SWALI 1: Je! wayahudi wote wataokolewa hata kama ni watenda dhambi,
Kwasababu wote ni uzao wa Ibrahimu? maana biblia inasema warumi
11:25-26" Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione
kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu
wa Mataifa uwasili. Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa,
Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. " kwahiyo
nahitaji ufafanuzi hapa aliposema israeli wote wataokoka.
JIBU: Watu wengi wanadhani hivyo, lakini ukweli ni kwamba Hapana! sio
waisraeli wote atakaookolewa bali wale tu walioishi maisha yanayolingana na
torati yao ila wengine wasioishi kulingana na maagizo ya dini yao(torati)
watahukumiwa kama tu watu wasioamini...
Warumi
9:6-7 '' Si
kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio
wa
uzao wa Israeli.Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali,
Katika
Isaka wazao wako wataitwa;; ''
si unaona hapo! ni kama tu vile si
"wakristo" wote walio "wa-kristo" kwelikweli isipokuwa wale waliozaliwa
mara ya pili.
Wapo wengi leo wanaojiita wakristo, kwasababu tu wamezaliwa kwenye
familia za
kikristo lakini ukiangalia mienendo yao, na matendo yao hayaendani na
ukristo,
sasa hao wanakuwa ni wakristo-jina vivyo hivyo na kwa wayahudi. Wapo
wayahudi
wengi leo hii japo ni wayahudi kweli kweli lakini hawaamini kama kuna
Mungu ni kama wapagani, na hata hawamtazamii Masihi wao, wanapinga kila
imani na baadhi yao hawaamini hata kuna Mungu sasa! mtu wa namna hiyo
hawezikuokeolewa isipokuwa labda atubu na kubadili mwenendo wake?.
Hata
katika biblia agano la kale wapo wengi ambao waliharibiwa na
Mungu japo walikuwa ni wayahudi kweli kweli mfano tunao Kora na Dathani,
na
wale wana wawili wa Eli n.k. Wapo wengine pia biblia inarekodi ni
wachawi, na wapinga-kristo mfano tunamwona yule aliyekutana na Paulo:
Matendo 13:
6 Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;
7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.
9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,
10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? "
7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.
9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,
10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? "
Kwahiyo
siyo wayahudi wote walio waisraeli, na sio
wayahudi wote watakaokolewa bali ni wale watakaozishika amri za Mungu
ambao majina yao yameandikwa kwenye kitabu cha uzima kabla misingi ya
ulimwengu kuwekwa.
Lakini ijapokuwa kwa sasa hivi wayahudi wengi
hawamkubali Yesu kama masihi wao, Hiyo Mungu karuhusu ni makusudi kabisa ya Mungu kufanya hivyo ili
sisi mataifa tupate neema ya kuokolewa, lakini utafika wakati nao umeshakaribia
ambapo neema itaondoka kwetu na kurejea tena israeli, wakati huo wayahudi wengi
(walio wayahudi kweli kweli wanaoishi kulingana na torati yao) watampokea
Kristo kama Masihi wao,na kuacha desturi zao za sheria na kuipokea neema ya
BWANA YESU KRISTO.
warumi 11:24-26"4 Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika
mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha
asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza
kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe?
25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. "
25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. "
Na baada ya hayo kutokea hapo ndipo ule
mwisho utakapokuja.(mathayo 24:14), je! jiulize wakati sasa neema inakaribia
kuondoka huku kwetu wewe imeipokea? kwasababu utafika wakati utatamani kuingia
utashindwa pale mwenye nyumba(Bwana Yesu) atakaposimama na kufunga mlango luka
13:25..biblia inasema mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani na
wanaoiona ni wachache, je! taa yako inawaka, maisha yako yanahakisi
wokovu? muda umekwenda kushinda tunavyofikiri kama Mungu aliweza kuwakatilia
mbali watu wake (wayahudi) ili sisi mataifa ambao tulikuwa makafiri tupate
neema, unadhani atashindwa kutukatilia na sisi mbali ili awarejee watu wake
wateule israeli??
Waebrania 2:3"sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna
hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale
waliosikia;"
SWALI 2: Je! wakristo wote wataenda kwenye unyakuo?
JIBU: Mtu aliyezaliwa mara ya pili ndiye atakayeenda kwenye unyakuo ila mwngine yeyote ambaye hajazaliwa mara ya pili (hajabatizwa kwa Roho Mtakatifu) atabaki hapa chini warumi 8:9 '' Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.'' Na pia warumi 8:14'' Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.'' Kwahiyo ukiwa na Roho wa Mungu utatoa yale matunda ya Roho nayo ni upendo,utu wema, uvumilivu, fadhili, kiasi(wagalatia 5:22) na utakatifu ambao pasipo huo biblia inasema hakuna atakayemwona Mungu,(waebrania 12:14) Kwahiyo mkristo yeyote ambaye hajabatizwa na Roho Mtakatifu hatoweza kwenda kwenye unyakuo. Kwahiyo jichunguze kujiita tu mkristo na kwenda kanisani jumapili kwa jumapili tu haitoshi, tafuta Roho Mtakatifu maana huyo ndiyo chapa/muhuri wa Mungu biblia inasema (waefeso 4:30).
SWALI 3: Ule mji yerusalemu mpya unaozungumziwa katika kitabu cha ufunuo sura ya 20 na 21 utakaoshuka kutoka mbinguni utakuwa ni wa dizaini gani, na utakaa wapi?
