Kwamfano
wewe kabla hujazaliwa ndugu zako walishajua kabisa utakuja kuwa mwafrika mwenye
rangi nyeusi, na nywele za katani, na sio mchina au mzungu! na ndivyo
ilivyokuja kuwa baada ya kuzaliwa kwako, hivyo hawakushangaa kukuona wewe uko jinsi
ulivyo leo. Lakini Kwanini hawakustaajabia kukuona hivyo, ni kwasababu mababa zako na wenyewe
wako hivyo hivyo kama wewe, Kadhalika kama jamii yenu ni watu warefu au wafupi, ni rahisi watu
kutabiri kimo chako kabla hata hujazaliwa. Pia Kama familia yenu ni ya kifalme, ni
rahisi watu kutabiri kuwa utakuwa mfalme kabla hata hujazaliwa..na siku
utakapokuwa mtu mzima na kuwa mfalme hawatastaajabia kukuona wewe hivyo.
Ni kwasababu gani?. Jibu ni kwamba wameweza kusoma ukoo wako, na kuangalia
tabia za mababa zako na mwenendo wao, na vyeo vyao wakaweza kuhitimisha maisha
yako yatakavyo kuja kuwa. kadhalika na vitu kama majina,mtu kabla hajazaliwa watu
wataishiakumuita majina ya ukoo kama Massawe, Wambura, Lema, Laiza, n.k. ni kwasababu gani?. Jibu ni kwasababu ni lazima aje kuyarithi kutoka kwa mababa zake, Vivyo hivyo kama mababa wana magonjwa
fulani ya kurithi, au tabia au laana fulani ni rahisi kutabiri hali ya mtoto atakayezaliwa itakuwaje
mbeleni.
Tukirudi
katika mambo ya rohoni kuna kuzaliwa pia mara ya pili.
Na ukishazaliwa mara ya pili moja kwa moja unaingizwa katika ukoo husika
ambao
utakufanya urithi kila kitu kinachohusiana na ukoo huo. Kuanzia jina,
tabia,
cheo, mwenendo n.k. Ukiamua leo hii kwa moyo wako wote kujiunga na Dini
ya
UBUDHA, kwa kufata taratibu zao walizokuwekea moja kwa moja utakuwa
umezaliwa na kujiingiza katika Ukoo wa Budha, hivyo mambo yote
yamuhusuyo
Bhuda utabeba na ndio maana huwezi kushangaa kwanini wale mabudha wote
wanafanana,. kimavazi, kimienendo na kitabia ni kwasababu wamezaliwa
humo katika roho..Kadhalika na dini nyingine zote
na vikundi vyote viwe vya kishirikina n.k..
Lakini pia kuna kuzaliwa mara ya
pili katika ukoo unaoitwa UKOO wa YESU KRISTO. Huu ni ukoo ulio juu sana
kuliko koo zote, ni uzao mteule, wa kifalme wa Mungu mwenyewe, Huku nako watu wanazaliwa.
Lakini kabla mtu hajaamua kuzaliwa katika huu ufalme ni lazima ajue ni nani
anayemzaa, pili jina la ukoo wake ni lipi, tatu tabia za huo ukoo ni zipi, nne,
je! ataweza kuendana nazo?. Kumbuka jina la ukoo huo Ni YESU KRISTO huo
ndio msingi kukutambulisha kwamba wewe ni unamilikiwa na mwenye huo ukoo.
kwasababu biblia inasema.
Matendo 4: 12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. "
Hivyo hatua ya kwanza ya kuzaliwa kama tunavyojua wakati wa
utungu kwa mwanamke huwa yanaanza kutoka kwanza maji, kisha damu baadaye kiumbe, kadhalika katika roho
mtu anapodhamiria kuzaliwa mara ya pili kwa KUTUBU kabisa kwa kumaanisha
kuziacha dhambi, anapaswa akabatizwe kwanza katika ubatizo sahihi wa MAJI MENGI.. Na
ni lazima abatizwe kwa JINA LA YESU KRISTO..Zingatia hilo JINA YESU huo ndio
msingi wa kukutambulisha wewe kuwa umezaliwa katika ukoo wa Yesu. Kumbuka wengi
wanabatizwa kwa jina la Baba, mwana na Roho Mtakatifu kimakosa. Mitume
hawakufanya hivyo soma
Matendo 2:37 "Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu".
Soma pia (Matendo 8:16, 10:48, na 19:5) utathibitisha jambo
hilo. Hivyo unapobatizwa kifasaha baada ya kutubu dhambi zako, zinakuwa zinaondolewa
na unakuwa umeingizwa katika Ukoo wa kifalme, Sasa hatua ya mwisho ni kupokea Roho
Mtakatifu mpaka hapo utakuwa una uhakika kuwa wewe ni mwana wa YESU KRISTO.
