"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Thursday, July 20, 2017

MASWALI NA MAJIBU: SEHEMU YA 17

SWALI 1: Biblia inasema 1wakoritho 6:2-3 "Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? HAMJUI YA KUWA MTAWAHUKUMU MALAIKA,basi si zaidi sana mambo ya maisha haya? " . Swali ni je! sisi tutahukumuje malaika?.


JIBU: Watakatifu wamefananishwa na BWANA wetu YESU KRISTO kwa sababu yeye aliitwaa asili ya mwanadamu na sio asili ya malaika wala kiumbe kingine chochote, maandiko yanamtaja yeye kama mzaliwa wa kwanza kati ya ndugu wengi (ambao ndio sisi), Waebrania 2: 16 " Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.
17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake".

 Unaona hapo na kama vile Mungu alivyompa vitu vyote vya mbinguni, na vya duniani na vya kuzimu vivyo hivyo alimpa pamoja na hukumu yote (Yohana 5:22), na pia tukisoma:
Waefeso 1:20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo
23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote. "

Kwahiyo kama Mungu amempa vyote ikiwemo na hukumu ya viumbe vyote  vya mbinguni na vya duniani, visafi na vichafu, vilivyopo na vitakavyokuja, hivyo ni dhahiri kuwa malaika wote watakatifu na walioasi wapo chini yake na watahukumiwa na yeye kulingana na njia zao, aidha ni nzuri au mbaya, kwa mfano ule ule atakavyowahukumu wanadamu wote watakatifu na waovu.Hivyo basi kama watakatifu watakuja kuketi pamoja na KRISTO (Ufunuo 3:21) ni wazi kuwa watahukumu pamoja na Kristo, maana wakati huo watasimama kama ndugu zake.
kwahiyo ndio ni kweli malaika wote watahukumiwa na watakatifu, wale malaika watakatifu watazidi kutukuzwa zaidi pamoja na  Kristo katika umilele ujao, na wale waovu (shetani na malaika zake) watahukumiwa na kutupwa katika lile ziwa la moto pamoja na wanadamu walioasi. kumbuka hizi hukumu zitafanywa na YESU pamoja na watakatifu wake tu!. Na ndio maana maandiko yanasema tutauhukumu ulimwengu na malaika wote. 

Ufunuo 20:4 inasema..." KISHA NIKAONA VITI VYA ENZI, WAKAKETI JUU YAKE, NAO WAKAPEWA HUKUMU; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. "

Kwahiyo wale tu watakaoshinda na KUKETI PAMOJA NAYE KATIKA KITI CHAKE CHA ENZI hao ndio watakaohukumu ULIMWENGU na MALAIKA. Amina.
Kumbuka watakaokuwa na mamlaka hayo ni wale watakaoshinda tu (watakaonyakuliwa)..


Kwahiyo tujitahidi tushinde maana biblia inasema..
Ufunuo 3:19-22 "Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 YEYE ASHINDAYE, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. "

SWALI 2: Naomba kujua  watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?


JIBU: Tukisoma Luka 13:23-28"  Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache?
 Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika MLANGO ULIO MWEMBAMBA, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. "
Ukisoma tena..Mathayo 7:13 -14 Inasema.. "Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. "
Maandiko hayo yanaeleza wazi kabisa kwamba watakaokolewa ni WACHACHE, kwasababu njia imesongwa sana! lakini swali linakuja je hii njia imesongwa na nini? Ni wazi kabisa imesongwa na mambo mengi  ya ulimwengu huu ambayo ni, anasa, upendaji fedha kupita kiasi, wivu, chuki,tamaa, uasherati uliokithiri ambao sasa upo mpaka kwenye mitandao mambo ambayo hapo zamani hayakuwepo, mitindo ya wanawake kutembea nusu uchi, burudani na miziki ya kidunia,ufisadi n.k. na zaidi ya yote ni kuongezeka kwa wimbi kubwa la manabii wengi wa uongo na hivyo kuifanya ile njia ya kweli isitambulike kirahisi, kwasababu imechanganyikana na njia nyingine nyingi za uongo mambo ambayo hapo nyuma hayakuwepo, na jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo ile njia ya ukweli inavyozidi kuwa nyembamba zaidi, imefikia hatua ya kwamba ukristo wa leo unapimwa na kiwango cha mafanikio ya kidunia aliyonayo mtu na sio mafanikio ya kiroho (yaani utakatifu), Neno la kweli limetupwa nje!. 

Bwana Yesu Kristo aliweka wazi pale aliposema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa siku za kuja kwake mwana wa Adamu? je! katika siku za Nuhu waliokoka watu wangapi? tunaona waliokoka watu 8 tu kati ya mabilioni ya watu waliokuwepo duniani wakati ule..na tena alisema kama ilivyokuwa katika siku za Lutu ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adama..je! wakati wa Lutu walipona watu wangapi?..Jibu ni dhahiri kuwa ni walipon watu 3   tu kati ya mamilioni waliokuwa wanaishi Sodoma na Gomora wakati ule. Na kumbuka Bwana Yesu hawezi kusema uongo,kizazi cha Nuhu na Lutu kimefananishwa na kizazi chetu.

