"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Wednesday, December 28, 2016

MASWALI YALIYOULIZWA NA MAJIBU YAKE: SEHEMU YA 7


SWALI 1; Je, kwa mwanamwali mpumbavu yeye katika Yerusalemu mpya ya milele itakayokuwa hapa duniani atakuwa na maisha ya kawaida ya kufanya kazi kama maisha tuliyonayo duniani ya kulima na kufuga?

JIBU:Mimi nadhani hili kundi linalojumuisha (wanawali wapumbavu, na wayahudi, pamoja na bibi arusi wa kristo) hawa watakuwa na miili ya utukufu hivyo basi kulima au kupanda itakuwa siyo sehemu yao, pengine watakuwa na shughuli nyingine tofauti na hizo. watakaokuwa wanapanda na kufuga watakuwa wale watu wenye miili ya asili watakapenya kuingia katika utawala wa miaka 1000. kwasababu watakuwa ni watu wa asili tu, wanaohitaji kula, kunywa n.k. lakini hao wengine watakuwa na miili kama ya malaika. Hivyo vitu havitakuwa vya muhimu kwao.

SWALI 2; Je, kule mbinguni kwenye maisha ya milele wanyama watakuwepo?
JIBU:Tukienda mbinguni sifahamu vizuri kama wanyama watakuwepo au la. lakini katika umilele tutakaotawala na Kristo hapa duniani biblia inasema wanyama watakuwepo, isaya 11:6" Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.
7 Ng'ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng'ombe.
8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.
9 Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari. " kwahiyo wanyama watakuwepo na biblia inasema pia warumi 8:29-22"19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.
20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;
21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.
22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa. " kwahiyo wanyama nao wataokolewa

 
SWALI 3; wale 144000 hata kule mbinguni watakuwa pia ni watumishi wa bibi arusi au ni katika utawala wa miaka 1000 tu?
JIBU:Hawa 144000 hawataenda mbinguni..kule mbinguni watakuwepo bibi arusi tu wa Kristo(watakaonyakuliwa). hawa wayahudi 144,000 hawatakufa wala kunyakuliwa, watakuja kuungana na bibi arusi baadaye katika utawala wa miaka 1000, biblia inawaita bikira ufunuo 14:4" Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa. " kwahiyo hawatakuwa watumwa wa bibi arusi, hawa nao ni bikira wa Mungu safi watakaokuja kutawala pamoja na watakatifu wengine katika utawala wa miaka 1000.

SWALI 4; Yule joka kubwa jekundu, na yule mnyama, na yule nabii wa uongo ni kitu kimoja au wanatofautiana?
JIBU: Hizi ni roho 3 za uovu lakini zinafanya kazi moja..kwa ufupi lile joka kubwa jekundu linalozungumziwa kwenye ufunuo 12 & 13 ni shetani mwenyewe (ibilisi/lucifer)..ukiendelea kusoma kwenye ufunuo 13:1"
1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.


tunaona hap lile joka  lilimpa nguvu zake yule mnyama aliyetoka kwenye bahari mwenye vichwa saba na pembe 10, sasa huyu mnyama mwenye vichwa saba na pembe 10 ni roho ya shetani iliyovaa mataifa kupambana na uzao wa Mungu, na utawala wa Mungu tangu zamani Mungu alipoanza kuweka agano na Ibrahimu. sasa vile vichwa saba vya yule mnyama ni falme 7. nazo ni MISRI, ASHURU, BABELI, UMEDI &UAJEMI, UGIRIKI, RUMI-ya kipagani, RUMI-YA KIDINI...ukifuatilia mataifa haya shetani aliyatumia kupambana na kuuteketeza uzao wa Mungu(wayahudi),

kumbuka taifa la kwanza ambalo lilianza kupambana na uzao wa Mungu lilikuwa ni MISRI, Tunaona jinsi shetani alivyomtumia Farao kuwatesa watu wa Mungu (wayahudi),hata walipokuwa wanatoka utumwani bado Farao alitafuta kwenda kuwaangamiza kabisa lakini jambo hilo halikufanikiwa kwasababu Mungu anawapigania watu wake.

Na baada ya miaka mingi baadaye lilinyanyuka taifa lingine lililotawala dunia kama Misri nalo ni Ashuru hilo liliwachukua wana wa Israeli tena (ukisoma 2wafalme 17 inaelezea ) yale makabila 10 yalichukuliwa kwenda ASHURU utumwani na hayakurudi tena mpaka ilipofika mwaka 1948.

