"Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake...ufunuo 16:15"

Friday, May 31, 2019

MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.


 
Jicho la Mungu kidogo kidogo linaanza kuondoka kwa mataifa na kurejea Israeli. Wakati wowote Hekalu la tatu nitaanza kujengwa pale Yerusalemu kwani maandalizi yote yapo tayari.Kilichobaki ni amri tu kutolewa, Na kumbuka ujenzi wa sasa hivi sio kama ule wa zamani, haitachukua tena miaka 7 au 20 kukamilika, itakuwa ni kitendo cha wiki kadhaa tu, au miezi kadhaa tu, kila kitu kitakuwa kimeshakamilika. Na tunafahamu likishakamilika tu, Mungu ataliweka JINA LAKE HAPO kama alivyomwahidia mtumishi wake Daudi na Sulemani zamani(1Wafalme 9:3), na mahali popote jina la Mungu lilipo basi WIVU wake utakuwepo pia.

Na biblia inatuambia mpinga-kristo akishaliona hilo ataondoka moja kwa moja na kwenda kutaka kuketi pale kama Mungu kupatia unajisi ili Mungu atiwe wivu alete uharibifu duniani kote ndio maana kimaandiko huyu mpinga-kristo anajulikana kama (CHUKIZO LA UHARIBIFU), Yeye ndio atakayeleta dhiki kuu, wakati huo unyakuo wa kanisa utakuwa umeshapita.
2Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
Unadhani muda tuliobakiwa nao sasa ni mwingi?.Uzuri ni kwamba hatuna haja ya kuelezeana kila kitu kwani mambo yote yapo wazi kwenye TV na Internet siku hizo zitakapofika.. Huu ni wakati wa kujifunga mkanda UNYAKUO upo mbioni.

Maran Atha.

10 comments:

 1. kweli kabisa maana shetani yuko kazini kila kuicha anaongeza maarifa tu

  ReplyDelete
 2. Ndio ni kweli tunapaswa tukaze mwendo

  ReplyDelete
 3. YESU tusaidie maaana wakati wa umekwisha kabisa

  ReplyDelete
 4. Muda hamna tena yaan navyoona tunasogeza dakika tuu. MUNGU NI YEYE YULE JANA, LEO NA HATA MILELE

  ReplyDelete
 5. Mungu likumbuke kanisa mda umekwisha wa kukaa duniani

  ReplyDelete
 6. Yah Kila mtu awe tayari kwa unyakuo myaonapo haya chagamken inueni vichwa vyenu

  ReplyDelete
 7. Yesu anarudi, hakikisha unajitakasaha mda wowote kanisa tunaondoka.

  ReplyDelete