 NA NI KWELI KABISA! watakaookolewa katika kizazi hiki cha mwisho tunachoishi ni WACHACHE MNO!!! Hivyo ndugu tujitahidi tuwe kati ya hao wachache watakaokolewa kwa kupita hiyo njia nyembamba iliyodharauliwa na kuchekwa na ulimwengu wote nayo ni UKRISTO ULE WA MTINDO WA KALE WA MITUME..ikiwa wewe ni mwanamke tupa nguo za kizinzi uvae kama mwanamke wa kikristo mwanamke wa kikristo havai vimini, suruali wala kaptula, hapaki wanja wala lipsticks, mwanamume wa kikristo hanywi pombe, sio mtukanaji, mkristo yoyote hapaswi kupenda mambo ya ulimwengu? Bwana Yesu alisema itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yako.? Ni wakati wa kutafuta vitu vya kimbinguni ile siku ile isitujie kama mwivi.
Muda umeenda sana tunaishi katika kizazi kibaya kushinda vyote, tuwe macho Bwana yu mlangoni kuja. Amen.


SWALI 3: Maandiko yanasema wakolosai 3:20" Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana. "..Lakini sehemu nyingine YESU alisema kwenye luka 14:26"Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. " ..Naomba ufafanuzi hapo sijaelewa heshima kwa mzazi ni ipi?.



JIBU: Biblia pia inasema Efeso 6:1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu 'KATIKA BWANA', maana hii ndiyo haki.Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia. " ..

Ni kweli tunapaswa tuwatii na kuwaheshimu wazazi lakini kuna 1) utii ambao hautokani na Mungu na 2) Utii unaochukua nafasi ya Mungu..huo ndio Kristo alioukataa..kwa mfano utii usiotokana na Mungu ni kama unakuta mzazi ni mshirikina halafu anataka kukufundisha na wewe kuwa mchawi, au mzazi ni mlevi anataka na wewe uwe mlevi au mzazi anafanya biashara haramu anakulazimisha na wewe ufanye biashara haramu kwa namna hiyo basi biblia imeruhusu kutokutii na sio dhambi mbele za Mungu kwasababu inakuharibia mahusiano yako wewe na Mungu kumbuka huo mstari hapo unaposema watiini wazazi wenu, unasema hivi watiini "katika BWANA" kwahiyo ulevi, uchawi, ufisadi, uasherati, uuaji n.k. hayo sio katika Bwana, Hivyo kwa kukataa kushirikiana naye Mungu hatahesabu kama hukumtii japo yeye ataona kama hukumtii.
Na namna ya pili ni ule utii unaotaka kuchukua nafasi ya Mungu, Kwamfano mzazi anakuzuia wewe usimpokee Kristo, anakuzuia usiombe, anakuzuia usitende matendo mema, anakuzuia usiitii sauti ya Mungu kwamfano pale Mungu anapokuambia acha kufanya jambo fulani  na mzazi hataki  hapo sasa hauna budi kutupa  chini la mzazi na kuchukua la Mungu hata kama mzazi wako ana maana nzuri kiasi gani kwako hapo ndipo  Bwana YESU aliposema ASIYEMCHUKIA baba yake au mama yake hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 

Na wengi hapa wanakwama unakuta Bwana kamwita mtu atoke katika imani fulani ya uongo inayoabudu masanamu ili amtumikie katika roho na kweli lakini kwasababu ya wazazi wake na ndugu zake ni washirika wazuri katika hiyo imani, anaamua kuwafuata wazazi wake kwa hofu kwamba atakuwa hajawaheshimu wazazi wake. Kumbuka YESU alisema adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe. Huo ndio wakati wa kubeba msalaba wako na kumfuata Kristo. soma mafungu yafuatayo;..


Mathayo 10:32-38" Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
34 MSIDHANI YA KUWA NIMEKUJA KULETA AMANI DUNIANI; LA! SIKUJA KULETA AMANI BALI UPANGA.
35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. "


Kwahiyo Mungu anapokuita hamaanishi kwamba anataka kukuletea maafa wewe katika familia yako au kati ya ndugu zako, Hapana lakini mwanzo lazima mafarakano yaje kwasababu hautaeleweka ila mwisho wake huwa mzuri. maana kwa kumtii wewe Mungu utawapata na ndugu zako lakini usidhani kwa kuwatii wazazi wako ukamweka Mungu kando ndio umewaokoa wazazi wako la! hasha kinyume cha hapo utaipoteza roho yako pamoja na zao. Mfano mzuri tunaye Bwana wetu alionekana amerukwa na akili kwa ajili ya Mungu, watu wa nyumbani mwake hawakumwamini maandiko yanasema hivyo soma Yohana 7:5 na (Marko 3:21" Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili. ") kama Bwana hakuona haya kuonekana amerukwa na akili inatupasaje sisi?..Lakini tunaona kwa kumtii kwake Mungu watu wa nyumbani mwake walikuja kuokolewa pamoja na dunia nzima. Haleluya.!
       UBARIKIWE NA BWANA YESU!

No comments:

Post a Comment