Na baada ya Ashuru lilinyanyuka taifa lingine tena lililotawala dunia nalo ni BABELI chini ya mfalme nebkadneza(2 wafalme 24), Hili lilichukua lile kabila la Yuda na benyamini lililobaki na kulipeleka utumwani, lakini baada ya miaka 70 kupita Mungu alilirejesha tena kwenye nchi yake ya ahadi.

Na baada ya Babeli kudondoka lilinyanyuka taifa lingine lililotawa dunia nalo ni UAJEMI & UMEDI,(Daniel 5:30-31).Wayahudi waliendelea bado kutiishwa chini ya huu utawala.

kisha likaja taifa UYUNANI(UGIRIKI),lilitawala kuanzia mwaka BC331-BC168.Wayahudi bado waliendelea kutiishwa chini ya utawala huu wa kipagani wa kigiriki.

Na baada ya hapo ndipo ikanyanyuka ngome ya RUMI (ya kipagani ilitawala dunia kuanzia mwaka BC 168-AD 476),hilo ndilo lililotawala kwa mabavu na nguvu, utawala wake biblia unaufananisha na utawala wa chuma.Adhabu kali zilikuwa zikitolewa kwa mtu yeyote atakayekwenda kinyume na utawala, na ndipo adhabu za kutundikwa kwa wahalifu msalabani zilipozaliwa.Wayahudi waliteseka sana chini ya utawala huu wakimtazamia MASIHI wao wanaomtarajia aje kuwakomboa na utawala wa kimabavu wa Rumi.

Baada ya huo ulinyanyuka utawala mwingine ambao ni uleule wa kirumi isipokuwa huu ni wa kidini zaidi (RUMI ya kidini).huu ulianza kutawala kuanzia mwaka (AD 476- hadi wakati wa sasa).Hichi ndicho kile kichwa cha saba cha yule mnyama chenye pembe 10,ndipo kiti cha enzi cha shetani kilipo sasa, Na ndio chimbuko la kanisa katholiki,na upapa.tunafahamu katika historia ni utawala uliongoza kwa kuuwa watakatifu wengi wa Mungu takribani wakristo milioni 68 waliuliwa kikatili, Na huu utawala ndio unaoendelea kutawala ulimwengu mpaka sasa na upo katika roho na pia katika mwili na unaendelea kuuwa watu kiroho unapeleka mamilioni ya watu kuzimu,ni utawala wa shetani unaowafanya watu wamwabudu yeye pasipo kujua wakidhani kuwa wanamwabudu Mungu.

Mafundisho ya kanisa katholiki ndiyo yaliyouharibu ukristo na biblia inaliita BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI (Ufunuo 17), kama kanisa katholiki ndiyo mama wa makahaba inamaanisha anao mabinti ambao ni makahaba na hao mabinti si mengine zaidi ya madhehebu yote yaliyosalia yanayoiga desturi za mama yao kahaba kanisa katholiki mfano wa hayo ni lutherani,anglikana,SDA,orthodox n.k.lakini biblia inasema ufunuo 18:4-5"..Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.
.Hivyo basi biblia inasema 
Unaona ni jinsi gani shetani alivyoweza kutumia hizi falme za dunia ambao ndio vile vichwa saba vya yule joka na yule mnyama kuharibu uzao wa Mungu?,

Kwahiyo ndugu kama upo huko toka haraka madhehebu hayakufikishi mbinguni,sio kutoka kwa miguu bali katika roho, uwe bikira safi iepuke alama ya mnyama.  
Kwahiyo falme tano za kwanza zilitumika kwa kuwaangamiza wayahudi pekee, lakini mbili za mwisho zinawatesa wayahudi pamoja na wakristo  na hata sasa bado yanawatesa. na yatawatesa zaidi wakati wa kipindi cha dhiki kuu. na zile pembe kumi juu ya kichwa cha yule mnyama ni mataifa 10 ya ulaya yaliyogawanyika (divided kingdoms ) ambayo hiyo roho inayaendesha, ikiongozwa na Roma.

