Kuna hatari kubwa sana, kumlinganisha Bwana wetu YESU KRISTO na mtu yeyote, ambaye kwetu sisi ni Bwana na ni Mungu. Tangu zamani Mungu amekuwa akiwatumia watumishi wake kutenda kazi zake akithibitisha kwa ishara na miujiza mingi iliyofuatana nao kiasi cha kwamba baadhi ya watu wasiokuwa na ufahamu kutaka kuwaabudu wao kama Mungu.
Jambo kama hili tunaweza tukaiona likijitokeza katika enzi za mitume, tukisoma
[matendo 14:8-15 inasema;
" Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mamaye, ambaye hajaenda kabisa.
9 Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; ambaye akamkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa
10 akasema kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawasawa. Akasimama upesi akaenda.
11 Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.
12 Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji.
13 Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng'ombe na taji za maua hata malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano.
14 Walakini mitume Barnaba na Paulo, walikpopata habari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakipiga kelele,
15 wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha].
Kama tunavyoona hapo mitume waliwaambia makutano kuwa wao sio miungu, na anayepaswa kuabudiwa ni mmoja tu!. Vivyo hivyo katika kizazi chetu hichi cha kanisa la mwisho la LAODIKIA, Mungu alimtumia mtumishi wake mwaminifu ndugu. William Marrion Branham kama mjumbe na nabii wa kanisa hili la mwisho, BWANA akilithibitisha Neno lake kwa ishara nyingi na miujiza isiyokuwa ya kawaidia iliyofuatana naye, kwa mfano ile nguzo ya moto iliyotokea juu ya kichwa chake wakati anahubiri, utambuzi wa siri za mioyo, sauti kusema naye kutoka mbinguni n.k. Na zaidi ya yote aliwafundisha watu wamgeukie KRISTO na kumwabudu yeye pekee.
Lakini cha kusikitisha ni kwamba yule ibilisi wa zamani ameingia na kunyanyua watumishi wake kumwabudu William Branham kama vile tu dini ya katoliki inavyomwabudu mariamu na kusujudia picha zake, hizi ni ibada za sanamu za hali ya juu.
Hivi karibuni mchungaji mmoja huko nchini Congo ambaye amekuwa akiabudu picha za William Branham kwa muda mrefu, alidiriki kutoa maneno ya makufuru dhidi ya Bwana Yesu Kristo. Siku moja katika mahubiri yake alisimama na kusema YESU ni nyoka, ni shetani na sio Mungu bali william branham ndiye Mungu, aliendelea kusema kama huyo YESU ni Mungu basi aniue sasa hivi. Lakini kabla hata hajamaliza kusema hayo maneno alidondoka saa ile ile na kufa, kwa hofu watu walikimbia na baada ya dakika kama kumi waliporudi walimkuta ameshaoza kaliwa na CHANGO na kuzikwa hapo hapo, kama tu vile Herode alipotaka kujifananisha na Mungu akaliwa na CHANGO(matendo 12:23). tazama video ya tukio hili chini...
Ndugu Mungu sio wa kudhihakiwa wala utukufu wake hagawani na mtu mwingine yeyote, ikiwa wewe unamwabudu bikira Mariamu, ikiwa unaabudu picha za William Branham, ikiwa unawaabudu watakatifu wa aina yoyote, ikiwa unamwabudu Buddha, n.k. Tubu umgeukie Mungu jiepushe na uzinzi wa kiroho.
BWANA alitoa amri na kusema katika Kutoka 20:3-6" Usiwe na miungu mingine ila mimi.Mungu akubariki.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. "
No comments:
Post a Comment