Kuanzia hapo unakuwa umepanda daraja una haki zote za
kukanyaga nguvu zote za yule adui, kwa Jina la YESU na hakuna lolote
litakalokusumbua kwasababu umepewa mamlaka yote ya kifalme. Lakini haishii
hapo, baada ya kuzaliwa unaanza kurithi zile tabia za ukoo huo uliouingia. Mfano
BABA yako YESU KRISTO alipenda kuishi maisha matakatifu, wewe nawe utaanza
kujiona mwenyewe unachukia maisha ya uovu, utaanza kuona hamu ya pombe, sigara,
uasherati, rushwa, wizi, utukanaji, tamaa vinaanza kuisha, ndani yako pasipo
hata kujilazimisha au kutumia nguvu,.. Ni kwasababu gani? jibu ni kwamba zile
tabia za Baba yako YESU zinaanza kujidhihirisha ndani yako pasipo hata wewe
mwenyewe kuamua hivyo. Huu ndio uwezo wa kufanyika mwana unaotoka kwa Mungu
aliouzungumzia katika
Yohana 1: 12 " Bali wote waliompokea ALIWAPA UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu".
Kadhalika kama Baba yako(YESU), na mababa (mitume na
manabii) walikuwa wanatabia za unyenyekevu, tabia za kusali, kufunga,
kuwapelekea wengine habari njema, n.k. vivyo hivyo na mtoto naye atarithi tabia
hizo, na zitatoka zenyewe ndani pasipo kulazimishwa kwasababu hizi unazaliwa
nazo, haujifunzi..na ndio maana ya Neno hatuishi chini ya sheria, kwasababu
sheria ya Mungu imefungwa ndani ya mioyo yetu haitutawali inatoka yenyewe.
Kadhalika pia kama baba yetu YESU
alichukiwa na ulimwengu, vivyo hivyo na watoto pia watarithi na hayo..kwasababu
yeye mwenyewe alitangulia kuwaonya akisema "mtakuwa watu wa kuchukiwa na
mataifa yote kwa ajili ya jina langu"..
Lakini huu UWEZO hauji hivi hivi na ndio maana tunasema kuna
watu WALIOJIUNGA na watu WALIOZALIWA. Wengi wanasema wamezaliwa mara ya
pili, lakini hawajazingatia hatua za kuzaliwa mara ya pili, ikiwa na maana kuwa
hawajatubu dhambi zao kwa kumaanisha kuziacha, na hawajabatizwa katika
ubatizo sahihi wa kuzamishwa, na kwa jina la YESU KRISTO. Hivyo zile
tabia za kurithi maisha ya YESU KRISTO haziwezi kuonekana ndani yao, hawa ndio
waliojiunga badala ya kuzaliwa. Watajilazimisha kuwa kama wakristo,
watajilazimisha waache uasherati watashindwa, watajilazimsha waache
sigara, pombe, watashindwa kwasababu wao wamejiunga na sio kuzaliwa.
Biblia inasema
Unaona hapo? Ule UZAO WA MUNGU unakaa ndani yako. Lakini kama haupo ndani yako kamwe hutakaa uweze kuishinda dhambi au kumshinda shetani.1Yohana 3:9 “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, KWA SABABU UZAO WAKE WAKAA NDANI YAKE; wala hawezi kutenda dhambi KWA SABABU AMEZALIWA KUTOKANA NA MUNGU ”.
Hivyo ndugu, kumbuka dunia nzima na vizazi vyote vinajua,
kuwa hakuna UFALME mwingine zaidi ya Ufalme wa YESU KRISTO. Huo ndio unaomiliki
sasa dunia, na ndio utakaokuja kumiliki baadaye. Ndugu BWANA YESU sio mtu wa
kawaida kabisa, sasahivi tunavyoongea anamiliki Mbingu zote, malaika wote, na
sayari zote, na dunia yote, na kuzimu yote, na tunavyovijua na
tusivyovijua,.amekaa katika mbingu za mbingu asikoweza kufika mtu yeyote huko
sio malaika yoyote au mwanadamu. Na atakuja tena kuwachukua walio wake ikiwa na
maana ule UZAO WAKE. kwenda kumiliki vyote naye, watu wa milki yake milele na
milele..
Kwanini ukose baraka zote hizo, kwa mambo yasiyokuwa na
maana ya kitambo tu?. Siku ile wenzako wanaenda kung'aa kama Jua kama
yeye alivyo wewe utakuwa wapi ndugu?. Bwana Yesu alisema dhahiri kabisa, katika
Yohana 3: 5 " Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa
maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili".
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili".
Hivyo
ndugu fanya juu chini uzaliwe mara ya pili kabla mlango wa neema haujafungwa.
Ubarikiwe.
Tafadhali "share" kwa
wengine ujumbe huu ili nao wapone. Na Mungu atakubariki.
No comments:
Post a Comment