Na
kwa jinsi walivyokuwa wanaendelea kukaa katika nchi ya Misri, pasipo kumsikia
kwa vizazi vingi, kidogo kidogo walianza
kumdhania Mungu wa Yakobo ni kama miungu
ya kimisri, walidhani kwamba Mungu wa
Yakobo baba yao anaweza akatengenezewa mfano wa kinyago Fulani kama wa-Misri
wanavyoifanyia miungu yao. Waliona kwasababu wa-Misri wanatolea dhabihu sanamu zao
huku wanaendelea na roho zao mbaya, na bado wanapata mvua nakufanikiwa wakajua
na Mungu wa Yakobo yuko hivyo hivyo, wanaweza wakamtolea dhabihu, na sadaka
lakini maisha yao yakaendelea kuwa vile vile, wakaendelea kuwa na kiburi chao,
matusi yao, malalamiko yao, uuaji wao, n.k.
Hivyo
kwasababu waliishi na Wa-Misri kwa muda mrefu, kwa zaidi ya miaka 400, ule
utamaduni au ule mfumo wa kuabudu walioutumia wa-Misri, uliwaingia na wao pia kudhani
kuwa Mungu wa Israeli naye anaabudiwa kama inavyoabudiwa miungu ya kimisri..
Hata
katika maisha ni kawaida kuona mazingira Fulani yakiwaathiri watu Fulani na
kudhani watu wote wako kama wao. Utakuta kwamfano familia Fulani ina utaratifu wa kukaa
pamoja, na kula pamoja mezani..lakini mmoja wa familia hiyo anatoka na kwenda
kutembelea familia nyingine na kutazamia kuikuta familia ile ipo kama ya kwao,
badala yake anakuta kila mtu yupo kivyake, baba na mama hawaongei, kila mtu na
ratiba zake..lazima itamshangaza kidogo kwasababu amekuta kitu
asichokitegemea..
Ndivyo
ilivyokuwa kwa Wana wa Israeli, Bwana Mungu wakati anakuja kuwatoa ilikuwa ni
shida sana wao kumwelewa na ndio maana tunaona Bwana Mungu aliwapitisha kwanza
jangwani kabla ya kuwaingiza nchi ya Ahadi ili awafundishe yeye ni nani, na anataka
nini kutoka kwao.
Utaona
baada tu ya kutolewa nchi ya Misri, pamoja na kufanyiwa miujiza yote ile, wakaanza
kunung’unika na kulalamika, ni kwasababu gani walikuwa wanafanya vile? Ni
kwasababu walikuwa hawamjui bado Mungu wa Israeli kuwa hapendi watu
wanaonungu’unika, wao walidhani Mungu wa Israeli ni kama miungu ya kimisri
ambayo ukiinung’unikia tu haiwezi kufanya lolote, walidhani ni kama ile miungu
ya kimisri ambayo ukiilalamikia na kuitukana haikufanyi chochote.
Na
ukiendelea mbele zaidi utaona wana wa Israeli wanaanza kufikiria kutengeneza
ndama ya kusubu ili iwarudishe Misri, ni kwanini walifanya vile? ni kwasababu
walidhani Mungu wa Israeli ni kama miungu ya kimisri, kwamba inafika mahali inashindwa
kufanya jambo Fulani, na hivyo kuitafutia njia mbadala.
Na
mambo mengine mengi, waliyoyafanya wana wa Israeli yaliyomkasirisha Mungu
yalitokana na kutomjua Mungu wa YAKOBO ni nani? Yalitokana na kumdhania Mungu
wa Baba yao Ibrahimu ni mfano wa mmojawapo wa miungu ya Misri, isipokuwa yeye
ana nguvu kidogo kipita yao.
Kwasababu
hiyo basi iliwachukua muda mrefu sana kumjua Mungu wa Israeli ni nani..Mpaka
Bwana alipoanza kuwapa sheria ndio kidogo kidogo ndipo Alipoanza kuwaambia yeye
ni MUNGU MMOJA, na hakuna mwingine zaidi
yake wala wa kufananishwa na yeye, hivyo wasiwe na miungu mingine ya kando ila
yeye peke yake. ALIPOANZA KUWAAMBIA YEYE NI MUNGU MTAKATIFU NA HIVYO ANAWATAKA
NA WAO WAWE WATAKATIFU KAMA YEYE ALIVYO..
Walawi
11: 45 “Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri,
ili kwamba niwe Mungu wenu; BASI MTAKUWA WATAKATIFU, KWA KUWA MIMI NI
MTAKATIFU”.
