“HAKUNA KUZIMU sehemu ambayo roho za wenye dhambi zitateswa milele”, Papa Francis amenukuliwa akisema hayo Alhamisi katika mahojiano na gazeti la Italian Repubblica.
Papa aliongezea na kusema “Baada ya kifo, roho za watu watakaotubu zitasamehewa na kwenda mbinguni, lakini zile roho ambazo hazitatubu, haziwezi kusamehewa na hivyo zitapotezwa.”
Alimalizia na kusema “JEHANUM haipo, kilichopo ni nafsi za wenye dhambi kupotea milele.”
Mtu huyu mwenye mamilioni ya wafuasi leo hii katoa kauli asizoweza kuzithibitisha ndani ya maandiko matakatifu. Bwana Yesu alitoa mfano wa yule Tajiri na Lazaro kuthibitisha kuwa yapo mateso baada ya kufa, na kuzimu ipo yenye funza wasiokufa, na mateso yasiyoelezeka kwa wale wote waliokufa katika dhambi.
Lakini yeye (Papa) anasema mtu akifa anayo nafasi ya pili ya kutubu, hili limekuwa ni neno la faraja kwa wafuasi wake wengi, lakini hawajui nia ya shetani ni nini!! Nia yake ni watu waendelee kustarehe katika dhambi wakijua hata wakifa ipo nafasi ya pili! Lakini kumbuka Yule Tajiri wa Lazaro aliomba nafasi ya kwenda kuwahubiria tu ndugu zake akakosa sembuse kutubu!!!!!...Hakuna toba baada ya kufa, kitakachofuata ni HUKUMU.
No comments:
Post a Comment