Na yule mnyama wa 3 ALIYE MFANO WA MWANAKONDOO naye ananena kama joka (ufunuo13:11) ni roho ile ile ya shetani iliyotoka kwa yule joka, ikaenda kwa yule mnyama mwenye vichwa saba na pembe kumi sasa imehamia kwa huyu mnyama aliyemfano wa mwanakondoo, biblia inamwita nabii wa uongo. na roho hii inaliendesha taifa la Marekani kwa sasa, na kazi yao ni moja tu. kupambana na kuuangamiza kabisa uzao wa Mungu kwa kutumia mifumo iliyojiwekea kwa kuunganisha  umoja wa dini zote na madhehebu yote  duniani kuunda ile alama ya mnyama.


kwa ufupi hawa 3, joka(ambaye ndiye shetani), yule mnyama na nabii wa uwongo. ni roho za mashetani..zinazotenda kazi kwa pamoja duniani.

 SWALI 5; Kwanini Mungu anawashugulikia Izraeli kama taifa na Mataifa mtu mmoja mmoja?
JIBU:Mungu siku zote, hashughuliki na taifa, bali anashughulika na mtu mmoja, mmoja, Mungu aliweka agano na Ibrahimu na uzao wake baada yake. sio pamoja na ukoo wa ibrahimu au na familia yake hakuweka na watu wanaoitwa wayahudi bali ibrahimu, basi wote waliofuata nyumba yake katika viuno vyake, watakaoenda katika imani ile ile ya ibrahimu hao ndio taifa la israeli.vivyo hivyo katika ukristo tunapozaliwa mara ya pili tunaingia katika taifa la YESU KRISTO (uzao wa kifalme) nasi tunakuwa wana wa uzao. kwahiyo tofautisha kati ya uzao wetu na uzao wa wayahudi, uzao wa wayahudi ni wa asili, lakini uzao wetu sisi ni wa rohoni, na taifa letu ni la rohoni. nasi ndio maana tunahesabika kuwa ni uzao wa Ibrahimu izrael wa kiroho.
kwahiyo Mungu anashughulika na Israel katika mwili kama watu wake kwa agano alilowekeana na Ibrahimu lakini sisi mataifa hakuna agano lolote Mungu aliloweka na mababa zetu katika mwili.

SWALI 6; Hosea 6:1-2 "Njooni rumeudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; nae amepiga na yeye atatufunga jeraha zetu. Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. Neno hili lina maana gani siku kufufuliwa baada ya siku mbili na siku ya tatu kuinuliwa na kuishi mbele zake?
JIBU:neno hili, picha ya kwanza tunayoiona hapo ni ya Bwana Yesu Kristo, kufa na kukaa kaburini na siku ya tatu kufufuka, na picha nyingine tunayoiona tunafahamu siku moja kwa Mungu ni sawa na miaka 1000 kwa wanadamu, hivyo basi ni miaka 2000 imepita tangu ujio wa Kristo mara ya kwanza, na sasa tupo au tunaukaribia mwaka wa 3000 ambayo ndiyo siku ya tatu,..ndiyo siku yetu sisi ya kuinuliwa mbele zake.

SWALI 7; Je wale ambao watakutwa wakiwa hai wakati wa unyakuo wakanyakuliwa wao watakuja wafe lini au hawatakufa maisha yao yote?
JIBU: Mtu akishanyakuliwa na kwenda mbinguni hawezi kufa tena kwasababu atakuwa na mwili wa utukufu kama wa malaika.wataishi milele.

SWALI 8; Ni kosa gani walilolifanya wana wa Izraeli lililofanya Mungu kuwapeleka utumwani Misri miaka 400?
JIBU: mimi ninadhani kosa  mojawapo walilofanya mpaka  Mungu kuwapeleka misri ni lile la kumuuza ndugu yao yusufu kule misri lakini pia sio sababu kuu iliyowafanya wakae utumwani miaka 400, kulikuwa na kusudi lingine la Mungu ndani yake kwamfano kwa kuenda kule Misri taifa la Izraeli pamoja na mataifa yote ulimwenguni kwa wakati ule na wakati tuliopo sasa tunaweza kujua na kufahamu uweza wa Mungu jinsi ulivyo na mkono wake unavyoweza kuokoa na kuangamiza, hebu fikiria bahari inagawanyika, maji yanakuwa damu, nchi inapigwa giza siku tatu, nzige, vyura, chawa taifa zima kulishwa mana na nyama kwa muda wa miaka 40 n.k. hakika tusingemjua Mungu pasipo maajabu hayo mi naona hii ndiyo sababu kuu ya wao kupelekwa Misri ...maana habari yao ya kukaa utumwani miaka 400 ilikuwa imeshatabiriwa hata hapo kabla.

No comments:

Post a Comment