Ndipo
walipoanza kumwelewa Mungu kuwa sio kama miungu ya Misri waliyoizoea kwamba
unaweza ukaitumikia na bado ukaendelea kuwa mwizi, unaweza ukaitolea dhabihu na
bado ukaendelea kuwa mnung’unikaji, unaweza ukaitumikia na bado ukaendelea kuwa
muuaji au mwizi unaweza ukaiabudu na kuiimbia na bado ukaendelea kuilalamikia,
unaweza ukaifuata na bado ukaendelea kuwa mzinzi, au mlaji rushwa, au mtu
mwenye chuki, kwamba unaweza ukawa na miungu mingine midogo midogo mingi ya
pembeni ya kukusaidia pale Mungu mkubwa anapokwama, n.k
ndipo walipojua kuwa Mungu wa Israeli sio kama walivyokuwa wanamdhania kama
miungu ya Misri waliyoizoea Ndipo walipomwelewa vizuri Mungu wa Israeli ni
Mungu mtakatifu sana na hana msaidizi na
yupo mmoja,Iliwachukua miaka zaidi ya 40 kumwelewa vizuri Mungu wa Israeli..
Na
baada akili zao kubadilishwa kumjua Mungu wa kweli ni Mungu wa namna gani,
ndipo wakaweza kutembea na Mungu.
Kaka/Dada
unayesoma haya..swali ni lile lile “Je!
Unamjua Mungu wa kweli??” Kumbuka unaposema umetoka kwenye dhambi ni sawa na
Bwana kakutoa nchi ya Misri ambayo ulikuwa ni mtumwa wa dhambi? Lakini je!
Baada ya kutoka huko umemfahamu Mungu unayemtumikia?? Au unamchukulia Mungu,
kama ile miungu uliyokuwa unaiabudu kabla ya kumpokea yeye??...
Biblia inasema
katika agano jipya pia..
1 PERTO 1: 13 “kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake yesu kristo.
14 kama watoto wa kutii msijifananishe NA TAMAA ZENU ZA KWANZA ZA UJINGA WENU;
15 bali kama yeye ALIYEWAITA ALIVYO MTAKATIFU, NINYI NANYI IWENI WATAKATIFU KATIKA MWENENDO WENU WOTE;
16 kwa maana imeandikwa, MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU.
17 na ikiwa mnamwita baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni".
Huwezi
ukasema umetolewa katika utumwa wa dhambi na bado unasujudia sanamu, huwezi
ukasema umetolewa katika utumwa wa dhambi na bado ukawa mwasherati, au mlevi,
au mtukanaji...Huwezi ukasema umeokolewa kutoka katika utumwa wa dhambi na bado
unavaa nguo zinazoonyesha maungo yako, unavaa nguzo zinazo kubana, unavalia
vimini, suruali na kupaka wanja..Hizo zote ni tamaduni za miungu ya ki-Misri na
huwezi kumtumikia Mungu wa kweli kwa tamaduni za ki-Misri.
Ndugu
yangu kama unataka kwenda na Bwana, mtii anayokuambia leo, Geuka upate ufahamu,
usidanganyike kwamba Mungu anaangalia roho haangalii mwili, usidanganyike
kwamba wanaopaka lipstick,na wanja na wanaovaa hereni, na wigi wataingia
mbinguni..Usidanganyike kuwa wanaofanya masturbation, na wanaotazama
pornography, na wanaoishi na wanawake/wanaume ambao hawajaoana kuwa wataingia
mbinguni, usidanganyike kuwa ukiwa vuguvugu, nusu Mungu nusu ulimwengu,
utaingia mbinguni.. Bwana anasema mwenyewe kuwa ATAKUTAPIKA!! Kwasababu yeye ni mtakatifu na hivyo tutakuwa
watakatifu kama yeye alivyo..
Waebrania
12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, AMBAO
HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO;”
Ni
maombi yangu kuwa utamjua Mungu wa kweli ni nani, kama hujamjua na utachukua
uamuzi thabiti wa kumfuata yeye kwa viwango anavyotaka yeye vya UTAKATIFU. Na
kama hujabatizwa nakushauri ufanye hivyo mapema, kwasababu ubatizo sahihi wa
kuzamishwa katika maji mengi, na kwa Jina la Yesu ni wa muhimu sana, katika kuikamilisha safari
yako ya wokovu.
Bwana
akubariki.
Tafadhali "Share"
ujumbe huu kwa wengine na Bwana atakubariki.
No comments:
Post a Comment