JIBU: Ule mji Yerusalemu mpya unaoonekana ukishuka kutoka mbinguni sio mji kama mji unaoelezewa pale ile ni lugha ya ishara tu ya kwenye biblia..ule mji unamaanisha bibi arusi wa Kristo..tunafahamu kuwa kanisa limejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, efeso 2:20 "Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho". mahali pengine Yesu alisema bomoeni hekalu hili nami nitalijenga ndani ya siku tatu, tunajua kuwa alikuwa hazungumzii juu ya jengo kama jengo bali mwili wake,alitumia jengo kufananisha na mwili wake, na mwili wake ni kanisa lililojengwa na viungo tofauti tofauti ambao ni sisi..ufu 21:2 'nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe'..hapa tunaona kuwa mji huo umefananishwa na bibi arusi ambao ni watakatifu watakaoenda kwenye unyakuo na kurudi kutawala na Kristo, hao ndio ule mji mpya Yerusalemu ambao Mungu anakaa ndani yake, Mungu hatumii ujenzi wa kibinadamu kuunda mji wake, watakatifu ndio mji wake ambao Mungu anaubuni na kuunda.
kwahiyo ule mji mtakatifu Yerusalemu utakuwa ni wale watakatifu(bibi arusi) atakayenyakuliwa, na kisha baadaye kurudi na kutawala na Yesu Kristo.
SWALI 4: Katika utawala wa miaka 1000 hapa duniani je, bibi arusi yeye atakuwa akioa na kuolewa au ni wale tu waliokuwa na dhambi ambao waliingia katika utawala wa miaka 1000 ili wazaane na kuijaza nchi tena ambao dhambi zao sasa zimewaacha kwa muda kwani shetani yuko kifungoni kwa muda?
JIBU: Bibi arusi atakayeenda kwenye unyakuo na wale wayahudi pamoja na wanawali wapumbavu yaani wote watakaokuwepo kwenye ufufuo wa kwanza hawataoa wala kuolewa kwani watapewa miili ya utukufu ufunuo 20:4-6. lakini kuna wengine watakaopewa neema ya kuingia katIka utawala wa miaka 1000 watakuwa na miili yao ya asili hao ndio watakaokuwa wakizaa na kuzaliana hawa watakuwa ni mabaki ya wanadamu wachache sana walisalia ambao hawakuangamizwa katika ile siku kuu ya Bwana ya kutisha biblia inarekodi kutakuwa na wanadamu wachache sana watakao salio, wanadamu wataadimika kama dhahabu, isaya 13:9-13" Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri. Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali". kwahiyo hawa katika utawala wa miaka 1000, ndio watakao oa na kuolewa na kuzaliana, na kufa.
lakini hao wengne yaani watakatifu watakaoenda kwenye unyakuo, pamoja na wayahudi na wale wanawali wapumbavu watakaofufuliwa, wote hao watapewa miili ya utukufu watakuwa hawafi, hawaoi wala hawaolewi watakuwa kama malaika mathay 22:30. hawa watatawala pamoja na Kristo milele na milele.
SWALI 5: Je, wakati Yesu anarudi kujitambulisha kwa ndugu zake waizraeli wakati huo mpinga Krisro tayari atakuwa ameisha livunja lile agano au ni baada ya dhiki kuu ndipo anarudi kujutambulisha kwa ndugu zake na anaoorudi kujitambulisha wale 144,000 tayari wameisha patikana au wako wapi? na Je; ile mizaituni miwili itakuwa wapi wakati Yesu anarudi kujitambulisha kwa nduguze?
JIBU: Ndio mpingakristo atakapolivunja tu lile agano katikati ya juma ndipo dhiki kuu itakapoanza, na wakati huo wale 144000 Watakuwa wameshahubiriwa injili na wale manabii wawili wa kwenye ufunuo 11 (ambao ndio ile mizeituni miwili), kwa kile kipindi cha miaka mitatu na nusu ya kwanza, na hawa wayahudi 144000 watafanikiwa kuiepuka ile dhiki kuu kwani Mungu atawahifadhi mbali na mpinga kristo kwa ufunuo watakaopata kupitia injili ya wale manabii wawili...lakini wayahudi waliosalia mbali na wale 144000 watapitia dhiki kuu kwasbabu hawakuamini ujumbe wa wale manabii wawili, kama vile tu katika kanisa la mataifa kuna wanawali wapumbavu na werevu vivyo hivyo kwa israeli pia watakuwepo wapumbavu na werevu, wale wapumbavu ndio watakaopitia dhki kuu, bali werevu(144000) Mungu atawaepusha na dhiki na kuingia katika utawala wa miaka 1000 kutawala na Kristo.
SWALI 6: Vita ya Har-magedon itakuwa vita kati ya nani na nani? na itapiganwa lini?
JIBU : Vita vya harmagedon itakuwa ni vita kati ya Mungu mwenyezi na wanadamu vikiongozwa na wafalme kutoka maawio ya jua (mataifa ya mashariki) na vitapiganiwa israel, na itapiganwa baada ya ile dhiki kuu kuisha ndani ya zile siku 75 zilizoongezeka zinazozungumziwa katika daniel 12:12,..na hata hivyo haitakuwa vita maana Bwana hawezi kupigana na wanadamu, vita vitaisha ndani ya muda mfupi sana kwa kuwa yeye ni BWANA WA MABWANA na MFALME WA WAFALME.ufunuo 17:14.
ufunuo 16:12-16 "Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni."
No comments:
Post a Comment