ndio yatakayowakuta watakaobaki.

SWALI 5; Kulingana na Biblia; Roho wa Eliya hana budi kuja mara 5; alikuwa ktk Eliya mwenyewe; akaja juu ya Elisha; Akaja juu ya Yohana mbatizaji; Atakuja juu ya manabii wawili watakaotumwa izraeli. je alikuwa tena juu ya nani?.
JIBU: Roho ya eliya ilikuja.mara ya kwanza kwa eliya, mara ya pili kwa elisha, mara ya tatu kwa yohana mbatizaji, mara ya nne kwa branham, na mara ya tano  itakuja kwa wale mashahidi wawili...Lakini ijulikane kuwa sio roho ya Eliya kama Eliya mwenyewe bali ni Roho ya Mungu iliyobeba huduma kama ya Eliya ambayo imekuja juu ya hao manabii.

SWALI 6: sawa ndugu ubarikiwe  Sasa wengi hawamjui Branham na huduma yake ni ipi; unaweza kutuelezea kwa faida ya wasiojua kuwa Branham ni nani, na ameandikwa wapi kwenye biblia?
JIBU : Amina. Biblia ilitabiri kuja kwa Eliya kabla ya kuja kwa ile 'siku kuu' na ya 'kuogofya' ya Bwana malaki 4:4-6..mbali na eliya na elisha ambao walishakwisha kutangulia, wote tunafahamu kuwa yohana mbatizaji alitimiza sehemu 'A' ya andiko hili yaani angekuja kabla ya ile siku kuu ya Bwana(siku kuu ya Bwana ni wakati wa Kristo akiwa duniani) yohana ndiye aliyeyatimiza haya maandiko kwasababu alitangulia kuja kwa kwanza kwa Kristo..lakini sehemu 'B' inasema eliya angekuja kabla ya  ile siku ya kuogofya ya Bwana (siku ya kuogofya ya Bwana ambayo haijaja bado,itakuja baadaye katika hukumu ya mataifa) kwahiyo angepaswa aje eliya mwingine kabla ya kuja kwa hiyo siku ya kuogofya..naye ataigeuza mioyo ya watoto iwaelekee baba zao kulingana na malaki 4:4-6..kwahiyo katika kizazi chetu cha siku za mwisho huduma hii ilipaswa itokee ili igeuze mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, na huduma pekee iliyoturudisha katika imani ya mababa yaani mitume(kuturudisha kwenye neno) hatujaona nyingine zaidi ya huduma ya william branham..kuna mengi ya kuzungumza lakini kwa ufupi tu mtu akitaka kufahamu zaidi atauliza tutamsaidia kwa neema za Mungu. Na pia Branham hajatajwa mahali popote katika biblia bali huduma yake ndiyo iliyotajwa, Kama tu vile yohana mbatizaji alivyotabiriwa huduma yake lakini jina lake halikutajwa kwenye biblia...ndivyo ilivyo kwa branham na ndivyo itakavyokuwa kwa mashahidi wawili wa kwenye ufunuo11, cha msingi sio kumjua mtu bali kupata ujumbe ulioletwa na Mungu kupitia huyo mtu.Amina

4 comments:

  1. mimi nina swali hapo kuhusu vita ya gogu na magogu.
    Bwana Yesu atakapokuwa anatawala
    miaka 1,000 atakuwa akitawala pamoja na watakatifu. Hii inamaanisha ulimwengu utakuwa na watakatifu tu pamoja na mfalme ambaye ndiye Bwana Yesu. Je, shetani akiachiliwa kutoka kuzimu atawadanganya hao watakatifu?

    ReplyDelete
  2. Hapana katika utawala wa miaka 1000 kutakuwa na watu wa aina mbili..1) watakatifu watakashuka na Bwana kutoka mbinguni, hawa ndio wale waliokwenda katika unyakuo na watakaofufuliwa katika siku ya mwisho,

    2)kundi hili la pili litakuwa ni la watu wa kawaida wachache sana watakaopata neema kusalimika katika ile siku kuu ya Bwana, hawa ndio watakaozaliana kwasababu watakuwa na miili yao ya asili, na shetani ndio atakaokuja kuwadanganya atakapofunguliwa japo sio wote..lakini wale wengine watakuwa na miili yao ya utukufu isiyoweza kuharibika ,hawatazaa wala kuzaliana, hawa ni watakatifu na ndio kambi yao itakayozungukwa na hawawezi kudanganyika.

    ReplyDelete
  3. Mbarikiwe kwa ufafanuzi wenu mzur wa mandiko

    ReplyDelete