SWALI 1: Ndugu zangu tunaweza kufahamu wale
wajumbe 5 wa kanisa kila mmoja katoka Nchi gani? "Ninafahamu ndugu Paulo
katoka Israel na ndugu Branham katoka marekani(ni kweli ndugu?)" je,hao 5?
JIBU: Paulo mjumbe wa kanisa la kwanza kama ulivyosema alikuwa ni MUISRAELI, IRENIO mjumbe wa kanisa la pili alizaliwa mji uliloitwa SMIRNA kwasasa ni UTURUKI ya magharibi, MARTIN Mjumbe wa kanisa la tatu alizaliwa nchi ya HUNGARY isipokuwa sehemu kubwa ya huduma yake ilikuwa ni Ufaransa, COLUMBA mjumbe wa kanisa la nne alitokea nchi ya IRELAND huko ulaya, MARTIN LUTHER mjumbe wa kanisa la tano alikuwa ni MJERUMANI, JOHN WERSLEY mjumbe wa kanisa la sita alitokea nchi ya UINGEREZA(UNITED KINGDOM)...na WILLIAM BRANHAM nabii wa Bwana kama ulivyosema alitokea Marekani, umeona injili inaenda na jua, kutokea mashariki mpaka magharibi, ilitokea israeli mashariki na inaishia marekani magharibi. kwahiyo tupo wakati wa jioni sana.
SWALI 2: Wale wajumbe ...5 waliomtangulia
ndugu Mjumbe wa kanisa la saba(Branham) walibatiza ubatizo sahihi wakuzamishwa
kwenye maji mengi na iwe Katika Jina La YESU KRISTO Kama alivyofanya mjumbe wa
kwanza (Paulo wa kanisa la kwanza Efeso na mjumbe wa 7 ndugu Branham???...) Na Kama
hawakufanya hivyo je,unaniambia hao wakristo waliowaamini tutakuwa nao kule
ng'ambo kwa BWANA (nakusudia hawataenda motoni?) na kama hawataenda motoni hauoni
hata hawa ambao sasa hawabatizwi katika jina la Yesu Kristo badala yake Baba,Mwana
na Roho mtakatifu nao watakwenda mbinguni?
B.na kama hawa wajumbe 5 walihitilafiana na
mjumbe 1 na wa7 hauoni tunawezakusema hawakuwa na Roho mtakatifu???Je kama
hawakuwa naye kwanini???Na wote tunafikiri walitumwa na Mungu?(sio kama
ninapinga sio wajumbe wa BWANA ndugu).
JIBU: Ubarikiwe ndugu swali zuri sana, ni kweli wajumbe waliotangulia sio wote waliobatiza ubatizo sahihi wa kwa jina la Yesu, nyakati za Paulo na Irenio wa kanisa la pili watu ndio waliobatizwa sahihi kwa ubatizo wa jina la Yesu lakini baada ya kanisa katoliki kuoana na ukristo mwaka 325AD(katika baraza la Nikea) ndipo ubatizo sahihi wa kwa jina la Yesu Kristo, ukauliwa(ukapindishwa) hivyo wajumbe waliofuata hawakupata ufunuo huo, kwasababu ile roho ilikuwa imetafuna mafundisho ya ukweli kwa sehemu kubwa, isipokuwa kikundi kidogo sana cha watu wachache Bwana aliopenda kuwafunulia, Hivyo Bwana alianza kuwatumia wale kurejesha nuru ya kweli kidogo kidogo, ila hawakufanikiwa kuirejesha yote. Hivyo kama waliokolewa au la! ni wazi kuwa wote waliokolewa hata kama hawakubatizwa kwa ubatizo sahihi,kwasababu kulingana na kiwango cha nuru Mungu alichowapa kwa wakati ule, kiliwatosha kuokolewa. hivyo Mungu ni Mungu wa rehema hawezi kumuhukumu mtu kwa jambo asilolijua, wataokolewa kama tu watu wa agano la kale walivyookolewa pasipo damu kumwagika kwani muda ulikuwa bado, wataokolewa kama Daudi, Samweli, Musa n.k sasa watu wa kizazi hiki cha mwisho wote ambao wamesikia ufunuo wa ubatizo sahihi na bado hawataki kubatizwa watahukumiwa kwasababu wameisikia kweli, na wameikataa, hivyo inakuwa ni dhambi kwao, jambo ambalo watu wa kanisa la tatu, la nne na la tano, hawakuipata hii neema. Na kuhusu wajumbe kuwa na Roho au la! Bwana pia anaweza kumpa mtu Roho hata kabla hajabatizwa kwamfano Kornelio alipokea ROho kabla ya kubatizwa lakini hiyo ni neema na inatokea mara chache sana, hivyo wakina luther japokuwa hawakubatizwa katika ubatizo sahihi lakini walikuwa na Roho Mtakatifu ndani yao,
SWALI 3:Mfano mtu alikuwa anafanya maovu alafu ikafika wakati wa kufa kwake akatubu, mfano saa 3:00 jioni alafu akafa saa 3:01jioni atakuwa na uzima wa milele?(mfano kuna bibi mmoja hapa kwetu alikuwa mkatoliki mnyenyekevu tu kama alivyokuwa anapenda alipenda kusali wakatialivyokuwa anaumwa sasa akasema alikufa akarudi wakati alipokuwa anaumwa sana akasema aliona nafiri kuzimu akasema nikubaya sana wale watu aliokuwa nao akawaambia wasali sana huko ni kubaya "nadhani lilikuwa ni ono" sasa hakuchukua siku nyingi akafa).
