JIBU: Ubarikiwe ndugu Yohana, Uongo mkubwa uliopo duniani leo hii, ni pale watu wanapodanganyika wakidhani kuwa shetani ni kiumbe chenye mapembe ya kutisha tu na kinakaa kuzimu, hivyo wanadhani wakikutana na kitu kama hicho kinachotisha sana ndio wamemuona shetani, hawajui kuwa yule alikuwa malaika kama wale wengine na alipoasi na malaika zake, ndio akawa shetani mara baada ya kulaaniwa na Mungu..na kulaaniwa kule sio katika maumbile(ya nje) hapana, bali katika roho, na ndio maaana hata leo hii wanadamu wakilaaniwa na Mungu hawabadilili maumbile yao na kuwa na vitu vya kutisha vyenye mapembe au viumbe visivyoeleweka, hapana bali roho zao ndizo zinazobadilishwa.
Kwahiyo shetani na malaika zake, wapo vilevile na ndio maana wanao uwezo wa kujigeuza jinsi wapendavyo hata kijifanya kama malaika wa Mungu, kadhalika pia hawajaondolewa ujuzi wao wote waliokuwa nao, isipokuwa hawana uwezo wowote wa kumshinda mtu aliye ndani ya Kristo..ukisoma 2Wakorintho 11: 3 Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. 14 Wala si ajabu. MAANA SHETANI MWENYEWE HUJIGEUZA AWE MFANO WA MALAIKA WA NURU. 15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. Kwahiyo unaona hapo?..
Hivyo watu wote walioasi pamoja na viumbe vilivyolaaniwa, wapo tu kama walivyoumbwa, isipokuwa tabia za roho zao ndio zinazowatofautisha kwasababu hao tayari wameshalaaniwa wakiongejea mauti ya pili katika lile ziwa la moto..(Hivyo Roho zao ndio zinazofananishwa na vitu vya kutisha).
SWALI 2: "Jini" ni nini? Wengine wanaita jini sharifu au wengine wanaita jini makata n.k.Sasa jini nini?
JIBU: Jini na pepo ni kitu kimoja, ulimwengu wa malaika umefananishwa na ulimwengu wa wanadamu kwa sehemu fulani, hivyo wale malaika baada ya kuasi walitupwa chini, na kulaaniwa,kumbuka walilaaniwa sio kwa kuoteshwa mapembe hapana! bali ni roho zao ndizo zilizobadilishwa, kwahiyo uwezo waliokuwa nao, ujuzi wao, nguvu zao, hawakupokonywa na Mungu, kilichofanyika ni kuwekwa tu kwenye vifungo vya giza vya roho zao wakisubiri kuuliwa katika lile ziwa la moto siku ya mwisho,Hivyo hawa malaika walioasi hakuna mtu anayeweza kuwaua sasa, kwa namna yoyote ile watakuja kufa katika lile ziwa la moto. Sasa kitu wanachofanya hawa malaika walioasi ni kutengeneza viumbe au vitu vitakavyowasaidia wao kufanya kazi zao mbovu za kuharibu uzao wa Mungu, ndio wanatengeneza vitu kama majini na mapepo, kwa ujuzi wao waliokuwa nao kabla ya kuasi Hivyo mapepo na majini ni viumbe/vitendea kazi vya shetani na malaika zake kuharibu watu, mfano halisi ni hata sisi wanadamu tunaweza kutengeneza maroboti yatufanyie kazi zetu kirahisi, mwanadamu anaweza kutengeneza simu ikamfanya aweze kuzungumza na mtu aliyeko Marekani, kadhalika anaweza akatengeneza virusi vya ugonjwa fulani mahabara na kuvipachika kwa mtu mwingine na kumsababisha madhara, anaweza pia akatengeneza ndege itakayomfanya apae hadi marekani kwa lisaa limoja, ndivyo ilivyo kwa malaika walioasi wanatengeneza mapepo fulani katika roho yatakayomwezesha mtu apae na ungo usiku kwenda kijiji fulani au nchi fulani kwa dakika moja, au mapepo/majini fulani labda ya ugonjwa fulani, au labda ya kumwezesha mtu kutambua mambo yanayoendelea sehemu fulani mbali (mapepo ya utambuzi hayo) kama wanadamu wanavyoweza kutengeneza simu zenye internet zinazowasaidia kupata habari zinazoendelea nchi za mbali, na hawa malaika walioasi baada ya kuyatengeneza hayo mapepo wanampachikia mtu fulani ambaye hana ulinzi wa kimungu, na kumfanya awe na uwezo fulani wa kipekee au ugonjwa fulani.Hivyo haya mapepo ndio tunaweza tukayaondoa kwa imani na kuyaambia "nakuharibu kwa moto wa Roho Mtakatifu kwa jina la YESU KRISTO" na yakaungua na kupotea kabisa kabisa, kwasababu ni vitu vilivyotengenezwa na hao malaika walioasi, lakini hao malaika wenyewe huwezi kuwaambia nakuchoma kwa moto wa Roho wa Mungu kwasababu hao watakuja kuchomwa kwenye ziwa la moto siku ile ya mwisho. Hivyo hao sharifu, makata n.k ni mfano wa mapepo.
SWALI 3:Kuna
watu wengine wanadai mtu anaweza akafa lakini roho yake inatumika kama
msukule (kumilikiwa na mtu fulani kwa wakati) hiyo ni kweli ndugu?
JIBU: Biblia inasema mtu ameandikiwa kufa mara moja na baada ya kifo ni hukumu, (waebrania 9:27). Hivyo mtu akishakufa, amekufa hawezi kurudi tena.Lakini hiyo unayosemea kwamba mtu kafa halafu anatumika mahali fulani, kiuhalisia ni kwamba mtu huyo bado hajafa, bali amehamishwa tu, roho yake bado ipo hapa hapa duniani..Huo ni uchawi tu wa shetani(watu wengine wanaita kiini macho) na mambo kama hayo yapo tu, Hivyo watu wa namna hiyo jinsi ya kuwatambua inahitaji ufunuo wa Roho mtakatifu, au usipofunuliwa ni kuomba kwa imani kwa jina la YESU KRISTO na mtu huyo atarudi (sasa hapo ni kulingana na imani yako mwenyewe). Kwasababu biblia inasema yote yawezekana kwake yeye aaminiye.. Na pia kuna vifo vingine vinatokea ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili baadaye aje kudhihirisha uweza wake, na hiyo tunaoina mfano kwa Lazaro. Na watu kama hao nao hawawi wamekufa kabisa(yaani kwenda sehemu za wafu) hapana bali wanakuwa wamelala (japo hata hilo linawezekana kwa Mungu). Hivyo nao pia kwa jina la YESU wanaarudishwa na kuwa hai tena.
No comments:
Post a Comment