JIBU: Kwanza ni vizuri kufahamu TOBA ni neno pana kuliko wengi tunavyofikiri. Huwezi kusema leo hii naamua kutubu, kwasababu naenda kufa na sitaki niende kuzimu, Hapana TOBA ni kitu ambacho Mungu mwenyewe anakileta ndani ya moyo wa mtu ( Yohana 6: 44 "Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho". )..Unaona hapo? Hivyo toba inatokea pale Mungu mwenyewe anapougusa moyo wa mtu, kisha yule mtu anajikuta anaona kila sababu ya yeye kubadilisha maisha yake ya kale, sasa kuanzia huo wakati na kuendelea aidha awe hai, au aende kufa anakuwa mtu mwingine.. Mtu kama huyo anajikuta anaingia katika majonzi ya kuyachukia maisha yake ya kale, pengine kwa kulia na kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha mambo ya nyuma aliyokuwa anayaishi. Kisha baada ya Mungu kuona kumaanisha kwake, anamjibu TOBA yake kwa kumpa Amani isiyo ya kawaida. Na hii ndiyo inayompa uhakika kwamba dhambi zake zimesamehewa.
Lakini hii TOBA haiji kwasababu mtu anaona anakaribia kwenda kufa, kwasababu anaogopa kwenda kuzimu, au anataka kwenda mbinguni ndio anatubu..Watu wengi wa dizaini hiyo ni dhahiri kuwa huko nyuma walishawahi kusikia injili ya neema na kuipuuzia. Na hata wakitubu wanafanya kama kubahatisha, hivyo hawawezi kuwa na ule uhakika (ambayo ni AMANI ya kiMUNGU ndani yao) kuwathibitishia kwamba wamesamehewa dhambi zao, labda neema ya Mungu iwe kubwa sana juu ya watu kama hao.
Kwahiyo safari ya wokovu sio ya bahati nasibu, kwamba naikataa injili sasahivi ili kipindi fulani kikifika ndipo nitubu.Hapana, Bwana kwa wakati huo hatakusikia ..kwa maana biblia inasema katika 2Wakoritho 6: 2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa.)
SWALI 4: Ndugu mzee mmoja alinihoji
nakuniambia "kuna wazee wengi waliokufa kabla hata injili haijafika
Tanzania akasema hata hawakubatizwa ama hawakujua kitu kinachoitwa injili
n.K...Ndugu naomba nijibuni hili swali lake akaniambia "Hao watu hawatakwenda
mbinguni???..Ndugu hili nilishindwa kulijibu..swali langu watu hawa wanateseka
kuzimu sasa hivi au???au wako wapi kwasababu hawakupata injili?! mbarikiwe
ndugu zangu wapendwa.
JIBU: Hao watu ambao hawajasikia injili kila mmoja atahukumiwa kulingana na maisha aliyoishi, kwa kawaida kila mwanadamu duniani anayo sheria ndani yake inayomuongoza huku DHAMIRA yake ikimshuhudia kabisa kwamba jambo analolifanya ni sahihi au sio sahihi(totauti na wanyama). Sasa (Hiyo ndiyo inayoitwa INJILI YA MILELE. ni tofauti na injili ya MSALABA. (Warumi 1&2)) . Watu wa kipindi cha Nuhu, Torati ilikuwa bado haijaja duniani, lakini walihukumiwa kwasababu walikuwa wanajua kabisa, uuaji, ni makosa, ushoga ni makosa, wizi ni makosa, ufiraji ni makosa, utoaji mimba ni makosa, kuzini na wanyama ni makosa, kuzini na wazazi wako ni makosa, kutukana ni makosa n.k. Hiyo ndio Injili ya milele ambayo mtu hahitaji kuhubiriwa na yeyote ili ahifahamu, ni injili iliyokuwepo tangu enzi na enzi, kwamba kila mwanadamu anaifahamu na anapaswa kuishi katika hiyo. Kwahiyo wale wote wasioijua torati ya Musa, au Injili ya msalaba..basi watahukumiwa kwa hiyo Injili ya milele..
Lakini kwa sasa Injili ya Msalaba imesambaa ulimwenguni kote. Hivyo sidhani kama kutakuwa na udhuru kwamba mtu yeyote kusema hajasikia.
Ubarikiwe.
Ukiwa na swali lolote lihusulo
biblia ..tutumie (kwa
e-mail/whatsapp/namba za simu )na kwa neema za Bwana litajibiwa.
Naomba muunganisho jamani
ReplyDelete